Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: MwanaHalisi yamshambulia Sitta

    Report Post
    Page 11 of 12 FirstFirst ... 9101112 LastLast
    Results 201 to 220 of 221
    1. #1
      Zak Malang's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th December 2008
      Posts : 4,835
      Rep Power : 1921
      Likes Received
      187
      Likes Given
      2

      Default MwanaHalisi yamshambulia Sitta

      Shutuma za Sitta dhidi ya Kubenea kwamba sasa kanunuliwa na mafisadi kama alivyozitoa katika kipindi chake katika ITV zimejibiwa na na gazeti hilo wiki hii katika tahariri yake iliyoanzia ukurasa wa mbele.

      Kubenea anataka kuonekana ni jembe lisilotetereka katika kuwaumbua mafisadi na wale wanaofuatilia kwa makini stori za gazeti hilo watagundua kwamba hana marafiki, na hasa wa mafisadi, wapambe wao na wote wale manafiki wanaojifanya kuupiga vita ufisadi, kumbe wao ndiyo mafisadi wakuu.

      Soma mwenyewe hiyo tahariri hapa chini.

      _____________________

      TAHARIRI: Sitta ‘kanyea kambi’

      SAMWEL Sitta ametuhumu gazeti hili, kuwa linatumiwa na watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini ili “kumchafua” yeye na wenzake.

      Alikuwa akiongea kwenye kipindi cha “Dakika 45” juzi Jumatatu, kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

      Sitta alionekana na kusikika akisema, gazeti hili lilikuwa madhubuti na imara; lakini sasa limeanza kuyumba kutokana na hatua yake ya kushambulia wale wanaopigana na ufisadi nchini, hasa yeye.

      Alikwenda mbali hata kutuhumu mtendaji mkuu wa Hali Halisi Publishers Limited (HHPL) na mchapishaji wa MwanaHALISI, Saed Kubenea, kuwa amenunuliwa na mafisadi.

      Waziri huyu wa Afrika Mashariki anajua fika kwamba gazeti la MwanaHALISI, wamiliki wake, waandishi wake, hawana mkataba naye wa kumwandika anayotaka.
      Sisi tuko kazini. Tunaangalia wale tunaowatumikia; nao ni umma wa Tanzania na jamii pana. Siyo Samwel John Sitta wa Urambo, kibarua katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

      Si gazeti, kiongozi wake wala mwandishi wa MwanaHALISI, aliye na mkataba wa kumwandika Sitta kama anavyotaka. Tuna kanuni ya kuandika yeyote na chochote kama alivyo au kilivyo na siyo kwa upendeleo.

      Kama Sitta aliwahi kuandikwa vizuri ajue; na labda akumbuke kuwa, hakuwa ametoa chochote, ameahidi chochote au amefurahisha gazeti kwa lolote lile; bali kwa kuwa alikuwa kwenye mstari wa ukweli na haki.

      Pale atakapotoka kwenye mstari; akajiingiza kwenye fikra, kauli na matendo ambayo tunaona na kuamini kuwa siyo sahihi; yanayokinzana na ukweli na haki kwa jamii tuliyomo; tutamwonyesha kwa jamii kama alivyo – bila woga wala upendeleo.

      Nani amemtuma Sitta kushiriki vita dhidi ya MwanaHALISI? Nani atamwamini kwa kauli zake ambazo hawezi kuthibitisha? Je, kwamba gazeti limeandika asichopenda au ambacho hapendi wengi wajue juu yake, huko ndiko kushirikiana na mafisadi?

      Siyo sahihi kutumia “ufisadi” kujenga urafiki au uadui. Fisadi na hata wanaowashabikia, watafahamika, hasa kwa matendo yao na mapema, kwa kauli zao. Lakini kwa Sitta kujaribu kukimbia kivuli chake, na kutafuta kuegemeza woga wake kwa MwanaHALISI; hakika ni woga uliopitiliza kwa mtu wa umri, elimu, uzoefu kazini na nafasi aliyonayo serikalini.

      Hata hivyo, Sitta siyo mwanzilishi wa “mapambano dhidi ya mafisadi” nchini. Hata kwa hatua ya Bunge kuchunguza mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond wakati yeye akiwa spika, hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuona ufahari na kujitwisha ushujaa.

      Bunge lilikuwa linafanya mwitikio tu wa mfululizo wa ripoti za vyombo vya habari jasiri ambavyo vilikuwa vikiandika, bila kukoma, ufisadi uliokuwa umefanywa nchini. Richmond ni “cha mtoto” kwa ufisadi mkuu ambao bunge lake halikushughulikia na bado liko kimya juu yake.

      Aidha, ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilichoanika orodha ya watuhumiwa 11 wa ufisadi hapo 15 Septemba 2007 kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam; wakati viongozi wa Sitta – katika chama chake na serikali wakidai kuwa “huo ni uzushi mtupu.”

      Ukweli ni huu: Walioanikwa ni viongozi wakuu wa nchi wa sasa na waliopita ambao wamekuwa waajiri wa Samwel John Sitta. Bado ni waajiri wake. Hawezi kujitenga nao. Hawezi hata kuwaambia uso kwa uso kwa ukali wa mkweli na mhalifu. Anarukia MwanaHALISI!

      Gazeti hili lina rekodi ya kuwa pekee lililoripoti kwa kina na ufasaha tuhuma ya kila mmoja miongoni mwa waliotajwa kwenye orodha ya mafisadi. Mara baada ya kuchapisha taarifa za watuhumiwa na picha zao, baadhi walitishia kwenda mahakamani; lakini tulisimama imara hadi wakayeyuka.

      Hata kinachoitwa “ujasiri wa wapinga ufisadi” ndani na nje ya bunge, kilitokana na mfululizo wa uibuaji uoza serikalini. Uibuaji huo ulifanywa na baadhi ya vyombo vya habari; gazeti hili likiwemo au likiongoza.

      Bali tukubali kuwa Sitta ana matatizo na wenzake. Ni muhimu amalizane nao vizuri au vyovyote vile bila kujenga viinimacho. Kwa mfano, Sitta anataka kujinasua kutoka kwenye tuhuma za usaliti wa chama chake kwa kile kinachoitwa “kuanzisha chama ndani ya chama.”

      Anatuhumiwa kuwa mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Jamii (CCJ) wakati bado ana nafasi ya juu katika uongozi wa serikali ya chama kilichoko madarakani. Hakika hili siyo tatizo la MwanaHALISI; hata pale gazeti litakapokuwa limeandika taarifa zake kwa kunukuu vyanzo ambavyo siyo rahisi kuvikanusha.

      Hapa, badala ya kutuhumu gazeti letu, ni vema akajibu madai ya “washirika wake,” hasa Fred Mpendazoe, anayelalamika kuwa Sitta alimtosa. Mpendazoe ambaye wakati huo alikuwa mbunge wa Kishapu (CCM), anasema aliamua kuacha ubunge ili kuimarisha CCJ, wakati wakisubiri “Sitta na wenzake.”

      Gazeti halihusiki na chochote walichoahidiana wakati huo. Halijapata ushahidi kama walidhulumiana. Halijapokea taarifa iwapo kuna ambao hawakupata mgawo wa fedha zilizochangwa na wahisani wa ndani au nje kwa ajili ya kazi ya akina Sitta na Mpendazoe.

      Tunachojua na tulichochapisha ni juu ya ujio wa CCJ, nani alikusanya fedha na kutoka kwa nani; nani alilipia kodi ya pango ya ofisi, nani alilipa mishahara ya watumishi wa mwanzo na nani alilalamika, kwamba “wenzangu wameniacha njiapanda.”

      Hadi sasa waanzilishi watatu wamesema kile wanachodai wanaelewa vema na hata kwa kiapo. Hao ni Mpendazoe, Dickson Ng’hily na Daniel ole Porokwa. Katika hili, na hasa kama Sitta anadhani tunalikuza kwa kuliandika, alaumu wenzake na siyo chombo cha habari wala wanaokimiliki.

      Jingine ambalo tunahisi linaweza kuwa limemfanya Sitta aanze kushambulia MwanaHALISI, ni pale gazeti lilipomtuhumu hujuma kwa kufunga mjadala wa kashfa ya Richmond. Wakati huo alikuwa spika. Hapa tulisema bayana kwamba hatukubaliani naye. Hata sasa hatukubaliani naye.

      Ni kunyenyekea kwake kwa serikali au kutafuta “mwafaka” wa haraka kwa maslahi binafsi ambako kulimfanya azime mjadala muhimu kwa taifa. Bado tunapinga hili. Tunalipinga kwa kuwa linaathiri vibaya hata kauli zake za sasa za kutaka kampuni ya kufua umeme ya Dowans isilipwe zionekana kama mzaha.

      Kama kwa msimamo wetu huo anaona ndio tunashirikiana na mafisadi kumchafua, basi amefikia ukingoni. Sharti arudi nyuma au abomoe ngome ya kiza kilichomfunika macho na akili.

      Na nani amempa Sitta madaraka ya kuamua kuwa hiki ndiyo ufisadi na kile siyo ufisadi? Kama angekuwa mkweli na safi, asingekuwa anatumikia ambao tayari wamethibitika kuwa mafisadi – kwa kauli, vitendo na kisheria.

      Gazeti hili haliwajibiki kuomba ruhusa kwa Sitta ili lirekodi kuyumba au kupotoka na hata kutetereka kwake. Tuna haki ya kuona, kuchambua, kutolea maoni na hata kuchapisha kile tunachoona na kusadiki juu yake na juu ya yeyote na chochote kile.

      Atakayejaribu kutunyang’anya haki na uhuru wetu huo, kwa kutuita washirika wa “mafisadi,” tutampinga. Tutaomba wadau wa habari kumpinga. Lakini pia tutamwita fisadi mkuu anayejaribu kutunyang’anya haki ya kufikiri, kuandika ukweli na kutoa kauli.

      Sitta ananyea kambi.

    2. Study Abroad

    3. #201
      KIM KARDASH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 4,252
      Rep Power : 0
      Likes Received
      564
      Likes Given
      55

      Default Re: Saed Kubenea, Very sory umepata zero kabisa Mtihani huu!

      Quote By Counterpunch

      Kubenea ni jembe lililowafunuwa Watz na kuwafanya chupi za mijizi ya CCM kuwaka moto. Wanavyomuandama, ni sababu tosha kabisa kwamba kwashika pabaya sana, kuanzia top wao JK kwenda chini.

      Wanahaha hovyo hawajui wasemalo, wala wafanyalo. haya tena madudu mengine ya TIB haya hela zilizorejeshwa zachotwa. Kubenea alilianzisha hili kwa kuwataja wezi hawa katika gazeti lake mwaka 2007 orodha ya wezi 11 kuanzia JK. hakuna gazeti jingine lilikuwa na balls la kutraja majina hayo.

      Kubenea ni mkombozi wa wanyonge -- HONGEERA SAANA. ENDELEA NA NYUNDO ZAKO!
      We kweli uko mbali na ukweli,kubenea unamtenganisha vipi na ccm wakati ni mwanachama hai wa magamba lakini kama unavyojua ccm imegawanyika mara mbili,pro-magamba na anti-magamba,kubenea yeye kaamua kuchagua kundi la pro-magamba,ili upate picha na kuelewa zaidi nini nasema ntakutajia wajumbe angalau waandamizi wa magenge yote hayo mawili:

      CCM Pro magamba:genge la Lowassa

      1:Januari makamba

      2:Peter Serukamba

      3:Makongoro mahanga

      4:James ole millya

      5:Msomali Bashe

      6:Benno Malisa

      7:Said kubenea

      8:Absalom kibanda(huyu sio ccm naona "kiu ya maendeleo" ya haraka imemsukuma)

      9:Freddy Lowassa

      10:Rostam Aziz

      11:Beatrice Shelukindo(huyu nae kiu ya uwaziri alioahidiwa na lowassa ndio imempeleka huko,akamsaliti hata mumewe mzee shelukindo)

      CCM anti-magamba

      1:Nape Nnauye

      2:Sam Six

      3:John Magufuli

      4:John Chiligati

      5:wakuu wote wapya wa mikoa walioteuliwa hivi karibuni

      6:Wazee wa nyerere foundation

      7:Bernard Membe

      8:Harrison Mwakyembe

      9:Lazaro Nyalandu(huyu anasukumwa na kiu ya kuutaka urais,unajua wengi wameona kama jk ameweza kuwa rais basi kila m2 anaweza)

      Angalau kwa uchache muwafahamu hao.
      Ben Saanane likes this.

    4. #202

      Quote By SPANNER
      Watanzania bwana, watu wamekubuhu kwa uwongo. Ni kwa sababu, taifa halina maadili.

      Mtu mzima anaandika Kubenea kanunuliwa kwa sababu, eti amekutwa akisalimiana na Lowassa?

      Mimi nilikuwapo siku ambayo picha hii imepigwa. Ilikuwa ni kwenye msiba wa Dany Mwakiteleko, ambapo Kubenea aliingia hapo na kumkuta Lowassa akiwa amefika kuhani. Sasa ulitaka asiende kumsalimia? Hata kama kuna ugomvi kiasi gani, kulikuwa hakuna njia ya kutoenda kumsalimia.

      Huyu jamaa alivyokubuhu kwa uwongo, anamtaja Ngurumo kwamba anamjua vema Kubenea, kwamba hakwenda shule. Lakini hasemi amesoma kwa kiwango gani.

      Lakini hata kama hakwenda shule kwa kiwango cha Chuo Kikuu, lakini anachokifanyia taifa ni kikubwa kuliko hao waliopata elimu – waliohesabu madarasa.

      Kisha mtoa mada anasema ‘Kubenea anatoka Mafia.” Ana uhakika na hilo? Mimi najua wapo watu humu ndani, kazi yao kuchafua wenzao. Ndiyo hao waliowahi kuandika humu ndani Kubenea kwenda kugombea ubunge Mafia.

      Uchaguzi umekwisha hakuoenekana na mpaka leo hajaonekana huko.

      Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Kubenea ni mmoja wa vijana wachache waliofanikiwa kuanzisha gazeti na kuleta mabadiliko nchini…
      Umemamua kujitoa akili makusudi,unajua kabisa issue sio picha hapa,sema unajaribu kupotosha makusudi,kwa kuwa kama umeweza kuwasha computer na kuweka maneno yako humu ni wazi unayo akili angalau ya kujua kusoma na kuandika hata kwa kiswahili tu!acha upotoshaji taifa liko ICU kwa ajili ya Lowassa na genge lake linaloungwa mkono na Kubenea wako!

    5. #203
      KIM KARDASH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 4,252
      Rep Power : 0
      Likes Received
      564
      Likes Given
      55

      Default Re: Saed Kubenea, Very sory umepata zero kabisa Mtihani huu!

      Quote By Counterpunch

      Kubenea ni jembe lililowafunuwa Watz na kuwafanya chupi za mijizi ya CCM kuwaka moto. Wanavyomuandama, ni sababu tosha kabisa kwamba kwashika pabaya sana, kuanzia top wao JK kwenda chini.

      Wanahaha hovyo hawajui wasemalo, wala wafanyalo. haya tena madudu mengine ya TIB haya hela zilizorejeshwa zachotwa. Kubenea alilianzisha hili kwa kuwataja wezi hawa katika gazeti lake mwaka 2007 orodha ya wezi 11 kuanzia JK. hakuna gazeti jingine lilikuwa na balls la kutraja majina hayo.

      Kubenea ni mkombozi wa wanyonge -- HONGEERA SAANA. ENDELEA NA NYUNDO ZAKO!
      Eti kubenea jembe! labda jembe la kukokotwa na ng'ombe...kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza kinene na mvua kubwa ya mawe yenye radi zenye hasira!haya bwana endeleeni kulikokota hilo jembe lenu mmalize kulima shamba la bwana mkubwa Ngonyani Lowassa...
      Ben Saanane likes this.

    6. #204
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,394
      Rep Power : 10868
      Likes Received
      3773
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By Fareed
      Kubenea kanunuliwa siku nyingi na mafisadi, ndio mabwana zake wapya. Hapo anamsalimia fisadi Lowassa kwa unyenyekevu kama mke amsalimiapo mume wake. Habari yenyewe ya wiki hii yenye kuhusu Richmond kumwandama Lowassa ni ya kinafiki. Ni danganya toto eti kutaka watu wadhani kuwa bado anaendelea kumgonga Lowassa, ndani ya habari yenyewe kaandika utumbo mtupu kuwa eti serikali nzima ndio iliyohusika na Richmond badala ya kusema ukweli kuwa wahusika wakuu wa rushwa hii ni Edward Lowassa, Rostam Aziz na Nazir Karamagi.

      Kubenea ana roho nyepesi kama kuku, ndio maana kanunuliwa na mafisadi na sasa anaelekea kufilisika.
      wewe uko kundi la Sitta

    7. #205
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,394
      Rep Power : 10868
      Likes Received
      3773
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By Waberoya

      Kaka sio wewe tu nilishasema sana humu na kuishia kutukanwa

      1. Kubenea ni mwana CCM, na uchaguzi uliopita alitaka kugombea ubunge huko kilwa au mafia na kujitoa dakika za mwisho
      2. Kubenea alijitahidi sana kuiua chadema kwa kumwandika zito vibaya , ili wanachadema wengi hawakuliona na wakamrarua zito vibaya ( niliulalamika sana hapa http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/92369-zitto-aisumbua-chadema%3B-chama-chafikiri-namna-ya-kumdhibiti-6.html#post1324607)

      3. Kubenea amejitahidi sana kuaaminisha umma kuwa alimwagiwa tindikali kwa sababu ya ufisadi ukweli anaujua mwenyewe, (mke wa mtu sumu!) kubenea mpaka leo hajaweza kuuelezea umma ni FISADI GANI ALIFANYA HIVYO, japo wamwagaji wa tindikali walikamatwa!!!

      4. Kubena huwa anaandika habari za kikwete kwa mlengo mmoja tu, kumwonyesha kuwa ni mpiganaji wa ufisadi na wanaomkwamisha ni watu wake wa chini

      5. Kubenea huyu, habari zake nyingi hazina vithibitisho ila ni imaginary na ku-create matatizo mengi

      NI MJASIRIAMALI, AMETUMIA WAKATI NA NYAKATI HIZI, AMESOMA WATANZANIA WENGI WANATAKA NINI, AMEENDA VILE WATANAZANIA WANAVYOTAKA NA LEO HII AMEKUWA TAJIRI ILI HALI UKIWAULIZA WASOMAJI WA MWANAHALISI wanagain nini? ni umbeya...ila umbeya wa kisiasa which is very unique and intersting kuliko umbeya wa kimapenzi na ma-star!
      mkuu kwanini anapotajwa Zitto unakasirika mpaka kupandisha povu? Mwanahalisi ndilo gazeti bora Tanzania.

    8. FemaTV & Radio

    9. #206
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,394
      Rep Power : 10868
      Likes Received
      3773
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By THE ROMANTIC
      Eti kubenea jembe! labda jembe la kukokotwa na ng'ombe...kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza kinene na mvua kubwa ya mawe yenye radi zenye hasira!haya bwana endeleeni kulikokota hilo jembe lenu mmalize kulima shamba la bwana mkubwa Ngonyani Lowassa...
      kundi la Sitta mtahangaika sana mwaka huu.

    10. #207
      Butola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2010
      Posts : 1,520
      Rep Power : 782
      Likes Received
      266
      Likes Given
      647

      Default Re: Saed Kubenea, Very sory umepata zero kabisa Mtihani huu!

      Quote By Albedo
      Hivi Ofisi ya Spika iliyoko Urambo nani anaitumia sasa. Hiki Kibabu kilidhani kitakuwa Spika wa Milele, Kimrithishe Mke wake, Mtoto wake na wajukuu zake. Huyu hana Tofauti na Gadafi aliyeamua Kujenga Makao Makuu ya AU kwao Siirte
      ...Last time i checked kuna ofisi ya Spika mjini Dodoma na ofisi ndogo mjini Dar es Salaam, sasa hiyo ofisi ya Spika wa Bunge wilayani Urambo imejengwa lini tena?hii ni habari mpya hii, ata ofisi ya Bunge na Serikali kuu hawana hii taarifa...

      Ebu utupe hapa data za kuthibitisha uwepo wa Ofisi hiyo wilayani Urambo au uombe msamaha kwa kuleta habari ya uongo, ndio ustaarabu..
      Last edited by Butola; 4th November 2011 at 19:32.

    11. #208
      raffiki's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th June 2011
      Posts : 163
      Rep Power : 435
      Likes Received
      40
      Likes Given
      0

      Thumbs up Re: Saed Kubenea, Very sory umepata zero kabisa Mtihani huu!

      Quote By THE ROMANTIC
      We kweli uko mbali na ukweli,kubenea unamtenganisha vipi na ccm wakati ni mwanachama hai wa magamba lakini kama unavyojua ccm imegawanyika mara mbili,pro-magamba na anti-magamba,kubenea yeye kaamua kuchagua kundi la pro-magamba,ili upate picha na kuelewa zaidi nini nasema ntakutajia wajumbe angalau waandamizi wa magenge yote hayo mawili:

      CCM Pro magamba:genge la Lowassa

      1:Januari makamba

      2:Peter Serukamba

      3:Makongoro mahanga

      4:James ole millya

      5:Msomali Bashe

      6:Benno Malisa

      7:Said kubenea

      8:Absalom kibanda(huyu sio ccm naona "kiu ya maendeleo" ya haraka imemsukuma)

      9:Freddy Lowassa

      10:Rostam Aziz

      11:Beatrice Shelukindo(huyu nae kiu ya uwaziri alioahidiwa na lowassa ndio imempeleka huko,akamsaliti hata mumewe mzee shelukindo)

      CCM anti-magamba

      1:Nape Nnauye

      2:Sam Six

      3:John Magufuli

      4:John Chiligati

      5:wakuu wote wapya wa mikoa walioteuliwa hivi karibuni

      6:Wazee wa nyerere foundation

      7:Bernard Membe

      8:Harrison Mwakyembe

      9:Lazaro Nyalandu(huyu anasukumwa na kiu ya kuutaka urais,unajua wengi wameona kama jk ameweza kuwa rais basi kila m2 anaweza)

      Angalau kwa uchache muwafahamu hao.
      HONGGERA UMEJARIBU KUCHAMBUA VIZURI ILA HUYU Januari makambaNADHANI BADO HAUJAMJUA VIZURI...HUYO YUPO PANDE ZOTE MBILI, ANACHUKUA HABARI KUTOKA KUNDI MOJA NA ANAPELEKA LINGINE...WOTE WANAAMINI YUPO KUNDI LAO...LAKE NI KUWA YEYOTE ATAKAYESHINDA BASI ATAAMINI PIA KULETA KWAKE HABARI ZA KUNDI LILILOSHINDWA LIMESAIDIA LILILOSHINDA

    12. #209
      KIM KARDASH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 4,252
      Rep Power : 0
      Likes Received
      564
      Likes Given
      55

      Default Re: MwanaHalisi yamshambulia Sitta

      Quote By fmpiganaji
      JF sio kijiwe cha majungu.Ni dhahiri Magamba kuna makundi mawili,kundi la Sitta na kundi la Lowassa.Wewe umejionyesha uko kundi la Sitta ambao ni wapinga ufisadi bandia.Mbona kundi la Sitta limenunua Raia Mwema hatusemi? Usijidanganye hakuna gazeti linalofikia kwa habari kali na za uchunguzi Tanzania kama mwanahalisi.
      Ahaa kwa hiyo unakubaliana na mleta thread kwamba mwanahalisi limenunuliwa na Ngonyani Lowassa lakini pia unatukumbusha kuwa hata raia mwema nalo limenunuliwa na sitta sio?halafu mwisho ndio umemaliza kabisa kusema gazeti la mwanahalisi ambalo mwanzo indirectly umekiri kufahamu kwamba limenunuliwa na lowassa lina "habari kali na za uchunguzi",hapa wewe mwenyewe utuambie unaonyesha picha gani kukuhusu wewe na lowassa?????

    13. #210
      KIM KARDASH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 4,252
      Rep Power : 0
      Likes Received
      564
      Likes Given
      55

      Default Re: MwanaHalisi yamshambulia Sitta

      Quote By fmpiganaji
      kundi la Sitta mtahangaika sana mwaka huu.
      sawa na mang'ombe wataendelea kulikokota hilo jembe lao kwa kulinunua na kusoma anayotaka lowassa yaandikwe!kila la heri na jembe lenu!

    14. #211
      KIM KARDASH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 4,252
      Rep Power : 0
      Likes Received
      564
      Likes Given
      55

      Default Re: Saed Kubenea, Very sory umepata zero kabisa Mtihani huu!

      Quote By raffiki
      HONGGERA UMEJARIBU KUCHAMBUA VIZURI ILA HUYU Januari makambaNADHANI BADO HAUJAMJUA VIZURI...HUYO YUPO PANDE ZOTE MBILI, ANACHUKUA HABARI KUTOKA KUNDI MOJA NA ANAPELEKA LINGINE...WOTE WANAAMINI YUPO KUNDI LAO...LAKE NI KUWA YEYOTE ATAKAYESHINDA BASI ATAAMINI PIA KULETA KWAKE HABARI ZA KUNDI LILILOSHINDWA LIMESAIDIA LILILOSHINDA
      Ngoja nitafuatilia kwa kina,lakini mimi ninavyomjua huyu hapindui kwa Rostam.....ni mfuasi mtiifu wa Rostam,zamani alikua kijana mwaminifu wa jk,lakini baadae baada ya lowassa kuondoka serikalini ikaja kuonekana anamuuza jk kwa kina lowassa kwa kupeleka habari za kila hatua anayotaka kuchukua muungwana dhidi ya maswahiba zake hao,jk alikua anamuamini sana huyu kijana,toka kipindi cha kampeni za 2005 na ndie aliyetengeneza ile kauli mbiu ya kisanii "ari mpya nguvu mpya kasi mpya"!lakini baadae hasa baada ya membe na ridhiwani kumshika masikio muungwana kuhusu ujanja ujanja wa dogo januari ndio jk akamtosa mazima,hata ile mipango ya kumpa wizara ya nishati ambayo amekua akiiota ikayeyuka kwa fitn za ridhi na membe,ndio maana dogo ana hasira na wizara ya nishati kupita maelezo....

    15. #212
      Thesi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th August 2010
      Posts : 727
      Rep Power : 4675
      Likes Received
      186
      Likes Given
      320

      Default Re: MwanaHalisi yamshambulia Sitta

      We romantic kila thread inayomhusu sita umo. ila ukweli ni kuwa sita is just political hypocrite who want to play hero.
      si kwamba hana mazuri anayo lakini hizo hadhi anazotaka tumuweke kwenye upambanaji sio. ni muoga anayetimiza matakwa ya mafisadi au kufisadi akipata nafasi kama alivojenga ofisi ya spika urambo na kutetea mishahara mikubwa ya wabunge na posho za kifisadi. kwa kifupi mnafiki.

    16. #213
      Thesi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th August 2010
      Posts : 727
      Rep Power : 4675
      Likes Received
      186
      Likes Given
      320

      Default Re: MwanaHalisi yamshambulia Sitta

      Kubenea, Kibanda na wengine tunawapongeza kwa jitihada zenu na muendelee kuwafinua hawa wanafiki wajiunge na kundi la mafisadi wenzao kina JK, Rachael na wengine. tukiwaacha ni kusema mtama nao ni mahindi shambani kws kuwa zote zina rangi ya kijani.
      ETI KUANIKA UNDUMILA KUWILI WA SITA eti umeajiriwa na Rachael. Navojua na Kibanda. kubenea hawawapambi kina sita vilevile wanawachana Rachael vilevile. Wakina sita wajue hakuna kuuma na kupuliza. ukiamua kuwa mpiganaji wa ufisadi uwe hivo sio unapigana ukiona wenzako wanagawiana mibrifkesi ya pesa unaacha kupigana unaenda kujipanga upewe cheo na hao mafisadi ili ule. Pumbaff!!!!!!!!!!!

    17. #214
      Alwatan's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th May 2009
      Posts : 391
      Rep Power : 587
      Likes Received
      105
      Likes Given
      186

      Default Re: MwanaHalisi yamshambulia Sitta

      Quote By Thesi
      Kubenea, Kibanda na wengine tunawapongeza kwa jitihada zenu na muendelee kuwafinua hawa wanafiki wajiunge na kundi la mafisadi wenzao kina JK, Rachael na wengine. tukiwaacha ni kusema mtama nao ni mahindi shambani kws kuwa zote zina rangi ya kijani.
      ETI KUANIKA UNDUMILA KUWILI WA SITA eti umeajiriwa na Rachael. Navojua na Kibanda. kubenea hawawapambi kina sita vilevile wanawachana Rachael vilevile. Wakina sita wajue hakuna kuuma na kupuliza. ukiamua kuwa mpiganaji wa ufisadi uwe hivo sio unapigana ukiona wenzako wanagawiana mibrifkesi ya pesa unaacha kupigana unaenda kujipanga upewe cheo na hao mafisadi ili ule. Pumbaff!!!!!!!!!!!
      Naona una bidiii kweli kuwaonesha nawewe unatetea mafisadi ili mambo yakikubali wakuvute jikoni nawe ule japo makombo... Kila la heri labda
      watakunotice.

    18. #215
      KIM KARDASH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 4,252
      Rep Power : 0
      Likes Received
      564
      Likes Given
      55

      Default Re: MwanaHalisi yamshambulia Sitta

      Quote By Thesi
      Kubenea, Kibanda na wengine tunawapongeza kwa jitihada zenu na muendelee kuwafinua hawa wanafiki wajiunge na kundi la mafisadi wenzao kina JK, Rachael na wengine. tukiwaacha ni kusema mtama nao ni mahindi shambani kws kuwa zote zina rangi ya kijani.
      ETI KUANIKA UNDUMILA KUWILI WA SITA eti umeajiriwa na Rachael. Navojua na Kibanda. kubenea hawawapambi kina sita vilevile wanawachana Rachael vilevile. Wakina sita wajue hakuna kuuma na kupuliza. ukiamua kuwa mpiganaji wa ufisadi uwe hivo sio unapigana ukiona wenzako wanagawiana mibrifkesi ya pesa unaacha kupigana unaenda kujipanga upewe cheo na hao mafisadi ili ule. Pumbaff!!!!!!!!!!!
      Umeongea vizuri sana,sipo hapa kumtetea sitta,kwanza hanijui wala sitaki kujuana nae na mimi simjui zaidi ya kumuona majukwaani,ila kubenea namjua ananijua yani tunajuana na tulikuwa wote kwenye upambanaji sasa ukiona mwenzako anatoka nje ya mstari na umefanya jitihada za kumrejesha anakua mkaidi ndio unakuja hapa jukwaani

    19. #216
      Ben Saanane's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th January 2007
      Posts : 6,699
      Rep Power : 32780
      Likes Received
      4970
      Likes Given
      6451

      Default Re: MwanaHalisi yamshambulia Sitta

      Quote By THE ROMANTIC
      We kweli uko mbali na ukweli,kubenea unamtenganisha vipi na ccm wakati ni mwanachama hai wa magamba lakini kama unavyojua ccm imegawanyika mara mbili,pro-magamba na anti-magamba,kubenea yeye kaamua kuchagua kundi la pro-magamba,ili upate picha na kuelewa zaidi nini nasema ntakutajia wajumbe angalau waandamizi wa magenge yote hayo mawili:

      CCM Pro magamba:genge la Lowassa

      1:Januari makamba

      2:Peter Serukamba

      3:Makongoro mahanga

      4:James ole millya

      5:Msomali Bashe

      6:Benno Malisa

      7:Said kubenea

      8:Absalom kibanda(huyu sio ccm naona "kiu ya maendeleo" ya haraka imemsukuma)

      9:Freddy Lowassa

      10:Rostam Aziz

      11:Beatrice Shelukindo(huyu nae kiu ya uwaziri alioahidiwa na lowassa ndio imempeleka huko,akamsaliti hata mumewe mzee shelukindo)

      CCM anti-magamba

      1:Nape Nnauye

      2:Sam Six

      3:John Magufuli

      4:John Chiligati

      5:wakuu wote wapya wa mikoa walioteuliwa hivi karibuni

      6:Wazee wa nyerere foundation

      7:Bernard Membe

      8:Harrison Mwakyembe

      9:Lazaro Nyalandu(huyu anasukumwa na kiu ya kuutaka urais,unajua wengi wameona kama jk ameweza kuwa rais basi kila m2 anaweza)

      Angalau kwa uchache muwafahamu hao.
      Duh.......! Hadi haya unayajua mkuu?

      Quote By fmpiganaji
      mkuu kwanini anapotajwa Zitto unakasirika mpaka kupandisha povu? Mwanahalisi ndilo gazeti bora Tanzania.
      Wewe Inakukera nini ?Mwache atoe mawazo yake......!
      Wametuonyesha Jeuri ya ukaburu,tuwaonyeshe jeuri ya Umkhontho we sizwe kupitia Red Brigade.Tukiwaonyesha woga wetu, itakua silaha imara zaidi kwao kutumaliza-Ben Saanane

    20. #217
      KIM KARDASH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 4,252
      Rep Power : 0
      Likes Received
      564
      Likes Given
      55

      Default Kubenea amtukana samuel sitta!!!!!!!!!!!!!!

      Shutuma za Sitta dhidi ya Kubenea kwamba sasa kanunuliwa na mafisadi kama alivyozitoa katika kipindi chake katika ITV zimejibiwa na na gazeti hilo wiki hii katika tahriri yake iliyoanzia ukurasa wa mbele.

      Kubenea anataka kuonekana ni jembe lisilotetereka katika kuwaumbua mafisadi na wale wanaofuatilia kwa makini stori za gazeti hilo watagundua kwamba hana marafiki, na hasa wa mafisadi, wapambe wao na wote wale manafiki wanaojifanya kuupiga vita ufisadi, kumbe wao ndiyo mafisadi wakuu.

    21. #218
      Game Theory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th September 2006
      Posts : 10,054
      Rep Power : 3352
      Likes Received
      238
      Likes Given
      0

      Default Re: Kubenea amtukana samuel sitta!!!!!!!!!!!!!!

    22. #219
      Mbopo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2008
      Posts : 2,531
      Rep Power : 1083
      Likes Received
      375
      Likes Given
      13

      Default Re: Kubenea amtukana samuel sitta!!!!!!!!!!!!!!

      Quote By THE ROMANTIC
      Shutuma za Sitta dhidi ya Kubenea kwamba sasa kanunuliwa na mafisadi kama alivyozitoa katika kipindi chake katika ITV zimejibiwa na na gazeti hilo wiki hii katika tahriri yake iliyoanzia ukurasa wa mbele.

      Kubenea anataka kuonekana ni jembe lisilotetereka katika kuwaumbua mafisadi na wale wanaofuatilia kwa makini stori za gazeti hilo watagundua kwamba hana marafiki, na hasa wa mafisadi, wapambe wao na wote wale manafiki wanaojifanya kuupiga vita ufisadi, kumbe wao ndiyo mafisadi wakuu.
      Gazeti la lini hilo?

    23. #220
      ukwelikitugani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th October 2010
      Posts : 659
      Rep Power : 567
      Likes Received
      294
      Likes Given
      854

      Default

      Quote By THE ROMANTIC
      Shutuma za Sitta dhidi ya Kubenea kwamba sasa kanunuliwa na mafisadi kama alivyozitoa katika kipindi chake katika ITV zimejibiwa na na gazeti hilo wiki hii katika tahriri yake iliyoanzia ukurasa wa mbele.

      Kubenea anataka kuonekana ni jembe lisilotetereka katika kuwaumbua mafisadi na wale wanaofuatilia kwa makini stori za gazeti hilo watagundua kwamba hana marafiki, na hasa wa mafisadi, wapambe wao na wote wale manafiki wanaojifanya kuupiga vita ufisadi, kumbe wao ndiyo mafisadi wakuu.
      Hujui ulisemalo. Nchi hii balaa tupu. Mafisadi wanajuana kwa majina kuanzia Lowasa hadi Zitto,mkullo hadi sitta,Kubenea hadi Rostam. Ubatili mtupu

    24. Miaka 50
    Page 11 of 12 FirstFirst ... 9101112 LastLast

    Similar Topics

    1. Replies: 23
      Last Post: 11th February 2011, 16:50
    2. Replies: 0
      Last Post: 20th November 2010, 08:18

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...