Kwa upande wake, Rais Kikwete alisema kuwa wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini wamemchagua Zitto kuwa mbunge wao, lakini pamoja na hilo Zitto hana serikali, bali Serikali ni ya Chama Cha Mapinduzi haina kinyongo kwa yoyote.
Alisema ndiyo maana licha ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, imeamua kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wote bila kinyongo wala ubaguzi.
IPP Media
Kwa uelewa wangu serikali ni wananchi ambao wana haki yao na kuchagua viongozi wa kuiongoza. CCM imeunda serikali baada ya kushinda uchaguzi na wala si kwamba serikali ni ya CCM. Na ndani ya serikali kuna wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa na watumishi wengine wasio wanachama wa chama cho chote cha siasa.
Kauli ya Rais Kikwete kusema serikali ni ya CCM anawadanganya wananchi.

Reply With Quote



Follow Us Here