Wapendwa wana JF bila shaka hamjambo,Asalaama Aleikhum; Bwana asifiwe!!!
Jamani natoa ushauri kwa chama cha CHADEMA, tegemeo la wanyonge wanaodhurumiwa Watanzania, fanyeni mambo ya uhakika yafuatayo:-
1. Kwanza kabisa hamasisha vijana wa vijijini ambao wako tayari kutumikia chama chetu, maana bila kuwa na vijana kwenye vijiji itakuwa vigumu kupata upenyo wa kupeleka sera za chama kwa jamaii!!!!!!
2. Tayarisha kadi, vipeperushi, matangazo ya sera za chama ili zifike vijijini kwa watu wa rika zote. Kusambaza kadi ni muhimu saana kuna watu wanapenda kuwa wanachama wa CHADEMA lakini hawajui watapata wapi kadi za chama.Peleka kadi nyingi vijijini tupate wanachama wapya wengi!!!!!!!! Nacho ni chanzo cha mapato ya chama!!!
3. Kipindi hiki ambacho watu wengine wana shughuli zingine ni muhimu kujitangaza kwa watu wa vijijini ( grass root), huko kuna wananchi wengi wanataka kujua habari za CHADEMA, msingojee mikutano ya hadhara watu wengine hjawafiki huko.
4. Kutokana na hali mbaya ya uchumi watu wanausongo na hii serikali ya CCM inayopandisha bei za kila kitu, kuanzia sukari, mafuta, sabuni hadi chumvi, watu wanataka njia mbadala kuondoa kero za majanga ya gharama za maisha na CHADEMA ndilo jibu lao wanatakiwa kuelezwa wajiandae!!!
5. Wakati huu wa kujivua maghamba ni muafaka kusambaza sera kwa watu wa kawaida, kama huku Arusha kina mama yeyo,Leighwanani, siankiki na molani wanataka kujua ukombozi utatoka wapi?????????
Wadau wa mapambano ya ukombozi wa TZ nawakilisha!!!!!!!!!


Reply With Quote

MEANS; DOING THE BEST YOU CAN WITH WHAT YOU HAVE.
Follow Us Here