Wanasayansi wamefanya utafiti na kugundua kila binadamu anayezaliwa chini ya uso wa dunia yetu hiii ni Mwanasiasa kwa kuzaliwa kwa kuwa asilimia kubwa ya maisha yake yanaimarika na kustawika au kuathirika kwa sababu ya siasa.
Ndio maana kuna chaguzi ambazo ni haki yake ya msingi ya kuchaguliwa yeye au kumchagua mtu yoyote ambae yeye kwa imani yake anaona anastahiki kumuongoza ili kumuonyesha njia apate ustawi binafis wa maisha yake, familia yake na Taifa lake kwa ujumla.Hivyo Viongozi Serikali na Wanasiasa wa CCM siasa ni sehemu ya maisha ya Watanzania wote Millioni 40.7.
Kupitia utafiti huo wa Wanasayansi hao hata mimi nae ni Mwanasiasa kwa kiwango changu. Kinachonikera katika siasa za chama cha Mapinduzi ni maneno ambayo viongozi wake wa kisiasa na wale walioko Serikali wanavyopenda kuyatumia sana kiasi kuwa kwa mwelevu yoyote yule maneno hayo yamesemwa sana kiasi kuwa Wananchi wameshagundua nyuma ya pazia ya matumizi ya maneno hayo kwa Viongozi na Wanasiasa hao. Japo kwa upofu wa Viongozi wetu wa Kisiasa na Serikali wanajisau na kuona Wananchi hawalijui hilo na wala hawaoni matendo yao.
Maneno kama Uchochezi, Uchonganishi, Kutishia Amani, Uvunjifu wa Amani,hizo ni hisia ,Uthibitisho,upotoshaji wa Wananchi,Wivu,Wapinga Maendeleo,fikra potofu, Intelegensia nk.
Yamekuwa ni maneno ambayo yameifikisha CCM hapo ilipo sasa ya kupoteza imani kwa Wananchi,kwa kuwa yamefikia kuwa yanasemwa na Viongozi wa Kichama na Serikali ambao Watu [Wananchi] huku site [Makongoro] wanawajua kuwa si wenye hadhi ya kuyatamka hayo.
Wananchi sio kuwa hawajui adui yao ni nani, wasichonacho ni nyenzo na mbinu za kupambana na adui wao huyo.Kwa kuwa wengi wa maadui zao wako ndani ya mfumo hivyo kuwakabili inakuwa kazi ngumu njia iliyopo kwa Wananchi ni kukwangua gamba la juu la Kobe taratibuuu!! Mpaka kufikia kichwa cha Kobe.Kwa wanaojua jinsi ya kutibu virus wa TB ,dawa yake ndio itakayotumiwa na Wananchi kama TIBA ya tatizo lao hivyo nguvu ya umma ndio siraha waliyonayo mkononi.
Chama cha Mapinduzi kitambue kuwa maneno hayo yanakera [Irritate] sana yanapotumika kwa sasa, yanaongeza ufa dhidi ya chama hicho dhidi ya Umma.Yangesemwa hivyo wakati Nchi na Wananchi wake wako kwenye ustawi yaani maisha BORA hakika kila Mwananchi angesimama kuyaunga mkono kama ambavyo Wananchi walivyounga mkono azimio la Arusha huko nyuma.
Viongozi wa CCM na Serikali Kwa faida yao waepuke nakuacha kabisa matumizi ya maneno hayo,kwa kuwa ndio yanayoongeza moto, kama ni wimbo basi ni mwimbo wa Mwaka 47. Kama mnabisha endeleeni kuyatumia muuone moto wake.
Sooooooooooon and very soooonnnnn!!!
Nawasilisha.

Reply With Quote





Follow Us Here