JamiiSMS
Show/Hide This

Topic: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Report Post
Page 3 of 8 FirstFirst 12345 ... LastLast
Results 41 to 60 of 145
1. #1
taffu69's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 26th February 2007
Posts : 2,098
Rep Power : 5034
Likes Received
526
Likes Given
432

Default Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA KWA UMMA   NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Katika kutekeleza Mamlaka hayo, Rais ametoa notisi ya kusudio la kuanzisha Mikoa minne (4) na Wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002 ni Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa na Tangazo la Serikali Na. 287 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Wilaya.
Madhumuni ya Notisi hizi ni kuzialika Taasisi na mtu mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa Mikoa mipya na siku 30 kwa Wilaya mpya kuanzia tarehe ya Notisi hizi.

Baada ya muda uliowekwa kupita, Rais atachambua maoni, mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha rasmi Mikoa na Wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.

Mikoa mipya inayoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

MKOA WILAYA ZAKE MKOA ZINAKOTOKA MAKAO MAKUU
1. Geita Geita Mwanza Geita

Nyang’hwale(Mpya) Mwanza

Chato Kagera

Bukombe Shinyanga

Mpya/Mbogwe Shinyanga

2. Simiyu Bariadi Shinyanga Bariadi

Itilima (Mpya) Shinyanga

Maswa Shinyanga

Meatu Shinyanga

Busega (Mpya) Mwanza

3. Njombe Njombe Iringa Njombe

Wanging’ombe(Mpya) Iringa

Ludewa Iringa

Makete Iringa

4. Katavi Mpanda Rukwa Mpanda

Mlele(Mpya) Rukwa

Wilaya mpya zinazoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

WILAYA MPYA WILAYA MAMA MKOA MAKAO MAKUU
1. Buhigwe Kasulu Kigoma Buhigwe
2. Busega Magu Mwanza Igalukilo
3. Butiama Musoma Mara Nyamisisi
4. Chemba Kondoa Dodoma Chemba
5. Gairo Kilosa Morogoro Gairo
6. Ikungi Singida Singida Ikungi
7. Itilima Bariadi Shinyanga Itilima
8. Kakonko Kibondo Kigoma Kakonko
9. Kalambo Sumbwanga Rukwa Kalambo
10. Kaliua Urambo Tabora Kalua
11. Kyerwa Karagwe Kagera Rubwera
12. Mbogwe Bukombe Shinyanga Mbogwe
13. Mkalama Iramba Singida Nduguti
14. Mlele Mpanda Rukwa Inyonga
15. Momba Mbozi Mbeya Ndalambo
16 Nyang’hwale Geita Mwanza Nyang’hwale
17. Nyasa Mbinga Ruvuma Mbamba Bay
18. Uvinza Kigoma Kigoma Lugufu
19. Wanging’ombe Njombe Iringa Waging’ombe

Kwa taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -

Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.

E-mail [email protected]
Fax- 026-2322116

Imetolewa na: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
9 Septemba, 2011

Wakuu kwa kuangalia hali halisi ya uchumi wa Tanzania kwa sasa na jinsi Taifa letu linavyokabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi pamoja na kijamii; ni sahihi kwa wakati huu kuanzisha mikoa mipya na wilaya mpya tena kwa idadi kubwa kama hiyo (Mikoa MINNE na Wilaya KUMI NA TISA).

Lipi jambo la muhimu kwa sasa, kuanzisha wilaya na mikoa mipya ama kuangalia namna ya kutatua matatizo yanayolikabili Taifa kwa sasa?

Swali la kujiuliza, Mbona wakati wa utawala wa awamu ya kwanza hadi ya tatu Marais wa vipindi hivyo hawakuongeza mikoa na wilaya kwa idadi kubwa kama hiyo? Iweje wakati wa awamu ya JK ndiyo tunashuhudia kila kitu kikiongezwa kama Baraza la Mawaziri, Uteuzi wa majaji, na hata Mikoa pamoja na Wilaya Mpya.

Kwa wale wenye kuliona jambo hili na madhara yake naomba tupaze sauti kukemea na kulikataa mapema.

Source: Pmoralg - Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government | Tanzania

Last edited by taffu69; 14th September 2011 at 15:26.

2. Bongolander's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 10th July 2007
Location : Tandale
Posts : 5,286
Rep Power : 1799
Likes Received
1728
Likes Given
249

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Quote By Ngisibara View Post
Na mie bado natafakari hii kitu ndani ya serikali yetu>... @yahoo.com......

Mkuu ukiona barua zenye contacts za yahoo au hotmail au hizi free e mails jua ni scam, hizo wanatumia sana wanigeria.

Mbali na hilo, kama ni kweli inabidi watwambie ni kwanini wanataka kuongeza mikoa na wilaya. Kigezo cha kuongeza idadi ya mikoa na wilaya ni nini? Idadi ya watu? ukubwa wa eneo la ardhi? uwezo wa kujiendesha kiuchumi? au sababu za kisiasa?

What is wrong with mikoa iliyopo sasa? ina kasoro gani? Watu wa mkoa unaoitwa Manyara kwa sasa wamenufaika nini na kuwa mkoa, tofauti na walipokuwa mkoa wa Arusha?

Au ndio njia ya kuwatafutia watu u-RC na u-DC...

Mkuu siaimini hata kidogo kama hii ni kweli hakuna sababu yoyote ya msingi inayoweza kuingia akili kuongeza idadi ya mikoa na wilaya, labda iwe siasa tu. Naona watendaji na wafanya maamuzi kuwa effective kutaondoa hilo, hakuna sababu ya kuongeza gharama za utendaji wa serikali wakati, hizo pesa wanaweza kupewa watendaji wa sasa na kukwa na impact hiyohiyo.

3. #42
Kiti's Avatar
Senior Member Array
Join Date : 2nd November 2010
Posts : 217
Rep Power : 608
Likes Received
33
Likes Given
0

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Wakuu wapya wa mikoa 4, wakuu wa wilaya 19. Mashangingi 23, Kujenga majengo mapya ya ofisi na nyumba za watumishi, n.k. jamani kulikoni? Ukiongezea na mawaziri wa wizara na mawaziri wadogo! Tutafika kweli. NAPING KWA NGUVU ZOTE.

4. MAMMAMIA's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 26th February 2008
Location : Near You
Posts : 3,827
Rep Power : 3395
Likes Received
1519
Likes Given
1261

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Quote By Mkandara View Post
Hapo sasa mkuu wangu na sidhani kama kuna kiongozi wetu yeyote anafahamu kwa nini Italy wamefanya hivyo!
Tatizo ni kuwa wakuu wetu wanafikiri kwa masaburi badala ya kutumia bongo, wao wanajali tu maslahi ya wachache na ya kisiasa.

5. Sometimes's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 28th December 2010
Posts : 3,606
Rep Power : 1339
Likes Received
733
Likes Given
1055

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Hayo ni mafanikio ya miaka50

6. #45
Katavi's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 31st August 2009
Location : Lyamba Lya Mfipa
Posts : 31,862
Rep Power : 271424177
Likes Received
5828
Likes Given
3414

Default

Quote By Matonange View Post
Katavi mkoa mzima una wilaya mbili tu. Hii imekaaje?
Niacheni jamani nami nijidai......lol..

7. #46
Katavi's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 31st August 2009
Location : Lyamba Lya Mfipa
Posts : 31,862
Rep Power : 271424177
Likes Received
5828
Likes Given
3414

Default

Quote By Rugas View Post

4.

Katavi

Mpanda

Rukwa

Mpanda

Mlele(Mpya)

Rukwa

Hizi ni dalili za kuipeleka nchi babaya zaidi!We unaanzishha mkoa una wilaya mbili?what for?

Mkoa mmoja,una RC,RAS,Wasaidizi km sita wa RAS,....RPC, na mabosi kibao!Ukiacha mishahara na marupurupu yao,wanahitaji nyumba.....magari...wasaidizi. ...

Ulianzishwa mkoa wa Manyara....ukienda pale ukaona ofisi za serikali utasema kweli kodi za wananchi zimeeishia pale.Maaana kuna jengo la R.C (of about 4b construction cost) RPC(ndo wanaanza kujenga),PCCb-like 1Billion,TRA- like 1billion,Tanroads- like 2billions,Hazina-like !billion na mengine. Ni gharama kubwa kuanzisha mkoa mmoja tu! kwa hii minnne sijuhi! Labda faida ni nyingi kuliko hasara,lakini kwa umaskini huu!haifai.

M
Sijui kumetokea nini mwanzo tuliambiwa kutakuwa na wilaya tatu, Kaliua kutokea mkoa wa Tabora ambayo sasa haipo.

8. brazakaka's Avatar
Senior Member Array
Join Date : 3rd March 2010
Posts : 119
Rep Power : 622
Likes Received
14
Likes Given
11

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Quote By Bongolander View Post
Mkuu ukiona barua zenye contacts za yahoo au hotmail au hizi free e mails jua ni scam, hizo wanatumia sana wanigeria.

Mbali na hilo, kama ni kweli inabidi watwambie ni kwanini wanataka kuongeza mikoa na wilaya. Kigezo cha kuongeza idadi ya mikoa na wilaya ni nini? Idadi ya watu? ukubwa wa eneo la ardhi? uwezo wa kujiendesha kiuchumi? au sababu za kisiasa?

What is wrong with mikoa iliyopo sasa? ina kasoro gani? Watu wa mkoa unaoitwa Manyara kwa sasa wamenufaika nini na kuwa mkoa, tofauti na walipokuwa mkoa wa Arusha?

Au ndio njia ya kuwatafutia watu u-RC na u-DC...

Mkuu siaimini hata kidogo kama hii ni kweli hakuna sababu yoyote ya msingi inayoweza kuingia akili kuongeza idadi ya mikoa na wilaya, labda iwe siasa tu. Naona watendaji na wafanya maamuzi kuwa effective kutaondoa hilo, hakuna sababu ya kuongeza gharama za utendaji wa serikali wakati, hizo pesa wanaweza kupewa watendaji wa sasa na kukwa na impact hiyohiyo.
mkuu anuani ya Katibu Mkuu wa TAMISEMI ni [email protected] imerekebishwa.
TBC1 na ITV mnashindwa hata kutuwekea recorded news bulletin kwenye website zenu?

9. #48
popiexo's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 26th October 2010
Posts : 748
Rep Power : 830
Likes Received
169
Likes Given
106

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Haya! Itafikia kila tarafa 2 ni wilaya, na kila wilaya mbili ni mkoa. Vilevile vitongoji 2 = na kijiji na vijiji viwili vitakuwa tarafa
Peace & Love

10. Mkandara's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 3rd March 2006
Location : T dot
Posts : 16,574
Rep Power : 124739544
Likes Received
8256
Likes Given
8156

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Quote By MAMMAMIA View Post
Tatizo ni kuwa wakuu wetu wanafikiri kwa masaburi badala ya kutumia bongo, wao wanajali tu maslahi ya wachache na ya kisiasa.
Lakini pia tusiwalaumu sana kwa sababu hawa viongozi wetu ni reflection yetu sisi. Nina hakika kuna wengi wanashindwa kuona ubaya ktk jambo hili kwa sababu ndivyo tunavyoendesha maisha yetu ya umaskini ktk Ulimbukeni wa kuiga makuu.

Kwa mfano:- Nchi tajiri utamkuta tajiri akifunga ndoa kwa kutumia mamilioni ya fedha na yeye mwenyewe ana mabillioni benki, lakini njoo kwetu tutatumia Tsh millioni 20 kwa harusi wakati bwana na bi. harusi hawana hata Laki benki na pengine hata kazi hawana. Sasa unaanza kujiuliza hizo fedha kwa nini wasipewe hao maharusi wakaanzie maisha?.. au kwa nini walifunga harusi wakati wanajua hawana kazi?.. Jibu ni - Maslahi binafsi na Wao watakwambia kwani maskini haruhusiwi kuoa?, wakati tunachozungumzia ni gharama za harusi ambazo haziwajengi maharusi wala kuwapunguzia matatizo..
Exploration of reality

11. #50
M-mbabe's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 29th October 2009
Location : here n' there
Posts : 1,932
Rep Power : 118273167
Likes Received
722
Likes Given
596

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Kwa mtizamo usio wa kitaalamu (yaani wa kawaida tu), wengi wetu tunaona hatua hii dhahiri ni ufujaji wa raslimali fedha.

Inawezekana mtizamo huu wa baadhi yetu ni potofu kutokana na ujinga (ignorance) ya context ya kitaalamu kwenye haya mambo.
Kama kuna mtaalamu tunaomba atupe objective assessment yake (+ves & -ves, giving his/her verdict on which one outweighs the other).....otherwise huu mpango tutauona kama mkakati wa "wale watu wetu" kuwatafutia ma-girl friend wao kibarua.

Teach me please, I beg!

12. LordJustice1's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 20th January 2011
Posts : 2,266
Rep Power : 2471
Likes Received
512
Likes Given
43

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

hivi zenj wana wilaya ngapi ukilinganisha na idadi ya watu?

13. ndetichia's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 18th March 2011
Location : Mwime - Buswangili
Posts : 27,405
Rep Power : 98146805
Likes Received
4352
Likes Given
383

Default

Quote By Matonange View Post
Katavi mkoa mzima una wilaya mbili tu. Hii imekaaje?
halafu inawezekana zitakuwa karibu karibu ngoja niende chimbo kuangalia imekaa vipi..

14. ndetichia's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 18th March 2011
Location : Mwime - Buswangili
Posts : 27,405
Rep Power : 98146805
Likes Received
4352
Likes Given
383

Default

Quote By Ezan View Post
Sasa menejimenti ifanyeje watoto wazuri wanazidi kumaliza vyuo na hakuna pa kuwapachika. Refer Ukuu wa wilaya Manyyoni
na hisi kitu kama hicho..

15. ndetichia's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 18th March 2011
Location : Mwime - Buswangili
Posts : 27,405
Rep Power : 98146805
Likes Received
4352
Likes Given
383

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

hivi ile thread ya gharama za kuanzia mkoa na wilaya hivi iko wapi ili tupate gharama zake..

16. kisururu's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 3rd January 2011
Posts : 331
Rep Power : 622
Likes Received
91
Likes Given
267

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Wakuu hapa ni majimbo mapya ya uchaguzi yanaandaliwa tena sehemu zile wanapodhani CCM najiweza kujitetea kulingana na watu wanaoishi huko

17. #56
Lua's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 19th May 2011
Posts : 706
Rep Power : 93975
Likes Received
303
Likes Given
6

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Hao hao wanalalamika kasungura chetu kadogo tugawane hivyo hivyo, halafu wanakuja wanaongeza mikoa, mawilaya huku nako si kuongeza za bure tu! Sidhani kama wananchi wanahitaji majina ya mikoa au wilaya mipya zaidi ya kuhitaji huduma za msingi, kama afya, elimu,miundombinu, siasa safi na ambayo wangepelekewa hata kwy mikoa na wilaya zao za zamani, kuliko hicho walichofanya ni kupeana zawadi na fadhira.

18. #57
RMA's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 10th October 2010
Posts : 410
Rep Power : 650
Likes Received
87
Likes Given
0

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Sijui ni vigezo gani vinatumika kugawa hizo wilaya! Ukiangalia wilaya inayoitwa SERENGETI mkoani Mara, attention yote inaelekezwa mbugani tu. Ni wilaya inayosifika kwa ajili ya utalii. Na hata baadhi ya wakuu wetu wa nchi wanakimbizana huko kujenga mahoteli. Lakini ukiangalia kata zote za Tarafa ya Ngoreme kwa mfano, ambayo inahesabiwa kuwa sehemu ya wilaya ya Serengeti utadhani haipo katika ramani ya Tanzania. Vijiji vingi vimesahauliwa na macho yote yanaelekezwa mbugani tu.

Ifike wakati sasa Eneo lote la Tarafa ya ngoreme na baadhi ya vijiji vya wilaya ya Musoma vijijini vinavyopakana na tarafa hii vipewe hadhi ya wilaya. Maisha ya watu huko yanasikitisha na kuhuzunisha. Na kwa sababu ya kusahaulika, vijana wengi wanakimbilia mijini. Na kila wakati wazo hili linapotolewa, utasikia wanasiasa wanasema kuwa wilaya ya Serengeti ni mbuga tupu na idadi ya watu ni ndogo. Iwapo kweli Serikali hii inawajali wananchi wote bila ubaguzi, iwafikirie upya wananchi wa maeneo ya mbali na mbuga na hasa wa tarafa ya Ngoreme na vijiji vilivyo kandokando yake!

19. Kibirizi's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 19th February 2011
Posts : 601
Rep Power : 669
Likes Received
106
Likes Given
13

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

ubarikiwe kwa kutupa taarifa za uhakika.

20. mashikolomageni's Avatar
JF Senior Expert Member Array
Join Date : 5th January 2010
Location : Jamhuri ya Ukenge
Posts : 1,561
Rep Power : 920
Likes Received
162
Likes Given
147

Default Re: Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Mhhh! Kweli nimeamini "kasungura kenyewe ni kadogo"

21. #60
mwaJ's Avatar
JF Tanzanite Member Array
Join Date : 27th September 2007
Location : Nowhere
Posts : 4,086
Rep Power : 14866
Likes Received
2925
Likes Given
2116

Default

Quote By juu kwa juu View Post
Hongera jk, wacha wapinzani wa maendeleo waseme au wabeze, kusogeza mamlaka jirani zaidi na wananchi ni muhimu sana. Hata hivyo tangu lini? Wapinzani wakapongeza kazi ya serikali iliopo itakuwa ajabu.

Kweli wewe hata akili yako inafanya kazi juu kwa juu! We huoni kuwa gharama za uendeshaji serikali zitaongezeka mara dufu? Hebu fikiria mfano ni mashangingi mangapi yatahitajika baada ya kuwa na hizo wilaya na mikoa? Hayo maendeleo unayosema kwani hayawezi kupelekwa bila sehemu hizo kuwa wilaya au mikoa? Mpaka hiyo miaka 3 iliyobaki iishe sijui tutakuwa na mikoa na wilaya ngapi? Lol! Nchi hii! Hatukawii kutangaziwa Kinondoni inakuwa mkoa na wilaya zake mpya 3 - ubungo, kawe na tegeta!

Page 3 of 8 FirstFirst 12345 ... LastLast

Similar Topics

1. Replies: 117
Last Post: 6th November 2014, 09:52
2. Honoraria za wakuu wa mikoa na wilaya
By Kiti in forum Habari na Hoja mchanganyiko
Replies: 1
Last Post: 20th September 2011, 20:28
3. Kikwete atangaza mikoa, wilaya mpya
By MziziMkavu in forum Habari na Hoja mchanganyiko
Replies: 26
Last Post: 25th June 2010, 12:32
4. Wakuu wa MIKOA/WILAYA Wanajeshi
By mwanamasala in forum Jukwaa la Siasa
Replies: 1
Last Post: 25th November 2009, 11:32

Posting Permissions

• You may not post new threads
• You may not post replies
• You may not post attachments
• You may not edit your posts

Who are WE?

JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

You are always welcome! Read more...

Where are we?

We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

For anything related to this site please Contact us.

Contact us now...

DISCLAIMER

JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

Read more...

Forum Rules

JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

You MUST read them and comply accordingly. Read more...

Privacy Policy

We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

Read our Privacy Policy. Proceed here...