Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

    Report Post
    Page 2 of 14 FirstFirst 123412 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 261
    1. #1
      nice 2's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th August 2011
      Posts : 699
      Rep Power : 942
      Likes Received
      503
      Likes Given
      285

      Default Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 Oct 2011

      Wana JF,
      Hii ni email kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe. Nimeona ni vyema niiweke hapa ili tuweze kujua kwapamoja hali yake inavyoendelea.
      Nawasilisha,
      Nice 2


      Ndugu zangu,

      Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha muda huu kuwa na nguvu za kukaa katika kiti na kuweza kuandika haya machache kwenu. Nawashukuru sana Wanamabadiliko kwa salaam zenu nyingi za pole mara mliposikia ninaumwa na kulazwa hospitalini. Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika).

      Mwanzo

      Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa siku ya Ijumaa tarehe 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa Mamlaka za Maji nchini.

      Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za Jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya kuinigilia ziara za Jimboni ikiwemo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.

      Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.

      Siku ya Jumapili saa kumi na moja jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla. Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba Dereva wa Mhe. Mhonga anifuate ili anisadie kunifikisha nyumbani.

      Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.

      Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).

      Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku. Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia Hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.

      Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.

      Hali kubadilika

      Siku ya Jumanne niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini sio vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi.

      Hata hivyo ilipofika saa sita kamili nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana!

      Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale. Joto lilifika degree 39.8 Hivyo wakanipa dawa za kupoza homa na maumivu ya kichwa kwa drips na sindano kadhaa.

      Siku ya pili hospitalini nikafanya vipimo zaidi ikiwemo ultra sound na vyote kuonekana sina tatizo lolote. Niliendelea kuwepo Hospitali na kwa kweli hali ilikuwa inatia moyo sana kwani nilipata nguvu na hata kuweza kuzungumza, homa ilikuwa imepungua sana.

      Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa 'a trigger' ya homa kali niliyokuwa napata.

      Hali kuwa Mbaya

      Usiku wa siku ya Jumatano Hali ilikuwa mbaya sana. Joto lilipanda tena kufikia 40 na kichwa kuuma zaidi. Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.

      Wageni waliokuwa wamekuja kunijulia hali wakati hali inabadilika ilikuwa ni pamoja na Ndugu Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya POAC, walishauri mara moja nihamishwe Hospitali kupelekwa Muhimbili.

      Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika Chumba wanachokiita Mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mama Blandina Nyoni alikuwepo Hospitalini tayari.

      Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. Full Blood picture pamoja na BS. Vile vile kufuatia malalamiko kuhusu maumivu ya kichwa ikaamuliwa kuwa nifanyiwe CT Scan usiku ule.

      Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana Daktari kijana Dkt. Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale Mini ICU.

      Asubuhi ya siku ya pili nikapata majibu ya tatizo la maumivu ya kichwa. Nimekuwa nasumbuliwa na kichwa kwa miaka zaidi ya Kumi sasa na katika kipindi hicho mara nne nilipoteza fahamu na kuanguka (Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Jijini Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, Mara Pili Mjini Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001 lakini ilikuwa usiku, Mara ya tatu Nikiwa chumbani, Hall II mara baada ya kutoka *Prep, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge (Ndugu Katulanda anakumbuka siku hii kwani yeye ndiye niliyemkamata njiani kunikimbiza Zahanati ya Bunge).

      Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.

      Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya 'dozi' nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza 'dozi' hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya 'surgery' hiyo.

      Sijafa

      Uvumi ulienezwa nimekufa. Kwa kupitia kwenu ndugu zangu Wanamabadiliko, napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya. Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.

      Shukran
      Nawashukuru sana Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Prof, Mwafongo kwa juhudi kubwa walioonyesha katika kunihudumia. Naishukuru Ofisi ya Bunge kwa Kutimiza wajibu wao kwangu kama Mbunge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na watumishi wote wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kwa ufuatiliaji wa karibu wa Afya ya Naibu wake, Wabunge wajumbe wa Kamati ya POAC, Dkt. Alex Kitumo, ndugu, jamaa na marafiki zangu wote.

      Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo.

      Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri

      Ndugu yenu

      Zitto
      Last edited by nice 2; 30th October 2011 at 09:46.


    2. #21
      BONGOLALA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th September 2009
      Posts : 5,403
      Rep Power : 1581
      Likes Received
      1187
      Likes Given
      194

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Pole sana ila huduma ya haraka ya matibabu uliyopewa wewe si watanzania wote tunapewa priority kama wewe mheshimiwa, watanzania wengi tunakufa kutokana na kukosa huduma haraka ya matibabu!

      Mara ngapi tunaona mtoto mdogo anapelekwa kwenye TV kuomba msaada wa matibabu kisa eti mganga mkuu wa wilaya au mkoa anataka shilingi 2milioni za opearation?

      HIVYO KUNA UBAGUZI MKUBWA KATI YA ALIYENACHO NA ASIYENACHO katika kupata huduma ya afya.
      Mchaka Mchaka likes this.

    3. #22
      MAYOO's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th February 2011
      Posts : 175
      Rep Power : 458
      Likes Received
      20
      Likes Given
      15

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Pole sana, Mungu atakupigania na utapona tu.

    4. #23
      Crucial Man's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th January 2011
      Posts : 1,350
      Rep Power : 698
      Likes Received
      272
      Likes Given
      16

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Get well soon mkuu.atleast tumefarijika kupata neno kutoka kwako.mungu akujalie upone haraka kiongozi.

    5. #24
      MNAMBOWA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th October 2011
      Posts : 833
      Rep Power : 554
      Likes Received
      84
      Likes Given
      39

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      wenye nia mbaya washindwe kwa jina la YESU KRISTO ALIYE HAI

    6. #25
      Felixonfellix's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th February 2010
      Posts : 1,673
      Rep Power : 809
      Likes Received
      165
      Likes Given
      95

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Pole sana kaka
      Tunakuombea uzima
      Tushirikiane Tutafika Tuendako


    7. #26
      sweetlady's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 24th December 2010
      Location : Tanzania
      Posts : 15,371
      Rep Power : 36544
      Likes Received
      7503
      Likes Given
      4604

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Tunakuombea upone upesi! Tunashukuru kwa kutujuza khali yako!

    8. FJM is offline
      FJM
      #27
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,213
      Rep Power : 2580
      Likes Received
      5344
      Likes Given
      4607

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Ndugu Zitto, ugua pole na asante sana kwa taarifa ya kina. Ni matumaini yangu kuwa madaktari wa India wataweza kutibu tatizo la muda mrefu kama ulivyotueleza.

      Kitu kimoja ambacho utakuwa umetusaidia sana sisi watanzania wenzako ni jinsi Aga Khan Hospital walivyo bomu. Kuna mama amefia hospitalini hapo kutokana na malaria. Narudia, yuko mama kafia hapo Aga Khan kutokana na malaria. Hawa watu pamoja na ku-charge hela nyingi ni bomu kabisa na ndio maana watu wanasema Aga Khan ni kitanda kizuri cha kufia. Na kiburi chao kinatokana na kwamba mashirika/makumpuni mengi wamejiunga nao hivyo wana uhakika wa kupata wateja. Upone usipone hilo sio juu yao, wao wanataka pesa!

      Pengine muda umefika sasa kwa wagonjwa kuwa na haki ya kuwashitaki madaktari/hospitali pale wanavurunda. Huu mtindo wa madaktari kuendelea kufanya biashara na maisha ya watu ukomeshwe. Ningefurahi kama waandishi wa habari wangewaanika hawa Aga Khan. Wanashindwaje kugundua malaria wakati hata vi-dispensary vidogo huku mtaani wanaona? Hawafai hawa.

    9. #28
      Lukansola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th September 2010
      Location : 6°48′S 39°17′E
      Posts : 3,336
      Rep Power : 1075
      Likes Received
      755
      Likes Given
      1005

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Asante kwa taarifa na Mungu akujali afya njema urudi kazini.
      NO SECOND CHANCE TO MAKE THE FIRST IMPRESSION

    10. #29
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,707
      Rep Power : 10935
      Likes Received
      3961
      Likes Given
      426

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Mungu wetu ni mkuu,usijali utapona.Pole sana!

    11. #30
      Bukyanagandi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Location : DSM
      Posts : 2,004
      Rep Power : 935
      Likes Received
      745
      Likes Given
      1480

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Pole sana Mh.ZITTO, mimi nilisha kataza familia yangu kwenda pale Agha Khan kwa maswala ya kupimwa malaria, huwa nashindwa kuelewa hao jamaa wa mahabara wana elimu ya kiwango gani - sisi imekwisha tutokea zaidi ya mara nne kuambiwa blood slide hazionyeshi vidudu vya malaria! Tukienda hospitali nyingine for a second opinion unakata vimelea vya malaria vimejaa tele, je kama utata unakuwa kwenye malaria je vipimo vingine watasema nini si hatari hii?

      Siwasemi vibaya Agha Khan lakini ukweli unabaki pale pale kwamba laboratory technicians wao wawafanyie usahiri tena, haiwezekani wakawa wanatoa majibu ya kufikilika/kubuni tu au huwa hawatumii darubini kabisa nini! Uongozi wa Hospitali hiyo unapaswa kulifanyia kazi swala hili.

    12. #31
      GATZBY's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th July 2011
      Posts : 27
      Rep Power : 404
      Likes Received
      5
      Likes Given
      3

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Pole sana kamanda wangu na mbunge wangu. Nakuombea kwa Mungu upone upesi ili urejee kwenye majukumu. Taifa hili na watu wake tunakuhitaji bado.

    13. #32
      kichomiz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 4,124
      Rep Power : 1250
      Likes Received
      670
      Likes Given
      80

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Mungu mkubwa pangalo hakuna mwanadam anayeweza kupangua,GET WELL SOON KAMANDA.

    14. #33
      Mpita Njia's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd March 2008
      Posts : 6,751
      Rep Power : 3269
      Likes Received
      992
      Likes Given
      785

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Mungu akujalie surgeryb iende vema. Tunazidi kukuombea
      I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.

    15. #34
      mmbangifingi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2011
      Posts : 2,573
      Rep Power : 862
      Likes Received
      454
      Likes Given
      2916

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Daaaaaah! afadhali Mh Kabwe umetupatia taarifa kupata mwanga wa ilivokuwa na hali yako ya sasa. Ugua pole. Jah will guide you!
      Who Jah bless, No one Curse!

    16. #35
      Gsana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th August 2010
      Location : Dar es salaam
      Posts : 2,259
      Rep Power : 898
      Likes Received
      227
      Likes Given
      45

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      pole kaka,pia nakushukuru kwa kutuondoa hofu juu ya afya yako. nakutakia afya njema ndugu,upone haraka tuendelee kulijenga taifa.

    17. #36
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,203
      Rep Power : 12279
      Likes Received
      6062
      Likes Given
      6927

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      ugua pole zitto/nice
      ....Time is the wisest counselor !!!

    18. #37
      Omutwale's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2008
      Location : Kanyigo
      Posts : 1,142
      Rep Power : 817
      Likes Received
      587
      Likes Given
      510

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Mungu aendelee kukulinda. Akuponye na maumivu. Na mwisho urejee salama kutimiza majukumu yako. Amen

    19. #38
      Zion Train's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2008
      Posts : 506
      Rep Power : 664
      Likes Received
      72
      Likes Given
      155

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      pole sana, Inshaallah huo upasuaji utaenda salama pia. kweli kila mwaadam atakufa lakini hospital zingine zinachangia, kama hii aga khan hata hiko namna pale, ukilazwa pale wajameni unashindiliwa midawa balaa, mradi tu bill hiwe nyoofu.
      Love is my Religion

    20. #39
      jmushi1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2007
      Posts : 14,426
      Rep Power : 16506
      Likes Received
      4327
      Likes Given
      5510

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.
      Sinusitis

      Sinusitis means your sinuses are infected or inflamed. Your sinuses are hollow air spaces within the bones surrounding the nose. They produce mucus, which drains into the nose. If your nose is swollen, this can block the sinuses and cause pain and infection.
      Sinusitis can be acute, lasting for less than four weeks, or chronic, lasting much longer. Acute sinusitis often starts as a cold, which then turns into a bacterial infection. Allergies, pollutants, nasal problems and certain diseases can also cause sinusitis.
      Symptoms of sinusitis can include fever, weakness, fatigue, cough and congestion. There may also be mucus drainage in the back of the throat, called postnasal drip. Treatments include antibiotics, decongestants and pain relievers. Using heat pads on the inflamed area, saline nasal sprays and vaporizers can also help.
      NIH: National Institute of Allergy and Infectious Diseases

      So ina maana kama wange mdiagnose mapema,then angetakiwa kuzingatia haya.....
      Treatments to relieve symptoms
      Your doctor may recommend treatments to help relieve sinusitis symptoms. These include:
      • Saline nasal spray, which you spray into your nose several times a day to rinse your nasal passages.
      • Nasal corticosteroids. These nasal sprays help prevent and treat inflammation. Examples include fluticasone (Flonase), budesonide (Rhinocort Aqua), triamcinolone (Nasacort AQ), mometasone (Nasonex) and beclomethasone (Beconase AQ).
      • Oral or injected corticosteroids. These medications are used to relieve inflammation from severe sinusitis, especially if you also have nasal polyps. Examples include prednisone and methylprednisolone. Oral corticosteroids can cause serious side effects when used long term, so they're used only to treat severe asthma symptoms.
      • Decongestants. These medications are available in over-the-counter (OTC) and prescription liquids, tablets and nasal sprays. Examples of OTC oral decongestants include Sudafed and Actifed. An example of an OTC nasal spray is oxymetazoline (Afrin). These medications are generally taken for a few days at most; otherwise they can cause the return of more severe congestion (rebound congestion).
      • Over-the-counter pain relievers such as aspirin, acetaminophen (Tylenol, others) or ibuprofen (Advil, Motrin, others). Because of the risk of Reye's syndrome — a potentially life-threatening illness — never give aspirin to anyone younger than age 18.
      • Aspirin desensitization treatment if you have reactions to aspirin that cause sinusitis. However, this treatment can have serious complications such as intestinal bleeding or severe asthma attacks.
      Antibiotics
      Antibiotics are sometimes necessary for sinusitis if you have a bacterial infection. However, chronic sinusitis is usually caused by something other than bacteria, so antibiotics usually won't help.
      Antibiotics used to treat chronic sinusitis caused by a bacterial infection include amoxicillin (Amoxil, others), doxycycline (Doryx, Monodox, others) or the combination drug trimethoprim-sulfamethoxazole (Bactrim, Septra, others). If the infection doesn't subside or if the sinusitis comes back, your doctor may try a different antibiotic.
      If your doctor does prescribe antibiotics, it's critical to take the entire course of medication. Generally, this means you'll need to take them for 10 to 14 days or even longer — even after your symptoms get better. If you stop taking them early, your symptoms may come back.
      Immunotherapy
      If allergies are contributing to your sinusitis, allergy shots (immunotherapy) that help reduce the body's reaction to specific allergens may help treat the condition.
      Kutokana na maelezo ya Zitto,tatizo hilo limekuwa likimsumbua na hakujuwa kuwa hiyo ni sinusitis hadi ilipogundulika juzi kabla ya kupelekwa India.

      Na kwahivyo daktari huyo hakuona umuhimu wa kufuata ushauri huo hapo juu,ametoa ushauri wa surgery kabla hata hawaja jaribu kumtibu through those ways kama inavyoshauriwa.

      Surgery ni last option kama walizingatia matibabu ya sinusitis na hayakufanya kazi.

      Ama kumtibu malaria ndiyo wana maanisha kuwa walikuwa wakiitibu hiyo sinusitis?

      Bado naona kuna ukurupukaji wa kiana,sijui wa kulaumiwa ni nani?

      Tatizo alilonalo Zitto halikuwa tatizo la kusumbua watu vichwa na hata kutumia gharama zote hadi India.Inaonyesha kabisa tuko hovyo hovyo.

      Hakuna taratibu za kufuatwa kama a civilised society!

      Mtu anaumwa one thing lakini anatibiwa something else,halafu wanapogunduwa hilo,bado hawajaribu kushughulikia tatizo jinsi lilivyo,yani this time try to contain the sinusitis proplem before opting for a surgery which should be the last resort!Imenikumbushia sana ile issue ya mgonjwa aliyehitaji upasuaji wa mguu alipopasuliwa kichwa instead!Na ilikuwa hapo hapo Muhimbili!
      Surgery
      In cases that continue to resist treatment or medication, endoscopic sinus surgery may be an option. For this procedure, the doctor uses an endoscope, a thin, flexible tube with an attached light, to explore your sinus passages. Then, depending on the source of obstruction, the doctor may use various instruments to remove tissue or shave away a polyp that's causing nasal blockage. Enlarging a narrow sinus opening also may be an option to promote drainage.
      "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

    21. #40
      THINKINGBEING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th August 2010
      Posts : 1,002
      Rep Power : 663
      Likes Received
      235
      Likes Given
      102

      Default Re: Ukweli kuhusu hali ya mh. Zitto Kabwe - 29 oct 2011

      Pole sana mpambanaji.Nakutakia afya njema.
      Mungu akujalie uliwahi bunge.
      create tension to anyone who wish not to think

    Page 2 of 14 FirstFirst 123412 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Hotuba ya Zitto Kabwe Bungeni Juni 15, 2011 - Bajeti Mbadala
      By Maxence Melo in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 103
      Last Post: 16th June 2011, 15:32
    2. Mchango wa mheshimiwa Zitto Kabwe Bajeti 2010/2011
      By Ntemi Kazwile in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 10
      Last Post: 14th June 2010, 17:55
    3. Hotuba Ya Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe Kuhusu Miundombinu Bungeni
      By Mpaka Kieleweke in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 39
      Last Post: 18th December 2008, 00:15
    4. Bunge laonya wanaharakati kuhusu Zitto Kabwe
      By BAK in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 28
      Last Post: 19th August 2007, 14:11

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...