Huwa najiuliza hivi serikali yetu inafikiria nini kuhusu huu mfululizo wa maonyesho (maonesho) mbalimbali ambayo yote yanahusu taasisi na idara za serikali. Maonyesho hayo ni kama ya Sabasaba (mwezi July kila mwaka); Nanenane (mwezi August kila mwaka); wiki ya utumishi wa umma na sasa miaka 50 ya uhuru ambayo maandalizi yake yanagharimu pesa nyingi. Kwa upande wangu naona kuna watumishi ambao wanatumia muda mwingi kwenye maonesho badala ya kufanya kazi za uzalishaji/kutoa huduma. Wanajamii naomba tulijadili hili.

Reply With Quote
Follow Us Here