Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

    Report Post
    Page 12 of 26 FirstFirst ... 2101112131422 ... LastLast
    Results 221 to 240 of 501
    1. #1
      allydou's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2009
      Posts : 262
      Rep Power : 570
      Likes Received
      28
      Likes Given
      0

      Default Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

      Habari wana JF

      Ni muda sasa, tangu mwezi wa sita hivi nimekuwa nikisikia kwamba Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuzuia wafanyakazi wa sector binafsi kuchukua NSSF zao mpaka wafikishe umri wa kustaafu uliowekwa na seerikali, like 60yrs.

      nilisikia kwamba mpango huu ulikuwa uanze mwaka huu mwishoni, lakini ikashindikana kutokana na maandalizi kutokuwa yamekamilika vizuri.

      Nimesikia tena leo mjadala huu ukiendelea kwenye forum moja ya watu wanaofanya kazi kampuni mmoja through outlook mails kwamba mpango huu utakuwa implemented kuanzia 1st march 2012 bila kukosa.

      Nilisikia pia kupitia wana forum hao kwamba bunge lilipisha muswada huu na Rais kuusaini kinyemela tangu mwaka jana, kitu ambacho kinaniumiza kichwa, inakuwaje muswada nyeti kama huu upitishwe kwenye bunge hili la sasa la ushindani wa kisiasa na hoja zenye mantiki kutoka upinzani bila wanachi kufahamu.

      mwenye uhakika na suala hili please naomba unifahamishe vizuri.

      Itakuwa ni vizuri zaidi kama utaleta na official data kuleta uhakika zaidi.

      Aksanteni.
      Quote By papag View Post
      Na Hellen Mwango | 23rd July 2012

      Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema kuanzia sasa mwanachama wa mfuko wowote hataruhusiwa kuchukua mafao yake kutokana na sababu yoyote mpaka hapo atakapofikisha miaka 55.

      Hata hivyo, licha ya kuzuia fao la kujitoa na kutoruhusiwa kuchukua mafao yao, mwanachama wakiwamo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma NSSF) atapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye sheria ya SSRA.

      Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, mabadiliko hayo yametokana na sheria za mamlaka hiyo kufanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge Aprili 13, mwaka huu na kwamba imeshasainiwa na Rais Jakaya Kikwete na imeanza kutumika rasmi.

      Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo.

      “Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi lakini kuanzia sasa mwanachama wa mfuko atapata mafao yake pale atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiari (55) au kwa lazima (60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu” ilisema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kufafanua kuwa:

      “Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni.

      Taarifa ya Mkurugenzi huyo iliendelea kusema kuwa mafao ya kujitoa yanapunguza na kuondoa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

      Hata hivyo, ilisema pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya madini yataendelea kutolewa kama kawaida ikiwemo kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.

      Ilisema wanachama wanatakiwa kuwa watulivu kuhusiana na mabadiliko hayo na kwamba maslahi yao yatalindwa na hakuna atakayepunjwa kutokana na utaratibu huo.


      CHANZO: NIPASHE
      Ufafanuzi Kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhitibi wa Hifadhi ya Jamii

      UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.

      Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

      20 JULAI, 2012

      1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

      2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

      3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

      4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia.

      Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

      5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

      6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria.

      Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

      7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu

      8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

      9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.

      Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.

      Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

      Wenu.
      Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii

      Irene Isaka
      MKURUGENZI MKUU



    2. #221
      KakaKiiza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th February 2010
      Location : Here Where you see me!!
      Posts : 6,088
      Rep Power : 16341
      Likes Received
      2275
      Likes Given
      1283

      Default re: Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

      Quote By Mnwele View Post
      Bargain,

      Hii sio tetesi maana haijawa kama hivyo. Lakini umefanya vizuri kuleta hii habari katika kipindi hiki na kuwafanya waajiriwa wote Tanzania wakae mkao wa kula.

      Ukweli ni kwamba serikali ina mpango wa kupeleka bungeni marekebisho ya muswada wa sheria wa mafao ya wafanyakazi kama ulivyopitisha ba bunge ili sasa kufanya wafanyakazi wote wanaokatwa akiba ya mafao (PPF,NNSF, PSPF,LAPF,GEPF n.k) kulazimika kutopata mafao yao kama hawajatimiza umri wa kustaafu(55-60).Mpango huu unaletwa kwa sababu serikali yenu haina namna ya kufanya na ingependa kupata boost ya mapato toka mifuko hii ili kuleta pesa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

      Mpango huu wa aibu na kandamizi utawaathiri wafanyakazi zaidi ya 700000 serikalini lakini kwa kipekee utaathiri na kuua ndoto za wafanyakazi zaidi ya 3000000 walio katika sekta binafsi kama vile makampuni, NGOs na wale waliojiajiri wenyewe na ambao wanatumia mifuko hii.

      (Una imani kubwa kwamba wabunge wetu hasa wa upinzani wataupigia ngumu mpango huu nyonyaji ambao ni wa aina yake katika nchi zote za Afrika. Hii pia inatoa fursa kwa wafanyakazi wote nchini (hasa vijana) kutafakari na kuona jinsi serikali yenu inavyopanga kufifisha mipango yenu ya muda mfupi na ile ya kati. Kazi kwenu simameni na Chukueni Hatua Sasa.

      HABARI NDO HIYO
      Je kama mimi ni mwanachama nafanya sekta binafsi nimefukuzwa kazi na nipo kijiweni je mimi nitakuwa kundi gani??je na pesa yangu ndiyo itakaa huko hadi nifikishe miaka 55???au inakuwaje?
      Its only crazy who will be against to CDM!,only a fool who will fly CCM flag while is hungry!!

    3. #222
      Bobuk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 2,181
      Rep Power : 949
      Likes Received
      889
      Likes Given
      1

      Default

      Jamani wana JF mbona mnakuwa kama sio GTs. Hata ukisoma kwenye utanguliza wa DG wa SSRA amesema hii SHERIA IMESHAPITISHWA NA BUNGE tangu 13 April 2012. WABUNGE WETU wameshaipitisha.

      Mimi ninajiuliza hivi itakuwa je kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwa contract za miaka 2,3,5 .... etc
      Contract imekwisha hajaiwa renewed na wewe una miaka 40, utasubiri hadi ufikishe miaka 55 au 60 ndiyo upate mafao yako.

      Mbona wabunge wao wakimaliza mda wao wa miaka 5 wanachukiwa kila kilicho chao? Kwanini nao hawasubiri hadi wafikishe miaka 60 kwa wale ambao hawajafikisha?

      Wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye NGOs, Private sectors hawa wote sio penshionable wanafanya kazi kwa CONTRACT. Nao watasubiri hadi wafikishe miaka 55 ua 60? Wafanyakazi kwenye MIGODI na hasa MINERS, WANAJESHI na POLISI ambao ni JUNIOR staff wao umri wao wa kustaafu sio miaka 55 is less than that.

      Hii SSRA ilianzishwa hasa kutokana na dai la wafanyakazi kutaka mifuko yote i-harmonise formula ya ukokotoaji wa mafao ya uzeeni, hasa baada ya kuona mfuko wa serikali kuu PSPF unalipa mafao mazuri kulinganisha na mafao duni yanayotolewa na NSSF na PPF. Ndiyo chanzo hasa cha kuundwa SSRA.

      Lakini ajabu badala ya SSRA kufanyia kazi hili DAI kubwa la wafanyakazi, wao wamerukia mambo mengi ambayo sio KERO ya wafanyakazi. Indeed badala ya kupunguza kero, sasa SSRA imeongeza kero kwa wafanyakazi.

      Kama kuna mfanyakazi yeyote Tanzania aliyempatia kura Kikwete na Mbunge wa CCM basi ALAANIWE kwani pamoja na JK kusema hana haja na kula za wafanyakazi bado kuna eti-mifanyakazi na familia zao walitoa kura kwa CCM. Sasa ngoja tukipate cha MOTO.

      Pesa zetu zote za NSSF na PPF zimekopwa na serikali/CCM na kughalamikia WHITE ELEPHANT PROJECTS sasa mifuko haina pesa ndiyo wanawatumia SSRA kuleteta hii sheri ya kijinga.

      Kule France serikali iliongeza MIAKA YA KUSTAAFU kwa wafanyakazi, France nzima iliwaka moto kwa maandamano ya kupinga. Pia hiyo ni mojawapo ya sababu zilizomu cost Sarkozy urais. Lakini eti hii Tanzania nchi ya AMANI, MIFANYAKAZI tumekaa kimya, hata TUCTA inashindwa kutoa tamko. KWELI Watanzania tuna laana!

    4. #223
      We know next's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2010
      Posts : 574
      Rep Power : 559
      Likes Received
      151
      Likes Given
      119

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      Quote By King of Kings View Post
      Urgent public call for @J.Mnyika, Zitto HKigwangalla, @Tundi Lisu (Sijui kama yupo humu)

      Tunaomba ufafanuzi hii sheria ya kuzuia withdraw benefit imepitishwa lini imekuwaje na nyie
      mkakubali hii sheria ipitishe?

      Wabunge wetu wakishidwa kutoa ufafanuzi wa kusadia wananchi wake napendekeza MASS STRIKE

      hii mbona ni kinyume na ILO conversion minimum benefit standard N0.102???

      Hii sio haki kabisa. Nyie SSRA toka lini mmeteuliwa na MUNGU kujua ni lini binadamu wa Tanzania wanaochangia mifuko ya hifadhi watakufa? Na kwa nini mtu asubiri mpaka miaka 55 au 60? Ni nani aliyewiaambia kuwa baada ya kustaafu mtu atategemea tu hizo pesa za hifadhi? Je ni nani aliyewaambia kuwa mtu akistaafu hawezi tena kufanya kazi? Mbona Serikali yenyewe iliwaita Madaktari wastaafu wakati ule wa mgomo wa Madaktari?

      Hii sheria yenu imepitwa na wakati, nadhani suala hili ilikuwa muamue kama watu wanataka kujiunga na hifadhi iwe huru na si lazima. Iwe ni michango ya hiari.

      Irene Isaka, nadhani utajenga uhasama na wafanyakazi walio wengi. Hembu kajipange na uje kwa upya.

    5. #224
      majany's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th September 2008
      Location : IKULU
      Posts : 1,080
      Rep Power : 1709
      Likes Received
      440
      Likes Given
      876

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      eh..eh..eh...hili ni bomu la B52.....mbona wanazilia mingo hela za wanyonge kiasi hiki??

    6. #225
      mchukiaufisadi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Posts : 295
      Rep Power : 488
      Likes Received
      92
      Likes Given
      101

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      Quote By We know next View Post

      Hii sio haki kabisa. Nyie SSRA toka lini mmeteuliwa na MUNGU kujua ni lini binadamu wa Tanzania wanaochangia mifuko ya hifadhi watakufa? Na kwa nini mtu asubiri mpaka miaka 55 au 60? Ni nani aliyewiaambia kuwa baada ya kustaafu mtu atategemea tu hizo pesa za hifadhi? Je ni nani aliyewaambia kuwa mtu akistaafu hawezi tena kufanya kazi? Mbona Serikali yenyewe iliwaita Madaktari wastaafu wakati ule wa mgomo wa Madaktari?

      Hii sheria yenu imepitwa na wakati, nadhani suala hili ilikuwa muamue kama watu wanataka kujiunga na hifadhi iwe huru na si lazima. Iwe ni michango ya hiari.

      Irene Isaka, nadhani utajenga uhasama na wafanyakazi walio wengi. Hembu kajipange na uje kwa upya.
      Irene Isaka katumwa na William Erio wa PPF aliyekuwa boss wake kuwa afute hilo fao maana mfuko wa PPF ungekufa hivi karibuni kama hilo fao la kujitoa lingeendelea.

      PPF hadi sasa hivi inatakiwa kuwa PROVIDENT FUND sio Pension Fund maana imepoteza sifa hiyo kisheria, ni maiti inayotembea. Wamefilisi pesa yote kwa kugawana kila mwaka wakurugenzi. Wanaochangia walio katika ajira za kudumu PPF ni 30% tu wakati wale ambao wanaweza kujitoa wakati wowote ni 70% na kulipwa withdrawal benefit.

      Zitto hana ubavu wa kumwambia chochote DG wa PPF maana amewekwa mfukoni, kila wakati yuko naye eg sabasaba, nanenane etc na kila akija lazima akilimiwe na ktitita. Alionyesha ujasiri kwenye suala la Group Endowment lakini kaishia mfukoni mwa Erio
      Last edited by mchukiaufisadi; 22nd July 2012 at 11:40. Reason: typo
      King of Kings likes this.


    7. #226
      ThinkPad's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2008
      Posts : 1,471
      Rep Power : 865
      Likes Received
      93
      Likes Given
      93

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      MMH! kazi ipo duh miaka 55

    8. #227
      Kachanchabuseta's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2010
      Posts : 2,977
      Rep Power : 1057
      Likes Received
      441
      Likes Given
      1133

      Default re: Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

      Iseeee inawezekana hii sheria imepitishwa zamani

      Kichwa kinauma maana nilitaka kuchukua mafao yangu kujiwezesha kimradi

      Maz^^^^&f**ck

    9. #228
      ndyoko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Posts : 4,517
      Rep Power : 1712
      Likes Received
      1199
      Likes Given
      1917

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      Ktk hili serikali ime-target kutumbua mihela ya NSSF maana ndiyo fuko ambalo limetuna kuliko mifuko yote na huko ndo wanakokopaga hata kulipia mishahara ya watumishi wake wa umma
      “If you can not get what you love, then love what you have”

    10. #229
      Abdulhalim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th July 2007
      Location : Taipei 101
      Posts : 15,866
      Rep Power : 3799
      Likes Received
      1229
      Likes Given
      593

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      sijaelewa nchi inaezaje kubadili sheria nyeti kama hizi kiholela..mi nafikiri ifike mahali na wachanganiaji nao wawe na sauti ktk hii mifuko..haiwezekani tunapelekwa tu kama ndama machinjioni wakti sisi ni watu wazima wenye fikra kamili..kama wanataka kupeleka mambo kwa staili ya ngomani basi mifuko hii iwe hiari maana naona inatumika ndivyosivyo kama fimbo ya kuwachapia wafanyakazi..
      ZeMarcopolo and King of Kings like this.
      Moola's the motive

    11. #230
      Abdulhalim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th July 2007
      Location : Taipei 101
      Posts : 15,866
      Rep Power : 3799
      Likes Received
      1229
      Likes Given
      593

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      Quote By Rejao View Post
      Kila siku mmnaambiwa jiajirini wenyewe hamsikii..haya sasa oneni yanayowakuta. Mwenzenu nimejiajiri na nachangia kwenye voluntary scheme. Naweza kujitoa saa yoyote cuz sheria hainibani.
      usiwe myopic..kama uso wote ungekua pua wapi lingekaa sikio na mdomo..ficha upumbavu wako.
      Moola's the motive

    12. #231
      Kachanchabuseta's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2010
      Posts : 2,977
      Rep Power : 1057
      Likes Received
      441
      Likes Given
      1133

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      CAG: NSSF hatarini kufilisika




      Na Reginald Miruko - Imechapwa 18 April 2012

      MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uko hatarini kufilisika na kupoteza fedha za wanachama wake.
      Hii inatokana na serikali kushindwa kurejesha katika mfuko huu, mabilioni ya shilingi iliyokopa au kudhamini katika miradi mbalimbali.
      Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya 2010/2011, fedha za wanachama, hata katika mifuko mingine ya jamii, ziko hatarini kupotea.
      Mbali na NSSF, mifuko mingine inayotajwa kuwa katika hatari hiyo ni Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF); Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali Kuu (PSPF), Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).
      Kulingana na taarifa ya CAG, sehemu kubwa ya fedha za wanachama ambazo hazijarejeshwa, zilikopeshwa kwa serikali kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
      Katika chuo hiki, NSSF peke yake iliingiza Sh. 234.1 bilioni. Mifuko iliyosalia ilitoa jumla ya Sh. 181.3 bilioni.
      Katika ujenzi wa UDOM, PPF ilitoa Sh. 39.99 bilioni, PSPF (Sh. 105.9 bilioni), LAPF (Sh. 22 bilioni) na NHIF (Sh. 13.4 bilioni). Fedha hizo na riba yake hazijarejeshwa.
      Ripoti ya CAG, Ludovick Utouh, inasema kutorejeshwa kwa mikopo hiyo, iliyochukuliwa au kudhaminiwa na serikali, ni kinyume cha sheria ya udhamini ya mwaka 1974.
      “Kutolipika kwa mikopo hii iliyodhaminiwa na serikali kunaiweka mifuko hii ya hifadhi katika hatari ya kupoteza fedha za wanachama na kuhatarisha uwezo wa mifuko kufanya uwekezaji zaidi,” anasema na kuongeza:
      “Kushindwa kulipa madeni taasisi hizi ambazo baadhi yake zilipata udhamini wa serikali, kunatia shaka iwapo upembuzi wa kina wa wakopaji ulifanywa na mifuko ya kijamii kabla ya kutoa mikopo hiyo.”
      Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau hakupatikana kwa maelezo kuwa alikuwa kwenye mkutano mkoani Mbeya.
      Lakini Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume amesema mikopo kwa serikali imetolewa kwa uangalifu na inalipwa bila matatizo na kwa misingi ya kibiashara.
      “Mikataba ya kisheria imesainiwa kukidhi mazingira mbalimbali ikiwa ni pamoja na iwapo itacheleweshwa…. Hakuna hatari yoyote ya fedha kutolipwa wala kupoteza fedha za wateja,” amesema Chiume.
      Lakini CAG katika taarifa yake ya kurasa 183, anasema, “Ukubwa wa kibiashara kati ya serikali na mifuko unatia shaka kutokana na kusuasua kwa serikali katika ulipaji madeni yake. Hii inahatarisha uendelevu wa mifuko hii.”
      Katika ukaguzi wake, CAG amebaini kuwa NSSF ilitoa Sh. 234.1 bilioni kwa mradi wa UDOM, lakini mkataba uliosainiwa ni wa Sh. 35.2 bilioni tu. Hii ni hatari kwa fedha za wafanyakazi na wastaafu.
      Akifafanua suala la fedha kwenye mkataba kutofautiana na fedha zilizotolewa, Chiume alisema mkataba ulitakiwa kuwa mmoja ambao ulisainiwa wakati wa awamu ya kwanza.
      Chiume alisema kwa awamu ya pili, kilichotakiwa ni kusaini addendum (makubaliano ya nyongeza), ambayo “yako mbioni kukamilika.”
      Utouh anaripoti, “Majengo kwa ajili ya awamu ya kwanza yalikamilika na kuwekwa katika matumizi mwezi Septemba 2008. Mpaka wakati wa ukaguzi 2010/2011, mfuko ulikuwa haujafanikiwa kukusanya malipo ya pango kutoka serikalini.
      Kwa msingi huo, hadi sasa limbikizo la riba limefika thamani ya Sh. 14 bilioni,” anasema Utouh.
      Mkopo huo ulitolewa kwa utaratibu wa kubuni, kujenga, kumiliki na kuhamisha ambapo mfuko ungepokea kodi iliyokokotolewa kwa riba ya asilimia 15 kwa kipindi cha miaka kumi.
      Vilevile CAG amebaini kuwa majengo yaliyojengwa kwa mkopo huo, hayako kwenye vitabu vya UDOM wala katika vitabu vya NSSF, kutokana na uelewa tofauti uliopo kati ya pande mbili zinazohusika.
      Kuna mikanganyiko katika uelewa kwa serikali na mifuko ya hifadhi, ameeleza CAG. Wakati mifuko inasema fedha zilizotumika kujenga majengo hayo zilikuwa mikopo kwa serikali, yenyewe serikali inadai fedha hizo ni uwekezaji wa kawaida wa mifuko hiyo.
      Mbali na UDOM, serikali pia haijalipa jumla ya Sh. 19.77 bilioni zilizotumika katika ujenzi wa ukumbi wa bunge, ambazo hazilipwi kulingana na makubaliano. Hadi wakati wa ukaguzi, NSSF ilikuwa inadai Sh. 8.96 bilioni, PPF (Sh. 7.9 na LAPF Sh. 2.91.
      Pia upo mkopo mwingine wa NSSF wa Sh. 5.33 bilioni na riba ya asilimia 15 kwa miaka kumi, uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa “taasisi ya serikali ya kiusalama” mwaka 2007.
      Mfuko mwingine uliowekeza katika mradi huo ni PSPF uliotoa Sh. 6.4 bilioni.
      Kwa mujibu wa ripoti hiyo, NSSF kwa udhamini wa serikali ilikopesha taasisi kwa shughuli mbalimbali.
      Kwa mfano, ujenzi wa nyumba za polisi kwa Sh. 20 bilioni na Sh. 12. 9 bilioni kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mwaka 2007 kwa ajili ya ujenzi wa Machinga Complex, Ilala.
      King of Kings and GITWA like this.

    13. #232
      samora10's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st July 2010
      Location : Kwa-Gude
      Posts : 3,271
      Rep Power : 1111
      Likes Received
      732
      Likes Given
      1170

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      Hii kitu imekaa vibaya sana.. hela yangu mwenyewe mnipangie siku ya kuichukua? Mateso mnayotupa nyie CCM yanatosha jamani au mnataka mpaka tufe kabisa ndio mfurahi? hela mnazopiga kwenye Meremeta,kagoda, EPA haziwatoshia saa mnataka mapaka hata hichi kidogo tunachokatwa kila siku? sasa life expectancy miaka 52 nyie mnaweka eti Mpaka 55 ili iweje?

      Tuhurumiane jamani.. mtu akiacha kazi apewe hela yake ajue anaifanyia nini wengine tu akazi za mikataba ya miaka miwili miwili.. sasa mnategemea mkataba ukiisha nisubiri mpaka miaka 55?
      King of Kings likes this.
      ''Mipango na Mikakati imekamilika na sasa tuko kwenye mchakato wa mazungumzo na wafadhili"- M Pinda

    14. #233
      GOOD SAMARITAN's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 22nd July 2012
      Posts : 4
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      Hawa jamaa wanadhani wataweza kubadilisha hizi sheria mpaka lini? Je hawajui kuwa leo watabadili sheria kwa kuona mwanya na kesho waone kuwa mifuko ina hela na kuendelea kukopa hatimae kijikuta wanakopa zaidi, je wataendelea kubadili sheria ili wastaafu wasubiri mpaka mfuko utakapo lipwa na serikali? Sisiem tafakarini sana, acheni kutumia mabavu katika kufikiri na kufanya maamuzi yasiyo kuwa na tija kwa walalahoi.
      King of Kings likes this.

    15. #234
      FUSO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th November 2010
      Posts : 3,057
      Rep Power : 1059
      Likes Received
      803
      Likes Given
      341

      Default re: Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

      utapeli mwingine, nani atafika miaka 60? and if they want to do that basi watoe fursa ya mikopo kwa wanachama wao otherwise wizi mtupu.

    16. #235
      asakuta same's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st March 2011
      Posts : 3,198
      Rep Power : 1199
      Likes Received
      882
      Likes Given
      594

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      natamani kuchinja mtu kwa hili
      King of Kings likes this.

    17. #236
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,554
      Rep Power : 5114
      Likes Received
      2603
      Likes Given
      2288

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      Ndio madhara ya vijana wa kitanzania kupelekeshwa na mtukio. Wakati mswada huu unajadiliwa watu waliconcentrate kufuatilia vitimbi vya mijadala ya mswada wa katiba. Kumbe Bunge kila linapokaa kuna kitu cha msingi cha kufuatilia, sio mpaka mbunge anapotolewa nje na spika. Sasa imeshakuwa sheria. Hata hivyo, its not too late, marekebisho yanaweza kufanyika.
      Kwa Tanzania kumwambia mtu angoje mpaka miaka 60 wakati life expectancy ya watu wengi wa sasa ni miaka 45, ni kudhulumu tu wafanyakazi.
      King of Kings likes this.
      "To greed, all nature is insufficient"

    18. #237
      che-guavara's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th July 2011
      Posts : 59
      Rep Power : 414
      Likes Received
      17
      Likes Given
      2

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      hapa ssra ilitakiwa kuzuia serikali kukopa kutoka kwenye mifuko na mafisadi wasikope huko, kuliko kulizunguka tatizo kwa kuondoa mafao ya kujitoa, ikumbukwe pamoja na sheria za pension, bado kwa upande wa haki za binadam pesa hizo zimetafutwa na kuwekwa na wafanyakazi kutoka kwenye jasho lao, hivyo wanauhuru wa kuzitumia.

    19. #238
      wikolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th October 2010
      Posts : 490
      Rep Power : 538
      Likes Received
      145
      Likes Given
      72

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      Quote By majany View Post
      eh..eh..eh...hili ni bomu la B52.....mbona wanazilia mingo hela za wanyonge kiasi hiki??
      Unaposikia akina mzee Mwanakijiji wanasema kuna mifumo ya kifisadi nchini mwetu inatuongoza hii ndo mifano yake mkuu. Mwisho wa siku watazikopa wao kufanyia biashara zao na kuendelea kuneemeka na familia zao na watajenga daraja la kigamboni kwa ajili ya mji mpya! Hebu niambie, una mtoto/watoto wanasoma na ghafla unapoteza kazi yako inayokuingizia kipato, una miaka labda 35 na kwa maana hiyo huwezi kuchukua vijisenti vyako na umeshindwa kupata ajira mpya. Hawa watoto wataishia kufukuzwa shule na familia inaweza kukosa hata mahitaji kwa sababu mishahara tunayoipata ndani ya ajira haitunziki! Sheria za namna hii zinalipeleka wapi taifa hili? Wanataka kila mtu awe mwizi katika sehemu yake ya kazi ili ajilimbikizie kwa ajili ya matumizi baada ya ajira? Nashindwa kuwaelewa kabisa!

    20. #239
      che-guavara's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th July 2011
      Posts : 59
      Rep Power : 414
      Likes Received
      17
      Likes Given
      2

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      Ukimbuka nyuma kidogo, sheria za pension (wakati huo zikiwa tofauti) zilifanyiwa mabadiliko kwa kupunguza umri wa kustahili pension kutoka 45 hadi 55 na 60 kwa lazima, hii yote kuhakikisha mifuko inakaa na pesa za wachangiaji muda mrefu, hivyo ni mwendelezo tu wa mambo, mwisho itapitishwa sheria ya wananchi kutolipwa pension!!!!!

    21. FJM is offline
      FJM
      #240
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,213
      Rep Power : 2580
      Likes Received
      5344
      Likes Given
      4607

      Default Re: PENSION BENEFIT; URGENT PUBLIC CALL FOR JJ Mnyika, Zitto, HKigwangal

      Quote By mchukiaufisadi View Post
      Irene Isaka katumwa na William Erio wa PPF aliyekuwa boss wake kuwa afute hilo fao maana mfuko wa PPF ungekufa hivi karibuni kama hilo fao la kujitoa lingeendelea.

      PPF hadi sasa hivi inatakiwa kuwa PROVIDENT FUND sio Pension Fund maana imepoteza sifa hiyo kisheria, ni maiti inayotembea. Wamefilisi pesa yote kwa kugawana kila mwaka wakurugenzi. Wanaochangia walio katika ajira za kudumu PPF ni 30% tu wakati wale ambao wanaweza kujitoa wakati wowote ni 70% na kulipwa withdrawal benefit.

      Zitto hana ubavu wa kumwambia chochote DG wa PPF maana amewekwa mfukoni, kila wakati yuko naye eg sabasaba, nanenane etc na kila akija lazima akilimiwe na ktitita. Alionyesha ujasiri kwenye suala la Group Endowment lakini kaishia mfukoni mwa Erio
      Unataka kusema hii sheria imeletwa na PPF? Vipi ulisoma report ya CAG?

      Serikali ndio mkopaji mkubwa kwenye hii mifuko, na kwa jinsi hali ilivyo haiwezekani kuendelea kutumikia vyote, serikali na watu wanaojitoa. Kwa bahati mbaya Tanzania hakuna unemployment benefit ambayo ingetakiwa itoke serikali kuu. Hivyo anayekuwa nje ya ajira kabla ya miaka 55 ana-hang hadi hapo atakapopata kazi nyingine au afikie umri wa kustaafu.

    Page 12 of 26 FirstFirst ... 2101112131422 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Mafao ya NSSF walivyo wazidi kete PPF in their own game
      By friendsofjeykey in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 15
      Last Post: 5th July 2012, 21:40
    2. mafao ya nssf
      By Raia Fulani in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 3
      Last Post: 6th November 2011, 17:20
    3. SHERIA INaSEMAJE JUU YA NSSF,PPF NA MAFAO MENGINE KWA MAHOUSEGIRL NA WALINZI MAJUMBAN
      By AMARIDONG in forum Jukwaa la Sheria (The Law Forum)
      Replies: 1
      Last Post: 17th January 2011, 09:12
    4. Mama azimia akifuatilia mafao yake NSSF Kinondoni Regional office
      By Mchekechoni in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 2
      Last Post: 14th January 2011, 16:20
    5. Replies: 7
      Last Post: 3rd February 2009, 14:43

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...