Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Watanzania tuache hizi hulka zetu: Si dili. Watanzania tunaangamia. Taifa linaangamia.

    Report Post
    Results 1 to 3 of 3
    1. #1
      Gobret's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th June 2010
      Posts : 215
      Rep Power : 502
      Likes Received
      42
      Likes Given
      7

      Cool Watanzania tuache hizi hulka zetu: Si dili. Watanzania tunaangamia. Taifa linaangamia.

      Tatizo kubwa la Watz ni ukosefu wa elimu, umasikini wa mawazo kwa wenye elimu. Maana ni vigumu sana kumtofautisha msomi na asiyesoma. Msomi ananena na kutenda sawa sawa na asiyepata nafasi hiyo. Tena bora huyu asiye na elimu darasa. Wasomi wamekaa kimya wanatetea vibarua yao. Nchi inaliwa na wachache. Nchi haina ndege lakini raisi ana ndege ya kufanya omba omba kila kukicha.

      Sijui niseme hili ni kosa la Mkapa maana ndiye aliyenunua hii ndege na yeye hakutumia na hakuwa omba omba. Sasa huyu ****** ndiyo kaona dili kweli. Akitembeza pua na bakuli. Anaikamua nchi kama kupe. Ndege ya nini ya raisi kwa nchi masikini? Watz. wamekaa kimya, Nchi ipo gizani. Wanachapa usingizi. Vyuo vikuu, vyuo vya kati, shule za sekondari nk kazi za taaluma haziendi kwa maana umeme ni tatizo.

      Tunapitisha siku ziende. Wapinzani nao hawayaoni matatizo ya watanzania. Sijui mpaka waambiwe ndiyo wachangamke. Wanafunzi wa vyuo vikuu kama watoto wasio na serikali, maana serikali haiwajali kabisa. Hawapati haki zao stahili. Na wao wamekaa kimya kuhusu suala la umeme, wamekazania fedha zao. Ndio lkn vipi kuhusu elimu wanayokosa???????? Kwa kukosa umeme? Siku hizi walimu wa vyuo vikuu na kati wamerudi kwenye enzi za kufundisha kwa chaki. Maana Mungu kama katulaani vile.

      Lkn kumbe ni sisi wenyewe. Hatuwawajibisha hawa viongozi ambao ni mizigo kwa ustawi wa Taifa la Tz. Tunawapa kura tena lukuki, kwa nini wasitutukane? Tuamkeni, Taifa linaangamia. Kila mtu kwa nafasi yake. Tusijali maslahi binafsi. Tutetee ustawi wa Taifa letu.

      Achana na Raisi na mke omba omba kama Matonya. Bora wakahamia Dodoma ili waungane na akina Matonya huko. Hatuoni faida ya kuwa na rais mbabaishaji wa aina hii. Mawaziri kama wahudumu wa baa vile. Watz kama wateja wao. Nchi inanuka rushwa kila kona. Wabunge kama machokoraa vile. Kazi kupiga makofi na kudai posho. Hakuna wa kusimamia haki.

      Angalia maendeleo ya mikoa fulani fulani ambapo CCM imekita mizizi. Watu wake ni omba omba, wanatembeza bakuli barabarani kama m/kiti wao. Hawana haya.

      Viongozi wa dini nao kama hawaamini vile ktk imani yao. Mara waseme Mungu katuchagulia huyu jamaa. Ni chaguo lake asilani. Hah! Nao wameshtuka. Wameingia mkenge. Sasa wanajutia, toba kila kukicha, Mungu naye hatakikuwasikiliza. Maana wamelitumia vibaya jina la Mungu kwa maslahi yao binafsi.

      Nyerere baba yetu; naye alituahidi kuwa atatuombea kwa Mungu. Sasa hata yeye katusahau. Maana kuna kila sababu ya kutusahau. Watz tumeacha ile misingi mizuri aliyoijenga na badala yake tunajali maslahi binafsi. Yeye alipigania haki, amani na upendo. Leo chuki, mifarakano ghilba nk ndio misimamo yetu.

      Tutasema nini kuhusu umasikini wetu? Jibu: (1)........................... .......(2).................... .............(3).............. ...............

    2. Miaka 50

    3. #2
      Mbayuwayu2008's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 10th April 2011
      Posts : 5
      Rep Power : 412
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Watanzania tuache hizi hulka zetu: Si dili. Watanzania tunaangamia. Taifa linaangamia.

      Watz. huwajui vizuri. Baadhi yao ni kama kondoo wa Maasai. Hawaoni mbele wala nyuma. KAzi yao kutia tick kwenye kisanduku cha CCM wakati wa kupiga kura. Mabadiliko ya kweli huanza na mtu mhusika. Usitegemee mabadiliko kama tunataka yaanze kwa wengine.

      Kuna sumu nyingi pandikizi za CCM. Na sasa tunajutia na tutajuta kweli. Kweli tuna raisi safi sana. Bingwa wa kuharibu majina mazuri ya watz. Hii hali ya kuona omba omba ni dili sijui imeanzia wapi. Risi bingwa wa omba omba na Watz wenyewe wamegeuka omba omba. Tutafika?

      We, sijui nani vile (Gobret) hapo ulipo na wewe omba omba tu. Usinibishie nakuona. Na mimi omba omba. Sote tu omba omba. Nani yupo salama?

    4. #3
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2885
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default Re: Watanzania tuache hizi hulka zetu: Si dili. Watanzania tunaangamia. Taifa linaangamia.

      Kuhusu kuombaomba mzee Ben nae alikuwa akiomba,aliwaita NCHI WAHISAN.......labda ndege ndio hakuitumia........nawahurumia sana wanafunz,kwani wanasoma kwa shida

    5. RukaaJuu Final

    Similar Topics

    1. Replies: 0
      Last Post: 3rd November 2011, 10:54
    2. Replies: 17
      Last Post: 13th June 2011, 18:59
    3. Kukata tamaa:je,ni hulka ya watanzania?
      By Technician in forum JF Chit-Chat
      Replies: 1
      Last Post: 19th May 2011, 09:50
    4. Watanzania wenye ulemavu 'dili' Kenya
      By BabuK in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 0
      Last Post: 10th October 2010, 13:22
    5. Common Market: Watanzania tuamke tuache woga
      By Ogonga in forum Jamii Intelligence
      Replies: 0
      Last Post: 28th April 2010, 08:16

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...