Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

    Report Post
    Page 4 of 14 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 261
    1. #1
      nice 2's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th August 2011
      Posts : 699
      Rep Power : 943
      Likes Received
      503
      Likes Given
      285

      Default Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

      Wana JF,
      Hii ni email kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe. Nimeona ni vyema niiweke hapa ili tuweze kujua kwapamoja hali yake inavyoendelea.
      Nawasilisha,
      Nice 2


      Ndugu zangu,

      Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha muda huu kuwa na nguvu za kukaa katika kiti na kuweza kuandika haya machache kwenu. Nawashukuru sana Wanamabadiliko kwa salaam zenu nyingi za pole mara mliposikia ninaumwa na kulazwa hospitalini. Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika).

      Mwanzo

      Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa siku ya Ijumaa tarehe 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa Mamlaka za Maji nchini.

      Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za Jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya kuinigilia ziara za Jimboni ikiwemo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.

      Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.

      Siku ya Jumapili saa kumi na moja jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla. Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba Dereva wa Mhe. Mhonga anifuate ili anisadie kunifikisha nyumbani.

      Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.

      Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).

      Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku. Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia Hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.

      Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.

      Hali kubadilika

      Siku ya Jumanne niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini sio vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi.

      Hata hivyo ilipofika saa sita kamili nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana!

      Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale. Joto lilifika degree 39.8 Hivyo wakanipa dawa za kupoza homa na maumivu ya kichwa kwa drips na sindano kadhaa.

      Siku ya pili hospitalini nikafanya vipimo zaidi ikiwemo ultra sound na vyote kuonekana sina tatizo lolote. Niliendelea kuwepo Hospitali na kwa kweli hali ilikuwa inatia moyo sana kwani nilipata nguvu na hata kuweza kuzungumza, homa ilikuwa imepungua sana.

      Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa 'a trigger' ya homa kali niliyokuwa napata.

      Hali kuwa Mbaya

      Usiku wa siku ya Jumatano Hali ilikuwa mbaya sana. Joto lilipanda tena kufikia 40 na kichwa kuuma zaidi. Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.

      Wageni waliokuwa wamekuja kunijulia hali wakati hali inabadilika ilikuwa ni pamoja na Ndugu Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya POAC, walishauri mara moja nihamishwe Hospitali kupelekwa Muhimbili.

      Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika Chumba wanachokiita Mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mama Blandina Nyoni alikuwepo Hospitalini tayari.

      Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. Full Blood picture pamoja na BS. Vile vile kufuatia malalamiko kuhusu maumivu ya kichwa ikaamuliwa kuwa nifanyiwe CT Scan usiku ule.

      Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana Daktari kijana Dkt. Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale Mini ICU.

      Asubuhi ya siku ya pili nikapata majibu ya tatizo la maumivu ya kichwa. Nimekuwa nasumbuliwa na kichwa kwa miaka zaidi ya Kumi sasa na katika kipindi hicho mara nne nilipoteza fahamu na kuanguka (Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Jijini Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, Mara Pili Mjini Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001 lakini ilikuwa usiku, Mara ya tatu Nikiwa chumbani, Hall II mara baada ya kutoka *Prep, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge (Ndugu Katulanda anakumbuka siku hii kwani yeye ndiye niliyemkamata njiani kunikimbiza Zahanati ya Bunge).

      Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.

      Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya 'dozi' nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza 'dozi' hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya 'surgery' hiyo.

      Sijafa

      Uvumi ulienezwa nimekufa. Kwa kupitia kwenu ndugu zangu Wanamabadiliko, napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya. Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.

      Shukran
      Nawashukuru sana Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Prof, Mwafongo kwa juhudi kubwa walioonyesha katika kunihudumia. Naishukuru Ofisi ya Bunge kwa Kutimiza wajibu wao kwangu kama Mbunge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na watumishi wote wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kwa ufuatiliaji wa karibu wa Afya ya Naibu wake, Wabunge wajumbe wa Kamati ya POAC, Dkt. Alex Kitumo, ndugu, jamaa na marafiki zangu wote.

      Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo.

      Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri

      Ndugu yenu

      Zitto
      Last edited by nice 2; 30th October 2011 at 09:46.


    2. SMU is offline
      SMU
      #61
      SMU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th February 2008
      Location : Mavurunza
      Posts : 4,606
      Rep Power : 3830
      Likes Received
      1350
      Likes Given
      1987

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      'Wadudu' 150!? Linapokuja suala la kupima malaria,hospitali ya aga khan wanalo tatizo.....inawezekana ni mpimaji au vifaa wanavyotumia. Nimeshawahi kusikia malalamiko kutoka kwa watu kadhaa juu ya hosp hii kutokuweza kuona malaria.

    3. #62
      rosemarie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 4,742
      Rep Power : 1372
      Likes Received
      285
      Likes Given
      143

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      mkuu zito pole sana na hiyo safari ndefu ya majaribu'upone haraka tuna kazi ngumu ya kumalizia tulioanza kuyafanya

    4. #63
      George Kahangwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2007
      Location : Dar es Salaam, Tanzania
      Posts : 517
      Rep Power : 699
      Likes Received
      108
      Likes Given
      41

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      HOH. ZITTO ZUBERI KABWE,
      TANZANIA LOVES YOU (ref. prayers from around the world). SIMPLY SMILE AND REST ASSURED YOU WILL GET WELL VERY SOON.
      GLK.

    5. #64
      MTAZAMO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th February 2011
      Posts : 4,448
      Rep Power : 2250
      Likes Received
      1903
      Likes Given
      2828

      Default

      Quote By Mwita25 View Post
      Kuna hospitali nyingine hata kama huna Malaria lazima watakuambia una vijidudu ili wakutibu wapate chao.
      Ni kweli mkuu ndio maana hata mimi nilikuwa napuuza lakini kwa shuhuda hizi,siwezi kuzipuuza!

    6. #65
      dotto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2010
      Posts : 1,475
      Rep Power : 738
      Likes Received
      169
      Likes Given
      30

      Default

      Quote By Kahangwa View Post
      HOH. ZITTO ZUBERI KABWE,
      TANZANIA LOVES YOU (ref. prayers from around the world). SIMPLY SMILE AND REST ASSURED YOU WILL GET WELL VERY SOON.
      GLK.
      Agakhan navyojua huwa ni hoteli ya dawa


    7. #66
      Uyole12's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd October 2011
      Posts : 102
      Rep Power : 407
      Likes Received
      32
      Likes Given
      5

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Nilikuwa nimfunga ngoja leo nifungue kwa hii habari. Alievumisha kuwa umekufa alaaniwe.

    8. #67
      mams's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th July 2009
      Posts : 604
      Rep Power : 625
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Bado hujamaliza kazi aliyokupangia Mwenyezi Mungu kwa Watanzania. Hakika Mungu tunayemtumai atakuponya ili uje kuendelea na ratiba yako.

    9. #68
      Buto's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd September 2011
      Posts : 247
      Rep Power : 440
      Likes Received
      28
      Likes Given
      16

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Pole kamanda Mungu akubariki urudi salama

    10. #69
      Dogo Tundu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Posts : 101
      Rep Power : 533
      Likes Received
      6
      Likes Given
      9

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Pole sana kaka, huo ugonjwa ulioutaja yaan sinusitis ni kweli huambatana na homa kali sana including maumivu makali ya kichwa, mi hii kitu ilinitesa zaidi ya miaka 10, nilikuwa na malaria isiyoisha, maumivu makali ya kichwa na homa kali. nilienda Indraprastha Apollo hospital India wakafanya sugery sasa niko poa, sipati homa wala malaria yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Naamini utarudi ukiwa salama na wa afya njema kabisa wakiishafanya surgery kwa kutumia kifaa maalumu kiitwacho functional endoscopic sinus surgery-FESS, India wako makini na matibabu na zaidi ya yote wako cheep gharama zao.
      Watanzania wenzangu
      huu ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine, mpambanaji wenzetu atarudi salama salimini, ni ugonjwa unaotibika kwa kufanya upasuaji na mgojwa hupona na kurudi hali yake ya kawaida. Tumwombee upasuaji ufanyike salama.
      MAKAH likes this.

    11. #70
      marejesho's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Location : MULA
      Posts : 3,647
      Rep Power : 25275
      Likes Received
      1749
      Likes Given
      1149

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Kwa kweli sikuwa na imani kabisa kwani uvumi ulichukua kasi kubwa...Nashukuru Mh Zitto umeamua kutuhakikishia usalama wako so far..Ukifanikiwa kupitia hii post, soma Hebrews 13:6...Bwana Mungu ndiye atakayekusaidia..mwanadamu atakutenda nini? Get well soon

    12. #71
      Mzee wa Rula's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th October 2010
      Posts : 6,522
      Rep Power : 24929
      Likes Received
      2234
      Likes Given
      1829

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Nadhani hii itakuwa imesaidia kuondoa doubt zote kuhusu ugonjwa wake.

    13. #72
      kuberwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Location : owaitu aha Mugongo
      Posts : 518
      Rep Power : 541
      Likes Received
      98
      Likes Given
      367

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      pole sana ndugu yetu, mwenyezi Mungu akuafu! Inshallah

    14. #73
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,661
      Rep Power : 4023
      Likes Received
      2944
      Likes Given
      5072

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Wish you quick recovery

    15. #74
      LATTICE BOND's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th May 2011
      Posts : 219
      Rep Power : 451
      Likes Received
      48
      Likes Given
      17

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Pole sana Mheshimiwa!!!!
      Kwa kweli Agha Khan kuna tatizo!! kuna haja ya watafiti kuichunguza hiyo hospitali!! kuna watu kadhaa ninaowafahamu wamewahi kukutana na mazingira yaliyokukuta wawili kati ya hao walipoteza maisha!!!!
      Kwangu mimi aliyekuokoa ni yule aliyeshauri upelekwe muhimbili!!
      AGAIN! POLE SANA MPIGANAJI WETU!!

    16. #75
      Ciril's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2011
      Posts : 2,015
      Rep Power : 893
      Likes Received
      252
      Likes Given
      19

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Pole sana mkuu usijali,tunakuombea Mungu upone ili uje ktk uwanja Wa mapambano.Ila nimejifunza jambo juu ya hospital zinazofanya biashara na zile zinazotoa matibabu,kweli hakika tutakufa sana.

    17. #76
      Kubingwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2010
      Location : Hapahapa
      Posts : 501
      Rep Power : 565
      Likes Received
      61
      Likes Given
      202

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Get well soon,Brother! Umati wa vijana wa kitanzania tunakuombea sana,Mh.

    18. #77
      MwanaHaki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th October 2006
      Posts : 1,415
      Rep Power : 1008
      Likes Received
      156
      Likes Given
      91

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Ndugu yangu Zuberi, nakuombea kwa Mola, Allah, SWT, upone haraka, na upasuaji utakaofanyiwa uende salama. Wewe ni shujaa wa Watanzania wote, bado tunakuhitaji kamanda!

      ./Mwana wa Haki
      Speaking Openly, without fear!

    19. #78
      Aggrey86's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2011
      Posts : 717
      Rep Power : 547
      Likes Received
      81
      Likes Given
      90

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      pole sana mkuu zitto Mungu atakusaidia utapona tu

    20. #79
      Bablii's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 19th April 2008
      Posts : 109
      Rep Power : 591
      Likes Received
      15
      Likes Given
      12

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Pole sana Kaka Zito, Allah akuponye haraka!
      Namimi nina tatizo kama hilo lako, ilinichukuwa muda sana kujuwa....!

      Nimekuwa na tatizo la kupoteza fahamu tangu 1996 nikiwa form I pale Ilboru Secondary, lakini sikuwahi kulihusisha tatizo hilo na ungonjwa huu wa sinusitis, bali nilidhani ni PRESSURE ndivyo nilivyokuwa naambiwa na madaktari wetu hapo Bongo, mpaka hii leo ninapoisoma hii taarifa yako ndo napata mwanga kwamba huenda hata huku kuanguka na kupoteza fahamu kwangu kunatokana na ugonjwa huu sugu wa sinusitis!

      Kilichonifanya nijue kama nna ugonjwa huu wa sinusitis, ni baada ya kupoteza uwezo wangu wa kunusa harufu na kuandamwa na flu zisizokwisha...mwaka 2007 nikiwa hapa Sweden, ndio niligundulika kwamba ni SINUSITIS, ambayo tayari ilishakuwa sugu, hizo dawa alizo suggests mdau hapo juu haziwezi kusadia tena ikishafikia stage hio ya usugu, kwa hiyo nilifanyia upasuaji mwaka huo 2007. Lakini hiyo pia si suluhisho la kudumu, sababu hizo polyps zinaota tena, hivyo basi baada ya muda (miaka 2) unatakiwa kurudi kwa checking, kama zitakuwa zimeota tena na ku block njia ya hewa, basi unapasuliwa tena!

      Mimi bado sijarudi tena, sababu upasuaji wangu wa kwanza ulikuwa na complication (ulichukuwa masaa 3.30 badala ya 1.45 zilizokusudiwa), sababu nilikuwa nilitoka damu mno, kiasi walishindwa kukata hizo polyps zote, hivyo imenijengea woga wakurudi tena. Inshaallah nikipata ujasiri ntarudi tena. Alienifanyia upasuaji ni daktari bingwa wa ENT hapa Sweden, Dr Morgan!

      Mh Zitto, nakutakia matibabu yenye mafanikio, Allah akujaalie uwe mwenye kupona haraka!

    21. #80
      Kimbojo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2009
      Posts : 300
      Rep Power : 579
      Likes Received
      40
      Likes Given
      26

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Kila la kheir ndugu yetu. Mungu akutangulie katika hiyo surgery ya kichwa, Amina

    Page 4 of 14 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Hotuba ya Zitto Kabwe Bungeni Juni 15, 2011 - Bajeti Mbadala
      By Maxence Melo in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 103
      Last Post: 16th June 2011, 15:32
    2. Mchango wa mheshimiwa Zitto Kabwe Bajeti 2010/2011
      By Ntemi Kazwile in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 10
      Last Post: 14th June 2010, 17:55
    3. Hotuba Ya Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe Kuhusu Miundombinu Bungeni
      By Mpaka Kieleweke in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 39
      Last Post: 18th December 2008, 00:15
    4. Bunge laonya wanaharakati kuhusu Zitto Kabwe
      By BAK in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 28
      Last Post: 19th August 2007, 14:11

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...