| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
|
#1 | |||||||||||
|
||||||||||||
|
Views: 10068
|
||||||||||||
|
#2
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Duh !!! Kuna vipengele kama vile vya Bunge na ushahidi hapa sasa wacha kwanza niwaze niunge ama nikatae vipengele hivyo maana vitattuziba sisi kulonga .
|
|
#3
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mzee Admin,
Heshima yako mkuu, kama hizo sheria zikipitishwa ninakuahidi kuwa nitakuwa wa kwanza kuondoka, forum haitakufa kwa sababu ya mimi kuondoka na baada ya hii message sitarudi tena mpaka nisikie kwanza hatima ya hizi rules, kwani nyingi kati ya hizi rules zinaashiria kuigeuza hii forum kuwa mahakama, Kwa maoni yangu, Wako Mtiifu, Mzee Es! & Es! Last edited by Invisible; 5th March 2007 at 07:18 AM.. |
|
#4
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mimi nnahisi tungemsaidia Mzee Fillga katika kutengeneza hizi sheria kama alivyoomba. Vipengele tunavyoone havifai tuvitolee sababu na tuvirekebishe au kuviondoa. Ambacho tunahisi kiwepo lakini hakipo basi tukipendekeze.
Mzee Admin, nadhani vitu kama 'kuwa na ushahidi' umemaanisha aina ya ushahidi unaoweza kutolewa katika forum kama hizi .. sio documents etc za kutolewa mahakamani .. au sio? Pia kuna wanaokerwa na multiple identities,ambazo mara nyingi hutumiwa vibaya, naona hakuna sheria inayokataza hilo .. are we OK with it? Last edited by Invisible; 5th March 2007 at 07:20 AM.. |
|
#5
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mzee Kulikoni,
Ninakuomba unionyeshe what is ushahidi valid so far katika hii forum to you! |
|
#6
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mzee ES,
Mfano mzuri wa karibuni ni ripoti ya Mzee Mwanakijiji on arms trafficking, ameweka references kadhaa za mahali alikozipata data alizoziweka, I consider that ushahidi valid. But your question made me think again, and I would agree with you kuwa issues nyingi zinaweza kutokuwa na ushahidi wa aina ile. My point is, kama hicho kipengele kinaleta matatizo .. let's re-word it in a way that will allow us kulonga ya ukweli bila woga ... and at the same time, ku-avoid watu kuzusha mambo ambayo hayapo. All we need is some form of rules to refer to when someone is going over board na inabidi kuadabishwa. My opinion. |
|
#7
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
wanajambo, wapenda ukweli na uwazi. Tuwe na lengo moja pia. Tusikubali kuwepo na "hadthi za watu" au matendo ya yatu ambayo si yakweli, yaani tusi entertain uzushi.
Amasivyo hii forum ni nzuri sana, tuwekeane heshima na pia kila kitukinacho wekwa hapa kichambuliwe kama kawaida na bila matusi na kupuziana. Ninge waombeni sana muende Tanzanet na kujifunza kwani pale watu ni so very cultured na debate huwaga zinaelimisha sana. Na hapa ningeomab pawe mahali pia pakuelimishana na mahala pa kutafuta ukweli. Je mnaonaje wenzangu?
__________________
mambo na: Ogmulik |
|
#8
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Binafsi bado naamini ni rules zinazofaa kabisa kuwekwa hapa. Sioni kama mtu kuombwa uthibitisho wa anachokisema ni reference kuwa atuwekee mafaili na vielelezo kadhaa.. tunaweza kusema tu kuwa itatosha kwa mtu kama huyo kutoa source ya nyeti zake au kusema wapi zinaweza kupatikana ili tujue ukweli manake wengine wana mtindo wa kupachika habari humu ndani ambazo ukiziangalia sana ni kama zinalenga character assassination zaidi kuliko ukweli.
Halafu naunga mkono hii habari ya multiple identities inabidi kuwe na kipengele. Pia tuambiwe matusi na kejeli maana yake ni nini manake inawezekana hata utani ukasababisha offence kwa mwingine. Ila naomba tuongozwe zaidi na uchungu wa nchi katika kueleza madukuduku yetu kuliko uchungu wa wivu kwa viongozi au watu wengine. Umejengeka mtindo tanzania wa ajabu sana kwamba kila mwenye mali ni mwizi au mla rushwa badala ya kuwa spirit ya kufanya kazi kwa bidii kufikia wengine walipofika. Yes wapo matajiri wengi walio walafi na wezi wakubwa na wapo viongozi wa serikali ambao kama sheria ingefuatwa basi mahala pao pa kuishi ingekuwa segerea state prison lakini haya hayafanyi kuwa kila tajiri ni mwizi kama ambavyo sio kila ccm ni muiba kura au kila anayetaka haki itendeke humu tunapojadili issues ni mtu wa kutumwa na usalama.. Nadhani Admin ameweka vipengele vizuri sana na kuwaomba watu aidha wachangie au waedit na kumtumia mapendekezo yao. Si busara kuondoka busara ni kuchangia mawazo namna ganio hii forum inaweza kuboreshwa ili kutufikisha katika nchi ya ahadi ya asali na maziwa tanzania. sidhani kwamba vipengele vyote havifai. tukiona mambo ni mazito sana basi tuwekewe kura humu ndani tupige ili kuweza kupata uamuzi wa kidemokrasia zaidi. naomba kutoa hoja. Last edited by Invisible; 5th March 2007 at 07:22 AM.. |
|
#9
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mzee,
Admin, hehsima yako mkuu, hapa ninakiona kilichotokea ni kwamba ile mada uliifunga ki makosa, maana uliruhusu mchango wa huyu mheshimiwa na wapambe wake wakamalizia bila Re-buttal, matokeo yake wakaamini kuwa waliyoyasema ni ukweli, kwa hiyo sasa wanaamini kuwa wana-authority ya ku-dictate how this forum should be run, sasa yes hebu tuwape nafasi wewe na hawa jamaa mtuamulie habari za kweli ni zipi na za barazani ni zipi? Huko tanzanet, niliombwa na marehemu professor kwa muda mrefu akiwa hai niingie huko, sikujali sana maana nilikuwa BCS na huwa sipendi kuwa sehemu nyingi, nataka moja tu, kwa hiyo sikuenda huko, na tunaambiwa huko habari zetu za hapa haziwezi kusimama, sasa tunajiuliza ni kwa nini mtu babu kubwa kama huyo marehemu Professor aliniomba nije huko huku akijua kuwa habari zetu ni za barazani na hazitasimama huko? Na hawa wenzetu kwa nini wasiende huko badala yake wanataka kutulazimisha hapa tuwe kama huko ambako kuingia ni kwa fee na uanachama, hapa tunapapenda kwa sababu ni free at its best, nendeni huko sisi tuko hapa hapa mlipotukuta, na mtatuacha hapa hapa tunakata issues kiroho mbaya! Last edited by Invisible; 5th March 2007 at 07:23 AM.. |
|
#10
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
naelewa.. kama imekukera wewe, itakera na wengine pia. lakini sasa nifanyaje ili tuweze tukaipitisha hizi rules. kwasababu bado, sio official. nahitaji mawazo yenu nyie, mniambia nini chakutoa.. mstari gani wa kurekebishwa. hii ndio malengo yangu ndio mana nikaiweka hapa tuijadili.
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 09:43 PM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||