Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: SAFARI za rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005!

    Report Post
    Page 4 of 39 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 770
    1. #1
      Jason bourne's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2011
      Posts : 1,385
      Rep Power : 1386
      Likes Received
      610
      Likes Given
      19

      Default SAFARI za rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005!

      Mheshimiwa wa magogoni alisafiri kinyemela bila kutuaga waajili wake na kwenda Juba South Sudani kwenye birthday ya taifa hilo!
      Hiyo ni safari ya 313 ta awe rais wa tz mwaka 2005

      UPDATES

      Mpaka leo tarehe 23/8/2011 tayari amesha safiri safari 315 tangu aingie magogoni octoba mwaka 2005
      Hii ni rekodi ya kipekee duniani ambayo watz tunatakiwa kujivunia na kutembea kifua mbele maatako nyuma


      UPDATES

      Kesho tar 9/9/2011 rais atasafiri kuelekea Kenya kwa ziara ya kikazi
      Hiyo ni safari ya 316 tangu rais aingie madarakani mwaka 2005!

      UPDATES:

      Safari ya 317 kwa rais wangu kipenzi!
      ameenda marekani katika ufunguzi wa UNGA.vilevile atashiriki katika sherehe za kuazimisha maendeo yaliyofikiwa na nchi zinazo endelea.
      wakati huo huo waziri mkuu pinda ametangaza kuwa serikali inakusudia kuongeza bei ya umeme kwa sababu tanesco inajiendesha kwa
      hasara.mia

      UPDATES
      Safari ya 318 ya rais mwenye maajabu duniani!
      JK anaondoka leo kuelekea Australia kwenye mkutano wa jumuiya ya madola...

      UPDATES
      Wakuu nimepata taarifa halisi za wastani wa gharama ya NAULI ya kila safari ya nje ambayo rais kikwete na ujumbe wake hutumia! Kwa mujibu wa vyanzo vyangu vya kuaminika toka wizara ya fedha,hazina na magogoni ni kuwa kila msafara hugharimu kadirio la juu milioni 300 na kadilio la chini ni milioni 250. Zingatieni hii ni NAULI ya ndege iende irudi tu!

      Sasa hebu chambueni wenyewe ikulu inatumia kiasi gani kwa safari za rais?

      UPDATES
      16/12/2011
      Safari ya 319, hivi sasa yupo nchi Uganda katika mkutano uitwao International Conference of Heads of State (ICGLR)


      Rais wetu anazidi kujijengea heshima katika mkakati wake wa kuvunja rekodi ya dunia kwa kusafi hata ziara zenye kumtuma waziri, yeye anasafi tu ilimradi lengo litimie

      Inashangaza sana kuona maraisi wenzake kwa kujali zaidi maslahi ya mataifa yao, hawakuona sababu za kuhudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika wakabaki na wengine kutuma wawakilishi tu, lakini jk hata kicheni pati akialikwa Urusi atasafiri bila kukosa.



      UPDATES

      Safari ya 320 ya Rais JK Ameenda Davos Kuikomboa Tanzania, acheni Kelele !
      ambakoatahudhuria mikutano ya WEF na ule wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU)mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili Jumamosi, Januari 28, 2012

      UPDATES:

      SAFARI ya 321
      ya Mh Rais Jakaya M. Kikwete, sasa leo anatua katika nchi ya Afrika kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili leo Jumamosi, Januari 28, 2012

      UPDATES: 21/2/2012

      SAFARI ya 322,

      Leo mheshimiwa Rais Jakaya M.Kikwete amesafiri kwenda Uingereza,hakuna sababu ya msingi inayompeleka huko japo kubwa ni kupangua Baraza la Mawaziri.

      UPDATES: 24/2/2012
      SAFARI YA 323,

      Leo Rais mwenye maajabu duniani, mutu ya musoga, aka msafiri kafiri, anatua Botswana ikiwa ni mwendelezo wa safari zake za kikazi, huku nyumbani amecha mbwa wamepatwa na kichaa wanaua raia wanaomba haki yao ya kulindwa!

      Inasikitisha, inashangaza aminini haya ndiyo ya FILAUNI.


      UPDATES:


      Safari ya 324!
      15/04/2012 Rais Jakaya Kikwete ametua Brazili kwa ziara ya kikazi!

      UPDATES:

      SAFARI YA 325
      Leo tarehe 22 rais Jakaya Kikwete amewasili Malawi kushiriki mazishi ya aliyekuwa rais wa Malawi Bingu wa Mtharika!

      Raitba inasema atarudi tz tarehe 24




      UPDATES:
      Leo tarehe 9/5/2012
      Safari ya 326 tangu mkuu wa nchi aingie madarakani!

      Rais amewasili Addis Ababa Ethiopia KWA KONGAMANO LA UCHUMI LA KIMATAIFA KWA AFRICA!


      UPDATES:
      Safari yake ya 327
      ,
      Rais Jakaya Kikwete yupo nchini Marekani tangu tarehe 16/5/2012 akisubiri kuhudhuria mkutano unaotarajiwa kufanyika tarehe 19/5/2012,

      UPDATES

      SAFARI YA 328:

      Leo tarehe 1/7/2012

      Rais wa Tanzania Mh Jakaya M. Kikwete na ujumbe wake wamesafiri mpaka lKigali Rwanda kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa nchi hiyo!

      Mungu ibariki Tanzania!


      UPDATES:

      SAFARI YA 329

      Tarehe 2/7/2012

      Rais Jakaya baada ya kutoka kuhudhuria sherehe za uhuru nchini Rwanda, ameunganisha kwenda nchini Burundi kuhudhurua sherehe za Uhuru wa nchi hiyo!


      UPDATES

      Tarehe 10/7/2012


      Safari ya 330:

      Hivi punde tumewasili nchini Uingereza,

      Msafara wa mh rais Jakaya Kikwete umewasili Hyatt Regency London-The Churchill

      Ziara hii imetufikisha hapa kwaajili ya mh rais kuhudhuria mkuta unaohusu mambo ya Family Plan!

      UPDATES:

      SAFARI YA 331


      Tarehe 14, rais Jakaya Kikwete amewasili Mjini Addis Ababa Ethiopia kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU),

      UPDATES:

      SAFARI YA 332.


      Rais Jakaya Kikwete amewasili Kampala, Uganda,*kuhudhuria mkutano wa*nchi*za Maziwa Makuu asubuhi Agosti*8, 2012




      UPDATES

      SAFARI YA 333
      .

      Rais Jakaya Kikwete yupo nchni Ghana kuhudhuria msiba wa rais wa nchi hiyo.

      UPDATES
      SAFARI YA 334

      Tarehe 16/8/2012 Rais JK alitua Maputo Msumbiji kuhudhuria mkutano wa wakuu wa Afrika,


      UPDATES.

      SAFARI YA 335

      Rais jakaya kikwete atua Addis Ababa Ethiopia leo kuhudhuria mazishi ya waziri mkuu wa nchi hiyo Melez Zenawi


      UPDATES:

      SAFARI YA 336

      Tarehe 1/10/2012

      THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIADIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


      Telephone: 255-22-2114512, 2116898
      E-mail: [email protected]
      [email protected]
      Fax: 255-22-2113425



      TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza Ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada akianzia mjini New York, Marekani leo, Jumatatu, Oktoba Mosi, 2012.

      Rais Kikwete na ujumbe wake uliondoka nchini usiku wa jana, Jumapili, Septemba 30, 2012, na utawasili mjini New York, Marekani mchana wa leo tayari kwa ziara hiyo ya Marekani.

      Rais Kikwete atakuwa Marekani kwa siku mbili kabla ya kwenda Canada kwa ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili.
      Katika ziara yake mjini New York, Marekani, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki Moon ofisini kwa Katibu Mkuu huyo kesho asubuhi Oktoba 2, 2012.

      Baada ya mazungumzo hayo, Rais Kikwete ataungana na Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya wa Jiji la New York na Mfadhili Mkubwa wa Misaada ya Kibinadamu Duniani, Mheshimiwa Michael Bloomberg; Mama Helen Agerup ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Misaada ya Kibinadamu ya H&B Agerup na Dkt. Kelly J. Henning, Mkurugenzi wa Mipango ya Sekta ya Afya ya Taasisi ya Bloomberg Philanthropies kwenye Uzinduzi wa Matokeo ya Mpango ya Ubunifu wa Afya ya Akinamama katika Tanzania.

      Kwenye sherehe hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi uitwao Green Room kwenye makao makuu wa Umoja wa Mataifa, Rais Kikwete, Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya Bloomberg na mama Helen Agerup kwa pamoja watazindua Matokeo ya Mpango huu uitwao Innovative Maternal Health Program.

      Kwenye shughuli hiyo pia Meya Bloomberg atatangaza matokeo ya miaka mitatu ya misaada ya kiafya chini ya mpango huo kwa akinamama iliyotolewa na taasisi ya inayomilikiwa na Meya Bloomberg ya Bloomberg Philanthropies.
      Aidha, kwenye shughuli hiyo, Meya Bloomberg atatangaza misaada mpya wa mabilioni ya fedha kuboresha afya ya akinamama katika Tanzania chini ya mpango huo na atatangaza mshirika mpya ambaye atasaidiana na taasisi ya Bloomberg Philanthropies katika kuunga mkono huduma bora za afya kwa akinamama wa Tanzania.

      Katika Tanzania, misaada ya taasisi ya Bloomberg Philanthropies huelekezwa katika maeneo ya vijijini yasiyokuwa na huduma bora zaidi kwa kiafya na huduma ambazo hutolewa ni zile za kuokoa maisha ya akina mama hasa wakati wa uzazi.

      Tokea mwaka 2006, taasisi hiyo imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 11.5 Fedha hizo ni sehemu ya kiasi cha dola za Marekani milioni 330 ambazo zilitolewa na taasisi hiyo kwa nchi mbali mbali duniani kwa mwaka jana peke yake.

      Taasisi hiyo hufanya kazi ya kuendeleza maeneo matano duniani ambayo ni Usanii, Elimu, Mazingira, Ubunifu katika Serikali na Afya ya Umma.
      Rais Kikwete ataondoka Marekani kwenda Canada keshokutwa Jumatano Oktoba 3, 2012 kwa ajili ya Ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika nchi hiyo kwa mwaliko wa Gavana Jenerali wa nchi hiyo, Mheshimiwa David Johnston.

      Imetolewa na
      :
      Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
      Ikulu.
      Dar es Salaam.
      1 Oktoba, 2012



      UPDATES: 03/10/2012

      SAFARI ya 337,

      Leo mheshimiwa Rais Jakaya M.Kikwete amewasili Canada kwa ziara ya kikazi!

      UPDATES: 15/10/2012

      SAFARI ya 338,

      Leo mheshimiwa Rais Jakaya M.Kikwete amewasili nchini Oman kwa ziara ya kiserikali


      UPDATES: 24/11/2012

      SAFARI ya 339,

      Mheshimiwa Rais Jakaya M.Kikwete yupo nchini Uganda kwa mkutano wa wakuu wa nchi za maziwa makuu!

      UPDATES: 29/11/2012

      SAFARI ya 340,

      Mheshimiwa Rais Jakaya M.Kikwete yupo nchini Kenya kwa uzinduzi wa barabara ya Namanga ambayo ni kiungo muhimu kwa nchi za maziwa makuu!

      UPDATES

      SAFARI ya 341

      Tarehe 23/01/2013 rais anawasili jijini Paris nchini Ufaransa kwa ziara maalumu ya kikazi.


      UPDATES:

      Safari ya 342 nchini Uswis ambapo rasi Jk amefika kwa ziara ya kiserikali.

      UPDATES:

      Safari ya 343,

      3/2/2013
      Rais anawasili Afrika ya kusini kwa ziara ya kikazi.

      UPDATES:

      09/04/2013
      Safari ya 344 nchini Kenya kwenye shere za kuapishwa rais mpya wa Kenya.

      UPDATES:

      15/04/2013

      Safari ya 345 nchini Uholanzi,

      Rais amewasili nchini Uholanzi kwa mwaliko wa malkia wa Uholanzi Betresx

      UPDATES:

      04/05/2013

      Safari ya 346 nchini Kuwait,

      Rais Jk amewasili jini Kuwait City kwa ziara ya siku mbili,

      UPDATES:

      10/05/2013

      Safari ya 347 nchini Afrika ya Kusini,

      Rais amewasili nchini Afrika ya kusini kuhudhuria mkutano wa SADC wa siku mbili.
      Last edited by Jason bourne; 11th May 2013 at 05:17.

    2. Miaka 50

    3. #61
      Jason bourne's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2011
      Posts : 1,385
      Rep Power : 1386
      Likes Received
      610
      Likes Given
      19

      Default Zingatieni Walimwengu! Rais JMK atimiza safari ya 314 nje ya tz! anakwenda SA!

      Amini usi amini takwimu zinazidi kupaa za sharobaro wetu wa magogoni! Anazidi kuigawa dunia mapandemapande vyovyote atakavyo na sasa huyooo kwa Madiba!!

    4. #62
      COMPLICATOR2011's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th July 2011
      Posts : 255
      Rep Power : 0
      Likes Received
      26
      Likes Given
      16

      Default Re: Zingatieni Walimwengu! Rais JMK atimiza safari ya 314 nje ya tz! anakwenda SA!

      Mwache aende coz anajua katiba mpya itaondoa kinga ya raisi mstaafu kutoshitakiwa na ikiwa hivyo kwa madudu aliyoyafanya lazima tumpige ndani. Huwezi amini ndg yangu hamna mwanasiasa niliyewahi kumpenda na kupoteza muda wangu mwingi kumsikiliza kama huyu lkn sasa viceversa is true namchukia huyu jamaa zaidi ya malaria.

    5. EMT
      #63
      EMT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2010
      Location : Mahuta
      Posts : 8,867
      Rep Power : 61719
      Likes Received
      7142
      Likes Given
      6417

      Default Re: Rais Kikwete Ziarani Afrika ya Kusini

      Quote By NDOFU
      Juzi juzi tu alikuwa huko south Africa kwa mambo haya haya ya uwekezaji! Hv kwanin asiende mkurugenzi wa EPZA,AU HUYO WA TIC AU HATA WAZIRI WA UWEKEZAJI NA UW EZESHAJI AU MEMBE BASI! Aaaaaah' inakera sana kuwa na raisi kama huyu!
      Safari zake zimekuwa nyingi mpaka anayeupdate blogu ya Ikulu kashindwa: Ikulu Mawasiliano
      Capitol Hill likes this.
      “Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.

    6. #64
      rosemarie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 4,732
      Rep Power : 1366
      Likes Received
      280
      Likes Given
      142

      Default Re: Rais Kikwete Ziarani Afrika ya Kusini

      Quote By EMT
      Safari zake zimekuwa nyingi mpaka anayeupdate blogu ya Ikulu kashindwa: Ikulu Mawasiliano

      namalizia course ya website dev,subiri utaona nitakavyopoteza hizi web za kipuuzi,kamwe hazitaonekana tena,nina hasira sana!!!!!!!!!!
      Capitol Hill likes this.
      ccm inakufa,asante mungu umesikia kilio chetu!!!!!!!

    7. EMT
      #65
      EMT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2010
      Location : Mahuta
      Posts : 8,867
      Rep Power : 61719
      Likes Received
      7142
      Likes Given
      6417

      Default Re: Rais Kikwete Ziarani Afrika ya Kusini

      Quote By rosemarie
      namalizia course ya website dev,subiri utaona nitakavyopoteza hizi web za kipuuzi,kamwe hazitaonekana tena,nina hasira sana!!!!!!!!!!
      Ile sio website. Ni blogu.
      Saigon likes this.
      “Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.

    8. FemaTV & Radio

    9. #66
      Jason bourne's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2011
      Posts : 1,385
      Rep Power : 1386
      Likes Received
      610
      Likes Given
      19

      Default

      Quote By COMPLICATOR2011
      Mwache aende coz anajua katiba mpya itaondoa kinga ya raisi mstaafu kutoshitakiwa na ikiwa hivyo kwa madudu aliyoyafanya lazima tumpige ndani. Huwezi amini ndg yangu hamna mwanasiasa niliyewahi kumpenda na kupoteza muda wangu mwingi kumsikiliza kama huyu lkn sasa viceversa is true namchukia huyu jamaa zaidi ya malaria.
      Pole sana! Namshukuru mungu mimi nilishamtoa akilini mwangu hata kabla hajaingia magogoni!

    10. #67
      Moghati's Avatar
      Member Array
      Join Date : 5th July 2011
      Posts : 88
      Rep Power : 415
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Jason bourne
      Mheshimiwa wa magogoni juzi alisafiri kinyemela bila kutuaga waajili wake na kwenda Juba South Sudani kwenye birthday ya taifa hilo!Hiyo ni safari ya 313 ta awe rais wa tz mwaka 2005!
      Acha umbea ww dogo...fanya research usikurupuke ni marais wangapi wanafanya ziara...kaz yko ni kuhesabu safari z rais zinakuhusu nn...kama huna huna hoja ondoka jf...au bado una ndoto za slaa kuwa rais nchi hii....acha jk ajinafasi ts tym 4 hm...

    11. EMT
      #68
      EMT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2010
      Location : Mahuta
      Posts : 8,867
      Rep Power : 61719
      Likes Received
      7142
      Likes Given
      6417

      Default re: Rais Kikwete afikisha safari 314 nje ya Tanzania - South Africa

      Quote By Moghati
      Acha umbea ww dogo...fanya research usikurupuke ni marais wangapi wanafanya ziara...kaz yko ni kuhesabu safari z rais zinakuhusu nn...kama huna huna hoja ondoka jf...au bado una ndoto za slaa kuwa rais nchi hii....acha jk ajinafasi ts tym 4 hm...
      Mkuu weka siasa pembeni, kwa miaka kumi ya kuwa madarakani, kuna uwezekano mkubwa Rais akawa amekaa nje ya nchi kwa mwaka mmoja. Safari za Rais zinatuhusu kwa sababu anatumia kodi zetu kusafiria.
      “Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.

    12. #69
      King Kong III's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Enaboishu-Umenyeni
      Posts : 11,876
      Rep Power : 5053
      Likes Received
      3194
      Likes Given
      2619

      Default Re: Zingatieni Walimwengu! Rais JMK atimiza safari ya 314 nje ya tz! anakwenda SA!

      Haaaa "anakesha hewani kama popo"-Mpoki

    13. #70
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14620
      Likes Received
      2841
      Likes Given
      1961

      Default Re: Zingatieni Walimwengu! Rais JMK atimiza safari ya 314 nje ya tz! anakwenda SA!

      Anzisheni maandamano.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    14. #71
      Gagurito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2011
      Location : Gangilonga....
      Posts : 5,263
      Rep Power : 1455
      Likes Received
      693
      Likes Given
      696

      Default

      Quote By Jason bourne
      Mheshimiwa wa magogoni juzi alisafiri kinyemela bila kutuaga waajili wake na kwenda Juba South Sudani kwenye birthday ya taifa hilo!Hiyo ni safari ya 313 ta awe rais wa tz mwaka 2005!
      Mkuu hapo hujajumlisha siku alizospend huko safarin or? Ni safari nyingi sana!

    15. #72
      Gagurito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2011
      Location : Gangilonga....
      Posts : 5,263
      Rep Power : 1455
      Likes Received
      693
      Likes Given
      696

      Default

      Quote By Moghati
      Acha umbea ww dogo...fanya research usikurupuke ni marais wangapi wanafanya ziara...kaz yko ni kuhesabu safari z rais zinakuhusu nn...kama huna huna hoja ondoka jf...au bado una ndoto za slaa kuwa rais nchi hii....acha jk ajinafasi ts tym 4 hm...
      Unajua ulichokiandika lakini? Nawasi wasi party affiliation feelings zinakutesa!

    16. #73
      Jason bourne's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2011
      Posts : 1,385
      Rep Power : 1386
      Likes Received
      610
      Likes Given
      19

      Default

      Quote By zomba
      Anzisheni maandamano.
      We ukiwa upande gani?

    17. #74
      Duble Chris's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2011
      Posts : 2,339
      Rep Power : 871
      Likes Received
      382
      Likes Given
      304

      Default re: Rais Kikwete afikisha safari 314 nje ya Tanzania - South Africa

      kwa maana hiyo anaelekea kumaliza mwaka akiwa safirini duh hii kali ivi nchi hii haina mawazari wa wizara husika au hawajui lafudhi za huko

    18. #75
      niweze's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st October 2009
      Posts : 1,010
      Rep Power : 697
      Likes Received
      112
      Likes Given
      82

      Default Re: Rais Kikwete afikisha safari 314 nje ya Tanzania - South Africa

      Kweli this fringe guy doesn't get it na sijui lini kichwa kitaingizwa utanzania. The only thing left ni kumwondoa madarakani, how can we accept these kinds of crimes?

    19. #76
      MtamaMchungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2011
      Posts : 1,539
      Rep Power : 805
      Likes Received
      710
      Likes Given
      64

      Default

      Quote By SHERRIF ARPAIO
      Mark my words......Nakuhakikishia before end of July mkuu wa nchi atasafiri tena kwenda nje ya nchi tena sio mara moja, kama kuna anyebisha let's bet a million $$$
      You were a bit incorrect, you should have said before the middle of this July. Yuko South Africa.

    20. #77
      Baba_Enock's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2008
      Location : Bunju "B"
      Posts : 5,812
      Rep Power : 1898
      Likes Received
      1155
      Likes Given
      964

      Default Re: Rais Kikwete afikisha safari 314 nje ya Tanzania - South Africa

      Safari 313 x Siku tatu (kwa wastani) = siku 1,000 (nje ya nchi)

      Katika miaka 6 ya utawala JK amekuwa nje ya Ikulu miaka 3!
      Ad Majorem Dei Gloriam - "For the greater glory of God"

    21. #78
      kimatire's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2008
      Location : Sydine- St. Roix's
      Posts : 349
      Rep Power : 607
      Likes Received
      43
      Likes Given
      20

      Thumbs up Kikwete to lead business delegation to SA forum

      President Jakaya Kikwete is expected to lead a Tanzanian delegation to a business forum in South Africa next Tuesday.Organisers of the event, which will take place in Pretoria, are the Tanzania Investment Forum (TIC), the ministry of Trade and Industry.
      I smile because I don't know what the hell is going on.

    22. #79
      mmakonde's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2009
      Posts : 976
      Rep Power : 673
      Likes Received
      33
      Likes Given
      0

      Default JK ameonekana London

      Kuna mtu anadai amemuona mkuu wetu UK.
      Safari hizi haziishi?

    23. #80
      The Analyst's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2011
      Posts : 380
      Rep Power : 501
      Likes Received
      133
      Likes Given
      107

      Default Re: JK ameonekana London

      UVCCM Mkoa wa Pwani walishasema, tena mbele ya Ridhwan kwamba ni zamu yao kula. JK anatekeleza hayo. Mtasema weee mwisho mtalala. Ushauri wangu mwacheni JK afanye apendalo kwa kuwa baadhi yetu wameapa kumtetea mpaka mwisho, lakini msiruhusu rais ajaye awe na uwezo mdogo wa kufikiria kiasi hicho maana tutauwawa kwa uongozi dhaifu.
      Viongozi Dhaifu na Mafisadi + Wananchi wavivu, walalamishi na wasiojua haki zao + Imani Iliyopotoshwa = Umasikini wetu.

    24. Study Abroad

    LinkBacks (?)


    Similar Topics

    1. Kikwete ameunda Tume ngapi tangu aingie Madarakani?
      By Mzalendo80 in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 6
      Last Post: 19th February 2011, 00:45
    2. Replies: 0
      Last Post: 5th May 2010, 13:27
    3. Kikwete amefanikisha lipi tangu aingie madarakani!?
      By Pdidy in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 44
      Last Post: 27th August 2009, 15:35

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...