Ndugu wana JF,
Ninajua kuna maswala mengi ambayo yako mbele yetu kwa ajili ya kuyajadili na kutafutia ufumbuzi. Lakini nimesikitishwa sana na list ambayo nimeona kwenye website ya wizara ya afya inayoonyoshe majina ya postgraduate students ambao watakuwa sponsored na wizara ya afya. List yenyewe ni hii hapa http://www.moh.go.tz/POSTGRADUATE-TO-BE-SPONSORED.pdf. Kilichonifanya niweke thread hii hapa ni kuwa Wizara imeamua kusomesha mtoto mmoja wa mkubwa UK ambaye kwa jina anajulikana SALAMA KIKWETE. Cha kusikitisha zaidi ukiangalia hitimisho la list hii kuna usemi huu: THOSE CANDIDATES WHO APPLIED FOR SPONSORSHIP FROM THE MINISTRY OF HEALTH AND SOCIAL WELFARE AND DO NOT APPEAR IN THIS LIST SHOULD CONSIDER THEMSELVES UNSUCCESSFUL .
Je, ni wanafunzi wangapi zaidi wangesomeshwa hapa bongo kwa pesa hii itakayoyumika kusomesha huyu mtoto mmoja wa kigogo?
Je, ni wanafunzi wangapi walipewa opportunity ku-compete na huyu mtoto wa kigogo kwa hii nafasi ya kusoma UK?
Je, hatuna pediatric dentistry educators hapa bongo?
Kama uliapply for sponsorship ukakosa na upo humu jamvini ni vizuri ukatujulisha ili tupate a true picture ya madakitari ambao hawakuweza kujiunga postgraduate kwa kukosa sponsor.
Pasco tafadhali ongea vitu unavyovifahamu. Gharama atakayolipiwa salma Uk ingetosha kusomesha specialists wengine 7 tanzania ambapo kozi anayoenda kusomea inatolewa pia Muhimbili na ninafahamu watu wanaosoma kozi hiyo Muhimbili (paediatrics dentistry).
Kama ni kusoma nje angejipeleka kwa private sponsorship ili pesa nyingine zitumike kugharamia watanzania wenye uhitaji. Nasisitiza angeweza kusoma Tanzania kwa gharama nafuu. Kama hujui wizara ndio wanaoamua nani anapata sponsorship na nani hapati, tena kwa vigezo wanavyojua wao.
Nimesikitishwa sana na mtoto huyu kulipiwa na wizara nje. Tunahitaji madaktari bingwa wengi, tungetumia kasungura ketu kadogo kupata specialists wengi.
Kwa sasa tuna tatizo kubwa sana la vifo vya akina mama na watoto, tunahitaji madaktari bingwa wengi kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama hawa. wanafunzi wa masters katika fani ya udaktari bingwa wa watoto waliodahiliwa na chuo kikuu Muhimbili mwaka huu wa masomo walikuwa 17, wizara imetoa udhamini kwa wanafunzi sita tu, 11 wamekosa udhamini, kwa hiyo watu hao hawawezi kuwa madaktari bingwa na akina mama wataendelea kufa. Hapo hapo mtu mmoja anaenda kusomeshwa UK kwa gharama kubwa kozi ambayo inapatikana hapa nchini na ambayo nadhani sio priority ukilinganisha na hao walonyimwa mikopo. Kma kweli ni mzalendo angesoma hapa hapa ili pesa nyingine zitumike kusomesha wenzake.
Naomba nieleweke sina tatizo la yeye kupata udhamini, tatizo langu ni yeye kwenda kusomeshwa UK na wengine wakakosa kabisa udhamini. Baba mwenye watoto wawili kumlipia mtoto mmoja UK na akashindwa kumlipia mwingine kabisha wakati angeweza kuwalipia wote hapa hapa huo ni ujuha. She might be capable lakini upendeleo umetumika.
Well said !!!!!
Kama bado hajaelewa atakuwa anafanya makusudi
Hayo ndio madhara ya mzazi kuwa omba omba, kwa status aliyonayo JK ilitakiwa asiwe hata na wazo la kumtuma mwanaye aombe scholarship serikalini na kumuweka katika mazingira ya kucompete na maskini. Ni wazo zuri kwa mwanaye kusoma sehemu nzuri na mimi nampongeza huyo binti kwani anaelekea anajituma sana. Ila kuchota hela za walipa kodi kusomesha watoto wa matajiri inavuruga kabisa mpango wa elimu bora kwa wote. Hapa nakubaliana kabisa na ile hoja ya wikilieaks kuwa jamaa alinunuliwa suti na muarabu, ndio maana yeye haoni gharama ya vitu vya bure, ndio maana anahangaika dunia nzima kutafuta misaada kwa kuwa haamini katika kujitegemea. Hawezi kujitegemea kusomesha mtoto ulaya ingawa hela anazo akina Miraj wanavutia bange tu.
naona MoH wana mpango wa kumfanya huyu binti achukiwe na umma.huyu binti ni mpole na hapendi kujionyesha kama yeye ni mtoto wa rais ila kwa unafiki wa watu wa wizarani wameona watoe sponsorship.labda tujiulize ni watoto wangapi leo hii hufa kutokana na matatizo ya meno hapa nchini?halafu tujiulize tena nini sababu za vifo vya mama na mtoto?jamani is paediatric dentistry a public health priority?mimi naona tunahitaji obstetricians,neonatologists,p aediatric cardiologists,paediatricians before we think of paediatric dentists!sio kwamba hawahitajiki lakini tunaweza kuwahitaji baadae mara baada ya kuhakikisha usalama wa mama mjamzito na vitoto vichanga.
MoH tumieni takwimu kufanya maamuzi na sio kuendekeza unafiki,jk ana uwezo wa kumsomesha salama na haitaji msaada wenu.
wanajamvi salama ni mfano mmoja wa madudu yanayofanywa na wizara kuhusiana na sponsorship wako wengi ambao hawajatumia surnames zao ili kukwepa lawama.
angalia list hii ya waliopata udahili MUHAS na linganisha na ile ya wizara utaona ni watanzania wangapi wamekosa udhamini, na pia utaona waliochaguliwa kusomea kozi hiyo hapa Tanzania ambayo mtoto wa JK anakwenda kusomeshwa UK kwa kodi zetu na kasungura kadogo.
jamani muda mwingine tusiwe tunalalamika sana, hawa kwanza wengi ni waajiriwa chini ya hii wizara, halafu kama watu hawana admision za huko UK basi wawape tu scholarship? tuwe tunajishughulisha jamani , mbona yupo mmoja amepata toronto , canada hujamwongelea? Hata mimi mara ya kwanza nilikuwa na mentality kama yako kuwa aaaah ni watoto wa vigogo tu wanapata , siyo kweli niliwahi kujaribu na mimi nikapata tena UK. Tatizo ni kupata admision UK ndiyo tatizo , by the way masters yenyewe hapa UK ni mwaka mmoja tu.
Wengi ya hawa wanafunzi wanafamilia tayari hivyo muda mwingine kwenda mbali sana inawawia vigumu.
Kwanza assumption iwe kwamba huyo Salma ni mtoto wa Jakaya na sio ndugu mwengine asiye na uwezo.
Kisha tujue tu kuna vitu viwili tusivichanganye hapa!!
Inawezekana ye ni muajiriwa wa MOH hivyo anaenda kuongeza ujuzi kwenye taaluma yake (labda hapa hakuna chuo cha huo ujuzi), hapo mbona sawa tu jamani.
Kinyume chake ni MOH wametoa scholarship (financial aid) kwa wanaotaka kwenda kusomea mambo ya afya.
Anaesaidiwa kifedha anatakiwa kweli anahitaji huo msaada, labda kwao hawana uwezo. Kama ni kwa kundi hili la pili ni wazi hakustahili.
Pasco tafadhali ongea vitu unavyovifahamu. Gharama atakayolipiwa salma Uk ingetosha kusomesha specialists wengine 7 tanzania ambapo kozi anayoenda kusomea inatolewa pia Muhimbili na ninafahamu watu wanaosoma kozi hiyo Muhimbili (paediatrics dentistry).
Mkuu tafadhali hebu watake radhi wanabodi.
Una uhakika hiyo kozi ya pediatric dentistry inatolewa Muhimbili sasa hivi au? Kwa wataalam gani walioko?
Halafu inaonekana unatatizo la uelewa jinsi magonjwa ya sehemu moja yanavyoweza kuathiri sehemu nyingine na baadae kwenye ukusanyaji wa data athari zikaonekana ni za kule sehemu ya mwisho. Je unaweza kuwaeleza wanabodi dental carries zispotibiwa vizuri badae complications zake zinaweza kuleta nini kinachoua sana watoto wetu?
Kwenye taaluma tuweke pembeni ushabiki wa siasa ndugu zangu.
Pasco tafadhali ongea vitu unavyovifahamu. Gharama atakayolipiwa salma Uk ingetosha kusomesha specialists wengine 7 tanzania ambapo kozi anayoenda kusomea inatolewa pia Muhimbili na ninafahamu watu wanaosoma kozi hiyo Muhimbili (paediatrics dentistry).
Kama ni kusoma nje angejipeleka kwa private sponsorship ili pesa nyingine zitumike kugharamia watanzania wenye uhitaji. Nasisitiza angeweza kusoma Tanzania kwa gharama nafuu. Kama hujui wizara ndio wanaoamua nani
anapata sponsorship na nani hapati, tena kwa vigezo wanavyojua wao.
Nimesikitishwa sana na mtoto huyu kulipiwa na wizara nje. Tunahitaji madaktari bingwa wengi, tungetumia kasungura ketu kadogo kupata specialists wengi.
Kwa sasa tuna tatizo kubwa sana la vifo vya akina mama na watoto, tunahitaji madaktari bingwa wengi kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama hawa. wanafunzi wa masters katika fani ya udaktari bingwa wa watoto waliodahiliwa na chuo kikuu Muhimbili mwaka huu wa masomo walikuwa 17, wizara imetoa udhamini kwa wanafunzi sita tu, 11
wamekosa udhamini, kwa hiyo watu hao hawawezi kuwa madaktari bingwa na akina mama wataendelea kufa. Hapo hapo mtu mmoja anaenda kusomeshwa UK kwa gharama kubwa kozi ambayo inapatikana hapa nchini na ambayo nadhani sio priority ukilinganisha na hao walonyimwa mikopo. Kma kweli ni mzalendo angesoma hapa hapa ili pesa nyingine zitumike kusomeshawenzake
Naomba nieleweke sina tatizo la yeye kupata udhamini, tatizo langu ni yeye kwenda kusomeshwa UK na winging
wakakosa kabisa udhamini. Baba mwenye watoto wawili kumlipia mtoto mmoja UK na akashindwa kumlipia mwingine kabisha
wakati angeweza kuwalipia wote hapa hapa huo ni ujuha. She might be capable lakini upendeleo umetumika.
A number of Profesionals have over a period of time been educated in UK and elsewhere abroad under the sponsorship of ministry of health. Though you are trying to argue on cost comparison, importance of exposing professional in an advanced environment can not be overstated. Though it is a privilege to be sponsored to study abroad you should understand that it is for Tanzanians with required qualifications and SALAMA KIKWETE MATE THOSE QUALIFICATIONS and for that we should congratulate her. Specialization journey is challenging and it is very good that she has decided to go for it. Tanzanian children will benefit out of this tour of duty. All the best Dr Salama Kikwete.
Una uhakika hiyo kozi ya pediatric dentistry inatolewa Muhimbili sasa hivi au? Kwa wataalam gani walioko?
Halafu inaonekana unatatizo la uelewa jinsi magonjwa ya sehemu moja yanavyoweza kuathiri sehemu nyingine na baadae kwenye ukusanyaji wa data athari zikaonekana ni za kule sehemu ya mwisho. Je unaweza kuwaeleza wanabodi dental carries zispotibiwa vizuri badae complications zake zinaweza kuleta nini kinachoua sana watoto wetu?
Kwenye taaluma tuweke pembeni ushabiki wa siasa ndugu zangu.
Angalia link hapa chini utaona waliochaguliwa kusomea hiyo kozi Muhimbili. naweza kukupa hata namba ya lecturer wa hiyo kozi ukamuuliza. Hatumkatazi kupata udhamini lakini wasikose wasio na uwezo kwa yeye kwenda kusoma nje.
Hivi dental carries inaweza ikawa priority over maternal health? Wewe muelewa hebu tupe complications za dental carries ambazo athari zake ni kubwa kuliko maternal deaths.
Hebu nisaidie wewe, kwa ninavyofahamu mimi, pamoja na mambo mengine hususani suala la uwezo wa mzazi...lingine la msingi ni academic standing; na more often than not, hii inakuwa ndiyo priority ya kwanza na zingine zinafuatia. sasa assume umebaki na majina mawili, salama kikwete na salama kintukute....salama kikwete ana second upper na kintukute ana second lower; je, scholarship ungempa nani hususani ukizingatia scholarship sio favor?!
kuna kitu wanaita priority... je tunaweza kumlipiammoja milioni mia kwa mwaka wakati tuneweka eatu zaidi ya 12 kwa mph? akirudi ana vifaa vya kazi vya kutosha?
alwatan tunaomba utuelezee dental carries zisipotibiwa zinaleta complication gani na kwa proportion ipi ya watoto wa kitanzania.je dental surgions wa kawaida wanashindwa kutibu hili tatizo.hivi unategemea salama atazunguka nchi nzima kutibu meno ya watoto?mikoa na wilaya hazijajitosheleza kuwa na dental surgions kwa nini hatuwekezi huku kwanza?
A number of Profesionals have over a period of time been educated in UK and elsewhere abroad under the sponsorship of ministry of health. Though you are trying to argue on cost comparison, importance of exposing professional in an advanced environment can not be overstated. Though it is a privilege to be sponsored to study abroad you should understand that it is for Tanzanians with required qualification and SALAMA KIKWETE MATE THOSE QUALIFICATION and for that we should congratulate her. Specialization journey is challenging and it is very good that she has decided to go for it. Tanzanian children will benefit out of this tour of duty. All the best Dr Salama Kikwete.
I would understand if this course is not taught in our local universities. I would also have no problem if all who applied for sponsorship to pursue their carriers in Tanzania would have been given sponsorship. My biggest problem is the distribution of our 'scarse' resources among us. I dont believe that Salma is the only one with the qualifications.
Olecranon, nakuomba usiingie kwenye long list ya 'hate preachers' wa humu jamvini.
Kila Mtanzania kwanza ni Mtanzania ndipo mengine yote yanafuati ni jinsia gani, ni kabila gani, ni familia gani, ameolewa na nani etc. Kuwa mtoto wa rais, hakumuondolei haki yake kama Mtanzania mwingine yoyote.
Bahati nzuri au mbaya, nimetokea kumfahamu huyu binti, Dr. Salama na pia nawafahamu baadhi ya watoto wengine wa JK japo sio wote nane, kwa opinion yangu, kati ya watoto wote wa JK ninaowafahamu mimi, Dr. Salama pekee ndie anaesimama mwenyewe kama Salama bila ile pride ya mtoto wa rais ambayo nduguze wanayo!. She is so humble na down to earth, fortunately kaolewa na kijana mwenye uwezo kumlipia shule popote, lakini huko hakumuondolei right yake ya kupata fellowship kama rai mwingine yoyote. Hata kama unatoka familia ya mamilioneo, kupata fellowship kunakuongezea heshima kwa sababu ili kuipata lazima uishindanie na wengine toka nchi mbalimbali duniani. Wizara sio determinant nani anapata, sponsors ndio determinant, japo recomendation ya wizara pia inanguvu.
Kama huyo dr ana sifa, na ameomba kama Mtanzania mwingine yoyote, sasa ndio anyimwe eti kwa sababu ni mtoto wa rais?.
Wanabodi, tuendelee kumsakama JK kwa maroroso yake, ya chama cheke na serikali yake, au tuwasakame watoto wake wanaofanya wanayoyafanya simply kwa sababu baba ni rais, lakini nawaomba sana tusiisakame familia ya rais kwa mambo yasiyohusika, hiyo scholarship ni issue ya proffesionalism hata kama preferential ime play part lakini she deserves and she is capable!
Please leave her alone!.
Kaka mambo mengine yanasikitisha sana, tunatengeneza ukaburu mwingine. Kwanini tushughulikie na majina badala ya hoja? Tujadili hoja kama hoja jamani, kama kuna ufisadi katika kupata nafasi, tujadili hiyo hoja.
hili ni tatizo dogo sana kwenye kusomesha inaloikabili serikali kwenye sekta ya afya......JK na serikali wametangaza kupandisha hadhi hospital za mikoa kuwa refferal na ili kukidhi vigezo kila hospital inahitaji atleast 7 specialist na kwa survey ndogo sana kwasasa hizi hosptali hazina hata specialist watatu kila mmoja....maajabu sasa ya JK na MOH wamepunguza kusponsor waliopata admission kwa asilimia 65 na saiv wanasponsor kwa asilimia 35 tu.
kwa mm naona hapo kuna tatizo. maneno hayaendani na dhamira ,nia na vitendo.
jamani muda mwingine tusiwe tunalalamika sana, hawa kwanza wengi ni waajiriwa chini ya hii wizara, halafu kama watu hawana admision za huko UK basi wawape tu scholarship? tuwe tunajishughulisha jamani , mbona yupo mmoja amepata toronto , canada hujamwongelea? Hata mimi mara ya kwanza nilikuwa na mentality kama yako kuwa aaaah ni watoto wa vigogo tu wanapata , siyo kweli niliwahi kujaribu na mimi nikapata tena UK. Tatizo ni kupata admision UK ndiyo tatizo , by the way masters yenyewe hapa UK ni mwaka mmoja tu.
nawe muda mwingine uwe unafikiria na kuchunguza kabla ya kuchangia. unahakika paediatric dentist inatolewa kwa mwaka mmoja?
una hakika ndio yeye tu aliyepata admission uk? hoja ilikua why kumfadhili mtoto wa mwenye uwezo wa kusomesha ,tena uk ambapo ni expensive sana,huku watanzania zaidi ya 100 wakikosa sponsor ktk vyuo vya ndani ya tz(waliopata admission ni zaid ya 200 na waliopata sponsor ni only 90).why asingesomeshwa muhimbili ambapo pia digree hiyo inatolewa?
Follow Us Here