Nimepata habari hivi punde imekuja ikiwa imevunjia vunjika gazeti la Mwanahalisi limefungiwa miezi 3 stay tuned...
Nimepata habari hivi punde imekuja ikiwa imevunjia vunjika gazeti la Mwanahalisi limefungiwa miezi 3 stay tuned...
Last edited by PainKiller; 13th October 2008 at 23:12. Reason: prefix removed
I hope na Rai nalo litafungiwa
I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.
Nguvu ya mafisadi Hiyo,hayo ni matokeo ya vikao Vya KALOKIRO Ambavyo vilifanyika huko Dodoma na Morogoro na kutoa maelekezo ya kulishughulikia gazeti la mwanahalisi na mengine kama KULIKONI NA THISDAY.nadhani mnakumbuka minutes za KALOKIRO zililetwa humu jamvini hapo nyuma na wengine waliziponda lakini ukweli unaanza kuonekana
Hivi hiyo sheria kandamizi ya vyombo vya habari itabadilika lini? Na uhuru wa kutoa maoni tunao usemea ni u zecomedy tu chini ya sheria kandamizi namna hii!
Bado naamini kwa nguvu ya pamoja linaweza funguliwa, labda mafisadi wa wagawe wahariri wasiwe kitu kimoja!
radio wani taarifa ya habari ya saa saba kamili mchana... serikali imelifungia mwanahalisi kwa miezi mitatu kutokana na kuandika habari ya uchochezi. Eti wamemdhalilisha rais. Aliyetangaza hivyo ni waziri wa habari na utamaduni G. Mkuchika. taarifa ya mkuchika imesema habari hizo ni za uchochezi ambazo zimeleta mtafaruku mkubwa ndani ya serikali na chama na kati ya rais na mtoto wake Ridhwani pamoja na familia yake.
Yeah,,, its true,,, limefungiwa miezi mitatu kwa kuandika habari za kumkashifu rais wa tz. Eti habari iliyoandikwa na mwanahalisi inamgombanisha na mwanae Rizwani. Haya tuone. Tujulishane yanayojiri
I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.
naamini kuwa hali halisi Publishers walisajili gazeti zaidi ya moja.
I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.
Dah...
Kwa hiyo safari ya kukandamiza vyombo vya habari bado ni ndefu eti eeh... Hopefully Kubenea alikumbuka kuwa na 'Emergency Exit' mambo kama haya yakitokea. Demokrasia Tanzania inakuwa ama maana naona uhuru wa vyombo vya habari umefinywa sana.
Aluta Continua.
Change will not come if we wait for some other person or some other time. We are the ones we've been waiting for. We are the change that we seek.
nadhani suala siyo tu MWANAHALISI kufungiwa itizamwe pia na sheria za habari zinazoongoza vyombo vya habari yakiwepo magazeti radio na runinga kwani hapa linaweza kuonekana gazeti hili limefungiwa kwa kutumia sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 1976 kama sikosei!!!
tujiulize yafuatayo
1. Je sheria husika inaendana na mazingira halisia tuliopo leo na kama haiendeni na mazingira ya kisiasa wala kiuchumi tulio nayo leo kuna mikakati ipi mathubuti ya kuhakikisha sehria hizi zinaondolewa ama kufanyiwa marekebisho!!!!!!
2. Je ni kweli kilichoandikwa na Mwanahalisi kama Waziri wa habari alivyoeleza kilikuwa ni kuchochea ugomvi!!! je wananchi wa mbeya nao waliagizwa ama kushawishiwa na mwanahalisi ???
3. Je gazeti la uhuru liloandika mgombea wa CCM kashinda kule mara halisababishi ama halipelekei wananchi kuwa na mtafaruku ama ukiandika linalomhusu Raisi ndo tatizo kwani yeye ndiyo anayepaswa kutetewa na kupatiwa haki kuliko watanzania takribani milioni 38 na ushehe? Je Raisi ni zaidi ya wananchi wengine katika suala la uraia ama ana share equal right!!!!!
4. Je Mwanahalisi ndilo gazeti pekee liandikalo uongo !!!
hiyo habari ni ya lini na je iko online kwenye tovuti yao??? iwekwe hiyo habari hapa ili tuchambue
Inasikitisha sana!
yaani hata baada ya kutuondoa jicho letu la kwanza sasa naona serikali inataka kutuondolea jicho letu la pili. hivi wanadhani kwa kulifungia gazeti ndio wananchi tutabadili mawazo yetu dhidi ya serikali hii inayoongozwa na Chama Cha Mafisadi(CCM)? hata kidogo, kamwe hawawezi kubadilisha ukweli kwa kutufumba macho kwani ukweli huu umekaa kwenye akili na sio machoni tu.
Saed Kubenea pole sana shujaa wetu, naamini Mungu yupo pamoja nawe na watanzania wote tupo pamoja nawe katika jitihada zako za kuitafuta ile nchi ya ahadi yenye mito ya asali na maziwa. ktk kipindi hiki jua wananchi wenye busara wote tupo nyuma yako na kuikubali kazi unayofanya japo serikali inataka uonekane sivyo, tunakuamini sana endelea na kazi mbele kwa mbele.
Muda huu nadhani utautumia vyema kuzipata habari zote za hao mafisadi na kufanya jitihada za kusajili gazeti lingine. na pindi mwanahalisi litakapoanz kutoka uwepo na uwezekano litoke hata mara mbili kwa wiki kwani ili hao mafisadi wa nchi hii wasipate nafasi ya kupumua.
Haki hainyang'anywi!
JK Ni Rais wa watu mil.5 kwenye nchi ya watu mil.50 (By vote)
''UBAYA UTASHAMIRI NA KUPATA NGUVU ZAIDI IWAPO WATU WEMA WAMEAMUA KUKAA KIMYA '', Edmond Burke
" What we believe, inevitably affects how we live," Howard Marshall
I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.
Hiyo ni njia moja ya kuwatisha waandishi na vyombo vyao vya habari lakini kama watu watakuwa kitu kimoja hakuna kitakachoharibika ingawa baadhi ya waandishi hutumika katika mambo kadhaa ya kiserikali.
hiyo taarifa hata TBC1 kwenye news ya saa saba nimeisikia wakisema limefungwa mwanahalisi kutokana na uchochezi dhidi ya mheshimiwa.
umoja ni nguvu kwa wanaotaka huo umoja maana wengine huwa hawataki umoja.
I love this country!
A positive thinker!
Follow Us Here