Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

    Report Post
    Page 6 of 23 FirstFirst ... 4567816 ... LastLast
    Results 101 to 120 of 455
    1. #1
      NYAGI DRY's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 10th September 2011
      Posts : 151
      Rep Power : 419
      Likes Received
      34
      Likes Given
      2

      Default Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Tuhuma za kuuawa kwa Mwakyembe na wenzake kwa IGP na Mwandishi wetu FEBRUARI 8, mwaka huu, Dk. Mwakyembe alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.

      Baada ya maelezo hayo, polisi walimtaka aweke madai yake kwenye maandishi na siku moja baadaye Dk. Mwakyembe aliwasilisha taarifa yake ya maandishi.

      Dk. Mwakyembe amesema kwenye barua hiyo, “Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takriban mwezi moja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake (kwa maana ya wahusika na maudhui) hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.

      Maelezo ya Barua ya Mwakyembe “Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

      “Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea Januari 22, 2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa Januari 21, 2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 68… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 68…).

      Gari hiyo iliwateremsha “abiria” hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T7…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea. “Majina ya baadhi ya watu hao saba ni Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a “Master”; Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na mtu mwingine (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.

      “Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya (kaitaja) akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina (linahifadhiwa). Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda “kulogwa” safari hii.

      Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Willibrod), Anne Kilango - Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe. “Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyika, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.

      “Usiku wa Jumamosi Januari 22, 2011 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo, (kwa gari aina ya Defender STK 26…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga’ …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve With Impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni’ hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa’. Walirejea Songea Januari 29, 2011 na kesho yake Januari 30, 2011 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

      “Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T7… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo).

      Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T8… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro. “Kufuatana na ‘mganga’ mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza “waliohukumiwa kifo” (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).

      “Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu’ hao walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: Februari 5, 2011, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili: moja ya polisi (PT 02…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).

      Ushiriki wa Al Shabaab “Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al- Mujahideen (kwa kifupi Al- Shabaab). “Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini.

      Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati’ wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini la Uislamu kutishiwa.

      Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu. “Niliweza vilevile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao.

      Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. “Utabiri” huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo. “Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari).

      Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu’ yamefanywa: “(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi Februari 5, 2011 kwa “maandalizi” hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile ‘portion’ ya mganga ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni); “(b) Kesho yake (Jumapili) Februari 6, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T3… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).

      “Waliomo kwenye kikosi hicho ni Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a “Master” na kijana mmoja ambaye Januari 19, 2011 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T6…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.

      “Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji. “Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili.

      Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi: “Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T8… AQS) Januari 8, 2011 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa polisi Morogoro. “Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life.

      Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli ya….(jina la hoteli na mmiliki tunalo). “Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T8… AQS, VX Land Cruiser STK 1…, Mercedes Benz (Station Wagon) T8… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T2… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T6… APF, Nissan Patrol T8… ADH.”

      “Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata vyanzo vyangu vya habari ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.

      “Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani iko siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake wasitake, hakika ni suala la muda tu. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa taifa letu, taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.

      “Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

      “Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi’ niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia Kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji.”

    2. Miaka 50

    3. #101
      mashikolomageni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th January 2010
      Location : Dar es Salaam, Tanzania
      Posts : 1,445
      Rep Power : 766
      Likes Received
      144
      Likes Given
      130

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Asante

    4. #102
      mwaJ's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th September 2007
      Location : Nowhere
      Posts : 3,450
      Rep Power : 14608
      Likes Received
      2288
      Likes Given
      1501

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Mafisadi ni wabaya kuliko tunavyofikiri! Kama ni kweli ugonjwa wake utakuwa na uhusiano na taarifa aliyoitoa basi TZ kama taifa linaloheshimu uhuru wa kuabudu tumekwisha! Zaidi ya hapo, kama ni kweli basi suala wala si ukristu bali ni kelele wanazopiga baadhi ya walengwa kupinga ufisadi.

    5. BAK
      #103
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,597
      Rep Power : 44964
      Likes Received
      8345
      Likes Given
      8330

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!


      Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt.Harrison Mwakyembe wakati alipomtembelea nyumbani kwake Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam juzi.
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    6. #104
      Nzogupata's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th April 2011
      Posts : 70
      Rep Power : 425
      Likes Received
      11
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Ni wazi wakristo hapa nchini sasa wana hali ngumu sana. Unafiki wetu pia unatuumiza. Uchaguzi ilikuwa wazi ni ukristo vs uislam tukawapigia kura waislamu kwakudhani mungu ndo atawalipa kwa ubaya wao. Yameanza kutufika kwa viongozi wa juu waliowatetezi wetu na kwa ukristo wao watamalizwa kama chuo kikuu kimoja hapa nchini ambacho nacho kinatumika kukuza dini badala ya taaluma. Lecture theatres ni msikiti, jengo la utawala nalo linasehemu ni msikiti ambako baadhi ya wanataaluma wakiislamu hukutana for briefing.

      Badala ya kufanya kazi wanazolipwa mishahara watu wakobusy kukuza dini yao tu. Tunangoja mpaka wafe?

    7. #105
      Jayfour_King's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th November 2009
      Location : Tanzania
      Posts : 1,148
      Rep Power : 713
      Likes Received
      84
      Likes Given
      186

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Tanzania nchi ya amani na yenye kufuata utawala wa sheria !
      Wrong is a mirror for the rights

    8. FemaTV & Radio

    9. #106
      JIULIZE KWANZA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th November 2010
      Posts : 1,591
      Rep Power : 751
      Likes Received
      249
      Likes Given
      678

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Kwanini hakusema siri yote bungeni??????ni mnafiki japo ana haya kidogo ila wacha wapungue tuchue jimbo kule hawaibi kama igunga rip Dr.
      There shall be no peace without right for all...By Bob Marley.

    10. #107
      mugo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th October 2011
      Posts : 10
      Rep Power : 387
      Likes Received
      0
      Likes Given
      1

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Mungu tenda muujiza Dr mwakyembe na Prof mwandosya wapone katika Jina la Yesu jina lenye uponyaji na nguvu za giza zikashindwe kabisa

    11. #108
      mzee wa njaa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th June 2011
      Posts : 1,340
      Rep Power : 669
      Likes Received
      194
      Likes Given
      107

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Lisemwalo lipo na kama halipo linakuja...Kuna kitu kimefichwa nyuma ya pazia hapo mwisho wake uko karibu. Ugua Pole Dr. Mwakyembe.

    12. #109
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,084
      Rep Power : 12251
      Likes Received
      6014
      Likes Given
      6851

      Default

      Quote By Rev Fr Masanilo
      Mwakyembe anatafuta sympathy na cheap popularity...nimemshauri akafanye CD4 T cells count!
      call it like it is.... Apime defence yake kwanza ili ajiridhishe

    13. #110
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,084
      Rep Power : 12251
      Likes Received
      6014
      Likes Given
      6851

      Default

      Quote By Patricius
      Ukiona mtu anaandika matusi usimwelewe vibaya haya mambo yanayoendele katika nchi yetu ni ya ki§#k¤@*u€€$*ma.. Hivi ni nini mustakabali wa nchi yetu ktk hali hii mbona kama inaendeshwa na watu wasio WaTanzania??????
      Nani aniambie kwa hakika hatima ya nchi yetu????? Watu wanang'ang'ania Ushirikina tu badala ya haki na kujenga Taifa..... Unakera sana... Hici Kiwete wetu anafanya nini??????? kama ameshindwa si astepp down Bwana...
      ulianza vizuri na kumtaja mungu sasa unaongea matusi

    14. #111
      Game Theory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th September 2006
      Posts : 10,054
      Rep Power : 3353
      Likes Received
      240
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Kwa nini wakatibiwe india na sio muhimbili?

    15. #112
      Patriote's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th July 2011
      Posts : 1,349
      Rep Power : 1091
      Likes Received
      704
      Likes Given
      136

      Default Re: Kuhusu mwakyembe na mwandosya this can be true kabisa!

      Quote By Sniper
      Fanya editing kidogo ya habari yako, uweke na paragraphs, hii inakuwa ngumu sana kuisoma mpakaa mwisho.
      Hiyo habari ipo unedited hivyo hivyo kwenye gazeti. Labda ni style tu ya uandishi..

    16. #113
      Patriote's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th July 2011
      Posts : 1,349
      Rep Power : 1091
      Likes Received
      704
      Likes Given
      136

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Quote By Jayfour_King
      Tanzania nchi ya amani na yenye kufuata utawala wa sheria !
      Tatizo sheria za nchi yetu linapokuja suala la uchawi au matumizi ya manguvu ya giza ipo kimya sana. Watu wengi wameshapotezewa maisha kwa kupitia hayo manguvu ya giza. Nadhan kwenye huu mchakato wa katiba mpya tuweke kajiclause at least ka kuwatisha hawa maengineer wa hayo manguvu. Hivi hivi tutataumizana sana. Kama hayo manguvu ya giza yana manufaa chanya si watutatulie tatizo la umeme kwa kutumia hizo nguvu zao za giza????wenzetu technologia inawapeleka mbele, sisi technologia giza inaturudisha nyuma??mhhhh kaaz kweli kweli, Pole mpiganaji ukirecover toka huko magambani watakumaliza. Nlihisi siku nyingi kuwa hata kile cheo cha unaibu waziri kapewa strategically ili wamkamatie chini. Afu pia nahisi hawa wachawi hata ss watanzania kwa ujumla wetu wameshaturoga, mana sio bure! Response yetu kwenye sensitive issues (km malipo ya dowans, kagoda, meremeta, kiwira, deepn green, na mengine meng) kwa kweli inatia shaka sana.
      Last edited by Patriote; 11th October 2011 at 02:09.

    17. #114
      Chiwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th April 2008
      Posts : 421
      Rep Power : 650
      Likes Received
      76
      Likes Given
      133

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      du! kazi ipo lakini hakuna jinsi maisha ndivyo yalivyo siku zote wenye kutetea haki hawahitajiki! matajiri ni wachache ila wanatuvuruga kwa umaskini wetu kwa kweli hakuna mazingira yanyonishawishi kuwa huu haukuwa mpango. lakini kinachoniuma zaidi ni kushiriki kikamilifu kwa serikali tunayofikiria tunaitegemea.
      hata kama hatusali basi tutafakari wimbo wetu wa taifa
      kama ni kweli inaumiza sana na sielewi unapata faida gani kwa kuhusika na mauaji yasiyo na hatia.
      tukisema viongozi wetu mmnejiunga na dini za mashetani mnaanza na sisi sasa hiki ni nini sasa?

    18. #115
      Patriote's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th July 2011
      Posts : 1,349
      Rep Power : 1091
      Likes Received
      704
      Likes Given
      136

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Quote By MTM
      ulianza vizuri na kumtaja mungu sasa unaongea matusi
      Mambo yenyewe yanachanganyachanganya hadi muungwana anaweza kupoteza sifa na kuanza kumkufuru mungu, yani mambo yanakwenda dhohoflihali.

    19. #116
      Game Theory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th September 2006
      Posts : 10,054
      Rep Power : 3353
      Likes Received
      240
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      kwa nini wasitibiwe Muhimbili?

    20. #117
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,084
      Rep Power : 12251
      Likes Received
      6014
      Likes Given
      6851

      Default

      Quote By SlidingRoof
      kwa nini wasitibiwe Muhimbili?
      ili iweje? Would u go to muhimbili wakati umesharipoti yote hayo agaisnt serikali na uwt?

    21. #118
      Game Theory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th September 2006
      Posts : 10,054
      Rep Power : 3353
      Likes Received
      240
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Quote By MTM
      ili iweje? Would u go to muhimbili wakati umesharipoti yote hayo agaisnt serikali na uwt?
      yule ni waziri mwandamizi serikalini
      angeonyesha njia kuwa ni mzalendo na yuko tayai kutibiwa wanakotibiwa watanzania wengine

    22. #119
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,504
      Rep Power : 46710
      Likes Received
      16366
      Likes Given
      8423

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Quote By SlidingRoof
      yule ni waziri mwandamizi serikalini
      angeonyesha njia kuwa ni mzalendo na yuko tayai kutibiwa wanakotibiwa watanzania wengine
      Watanzania wengine wanatibisa sehemu mbalimbali nchini, na wengine wanatibiwa Nairobi, na wengine London na siwezi kushangaa wapo wanaotibiwa Dubai au India. Ni dhana isiyo sahihi kusema kuwa uzalendo ni kuchagua mahali ambapo unatibiwa. Watanzania siyo wote wanatibiwa Muhimbili; wapo wanaotibiwa kwa waganga wa kienyeji - tena inadaiwa kuwa watanzania wengi bado wanategemea tiba za jadi. So kwanini iwe kutibiwa Muhimbili (swali lako la awali).

      Mgonjwa ni mgonjwa na ugonjwa hauna uzalendo. Sijawahi kusikia mahali popote ambapo mgonjwa anatakiwa kuonesha uzalendo kwa kukataa matibabu kwa sababu ati yanapatikana nje ya nchi. Ni uzalendo usio na mantiki wa mtu kusema ati usikubali kutibiwa nje ya nchi kwa sababu Watanzania wengine wanatibiwa ndani ya nchi. Hiki kipimo cha uzalendo kwanini kisiende mbali zaidi; Watanzania wangapi wanaenda shule na vyuo ndani ya TAnzania - ni wengi sana? Sasa kwanini wengine waende nje ya nchi? Je kwenda kutafuta elimu nje ya nchi ni kukosa uzalendo? Na unaweza kwenda mbali kwenye mambo mengine vile vile. Vipi watu wanaoenda kufanya biashara nje ya nchi; kwanini wasifanye biashara hizo ndani ya nchi kama ni wazalendo?

      Nadhani hoja ambayo watu wanataka kuitoa ni hoja ya tofauti kabisa na wala haihusiani na uzalendo. Ni hoja ya kwanini taasisi zetu za afya hazijafikia kiwango cha kutoa huduma ya tiba hadi kufanya magonjwa kama haya na mengineyo yatibike hapa hapa nchini vile vile? Hili ni swali zuri sana na kwa kweli watawala wetu hawana majibu. Lakini halihusiani na uzalendo.
      Wa Ndima and masopakyindi like this.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    23. #120
      sexon2000's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th April 2010
      Posts : 301
      Rep Power : 522
      Likes Received
      54
      Likes Given
      59

      Default Re: Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

      Quote By JIULIZE KWANZA
      Kwanini hakusema siri yote bungeni??????ni mnafiki japo ana haya kidogo ila wacha wapungue tuchue jimbo kule hawaibi kama igunga rip Dr.
      PENYE RED:
      Ina sikitisha sana kama binadamu mwenye akili timamu unaweza mtakia mwenzako kifo. Mungu akurudishie hayo maombi yako MARA SABA. mtu yupo hai unamwambia RIP DR. Mungu akusamehe na kukupa haki yako kama nilivyoomba.

      Bado DR na Prof tunawahitaji Mbeya na Tanzania nzima

    Page 6 of 23 FirstFirst ... 4567816 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Hali ya Mwakyembe, Mwandosya na Chami India
      By Kanigini in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 13
      Last Post: 15th November 2011, 09:29
    2. Vipi hali za kina Mwakyembe, Zitto na Mwandosya?
      By Noti mpya tz in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 5
      Last Post: 7th November 2011, 20:34
    3. Ugonjwa wa Mwandosya na Mwakyembe
      By Tujisenti in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 16
      Last Post: 20th October 2011, 09:49
    4. Tetesi: Profesa Mwandosya na Dr. Mwakyembe hawapikiki
      By Ntambaswala in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 71
      Last Post: 27th July 2011, 06:17

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...