JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

  Report Post
  Results 1 to 13 of 13
  1. BAK's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th February 2007
   Location : Mfaranyaki
   Posts : 43,970
   Rep Power : 429505982
   Likes Received
   26189
   Likes Given
   28962

   Default Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   Waungwana kama kuna yeyote mwenye more info kuhusu kamati hii au kama akipata hizo info siku za usoni azimwage hapa ukumbini.

   Alutta Continua

   Date::7/8/2008
   Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi
   Na Kizitto Noya na James Magai
   Mwananchi

   KAMATI ya Kupambana na Uporaji wa Nchi (PILCOM) imesema hairidhishwi na kitendo cha baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi, kutumia makanisa kujisafisha.

   Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo na kiongozi wa Kanisa la Full Salvation, Christopher Mtikila, alidai jana katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam kwamba, ni ukiukwaji wa haki na misingi ya sheria za nchi, kwa wezi wa kuku na vibaka kufungwa gerezani na mafisadi wa fedha za umma kuachwa huru.

   Alidai kuwa kamati hiyo inakusudia kufungua kesi mahakamani dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

   ''Moja ya kazi za kamati hii ni kuwafikisha mbele ya sheria watu wote walioshiriki katika wizi wa matrilioni ya fedha za nchi yetu katika Benki Kuu na kurejesha mapesa yote waliyoyaiba pamoja na riba na gharama kutoka kila walikoyaweka nje na ndani ya nchi,'' alisema Mchungaji Mtikila.

   Alisema katika maandalizi ya kufungua kesi hiyo, jana kamati ilimwandikia barua Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi kuwataka waharakishe hukumu ya kesi ya Katiba namba 86/2006, iliyofunguliwa na kamati hiyo kuitaka iruhusu watu binafsi kuendesha kesi za jinai.

   Alisema hivi sasa kamati hiyo inangoja hukumu ya kesi hiyo, ili iweze kufungua kesi dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.

   Alidai kuwa wamemwandikia Gavana wa BoT na Spika wa Bunge waipatie taarifa muhimu za wizi huo, ili sheria ichukue mkondo wake.

   ''Tunawahakikishia wananchi kwamba, kama inavyosema Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hakuna mwizi aliye juu ya sheria, awe rais mstaafu au aliye madarakani, waziri, kigogo wa CCM au --------- jeupe au jeusi, mradi ameshiriki katika wizi wa mali za umma lazima atafikishwa mahakamani,'' alisema Mtikila

   Kwa mujibu wa Mtikila, Kamati hiyoambayo inawahusisha viongozi wa makisa kadhaa, inashughulikia wizi wa Sh216 kutoka Mfuko wa Import Support, mabilioni ya EPA, DCP na OGL, ufisadi katika mkataba wa Richmond na Dowans, Meremeta na Tangold, IPTL, Songas, Aggreko, Netgroup Solutions, TICTS, Radar, TTCL, Benki ya Taifa ya Biashara,Tanzanite, migodi ya dhahabu na uporaji wa majumba ya serikali na vigogo wa CCM.

   Kamati pia ilimtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kushiriki kikamilifu katika vita hiyo ya ufisadi na kuhakikisha kuwa wahusika wote umma wanazirejesha na kufikishwa mahakamani.

   Akizungumza katika mkutano huo, Askofu Gordon Kiaro wa kanisa la Pentecostal Fellowship (INT) alisema suala la kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi sio la kidini wala dhehebu na kwamba, linapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote.
   Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

  2. Mahesabu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th January 2008
   Location : manzese
   Posts : 4,068
   Rep Power : 1656
   Likes Received
   564
   Likes Given
   5929

   Default Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   Nami Nataka Kujiunga Na Kamati Hiyo......!
   Big Up ......!
   Big Up....!
   BILA RUSHWA..HAKI HAIPATIKANI....TOA RUSHWA UPATE HAKI.....(?)
   RUSHWA NA TANZANIA DAM-DAM.....!
   TAASISI IPI RUSHWA KWAO MWIKO?
   NASEMA KWA KUWA YAMENIKUTA......!

  3. Mahesabu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th January 2008
   Location : manzese
   Posts : 4,068
   Rep Power : 1656
   Likes Received
   564
   Likes Given
   5929

   Default Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   Haiwezekani Wenye Makosa Madogo Wawe Wamejaa Lupango Hali Magabacholi Wanatanua Nje...!
   BILA RUSHWA..HAKI HAIPATIKANI....TOA RUSHWA UPATE HAKI.....(?)
   RUSHWA NA TANZANIA DAM-DAM.....!
   TAASISI IPI RUSHWA KWAO MWIKO?
   NASEMA KWA KUWA YAMENIKUTA......!

  4. mambo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th June 2007
   Posts : 292
   Rep Power : 800
   Likes Received
   35
   Likes Given
   35

   Default Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   Jana mchungaji mtikila kwenye taarifa ya habari ITV aliongea sana kuwa mafisadi wasitumie nyumba za mungu kama sehemu ya kusafisha maovu yao,alisema ibilisi hawezi kuingia chumbani kwa bwana mungu na kujifanya eti yeye ni msafi.kwa kweli aliongea maneno makali sana ya kumshutumu rostam kuwa ni dharau mbele za mungu kuja kusimama kwenye mimbari ya kanisa na kuongea uchafu wake.
   Lakini Askofu mkuu jana hakupatikana kuongelea hilo jambo...,

  5. Kungurumweupe's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th June 2008
   Posts : 318
   Rep Power : 752
   Likes Received
   33
   Likes Given
   0

   Default Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   watanzania Wasitegemee Lolote La Maana Baada Ya Hii Kesi. Hii Ndio Silaha Kubwa Ya Mwisho Waliyobakiwanayo Mafisadi.

   Si Jambo Geni Kwa Mchungaji Mtikilo Kufungua Kesi Dhidi Ya Aidha Serikali Yenyewe Au Waandamizi Wakuu Wa Hiyo Serikali Kisha huifuta Kwa Kisingizio Cha Kukosa Ushahidi. Hata Hii Mwisho Wake Ni Kufutwa.

   Ninalazimika Kuamini Kwamba Mtikilo Na wenzake wameandaliwa Ili Kupotosha Na Kuua Swala Zima La Epa. Watanzania Tusisahau Kwamba Hawa Mafisadi Ndio Watoaji Wakubwa Wa Sadaka Na Zaka Huko Makanisani Na Misikitini Hivyo Tusitegemee Viongozi Wa Kidini Kuwageuka wawezeshaji Wao. Kwani Bado Wanayahitaji Hayo Mabilioni Ya Pesa Yasaidie Kujenga Makanisa Na Misikiti Zaidi. Angalieni Jinsi Akina rostoam Aziza wanavyohaha Kupeleka Vijisenti Vyao Makanisani. Kwani Wanafahamu Fika Viongozi Wa Kidini Si Lolote Wala Chochote Bali Nao Ni Mafisadi Wenzao Wanaoendeleza Ufisadi Kwa Waumini Wao Kwa Kuwakamua Kila Kidogo Walichonacho Kwa Njia Ya sadaka Na Michango Mingi Ya Ajabu!

   Tukumbuke, Siasa Za Tanzania Zimejikita makanisani Na Misikitini Tangu Enzi Za Mwalimu. Ndo Maana Serikali Iliwaundia Viongozi Hawa Wa Kidini Vyombo Kama Vile bakwata Na Mengineyo ili Kuwaweka Karibu Zaidi Na Serikali Pamoja Na Wanasiasa Kwa Ujumla.

   Hii Ndiyo Sababu Ya Kwanini Mafisadi hawajatengwa Na Makanisa Au Misikiti yao. Sanasana Wnadai Ati Wanaendelea Kuwakumbatia Kwa Kisingizio Cha Kwamba Wanawaombea Ili Waache Zambi Ya Ufisadi! Ajabu!

   *Mafisadi hawa Ni Wafadhili Wakubwa Wa Misikiti Na Makanisa. Ndio Wanaowawezesha Viongozi Wa Dini Wamiliki Majumba Na Magari Ya Anasa. Tusitegemee Lolote*. tumekwisha!

  6. Nyadundwe's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 16th January 2008
   Posts : 123
   Rep Power : 735
   Likes Received
   27
   Likes Given
   5

   Default Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   Quote By mambo View Post
   Jana mchungaji mtikila kwenye taarifa ya habari ITV aliongea sana kuwa mafisadi wasitumie nyumba za mungu kama sehemu ya kusafisha maovu yao,alisema ibilisi hawezi kuingia chumbani kwa bwana mungu na kujifanya eti yeye ni msafi.kwa kweli aliongea maneno makali sana ya kumshutumu rostam kuwa ni dharau mbele za mungu kuja kusimama kwenye mimbari ya kanisa na kuongea uchafu wake.
   Lakini Askofu mkuu jana hakupatikana kuongelea hilo jambo...,
   Ninavyofahamu mimi, Rostam alialikwa na kanisa kama mgeni rasmi katika hafla fulani, iliyohusisha pia kuchangia kwaya. Sidhani kama mualiko huo ulitokana na uwezo wake wa kushawishi wadau watoe, bali uwezo wa yeye mwenyewe kutoa miongoni mwa 'vijisenti' vyake. Yasemekana alitoa 7m. Wa kulaumiwa hapa ni kanisa ambao walitoa mwaliko huo huku wakijua kwamba watanzania wako katika juhudi za kuhakikisha watuhumiwa wa Ufisadi akiwemo RA wanachukuliwa hatua za kisheria. Hata hivyo, aibu hii kwa kanisa ni funzo kwa taasisi nyingine zinazonyemelewa na mafisadi kwa lengo la kujisafisha (Dini, majimbo, magazeti, vyama vya siasa n.k). Ni funzo pia kwa mafisadi kwamba katika vita inayoendelea dhidi yao, hawana pa kujificha!

  7. Kaa la Moto's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th April 2008
   Location : Bristol
   Posts : 7,445
   Rep Power : 83685495
   Likes Received
   588
   Likes Given
   5401

   Default Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   Quote By Nyadundwe View Post
   Ninavyofahamu mimi, Rostam alialikwa na kanisa kama mgeni rasmi katika hafla fulani, iliyohusisha pia kuchangia kwaya. Sidhani kama mualiko huo ulitokana na uwezo wake wa kushawishi wadau watoe, bali uwezo wa yeye mwenyewe kutoa miongoni mwa 'vijisenti' vyake. Yasemekana alitoa 7m. Wa kulaumiwa hapa ni kanisa ambao walitoa mwaliko huo huku wakijua kwamba watanzania wako katika juhudi za kuhakikisha watuhumiwa wa Ufisadi akiwemo RA wanachukuliwa hatua za kisheria. Hata hivyo, aibu hii kwa kanisa ni funzo kwa taasisi nyingine zinazonyemelewa na mafisadi kwa lengo la kujisafisha (Dini, majimbo, magazeti, vyama vya siasa n.k). Ni funzo pia kwa mafisadi kwamba katika vita inayoendelea dhidi yao, hawana pa kujificha!
   kanisa la KKKt Kinondoni kwa nini lilimualika Rostam? si walijua anazo feza za wizi na wao feza za wizi kwao halikuwa tatizo bali tatizo kwao ilikuwa ni vipesa hivyo vya wizi tu.
   Naona ndugu zangu wa makanisa wanachojali ni pesa tu hata kama wataambiwa zimetokana na wizi wao watapokea tu. Nawasikitikia sana.
   wakati Cuf wanataka kuchukua nchi mwaka 2000 CCM walikuja na single ya kusema Cuf ni waislamu na kwa sasa wanadai sisi Chadema ni chama cha wakristo sasa CCM nacho ni cha watu gani? Watu wakajibu mashetaaaaaniiiiii.!---Wana Kigoma.

   ....Pamoja na kansa ya uongozi wa CCM watu wataendelea kukichagua,au watu wanaweza wakachoka na kusema potelea mbali wakachagua chama KINGINE....Julius. Kambarage. NYERERE"

  8. emedichi's Avatar
   Member Array
   Join Date : 1st March 2008
   Location : Asia
   Posts : 47
   Rep Power : 713
   Likes Received
   5
   Likes Given
   0

   Default Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   Kila kesi anayofungua huyu huanza kwa kishindo then huishia hewani
   A child who is afraid of darkness can easily be forgiven, but what about an adult who is afraid of light?

  9. Kungurumweupe's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th June 2008
   Posts : 318
   Rep Power : 752
   Likes Received
   33
   Likes Given
   0

   Post Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   Quote By emedichi View Post
   Kila kesi anayofungua huyu huanza kwa kishindo then huishia hewani
   Yeye na viongozi wenzake wa din hawanalolote bali wanataka kuwayumbisha watanzania. Hawa viongozi wa dini wanachotafuta ni uhalali wao wa kuweza kuliongelea hili makanisani mwao kwa lengo la kuua mjadala ili watimize azima yao ya kuisadia serikali yao ya kifisadi. Hii ndiyo kazi yao siku zote, yaani kusaidiana na serikali kunyonya watanzania. Wanakusanya peasa makanisani kwao kwa lengo hilo hilo la kunyonya wananchi kwa kwenya mbele.

   MUNGU WASAMEHE HAWA VIONGOZI WA MAKANISAAE NA MISIKITIKO YA TZ KWANI HAWAJUI MALITENDALO.

  10. Koba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd July 2007
   Location : Pasadena California
   Posts : 5,719
   Rep Power : 1971
   Likes Received
   796
   Likes Given
   845

   Default Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   Alisema katika maandalizi ya kufungua kesi hiyo, jana kamati ilimwandikia barua Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi kuwataka waharakishe hukumu ya kesi ya Katiba namba 86/2006, iliyofunguliwa na kamati hiyo kuitaka iruhusu watu binafsi kuendesha kesi za jinai.

   ...katika vitu muhimu vya kupigania katika katiba mpya hii ni muhimu sana na itawapa weapon wananchi kupambana na system mbovu iliyopo na hii ndio imefanya nchi kama states serikali ifanye kazi yake maana wanajua wasipofanya individuals wanaweza kuleta lawsuit katika mahakama kwa chochote as long as judge anaona kuna kesi ya kusikiliza
   "Freedom is incomplete if it is exercised in poverty."-Harry Schwaz

  11. Kungurumweupe's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th June 2008
   Posts : 318
   Rep Power : 752
   Likes Received
   33
   Likes Given
   0

   Post Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   Quote By Kungurumweupe View Post
   watanzania Wasitegemee Lolote La Maana Baada Ya Hii Kesi. Hii Ndio Silaha Kubwa Ya Mwisho Waliyobakiwanayo Mafisadi.

   Si Jambo Geni Kwa Mchungaji Mtikilo Kufungua Kesi Dhidi Ya Aidha Serikali Yenyewe Au Waandamizi Wakuu Wa Hiyo Serikali Kisha huifuta Kwa Kisingizio Cha Kukosa Ushahidi. Hata Hii Mwisho Wake Ni Kufutwa.

   Ninalazimika Kuamini Kwamba Mtikilo Na wenzake wameandaliwa Ili Kupotosha Na Kuua Swala Zima La Epa. Watanzania Tusisahau Kwamba Hawa Mafisadi Ndio Watoaji Wakubwa Wa Sadaka Na Zaka Huko Makanisani Na Misikitini Hivyo Tusitegemee Viongozi Wa Kidini Kuwageuka wawezeshaji Wao. Kwani Bado Wanayahitaji Hayo Mabilioni Ya Pesa Yasaidie Kujenga Makanisa Na Misikiti Zaidi. Angalieni Jinsi Akina rostoam Aziza wanavyohaha Kupeleka Vijisenti Vyao Makanisani. Kwani Wanafahamu Fika Viongozi Wa Kidini Si Lolote Wala Chochote Bali Nao Ni Mafisadi Wenzao Wanaoendeleza Ufisadi Kwa Waumini Wao Kwa Kuwakamua Kila Kidogo Walichonacho Kwa Njia Ya sadaka Na Michango Mingi Ya Ajabu!

   Tukumbuke, Siasa Za Tanzania Zimejikita makanisani Na Misikitini Tangu Enzi Za Mwalimu. Ndo Maana Serikali Iliwaundia Viongozi Hawa Wa Kidini Vyombo Kama Vile bakwata Na Mengineyo ili Kuwaweka Karibu Zaidi Na Serikali Pamoja Na Wanasiasa Kwa Ujumla.

   Hii Ndiyo Sababu Ya Kwanini Mafisadi hawajatengwa Na Makanisa Au Misikiti yao. Sanasana Wnadai Ati Wanaendelea Kuwakumbatia Kwa Kisingizio Cha Kwamba Wanawaombea Ili Waache Zambi Ya Ufisadi! Ajabu!

   *Mafisadi hawa Ni Wafadhili Wakubwa Wa Misikiti Na Makanisa. Ndio Wanaowawezesha Viongozi Wa Dini Wamiliki Majumba Na Magari Ya Anasa. Tusitegemee Lolote*. tumekwisha!
   Hakika nimeamini kuwa watanganyika ni wadanganyika. Yaani kweli wamedanganyika na wakaamini kwamba Mtikila "anaubavu" wa kupambana na "mafisadi" kwa kufungua kesi mahakamani?! Yaani mtikila huyuhuyu ambaye anadaiwa tuvijisenti alitotukopa toka kwa mafisadi?! Hivi ni kweli inawezekana mtu mwenye akili timamu akaamua kuvua nguo zake zote, hata ile ya ndani, kisha akaamua kutembea barabarani akiwa uchi wa munyama??!!! Hivi kweli inawezekana mtikila akawashitaki wawezeshaji wake??!! Kweli??!!

  12. Koba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd July 2007
   Location : Pasadena California
   Posts : 5,719
   Rep Power : 1971
   Likes Received
   796
   Likes Given
   845

   Default Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   ...Mtikila credibility ni sifuri na kikatiba hana uwezo huo yaani kaamua kuchezea watu akili tuu na hii ndio kula yake mjini,huyu jamaa ni hatari kuliko hao mafisadi wenyewe..... saa ya ukombozi my azz!
   "Freedom is incomplete if it is exercised in poverty."-Harry Schwaz

  13. Chuma's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th December 2006
   Posts : 1,463
   Rep Power : 1058
   Likes Received
   16
   Likes Given
   4

   Default Re: Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi

   Mods...pls mada ya mtikila iunganishwe.......

  Similar Topics

  1. Procedures za kushitaki/kufungua kesi
   By Kalunguine in forum Jukwaa la Sheria (The Law Forum)
   Replies: 7
   Last Post: 29th June 2015, 07:00
  2. Tuhuma za mauaji dhidi ya Dr. Mwakyembe na wenzake
   By banyimwa in forum Jamii Intelligence
   Replies: 23
   Last Post: 11th August 2011, 12:20
  3. Simba wanataka kufungua kesi dhidi ya tanesco
   By Lighondi in forum Jokes/Utani + Udaku/Gossips
   Replies: 3
   Last Post: 12th July 2011, 13:21
  4. Replies: 4
   Last Post: 28th March 2011, 12:59
  5. Mfululizo wa Kesi ya Zombe na wenzake
   By Nyamgluu in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 157
   Last Post: 18th August 2009, 12:08

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...