Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: CUF yakerwa kuitwa CCM-B; Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 26 of 26
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,235
      Rep Power : 3562
      Likes Received
      3062
      Likes Given
      462

      Default CUF yakerwa kuitwa CCM-B; Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu


      *Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu

      Na Peter Mwenda, Igunga

      CHAMA cha Wananchi (CUF) kimekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha mara moja kutangaza
      kudanganya wananchi wa Jimbo la Igunga kuwa chama hicho kisipewe kura kwa madai kuwa ni CCM-B.

      Akizungumza katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga juzi, Kaimu Katibu Mkuu wa CUF-Bara, Bw. Julius Mtatizo alisema CHADEMA imekuwa ikiwadanganya wananchi kuwa CUF ni CCM-B, wasikichague kwa sababu hakitaleta maendeleo jambo ambalo ni udanganyifu ambao unastahili adhabu.

      Alisema CUF imevumilia sana kauli hizo na sasa imefika kikomo, hivyo kilichobaki ni wao kuweka hadharani mabaya ya CHADEMA kwa sababu ya upotoshaji huo kwa wapiga kura wa Igunga.

      Bw. Mtatiro alisema cha kushangaza, ni kwa nini CHADEMA iseme uongo wakati CUF haijawahi kusema mtindo wa uongozi wa upendeleo uliopo katika chama hicho, ambao hauna tofauti na yale yanayofanywa na chama tawala CCM.

      "Mfumo wa uongozi wa CHADEMA hauna tofauti na ule wa CCM kwa sababu ule mfumo wa uongozi wa kupeana ulipo CCM ambao hautawahi kutokea CUF," alisema Bw. Mtatiro.

      Alisema CHADEMA ilipata viti maalumu 36 na kushindwa kugawa kwa kuzingatia uwakilishi wa wananchi, bali walipendeleana wao kwa wao kwa kugawa viti 16 kwa mkoa wa Kilimanjaro pekee ambako viongozi wa chama hicho, walitoa kwa wake zao, wadogo zao na jamaa zao.

      Alisema CUF Tanzania bara na Zanzibar walipata viti maalum kumi ambavyo ilivigawa bila upendeleo Dodoma (Bi. Moza Abeid), Mwanza (Bi. Mkiwa Kimwanga , Tanga Bi, Amina Mwidau, Mtwara (Bi. Clara Mwatuka, Kaskazini Pemba (Bi. Riziki Omar Juma), Mjini Magharibi Bi. Amina Amour na Kusini Magharibi (Bi. Thuwaiba Idris) ambao wanakilisha wa wananchi badala ya kulimbikizia kundi chache.

      Alisema suala la Serikali ya Umoja Zanzibar ni mfumo uliofikiwa na Wazinzibari wenyewe ili kuondoa uhasama uliokuwepo, sasa inakuaje CHADEMA iseme CUF imeingia mkataba wa urafiki na CCM.

      Wabunge waongeza nguvu

      Wabunge sita wa CUF kutoka Zanzibar waliokuwa katika msiba wa meli ya M.V Spice Islanders wamewasili Igunga kuanza kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho, Bw. Leopold Mahona.

      Wakitambulishwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Nanga juzi jioni, Kaimu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Bw. Julius Mtatiro alisema pamoja kuwa msiba huo ni mkubwa na umegusa familia za wabunge hao, wamekuja kuongeza nguvu kuhakikisha chama hicho kinachukua kiti.

      Waliotambulishwa ni Mbunge wa Nungwi ambako meli hiyo ilizama, Bw. Yusuf Haji Khamis, Bw. Rashid Ali Omar (Kojani), Mohamed Habib Mnyaa (Mkanyageni), Haroub Mohamed Shamis (Chonga), Bw. Salim Hemed Khamis (Chambani).

      Katika mkutano huo mgombea ubunge wa CUF, Bw. Leopold Mahona alisema akichaguliwa atahakikisha wananchi wa Kata hiyo wataondokewa na kero zinazowasumbua kwa miaka mingi bila kupatiwa ufumbuzi










      Last edited by nngu007; 21st September 2011 at 05:43.

    2. Miaka 50

    3. #21
      THINKINGBEING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th August 2010
      Posts : 991
      Rep Power : 657
      Likes Received
      233
      Likes Given
      101

      Default Re: CUF yakerwa kuitwa CCM-B; Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu

      Hawapendi kuitwa CCM B kwani wameshakwalfai kuwa CCM A?
      create tension to anyone who wish not to think

    4. #22
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,235
      Rep Power : 3562
      Likes Received
      3062
      Likes Given
      462

      Default Re: CUF yakerwa kuitwa CCM-B; Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu

      Quote By RUMANYIKA
      Mbona Shinyanga hamna hata mmoja wakati kuna wabunge wanne wa CDM? Mgawanyo ulikuaje kwa mkoa wa Shinyanga.
      Walifanya uteuzi kwa Strategy yao; Mbona Mkoa wa Tabora hakuna Mbunge wa CAF lakini wana Mbunge wa Viti Maalum? CAF had their own strategy as well...

      Hawawachagui hivi hivi wanaangalia hadi issue ya Udiwani kuteua hao wabunge wa viti maalum

      Umeona wa Mwanza alivyo fanya kura yake imeipa Umeya wa Mji wa Mwanza kwa Chadema? - example of one of their strategy

    5. #23
      Albimany's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 187
      Rep Power : 448
      Likes Received
      59
      Likes Given
      0

      Default Re: CUF yakerwa kuitwa CCM-B; Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu

      Quote By nngu007
      Sikujua kuwa Bw. Mtatiro pia anadanganya kuwa wabunge wa kuteuliwa 16 wametoka Kilimanjaro
      Sikujua ana matatizo ... Ana Matatizo huyu kijana

      Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA ambao majina yao yamepitishwa na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Lucy Owenya (Kilimanjaro), Esther Matiko (Mara) Mhonga Luhanywa (Kigoma), Anna Mallac (Katavi), Paulina Gekul (Manyara) na Conchesta Rwalumulaza (Kagera).

      Wengine ni Suzan Kiwanga (Morogoro), Grace Kiwelu (Kilimanjaro), Suzan Lyimo (Kilimanjaro), Regia Mtema (Morogoro), Christowaja Mtinda (Singida), Anna Komu (Dar es Salaam), Mwanamrisho Abama (Zanzibar), Joyce Mukya (Arusha), Leticia Mageni Nyerere (Mwanza) na Naomi Kaihula (Dar es Salaam).


      Majina mengine ya wateule hao ni Chiku Abwao (Iringa), Rose Kamili (Manyara), Christina Lissu (Singida), Raya Ibrahim Khamis (Zanzibar), Philipa Mturano (Dar es Salaam), Mariam Msabaha (Zanzibar) na Rachel Mashishanga (Dar es Salaam).

      Tuliambiwa vitimaalum 36 lakini umetutajia 23 bado 13 nafasi zilio bakia tumalizie mkuu,tupate kujua nani mkweli.

    6. #24
      takeurabu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd July 2011
      Posts : 256
      Rep Power : 452
      Likes Received
      37
      Likes Given
      0

      Default Re: CUF yakerwa kuitwa CCM-B; Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu

      jamani mimi ci shabiki wala mwanachama wa chadema, ila katika hili naomba niwatete! mimi nikingalia mgawanyo wa chadema ulizingatia vitu vikubwa viwili:
      1. maeneo ambayo wana nguvu kubwa mfano mwanza arusha na baadhi ya maeneo ya dar
      2. hawakutaka kuwapoteza akina mama waliokwenda kujaribu kugombea kwenye majimbo kisha wakakosa

      ila kwa kweli sijaelewa kwa nini akina lisu wapo wawili?

      kuhusu cuf nao wamegawanya vizuri kulinga pande mbili za muungano, swala la dini kwangu halina nafasi tunachoangalia ni uwezo wa mtu!

    7. #25
      Tuko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th July 2010
      Posts : 4,637
      Rep Power : 13838
      Likes Received
      2277
      Likes Given
      2205

      Default Re: CUF yakerwa kuitwa CCM-B; Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu

      Jimbo la Igunga halina tofauti na ligi ya mabingwa ulaya ambapo wachezaji wanacheza sio kupata kombe, bali kutangaza majina. Nguvu nyingi inayotumika na vyama huko sio kwa sababu wanalitaka jimbo tu, bali kwa sababu wanataka kujitangaza nchi nzima kwa sababu vyombo vya habari kwa sasa vinamulika huko...

    8. RukaaJuu Final

    9. #26
      Tuko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th July 2010
      Posts : 4,637
      Rep Power : 13838
      Likes Received
      2277
      Likes Given
      2205

      Default Re: CUF yakerwa kuitwa CCM-B; Wabunge sita watua Igunga kuongeza nguvu

      Quote By Albimany
      Tuliambiwa vitimaalum 36 lakini umetutajia 23 bado 13 nafasi zilio bakia tumalizie mkuu,tupate kujua nani mkweli.
      Mtatiro nae alisema walipata 10, lakini hapa vimetajwa 7. Tunaomba hivyo vitatu pia.

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    Similar Topics

    1. Replies: 8
      Last Post: 30th September 2011, 10:35
    2. CHADEMA kuongeza nguvu Igunga
      By Idimulwa in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 20
      Last Post: 20th September 2011, 09:41
    3. kuongeza nguvu za semens
      By RealTz77 in forum JF Doctor
      Replies: 0
      Last Post: 21st October 2009, 16:18
    4. Dawa mpya ya kuongeza nguvu za kiume
      By Bao3 in forum JF Doctor
      Replies: 32
      Last Post: 3rd October 2009, 18:56

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...