JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

  Report Post
  Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast
  Results 21 to 40 of 60
  1. Mzee Mwanakijiji's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2006
   Location : Kijijini
   Posts : 32,118
   Rep Power : 87995664
   Likes Received
   24671
   Likes Given
   13382

   Default Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Baada ya kupigia kelele rasimu ya kwanza Serikali iliondoa mswada na kwenda kuufanyia marekebisho mbalimbali. Je kilio cha Watanzania kimesikika na hoja tulizozitoa wakati ule zimezingatiwa? Binafsi sijapata muda wa kusoma - ndio nimepata tu mswada huu - lakini natumaini wengijne watapitia na kutoa maoni yao kama ni mswada unaofaa kusimamia uandishi wa Katiba yetu mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015. Jipatie nakala yako.

   Mswada uliokataliwa Aprili 2011: BONYEZA HAPA

   Mswada Mpya wa Oktoba 2011: BONYEZA HAPA
   Last edited by Mzee Mwanakijiji; 26th October 2011 at 12:05.
   [email protected]
   The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

  2. Ngonini's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st September 2010
   Posts : 2,016
   Rep Power : 5776
   Likes Received
   556
   Likes Given
   43

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
   Baada ya kupigia kelele rasimu ya kwanza Serikali iliondoa mswada na kwenda kuufanyia marekebisho mbalimbali. Je kilio cha Watanzania kimesikika na hoja tulizozitoa wakati ule zimezingatiwa? Binafsi sijapata muda wa kusoma - ndio nimepata tu mswada huu - lakini natumaini wengijne watapitia na kutoa maoni yao kama ni mswada unaofaa kusimamia uandishi wa Katiba yetu mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015. Jipatie nakala yako.

   Mswada uliokataliwa Aprili 2011: BONYEZA HAPA

   Mswada Mpya wa Oktoba 2011: BONYEZA HAPA

   Wakuu mimi kwanza naanza na Title="Constitutional Review Act". Are we reviewing or are we making a new constitution? Sijui ya kiswahili inasemaje maana sijaiona.

  3. Ngonini's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st September 2010
   Posts : 2,016
   Rep Power : 5776
   Likes Received
   556
   Likes Given
   43

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Na hiki kipengele cha Rais mpaka ajiridhishe na hali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ndipo afanye maamuzi ya kuunda tume ya katiba ni sawa? Au ndo wametutega waje kutukia kipengele hiki kuchelewesha katiba mpya kwa madai hali ya kiuchumi si nzuri mwaka huu?

  4. Rweye's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th March 2011
   Posts : 10,041
   Rep Power : 0
   Likes Received
   2341
   Likes Given
   0

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Jamani jamani jamani...miezi6 yote mvinyo ni uleule kwenye birika sasa make ule wa awali ulikuwa kwenye chupa..niulize tu,hivi rais wetu ni kiziwi,kiwete,tahira ama ni dharau?anadharaudharau tu.

   Na asubiri aone hata kwa Ocampo hatafika huyu tayari tutakuwa tumemlaza na Gaddafi jangwani

  5. ntamaholo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2011
   Location : Mwilavya
   Posts : 6,566
   Rep Power : 2141
   Likes Received
   1561
   Likes Given
   505

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Quote By mzee mwanakijiji View Post
   naona kulikuwa na shida kwenye attachment ya hapa. Ila angalia post ya awali nimeweka link ya miswada yote miwili - ule uliokataliwa mwanzoni na huu wa sasa. Na kwa vile umendikwa kwa lugha nyepesi tu ya kiingereza unahitaji uelewa tu nadhani wa pili upo kwa kiswahili pia.
   mkuu bado sijaipata. Natamani niipate, naiprint copy za kutosha na kuwapelekea wananchi mtaani kwangu, tuisome na tuijadili.
   UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

  6. ntamaholo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2011
   Location : Mwilavya
   Posts : 6,566
   Rep Power : 2141
   Likes Received
   1561
   Likes Given
   505

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
   Baada ya kupigia kelele rasimu ya kwanza Serikali iliondoa mswada na kwenda kuufanyia marekebisho mbalimbali. Je kilio cha Watanzania kimesikika na hoja tulizozitoa wakati ule zimezingatiwa? Binafsi sijapata muda wa kusoma - ndio nimepata tu mswada huu - lakini natumaini wengijne watapitia na kutoa maoni yao kama ni mswada unaofaa kusimamia uandishi wa Katiba yetu mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015. Jipatie nakala yako.

   Mswada uliokataliwa Aprili 2011: BONYEZA HAPA

   Mswada Mpya wa Oktoba 2011: BONYEZA HAPA
   Bonyezeni kwenye neno HAPA, bolded green
   UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

  7. Mbalinga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th April 2010
   Posts : 1,077
   Rep Power : 810
   Likes Received
   254
   Likes Given
   9

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Mswaada huu wa October hauna tofauti sana na ule wa April, ninachoona wamejitahidi kukifanya ni kuiingiza sana Zanzibar. Mwanasheria mkuu wa Zanzibar atahusishwa kwa kila kitu na Rais wa Zanzibar pia tofauti na ule wa mwanzo.

   Hii ina maana ni lazima tuukatae tena kwani huu ni mzaha, maoni na mawazo yote ya wadau na wasomi yamezikwa.

   CDM jiandaeni huu ndio wakati wa kuonyesha nguvu ya umma. Tumekataa tena.

  8. #27
   Ame's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th March 2011
   Location : Global Citizen
   Posts : 2,139
   Rep Power : 27620172
   Likes Received
   972
   Likes Given
   3023

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Quote By Masanja View Post
   Mwanakijiji,

   Mimi personally huu mswada nimeusoma na kuuelewa. Serikali is really being clever. Wameuma na kupuliza. How? kwanza Constitution Commissioners watateuliwa na rais kwa kushauriana na rais wa Zanzibar. Hapa nadhani ndo penye tatizo kwa sababu Rais anajua fika kwamba anaweza kuteua team yoyote anayoona ita-bend kwenye matakwa ya chama na serikali. Hapo naona hajatutendea haki watanzania. Ushauri wangu: Hii tume ya kurekebisha katiba ingeundwa na watu mbali mbali. Hata kama rais atateua wajumbe, lakini vile vile sheria imuamuru kushauriana na makundi mbali mbali especially vyama vya upinzani. Kwa sababu composition ya tume ndo kila kitu.

   Pili, sheria inampa mamlaka rais ya kuteua Constitutent Assembly (baraza la katiba). Hapa serikali imetupiga changa la macho kwa nini? Kwa sababu, sheria inasema kwamba wabunge wote (bara na visiwani) watakuwa wajumbe wa hii Constituent Assembly-automatically!. Hapa ni dhahiri kwamba hili bunge la katiba litakuwa dominated na wabunge wa CCM. Fair enough kwa watanzania, sheria inatoa nafasi 116 kwa 'wadau mbali mbali' kutoka makundi kama dini, NGOs, vyama vya siasa nk. kuingia kwenye Constituent Assembly (baraza la katiba). Sasa hapa tunadanganywa kwa sababu kiukweli ni kwamba watanzania wa kawaida ambao ndo hii katiba inaandikwa kwa niaba yetu tutakuwa na wawakilishi 116 tuu! (maana wabunge watawakilisha maslahi ya vyama vyao-as experience has shown). Halafu vile vile, sijui wametumia vigezo gani kuamua kwamba kuwe na wajumbe 116. Hapa panahitaji majibu.

   To be fair, serikali imeweka 'referendum' kama nafasi ya wananchi kupiga kura ya kuikubali au kuikataa katiba mpya. This is a very good component and I applaud my government. Lakini kiukweli, uwakilishi wetu sisi wananchi kwenye utengenezaji wa hii katiba ni mdogo sana. Na kama mswaada utapitishwa kama ulivyo basi ni dhahiri, katiba ita-reflect matakwa ya CCM. Maana to be fair to the opposition, ni wachache sana kuweza kuweka maslahi na mategemo ya wengi mbele.

   Ushauri wangu: Huu mswada, una mapungufu ambayo kama yangefanyiwa kazi ingetusaidia kuwa na katiba nzuri inayoendana na matakwa na maoni ya wananchi walio wengi. Otherwise, wale wote ambao hawakubaliani na huu mswada nafasi yao ya pekee ni kuipinga katiba wakati wa referendum. Kitu ambacho kwangu mimi naona kingetafutiwa ufumbuzi kwa kuhakikisha kwamba kuanzia mwanzo mchakato wa katiba unawashirikisha wengi.

   Maoni yangu ni hayo,

   Masanja
   Mine interest was also the same kuhusu tume nani anaiteua then nikaona wameongeza tu vi maneno huko juu ya ile ya kwanza and the part three context remained as it is bila amendment yoyote wakati ndichokilichopigiwa kelele sana wakati waki table for the first time. Huu ujanjaujanja na usanii hautufikishi popote. Hii nchi ni yetu sote tukubali kuwa objective tu kwa faida ya wote.

  9. #28
   Ame's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th March 2011
   Location : Global Citizen
   Posts : 2,139
   Rep Power : 27620172
   Likes Received
   972
   Likes Given
   3023

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
   Kama watu wanaona kuwa mambo muhimu hayamo kwenye mswada huu ni wa kuukataa tu. Ni bora watu wasubiri chama ambacho kitakuja kuandika katiba mpya kwa misingi ya uwazi, usawa, demokrasia na utu wa Watanzania kuliko kuburuzwa kwa sababu watu wanataka Katiba Mpya. Tusiburuzwe kwani tutakachoandika ndio urithi wetu kwa kizazi kijacho.
   The main problem with the bill ni kuwa the powers vested into individuals which is the main problem/complain to the existing katiba is still confered to these very individuals kiasi ambacho hakuna jinsi ya kuweka effective checks and balances to their individual/groups/party's biases. How can three people (From the same idealogy in reference to political parties) decide on behalf of all Tanzanians which are about 20 millions of udults for who are good representative in terms of their capabilities and preferences to coordinate us into taking our preferences which would determine a type of katiba we want? Tanzanians let us be serious....

  10. #29
   Welu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th July 2011
   Posts : 691
   Rep Power : 16230
   Likes Received
   168
   Likes Given
   33

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Wanakosea makusudi ili kila mara uwe unarudishwa ili siku ziwe zinaenda (delay technic). Nadhani tuweke ukomo.

  11. Mp Kalix2's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th October 2010
   Posts : 3,425
   Rep Power : 97573
   Likes Received
   1163
   Likes Given
   280

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Asante mkuu.
   Ni kosa la kimfumo kwa Raisi wa Nchi kuwa Mwenyekiti chama cha Kisiasa.Serikali ya Majimbo muwaarobaini wa Muungano wetu!

  12. #31
   Nono's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th February 2008
   Location : Bulyanhulu
   Posts : 1,203
   Rep Power : 947
   Likes Received
   206
   Likes Given
   122

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Mimi sioni kilichocha maana katika Muswada huu. Huu ni Muswada wa Rais na ccm kwa ajili ya kuandaa katiba ya kuibeba ccm kwa miaka kadhaa ijayo, na sio kuwasaidia watanzania kujitengenezea taifa lao na kujiletea maendeleo. Naiona huu mchakato ukiwa mbaya hata kuliko wa kuunda katiba ya ccm yenyewe, kwani kwa ndani lazima mawazo ya wanachama yazingatiwe.

   Sielewi pale anaposema kuwa uwakilishi wa wajumbe utakuwa sawa kwa pande zote za muungano. Huu utakuwa ni uwiano kulingana na ukubwa wa nchi, watu au vipi?

   Rais wa Muungano (ccm) kwa kushirikiana na rais wa zenj (ccm) wakisaidiwa na mawaziri (ccm) wanaasisi na kuunda tume kwa kuchagua wajumbe kadri wanavyoona inafaa. Hakuna mahali popote inaposemekana kuwa hawa watu kuwa watathibitishwa na vyombo huru (hususan bunge). Yet wote hawa wanaapishwa na rais, japo anasema hana mamlaka kuingilia utendaji wake wa kazi.

   Uteuzi wa bunge la katiba ndio mbaya zaidi kwani wajumbe wote ukiacha wale wataotokana na vyama vya siasa, asasi chache za kijamii na wabunge wasiokuwa wa ccm, wataendelea kuwa wenye mlengo uleule wa kuibeba ccm kuendelea kuitawala na sio kuiongeza nchi. Utaratibu gani uliotumika kuyapitisha mabunge yaliyopo ya ccm kutengeneza bunge la katiba? Hao 116 walipatikana vipi na watawakilishaje matakwa ya watanzania waliobaki ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa nje ya ccm?

   Tume ile ile inayolalamikiwa zaidi ya miaka 20 kuwa imeendelea kuibeba ccm ndio hiyo hiyo itakayoendeleza chaguzi zile zile za wizi, ambazo mswada huu hauonyeshi kuwa zinaweza kuhojiwa wapi.

   Katika kipengele cha kura wanasema kuwa upnade utashinda endapo sehemu zote za muungano zitafikisha zaidi ya kura 50%, lakini hazisemi kuwa upande mmoja (bara au visiwani) usipotimiza 50% nini kitafanyika.

   Kwa ujumla mchakato huu unaweza kuleta katiba mbaya kuliko; huenda ni mpango wa kutengeneza katiba ya kuwalinda wafalme na watoto wao bila kusahau matakwa ya mafisadi!

  13. Tutafika's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th November 2009
   Posts : 1,182
   Rep Power : 962
   Likes Received
   448
   Likes Given
   247

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Ngoja nirekebishe miwani nisome vizuri

  14. Ngonini's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st September 2010
   Posts : 2,016
   Rep Power : 5776
   Likes Received
   556
   Likes Given
   43

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   kuna mzaha mkubwa unafanywa na hawa watu. Sisi tumeona mfano kule Tunisia. Kuna ugumu gani tukipiga kura kuchagua tume na wabunge wa baraza katiba? Hiki kitu muhimu kuliko hata uchaguzi wa Raisi na wabunge maana ndo mama wa yote. Na shida tulizonazo leo ni kwasababu wananchi tumeporwa nguvU yetu na kupewa watawala. Tunataka katiba mpya irejeshe nguvu hiyo kwetu ili tupambane na watawala wabovu kama hawa wa leo.

  15. Mp Kalix2's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th October 2010
   Posts : 3,425
   Rep Power : 97573
   Likes Received
   1163
   Likes Given
   280

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Tayari wameshanichosha na kunipotezea ladha ya kuusoma mswada wenyewe.
   Angalia na soma sect.2
   '' This Act shall come into operation on 1st December 2011''.
   Huwa na shindwa kuelewa hawa mabwana ni wasomi wa aina gani.Huu ni mswada tu na tayari umekwisha halalishwa kuwa utaanza kutumika 1/12/2011 bila hata kufika Bungeni.Kweli NCHI !!!!!!!!!!!!!!!!!!
   Nitarudi kwa maoni zaidi ngoja ni pooe kwanza koo.
   Last edited by Mp Kalix2; 26th October 2011 at 21:57. Reason: correction
   Ni kosa la kimfumo kwa Raisi wa Nchi kuwa Mwenyekiti chama cha Kisiasa.Serikali ya Majimbo muwaarobaini wa Muungano wetu!

  16. Kiungani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd February 2007
   Location : Nabangaiza huku na kule
   Posts : 310
   Rep Power : 827
   Likes Received
   57
   Likes Given
   1

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
   Kama watu wanaona kuwa mambo muhimu hayamo kwenye mswada huu ni wa kuukataa tu. Ni bora watu wasubiri chama ambacho kitakuja kuandika katiba mpya kwa misingi ya uwazi, usawa, demokrasia na utu wa Watanzania kuliko kuburuzwa kwa sababu watu wanataka Katiba Mpya. Tusiburuzwe kwani tutakachoandika ndio urithi wetu kwa kizazi kijacho.
   Binafsi, haya ndiyo maoni na mtazamo wangu.

   Nimekuwa naufuatilia sana na kuzungumza na watu mbalimbali kuhusu huu mchakato au msukumo wa kubadili Katiba. Sikubaliani na huo msukumo.

   Mimi mawazo yangu ni kuwa, tuendelee na Katiba hii iliyopo na tusukumane hivyo hivyo hadi mabadiliko ya kweli, siyo tu katika uongozi wa taifa/bunge uwepo, bali hadi mabadiliko ya kweli katika ngazi za chini yatakapokuwepo.

   Kukazania kubadili Katiba katika misingi hii ya utawala wa sasa, ni kuzidi kujinyonga tu kwa kupewa kamba fupi.

   Tuchukue mifano ya Kenya, Rwanda, Ukraine, Afrika Kusini, Zambia, Urusi (Gorbachev), Nigeria (Obasanjo), Poland (Walesa), na kwingineko.
   Hizi nchi kwa wakati mmoja au mwingine, tawala zilizokuwepo zilipinga na kukataa sana kubadili Katiba zao kwa kuwa ziliweka misingi katika hizo Katiba iliyokuwa inawasaidia kuendelea kuwepo. Mabadiliko ya utawala yalipelekea kuwepo uwanja mpana wa kubadilisha Katiba zao, kiasi kwamba waliokuwa watawala wanashindwa au wameshindwa kurudi tena madarakani.

   Tunaona Kenya jinsi TANU ilivyofifia na kudhoofika, NP ya akina Botha/De Clerk Afrika Kusini wala haisikiki tena, UNIP ya Zambia imebaki jina, n.k. Hivi vyote ni vyama ambavyo viling'angania Katiba kandamizi kama ambavyo CCM inafanya sasa. Vyama hivi vilipoachia madaraka, Katiba zao wenyewe ziliwakandamiza na kuwamaliza kabisa. Mabadiliko ya Katiba yaliyofuatia, yalihakikisha kuwa vipengele vilivyowapa nguvu vimeondolewa na hivyo kupelekea kufa au kufifia sana kwa vyama hivyo.

   Kwa hiyo, kwa mtazamo wangu hili ni muhimu lifanyike hivyo ili kuhakikisha kuwa muda muafaka utakapofika basi chembe chembe za masalia ya utawala wa sasa, zitaondoka na kupotea kabisa kwanza kwa kutumia Katiba hiyo hiyo kandamizi, na pili kwa kuondoa au kuweka vipengele vinavyoondoa udhalimu.
   "PCCB ndani ya CCM ni kama sisimizi........." John Guninita, Mwenyekiti CCM Mkoa Dar (3 Feb 2012)

  17. Julius Mtatiro's Avatar
   Member Array
   Join Date : 20th June 2009
   Posts : 43
   Rep Power : 645
   Likes Received
   169
   Likes Given
   1

   Default Muswada mpya wa kuanza mchakato wa katiba mpya huu hapa - nao umechakachuliwa, by julius mtatiro

   Wadau,
   Baada ya kuukataa muswada wa sheria ya uundwaji wa tume maalum itakayoshughulika na kukusanya maoni ya wananchi ili kuleta katiba mpya, Serikali imeandaa muswada mwingine ambao ndio utawasilishwa bungeni hivi karibuni.
   Muswada huu mpya umeingiza mambo kadhaa ambayo wadau waliyalalamikia kama vile:
   1. Ushiriki sawa wa rais wa Zanzibar katika uteuzi kama ilivyo kwa rais wa muungano.
   2. Muswada kuwa katika lugha za kiswahili na Kiingereza.
   3. Kuwepo kwa bunge la katiba(japo wamelichanganya na wabunge wa sasa na wajumbe wa baraza la wawakilishi wa sasa).
   4. Time frame zinazoeleweka kidogo n.k

   Tatizo kubwa ambalo tunalikataa na bado serikali imelirudisha ni madaraka ya rais katika uundaji wa katiba mpya. u-Rais wa Tanzania ni cheo kinacholalamikiwa kuwa na madaraka makubwa mno, na sasa katika uandikaji wa katiba ya watanzania wote bado rais anapewa kusimamia kila kazi inayohusiana na katiba hii.

   Tume ya taifa ya uchaguzi NEC na tume ya taifa ya uchaguzi ya Zaznibar ZEC bado zinapewa mamlaka yaleyale ya kusimamia masuala ya kura za maoni za wananchi wakati wa kupitisha katiba.

   Serikali ya CCM ina kichwa kigumu sana, haisikii wala kusikiliza. Yaani tume ile ile inayochakachua matokeo ya uchaguzi kila kukicha ndiyo inapewa kazi ya kusimamia suala muhimu la katiba. Tume ya rais, katiba ya rais,nchi ya rais.

   Ati mkuu wa wilaya, mtendaji wa kata,mtendaji wa kijiji na mtendaji wa mtaa ndio wanapewa kazi ya kusimamia taratibu za ukusanyaji wa maoni ngazi ya chini, ARE WE SERIOUS?

   Kwani mpaka watu wabebe bunduki ndiyo serikali ione wananchi wanahitaji katiba mpya ya wananchi na siyo ya rais, DC,WEO,VEO,NEC,ZEC n.k?

   Hivi ikulu ina hofu gani ikitengeneza utaratibu wa uhakika na wa haki wa kuleta katiba mpya? Kwa nini kila jambo katika kuleta katiba anapewa rais, kwa nini tusiunde tume maalum itakayoteuliwa kwa utaratibu maalum ikiwa na watu maalum ambao hata upatikanaji wao utatokana na uadilifu wao na watu hao watahojiwa kikamilifu live mbele ya watanzania wote katika televisheni n.k?

   Kuna biashara gani katika ku-complicate hivi suala la katiba? Kwani serikali haijui ma-WEO, VEO, NEC, ZEC, DC, RAIS na kadhalika ni watu ambao wamelaumiwa sana kwa udhaifu mkubwa ambao wamekuwa wakiuonesha katika chaguzi mbalimbali na katika utendaji wao kwa ujumla kwa maana ya kuisaidia CCM?

   Hivi sasa nchi inayumba sana kiuchumi, mfumuko wa bei, matatizo ya umeme na mauchafu kedekede, kwa nini rais wetu asishughulikie haya suala la katiba likawekwa katika mikono ya watu safi wanaoaminiwa na jamii ya watanzania?

   Wasiwasi wangu ni kwamba, CCM wana hofu kuwa tukipata katiba ya haki ya ukweli ya maadili ya dira safi - wanajua wataondoka madarakani immediately. Lakini njia ya mwongo ni fupi sana, hii katiba ya RAIS na IKULU yake na chama CHAKE, tutaipinga kwa nguvu zote.

   Kwa bahati mbaya hapa duniani, tangu ulimwengu uumbwe, haijawahi kutokea SERIKALI na MAJESHI yaliyowashinda wananchi wenye kiu ya haki na mabadiliko ambavyo ni haki yao.

   TEMBELEENI TOVUTI YA BUNGE ,SOMENI KWA MAKINI - SOTE TUCHUKUE HATUA KWANI KATIBA HII SIYO YA MTU MMOJA NA FAMILIA YAKE NA MARAFIKI ZAKE, NI KATIBA YETU SOTE, WATANZANIA!

   Julius Mtatiro,
   26 Oktoba 2011.
   Wengi wetu hatupendi kuambiwa ukweli,SIASA SIYO MECHI YA SIMBA NA YANGA!

  18. ntamaholo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2011
   Location : Mwilavya
   Posts : 6,566
   Rep Power : 2141
   Likes Received
   1561
   Likes Given
   505

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   kati ya mambo yaliyopelekea kudai katiba mpya ni
   1. Mamlaka ya Rais kuteua teua. Hii huwafanya wateule kuwajibika kwa aliyewateua.
   Sasa muswada huu, unampa Rais nafasi ya kumteua wajumbe wa tume na pia kumteua katibu wa secretariat ya tume huku kilaza Kombani akipewa nafasi ya kukamilisha wajumbe wengine wa secretariat ya tume yaani katibu msaidizi na wajumbe wengine. Mbaya zaidi, wote wataapa kwa rais. kosa kubwa hili na tusitegemee katiba inayokidhi haja.
   2. Baadhi ya makundi mhimu ya jamii yameenguliwa kuwepo kwenye tume. Niwatakao ni viongozi wa vyama vya siasa ambao kuanzia ngazi ya wilaya, wamepigwa ban. kuna mambo mazuri ambayo yanawafanya siku zote kulalamika, na sidhani kuenguliwa kwao mawazo yao yatapatikana vipi na kuingizwa kwenye rasimu ya katiba.
   lakini pia, watumishi wa umma katika idara za usalama wameenguliwa. Siku zote sheria ikiuundwa bila kuwashirikisha watu hawa, hasa POLISI walio na dhamana ya kusimamia sheria moja kwa moja, ndiyo hupelekea mauaji mengi na kuliacha jeshi katika kashifa ambazo kimsingi zimeaandaliwa na wengine, polisi wanatekeleza tu. hivyo kupigwa ban taasisi hii, nadhani tume itakosa mwongozo mzuri wa namna gani kuepuka matatizo katika jamii.
   Rai yangu ni kwamba, katiba ni ya watu wote hivyo ni mali ya jamii. kwa hivyo ili kuleta uwiano uliosawa, taasisi zote zilizopo kwenye jamii, zihusishwe na hili litawezekana kwa kuwapata wataalamu watakao pendekezwa na wadau wa taasisi husika na sio rais/waziri komabani.

   IUNDWE TASK FORCE, itakayojumuisha watu kutoka taasisi zote zilizopo kwenye jamii na kupatikana kwao, rais/waziri wasihusike kabisa bali taasisi zenyewe kwa kuwajua members wao ndio wahusike.

   Mwisho, nina mashaka kwa taarifa kupelekwa kwa raisi.........
   UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

  19. ntamaholo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2011
   Location : Mwilavya
   Posts : 6,566
   Rep Power : 2141
   Likes Received
   1561
   Likes Given
   505

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Quote By Kiungani View Post
   Binafsi, haya ndiyo maoni na mtazamo wangu.

   Nimekuwa naufuatilia sana na kuzungumza na watu mbalimbali kuhusu huu mchakato au msukumo wa kubadili Katiba. Sikubaliani na huo msukumo.

   Mimi mawazo yangu ni kuwa, tuendelee na Katiba hii iliyopo na tusukumane hivyo hivyo hadi mabadiliko ya kweli, siyo tu katika uongozi wa taifa/bunge uwepo, bali hadi mabadiliko ya kweli katika ngazi za chini yatakapokuwepo.

   Kukazania kubadili Katiba katika misingi hii ya utawala wa sasa, ni kuzidi kujinyonga tu kwa kupewa kamba fupi.

   Tuchukue mifano ya Kenya, Rwanda, Ukraine, Afrika Kusini, Zambia, Urusi (Gorbachev), Nigeria (Obasanjo), Poland (Walesa), na kwingineko.
   Hizi nchi kwa wakati mmoja au mwingine, tawala zilizokuwepo zilipinga na kukataa sana kubadili Katiba zao kwa kuwa ziliweka misingi katika hizo Katiba iliyokuwa inawasaidia kuendelea kuwepo. Mabadiliko ya utawala yalipelekea kuwepo uwanja mpana wa kubadilisha Katiba zao, kiasi kwamba waliokuwa watawala wanashindwa au wameshindwa kurudi tena madarakani.

   Tunaona Kenya jinsi TANU ilivyofifia na kudhoofika, NP ya akina Botha/De Clerk Afrika Kusini wala haisikiki tena, UNIP ya Zambia imebaki jina, n.k. Hivi vyote ni vyama ambavyo viling'angania Katiba kandamizi kama ambavyo CCM inafanya sasa. Vyama hivi vilipoachia madaraka, Katiba zao wenyewe ziliwakandamiza na kuwamaliza kabisa. Mabadiliko ya Katiba yaliyofuatia, yalihakikisha kuwa vipengele vilivyowapa nguvu vimeondolewa na hivyo kupelekea kufa au kufifia sana kwa vyama hivyo.

   Kwa hiyo, kwa mtazamo wangu hili ni muhimu lifanyike hivyo ili kuhakikisha kuwa muda muafaka utakapofika basi chembe chembe za masalia ya utawala wa sasa, zitaondoka na kupotea kabisa kwanza kwa kutumia Katiba hiyo hiyo kandamizi, na pili kwa kuondoa au kuweka vipengele vinavyoondoa udhalimu.

   Kati ya vitu vinanyotugharimu leo, ni kwa kuwa rais anamamlaka makubwa yeye na mawaziri wao, kuteua watu wanaowataka na wanaowasaidia. mwisho wa siku mtu anaitwa mtumishi wa umma lakini hawajibiki kwa wananchi bali kwa raisi.

   tunacho hitaji kwa sasa, ni katiba itakayopokonya madaraka hayo ya waziri na rais. ili zile nafasi za kuteuliwa, zife kabisa, tuwe na mchakato wa kuwapata watumishi wa umma wanawajibika kwa wananchi. tukifikia hapa, tutakuwa na majeshi hur, tume za uchaguzi huru, watendaji serikalini huru ambao uhuru wao utawasaidia wananchi na si raisi kama ilivyo sasa
   UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

  20. ntamaholo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2011
   Location : Mwilavya
   Posts : 6,566
   Rep Power : 2141
   Likes Received
   1561
   Likes Given
   505

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Quote By Ngonini View Post
   kuna mzaha mkubwa unafanywa na hawa watu. Sisi tumeona mfano kule Tunisia. Kuna ugumu gani tukipiga kura kuchagua tume na wabunge wa baraza katiba? Hiki kitu muhimu kuliko hata uchaguzi wa Raisi na wabunge maana ndo mama wa yote. Na shida tulizonazo leo ni kwasababu wananchi tumeporwa nguvU yetu na kupewa watawala. Tunataka katiba mpya irejeshe nguvu hiyo kwetu ili tupambane na watawala wabovu kama hawa wa leo.
   ni sahihi Ngonini. uhuru wetu haupo tena, tunaishi si kama tutakavyo, bali kama wanasiasa watakavyo. hii ni mbaya mno. ona sasa kwa sababu hiyo, dowans inatutafuna, richmond lowasa anatutafuna, aggreco inatutafuan, buzwagi, ggm, na ndugu zao wanatufauna. kisa, madaraka makubwa ya rais na mawaziri wake. wanatutesa, tunakuwa watumwa ndani ya nchi yetu.
   UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

  21. ntamaholo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2011
   Location : Mwilavya
   Posts : 6,566
   Rep Power : 2141
   Likes Received
   1561
   Likes Given
   505

   Default Re: Rasimu ya Mswada wa Sheria ya Kuandika Katiba Mpya - The Proposed Constitutional Review Act

   Quote By Nono View Post
   Uteuzi wa bunge la katiba ndio mbaya zaidi kwani wajumbe wote ukiacha wale wataotokana na vyama vya siasa, asasi chache za kijamii na wabunge wasiokuwa wa ccm, wataendelea kuwa wenye mlengo uleule wa kuibeba ccm kuendelea kuitawala na sio kuiongeza nchi. Utaratibu gani uliotumika kuyapitisha mabunge yaliyopo ya ccm kutengeneza bunge la katiba? Hao 116 walipatikana vipi na watawakilishaje matakwa ya watanzania waliobaki ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa nje ya ccm?

   Kwa ujumla mchakato huu unaweza kuleta katiba mbaya kuliko; huenda ni mpango wa kutengeneza katiba ya kuwalinda wafalme na watoto wao bila kusahau matakwa ya mafisadi!
   bunge la katiba ni litakuwa baya zaidi. kwa maoni yangu, liundwe na watu huru kutoka katika jamii then kupunguza nmatumizi ya pesa za walipakodi, wabunge wa jamhuri waingie kwa uwakiishi sawa. kama watakuwa watano, basi wawe watano kila chama na vyama vingine ambavyo havina uwakilishi bungeni, wapewe nafasi sawa kabisa.
   UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

  Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast

  Similar Topics

  1. Breking Newz: Mswada wa sheria ya Katiba mpya kufutwa!
   By Yericko Nyerere in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 24
   Last Post: 27th November 2011, 01:46
  2. Jamanii tuanze kuandika rasimu ya katiba mpya
   By kaskas in forum KATIBA Mpya
   Replies: 1
   Last Post: 13th January 2011, 21:44
  3. Replies: 0
   Last Post: 3rd January 2011, 13:26
  4. rasimu ya Cuf kuhusu katiba mpya
   By Mallaba in forum KATIBA Mpya
   Replies: 0
   Last Post: 29th December 2010, 15:01
  5. Waislam waandaa rasimu ya katiba mpya
   By Luteni in forum KATIBA Mpya
   Replies: 6
   Last Post: 24th December 2010, 01:47

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...