Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Tanzania: Dua ya Kuliombea Bunge...

    Report Post
    Results 1 to 19 of 19
    1. #1
      Maamuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2008
      Posts : 658
      Rep Power : 662
      Likes Received
      153
      Likes Given
      93

      Default Tanzania: Dua ya Kuliombea Bunge...

      Dua ya kuiombea nchi yetu na kuliombea Bunge - husomwa hivi:

      “Ewe MWENYEZI MUNGU Mtukufu, Muumba Mbingu na Dunia, Umeweka katika Dunia Serikali za Wanadamu na Mabunge ya Mataifa ili haki yako itendeke.

      Twakuomba, uibariki nchi yetu idumishe uhuru, umoja, haki na amani, Umjalie Rais wetu hekima, afya njema na maisha marefu ili pamoja na wanaomshauri, wadumishe utawala bora.

      Utuongezee hekima na busara, sisi Wabunge wa Bunge hili
      la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utupe uwezo wa kujadili kwa dhati, mambo yatakayoletwa mbele yetu leo, ili tufanye maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na ustawi wa nchi yetu. Amina.”
      (Msisitizo ni wangu)

      Nimekuwa nikisikiliza kwa makini sana dua ya kuliombea Bunge inaposomwa na Spika au Naibu wake. Siku zote nimekuwa na mashaka kama kweli kinachoombwa ndicho hasa kinachohitajika na Wabunge wetu. Pamoja na upungufu uliomo kwenye dua hii nadhani hili la kuomba kuongezewa hekima na busara kwa wabunge haliombwi ipasavyo.

      Nijuavyo ni kwamba mtu huongezewa kitu ambacho anacho tayari ila anahitaji nyongeza. Sidhani kama baadhi ya wabunge wetu wana hekima na busara kiasi cha kuhitaji nyongeza. Matokeo yake aliye na hekima huongezewa (kama inavyoombwa) na asiye nayo hapewi (maana hakuna cha kuongeza). Kwa maana hiyo wale wabunge wachache ambao huongezewa hekima na busara huwa wanapishana kwa mbali sana na wale ambao hawana, na hii huleta mgongano na mabishano makubwa yasiyo na tija.

      Nimelazimika kusema haya kutokana na hoja ya hivi karibuni ya wabunge kutaka kuongezewa posho. Hivi kweli wabunge wetu, hayo ndio maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na ustawi wa nchi yetu?

      Waheshimiwa wabunge, ombeni mjaliwe hekima na busara kama vile anavyoombewa Rais wetu. Ili yule asiye navyo apewe angalau kidogo.

      Wakatabahu,

      Maamuma.
      Kakuru and kamtu33 like this.
      Msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana..... Warumi 13:8.

    2. Miaka 50

    3. #2
      jogi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2010
      Posts : 4,028
      Rep Power : 1221
      Likes Received
      982
      Likes Given
      247

      Default Dua ya kuliombea bunge!!!!!

      Serikali haina dini, bunge lina dini gani? Hiyo dua huwa wanamuomba mungu aitwaye nani?

      Kama tambueni kuwa mungu wamuombaye anaonekana kuwa ni mkuu wa itikadi ya taaluma ya maji marefu mbunge wa korogwe.

    4. #3
      mbumbumbu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th December 2010
      Location : Nyasamba, Shinyanga vijijini
      Posts : 471
      Rep Power : 523
      Likes Received
      75
      Likes Given
      13

      Default Dua ya kuliombea taifa - kutoka bungeni..

      "ee Mwenyezi Mungu tusaidie tufanye maamuzi kwa manufaa ya watu wote"

      Je maamuzi ya Bunge huwa kwa manufaa ya wote??

    5. #4
      Bobuk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 2,069
      Rep Power : 923
      Likes Received
      837
      Likes Given
      0

      Default Re: Tanzania: Dua ya Kuliombea Bunge...

      "Umjalie Rais wetu hekima, afya njema na maisha marefu ili pamoja na wanaomshauri, wadumishe utawala bora"

      Hii dua ni ya KULIOMBEA BUNGE (read Bunge), Huyu RAIS na washauri wake wanaingiaje tena kwenye dua ambayo ni SPECIFIC kwa BUNGE na WABUNGE?!

    6. #5
      zuberi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th June 2009
      Posts : 138
      Rep Power : 532
      Likes Received
      5
      Likes Given
      0

      Default Re: Tanzania: Dua ya Kuliombea Bunge...

      mkuu kuna mjumbe mmmoja Bukoba aliwahi mapema kupeleka maoni yake katika tume ya katiba na kusema WIMBO WA TAIFA UFUTWE KWA MAANA WIMBO HUU HUWA OMBEA VIONGOZI LAKINI CHA AJABU VIONGOZI HAO NDIO MAFISADI WAKUBWA TENA WALA HAWA WAHURUMII WAWAOMBEAO kwa mantiki hiyo basi naungana na wewe juu ya dua la kuliombea bunge

    7. RukaaJuu Final

    8. #6
      Suzie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th May 2010
      Posts : 1,086
      Rep Power : 0
      Likes Received
      339
      Likes Given
      309

      Default Sala Bungeni

      Siku hizi sala au Swala linachukuliwa ni sheria na wala sio imani na unyenyekevu kwa Mungu wetu, kitu muhimu kama bunge alafu muombeaji ni kiongozi wa bunge ambaye ni mtu wa kawaida (kuombea bunge), kwanini wasitoe ajira kwa viongozi wa dini? Nahisi ndo maana vurugu na matusi hayaaishi, nahisi serikali iliangalie hili

    9. #7
      Jabulani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th March 2009
      Location : Kituo cha Polisi Jamii
      Posts : 2,978
      Rep Power : 1371
      Likes Received
      825
      Likes Given
      254

      Default Re: Sala Bungeni

      Jana Msigwa ameingia bungeni na Biblia, mapepo yamepagawa hadi yakaanza kutaja taja neno 'nguruwe'
      Kamanda wa Polisi Jamii - Kanda Maalumu

    10. #8
      kinauche's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th October 2012
      Posts : 566
      Rep Power : 445
      Likes Received
      91
      Likes Given
      12

      Default Re: Sala Bungeni

      Nasikia kuna profesa mmoja aliseama neno 'Mungu' liondolewe kwenye sala ya bunge kwa kuwa linawabagua wapagani. Ûnaweza kuona? Wakati wenzao Kenya rais anapiga magoti huku tunasema tusitaje Mungu. Mijitu mingine îmelaaniwa kwa laana. Sasa hii nchi itaendeleaje kama tunamkataa Mungu?

      Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

    11. #9
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,489
      Rep Power : 6171
      Likes Received
      3059
      Likes Given
      1020

      Default Re: Sala Bungeni

      Quote By Suzie
      Siku hizi sala au Swala linachukuliwa ni sheria na wala sio imani na unyenyekevu kwa Mungu wetu, kitu muhimu kama bunge alafu muombeaji ni kiongozi wa bunge ambaye ni mtu wa kawaida (kuombea bunge), kwanini wasitoe ajira kwa viongozi wa dini? Nahisi ndo maana vurugu na matusi hayaaishi, nahisi serikali iliangalie hili

      Duh mkuu naona una kahoja. Hii kitu inabidi iangaliwe upya lakini sasa kwa kuwa tuna imani nyingi hapa nchini itabidi waajiriwe viongozi wa Budha, Katoliki, Sabato, Islamu, Bahai, nk. Kwa jinsi hiyo huenda suala la sala/swala likachukua nusu saa nzima manake kuna wenzetu wakianza kuomba inabidi wekemee hasa wakiingiwa na roho na kuzanza kunena!
      CCM na CDM vyote ni vyama vya siasa vinavyoongozwa na wanasiasa; tofauti yao kubwa ni moja kwamba kimoja kina dola kingine kinataka kushika dola.

    12. mob
      #10
      mob's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th December 2009
      Posts : 594
      Rep Power : 600
      Likes Received
      103
      Likes Given
      39

      Default Re: Sala Bungeni

      MUNGU mwenye rehema tunakuomba utujalie amani na tuishi kwa amani na kila mtu bila ubaguzi

    13. #11
      kelao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2012
      Posts : 961
      Rep Power : 923
      Likes Received
      141
      Likes Given
      8

      Default Re: Sala Bungeni

      Pale bungeni ni unafiki mtupu na ndo maana Mungu amewalaani sasa bunge linaonekana kituko!

    14. #12
      Elli's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 17th March 2008
      Location : Kijito-Upele
      Posts : 8,584
      Rep Power : 2553
      Likes Received
      2143
      Likes Given
      1862

      Default Re: Sala Bungeni

      Sasa wabunge wanataka kuwe na vyuo vya kutongozea, na kuhalalisha Bangi mmmhhh mwisho watakuja kuthibitisha ndoa za jinsia Moja
      ...but what MAN is entirely without Evil intent in the Silence of his Soul???

    15. #13
      Kongosho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Location : Location loading...
      Posts : 25,279
      Rep Power : 13088
      Likes Received
      14159
      Likes Given
      15016

      Default Re: Sala Bungeni

      Waajiri wa dini gani?
      Na watatumia muda gani wote kuomba?
      Na wapagani je? Wakatambike?
      No matter how hot your anger is, it can not cook yams-Nigeria

    16. #14
      NasDaz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2009
      Location : Ushenzini
      Posts : 3,104
      Rep Power : 5354
      Likes Received
      1469
      Likes Given
      1685

      Default Re: Sala Bungeni

      Kwa tanzania hii ambayo leo hii udini umeota mizizi sijui kama sala hizo zitafanya kazi!! Hiki ndicho kitakachotokea:
      • Wakati Sheikh anasoma dua, wabunge Wakristo watakuwa wanakemea kimya kimya Sheikh ashindwe kwa jina la YESU!
      • Wakati Mchungaji anasoma dua, Waislamu watakuwa wanasema kimya kimya "astaghfurall! astaghfurall!!"

      Sasa unazani dua hizo zitapokelewa kweli?
      Waacheni hivyo hivyo, wachanane kavu kavu na ikibidi ifike siku hat watiane mikono hadi waheshimiane!
      mjasiria likes this.
      I am a free thinker! It's only my free thinking that leads me, to what am commenting. Thus, I've no doubt that today I can be your fellow but tomorrow your enemy, and the agent between us being my comments!! So, If today we agree with cheers, tomorrow we'd not disagree with jeers!


    17. #15
      Bangoo's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 3rd November 2011
      Posts : 2,293
      Rep Power : 0
      Likes Received
      374
      Likes Given
      0

      Default Re: Tanzania: Dua ya Kuliombea Bunge...

      :Wasomi wa kiislamu wanasema ni sala ya kikristo....!

    18. #16
      john tongo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th April 2012
      Location : I.T room
      Posts : 334
      Rep Power : 426
      Likes Received
      46
      Likes Given
      16

      Default

      Quote By Maamuma
      Dua ya kuiombea nchi yetu na kuliombea Bunge - husomwa hivi:

      (Msisitizo ni wangu)

      Nimekuwa nikisikiliza kwa makini sana dua ya kuliombea Bunge inaposomwa na Spika au Naibu wake. Siku zote nimekuwa na mashaka kama kweli kinachoombwa ndicho hasa kinachohitajika na Wabunge wetu. Pamoja na upungufu uliomo kwenye dua hii nadhani hili la kuomba kuongezewa hekima na busara kwa wabunge haliombwi ipasavyo.

      Nijuavyo ni kwamba mtu huongezewa kitu ambacho anacho tayari ila anahitaji nyongeza. Sidhani kama baadhi ya wabunge wetu wana hekima na busara kiasi cha kuhitaji nyongeza. Matokeo yake aliye na hekima huongezewa (kama inavyoombwa) na asiye nayo hapewi (maana hakuna cha kuongeza). Kwa maana hiyo wale wabunge wachache ambao huongezewa hekima na busara huwa wanapishana kwa mbali sana na wale ambao hawana, na hii huleta mgongano na mabishano makubwa yasiyo na tija.

      Nimelazimika kusema haya kutokana na hoja ya hivi karibuni ya wabunge kutaka kuongezewa posho. Hivi kweli wabunge wetu, hayo ndio maamuzi sahihi yenye manufaa kwa watu wote na ustawi wa nchi yetu?

      Waheshimiwa wabunge, ombeni mjaliwe hekima na busara kama vile anavyoombewa Rais wetu. Ili yule asiye navyo apewe angalau kidogo.

      Wakatabahu,

      Maamuma.
      chunga sana kitu kinachoitwa kiapo,wabunge wetu wakiapishwa wanashika biblia au quran kama comitment,lakini wanayoyafanya ni kinyume kabisa,unategemea nini hapo kama si "kudata"

    19. #17
      iseesa's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 940
      Rep Power : 0
      Likes Received
      204
      Likes Given
      53

      Default Re: Tanzania: Dua ya Kuliombea Bunge...

      Quote By Bangoo
      :Wasomi wa kiislamu wanasema ni sala ya kikristo....!
      HOJA: SPIKA wa BUNGE lijalo ni lazima awe MUISLAMU kama hoja iliyopita ya kuwa MWANAMKE

    20. #18
      kamtu33's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th March 2012
      Location : mjini kati
      Posts : 339
      Rep Power : 430
      Likes Received
      56
      Likes Given
      69

      Default Re: Tanzania: Dua ya Kuliombea Bunge...

      Tatizo siyo DUA, tatizo liko kwa hao wanaoombewa hiyo DUA maana hata kwenye viapo vyao wanaapa vizuri ila wakisha apa wanasahau kama walisha apa

    21. #19
      Kikwajuni one's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2013
      Posts : 434
      Rep Power : 396
      Likes Received
      103
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Kongosho
      Waajiri wa dini gani?
      Na watatumia muda gani wote kuomba?
      Na wapagani je? Wakatambike?
      Hawa wapagani hawajajiandikisha serekalini,wangejisajili,wakaj ulikana,ingekwa wepesi kujulikana ni kina nani na wako wapi na wanafanya nini

    Similar Topics

    1. Sala ya Kuliombea Taifa letu Watanzania
      By AirTanzania in forum JF Chit-Chat
      Replies: 2
      Last Post: 16th September 2011, 12:31
    2. Maaskofu kuliombea Bunge
      By Mpaka Kieleweke in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 23
      Last Post: 15th August 2011, 19:35
    3. Replies: 0
      Last Post: 18th April 2011, 02:01

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...