| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
|
#1 | |||||||||||
|
||||||||||||
|
Views: 291
|
||||||||||||
|
#2
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Bubu,
Kila mwezi mapato ya Serikali kupitia kodi yanaongezeka na ni mara chache sana kushuka. Kitu cha kujiuliza, kwa mapatao kuongezeka WaTz tumepata nafuu gani? Mbona kila siku ikipita heri ya jana? Mapato yakiongezeka, mafisadi nao matumbo yao yanaongezeka.
__________________
"Then you will know the truth, and the truth will set you free; I am the way, the truth and the life." Jn 8:32; 14:6 |
|
#3
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Kweli kabisa, ongezeko la makusanyomya kodi yanatakwia yaonekane kupitia mabadiliko kwa maisha ya wananchi, si rekodi za TRA
|
|
#4
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Kiwira coal mine wanalipa tax kupitia Ileje na sio Kyela kwanini?
Kwa ufahamu wangu Kiwira coal mine iko Kyela na sio Ileje. Kama hawalipi kodi si wanyang'anywe leseni? Wanalipa hata akina mama Ntilie ndio iwe kampuni ya mafisadi? |
|
#5
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Halafu hawa TRA huwa wananiudhi mimi.
Sijui labda ni umbumbu wangu au vipi,,,,, ila wanakera, wanakera sana tu! AAgh Labda tujadili haya:- Mtanzania anayefungua kibanda tu cha kuuza tumaandazi twa watoto,,, kabla hajafungua lazima alipe kodi! jamani kodi hata sijaua biashara italipa ama vipi? Biashara ya mkopo pale pride? Lipa kodi kwanza,,, tax clearance!!! ptuuuuu,,, inanuka hiyo. Aibu hawaoni hawa jamaa hata kidogo,,,, aagh Upande wa pili anakuja jamaa na mahela yake,,,, nywele zimekaa upande,, sijui mzungu,,, sijui mhindi,,,,anapewa TAX HOLIDAY YA MIAKA MITANO!!!!! five years my friend!!!! UUUUUwi. Eeee habari ndo hiyo bwana. wakimaliza 5years wanabadilisha jina kwenda kwa mtoto, mke au hata mjomba au jina lake la utotoni,,, makampuni yote tunayajua na hawa TRA wanaangalia tu! aah! Hapa ni sawa na mtoto anataka kwenda shule unamwambia kabla hajaenda shule akupe kitu kidogo kwanza. Kwa nini TRA WASIWAPE WAZAWA WA TANZANIA HATA MWAKA TU WATU WASTUDY BIASHARA KAMA INAGENERATE THEN WALIPE KODI BAADA YA MWAKA TU. Haya kuna biashara niliona sehemu fulani hapa Tanzania,,,,TRA wanakamata wamama wanaoenda kununua vibidhaa border ambavyo havina hata faida ya shs 10,000. at the same time kuna mfanyabiashara anapitisha container la 40 feet bila kulipia ushuru,,,, oooh my God! na wanajua,, wanamwona ila huyu aliyeenda kununua vijisabuni ili tu ajepushe na balaa anakamatwa na kupelekwa TRA eti wamekamata magendo! Huyu dada yako amesema umalaya basi atafuta tu mia twa mafuta ya taa unamkamata na mara ingine wanalazimishwa hongo ya ngono! Kweli? Halafu mnasema tutafika! Kwa namna hiii? TRA wamelaaniawa na hata maandiko yaliwalaani watoza ushuru!!!!!!!!!!! Sisemi tusilipe kodi, la hasha, tuwe utaratibu wa kumsaidia Mtanzania ajikomboe na shuruba na ukata unaotukabili. Narudia sijui kama ni umbumbu wangu ama vipi ,,,,, ila INAKERA MNO!!!!! |
|
#6
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Hivyo basi pamoja na ongezeko kubwa la mapato ya TRA Watanzania hawajanufaika na lolote bado hospitali zetu hazina dawa, hazina vitanda hazina vifaa muhimu, bado mashule yetu hayana madarasa yenye hadhi hayana madawati na vifaa vingine muhimu mashuleni, bado wataalamu wetu mbali mbali wanalipwa ujira mdogo ambao hauendani na hali halisi ya maisha pamoja na kulalamika miaka nenda miaka rudi, bado usafiri wetu wa barabara, reli na hata majini ni wa kusikitisha na kutishia afya na maisha ya Watanzania. Kwa kifupi maongezeko hayo makubwa hayakuleta ahueni yoyote kwa Watanzania.
__________________
~*~Life is Good~*~ |
|
#7
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
JK amshukia mwekezaji wa mgodi Kiwira
2008-10-13 10:24:56 Na Thobias Mwanakatwe, Kyela Rais Jakaya Kikwete, amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mashimba Hussein Mashimba, kumbana mwekezaji wa mgodi wa makaa ya mawe Kiwira, ili ahakikishe anawalipa afanyakazi wa mgodi huo mishahara ya miezi miwili wanayodai. Rais Kikwete alitoa agizo hilo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela kuomba msaada wa serikali wa kumbana mwekezaji wa mgodi huo ambao pia Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amekuwa akihusishwa kuwa mmoja wa wamiliki wake, ili aweze kuwalipa mishahara wafanyakazi ambao hivi sasa wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha. Mwingine anayehusishwa na mgodi huo ni aliyekuwa waziri katika serikali ya Mkapa, Daniel Yona. Rais Kikwete alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa, suala hilo lipo chini ya uwezo wake na kumtaka afanye kila jitihada za kumbana mwekezaji wa mgodi huo ambaye ni kampuni ya Kiwira Tanpower aweze kuwalipa wafanyakazi mishahara iliyobaki. ``Kama umeweza kumbana mwekezaji akalipa mishahara ya miezi mitatu, sasa unashindwaje kumbana tena amalizie mishahara ya miezi miwili iliyobaki. Hakikisha unambana tena awalipe, hili lipo chini ya uwezo wako,`` Rais Kikwete alisisitiza. Inadaiwa kwamba, mbali na wafanyakazi kutolipwa mishahara yao, kumekuwepo na hujuma ambazo zimekuwa zikifanyika kwa kuuza kinyemela mali za mgodi huo. Wafanyakazi waliotoa maombi hayo ni wale waliopunguzwa kazi na na serikali mwaka 2005, ambao wanaidai serikali zaidi ya Shilingi bilioni 47. Wafanyakazi hao walidai kusikitishwa na hali hiyo, kwani hata kamati ya rais aliyoiunda kuchunguza sekta ya madini na mikataba, chini ya uenyekiti wa Jaji Mark Bomani, ilipita katika mgodi huo na kupokea kilio cha wafanyakazi hao, lakini bado hawajalipwa fedha zao. Wafanyakazi hao wanaililia serikali kwamba hawajalipwa mafao na mishahara yao ya miezi kadhaa waliyokuwa wakidai tangu mgodi huo ulipokuwa chini ya serikali na kuwafanya washindwe kuondoka kwenye nyumba za mmiliki mpya aliyekabidhiwa mgodi huo. ``Baada ya suala letu kushindikana kwa muda mrefu, sasa tunataka kutumia ujio wa rais kuwasilisha kilio chetu kwake kwani ndiye pekee tunadhani anaweza kutusaidia,``alisema mmoja wa wafanyakazi hao zaidi ya 500. Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodini (TAMICO), Thomas Cheyo, alisema hali za wafanyakazi hao waliopunguzwa kazi tangu mwaka 2005 ni mbaya na wengi hawana chakula, hivyo ujio wa Rais Kikwete ni faraja kwao. ``Tumepata taarifa kuwa Rais Kikwete anakuja Mbeya, tunaomba atembelee hapa mgodini ili tuweze kumfikishia kilio chetu,`` alisema. SOURCE: Nipashe
__________________
~*~Life is Good~*~ |
|
#8
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Hiyo article hapo juu inaashiria umiliki wa Kiwira hautarudishwa kwa Watanzania pamoja na fisadi Mkapa kuukupua mgodi huo alipokuwa Rais na kuamua bei yake ni shilingi milioni 700 pamoja na kuwa una thamani ya shilingi bilioni 4, mapaka sasa amelipa shilingi 70 millioni tu, kisha kuwashinikiza wazungu wa NET GROUP aliowaleta kuiendesha TANESCO kusaini mkataba wa shilingi bilioni 326 ambapo fisadi Mkapa analipwa shilingi 146 milliono kwa siku na TANESCO.
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 10:33 PM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||