TiGo Says
    Show/Hide This

    Topic: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

    Report Post
    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 31 to 60 of 171
    1. #1
      KAMBOTA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Posts : 151
      Rep Power : 392
      Likes Received
      55
      Likes Given
      69

      Default Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Siku za hivi karibuni kumekuwa na kundi kubwa la watu waliojipambanua kuwa wao ni wakosoaji wa Nyerere na hata baadhi yao wamethubutu kumwita dikteta ingawaje kwa miaka mingi Nyerere amekuwa akiheshimiwa sana miongoni mwa wananchi wa kawaida wa Tanzania.

      Mara nyingi ukosoaji huwa umekuwa ukifanywa na vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na magazeti, blogs na wakati mwingine wanasiasa na watu binafsi mpaka sasa sitakosea nikisema ukosoaji dhidi ya Nyerere umekithiri kwa siku za karibuni.

      Kwa bahati mbaya mimi nimezaliwa miaka ambayo Nyerere ameshastaafu ingawaje nilifanikiwa kusoma vitabu vyake na hata kumwona. Kupitia maandiko yake sijaona jambo baya lakini bado sishawishiki kuwa alikuwa anapatia kila kitu.

      Hivyo ndugu wadau naomba kufahamu juu ya Nyerere, sihitaji sifa zake tu abadani sihitaji udhaifu wake pekee bali nahitaji kumfahamu Nyerere zaidi ya yale yaliyoandikwa vitabuni, nataka kumjua kiundani ili mwisho wa siku nifahamu je wanaompinga Nyerere wana hoja za msingi au wanatafuta umaarufu ama kutoka?

      NAWASILISHA

    2. #31
      X-PASTER's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Firdaws (Paradise)
      Posts : 11,441
      Rep Power : 7552
      Likes Received
      1220
      Likes Given
      0

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Zidumu Fikra sahihi za mwenyekiti wa ccm!
      “I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”

      'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.

      (¯`·._.•X-Paster™•._.·´¯)

    3. #32
      Waberoya's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,773
      Rep Power : 1655
      Likes Received
      1372
      Likes Given
      2560

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By RAJ PATEL JR View Post
      The Boss, please help me to understand when and why people are referred to as "Engineer...so and so".
      I've heard and am aware of the titles or prefixes like Sir, Dr. Prof. Ambassador etc, but not engineer Ahamedinajad or Engineer Mark Mwandosya....What's gonna be next, Journalist Ulimwengu? Entomologist Kweka, Geologist Mbise, Sociologist Mkwasa, Hair Stylist Mwajuma, Barber Hassani or Accountant Hussein?????
      where are you my dear? engineer is a sign of responsibility nothing else, bungeni iliishajadiliwa, mtu hawezi kusimamisha gorofa 100 inayobeba roho maelfu na asiitwe kwa titile yake..ni title ya responsibility na unatakiwa uitwe kisheria, kama haujasajiliwa na serikali ni illegal kujiita engineer so and so!!! na ni kosa kutojiita!!!1 ni sheria, najua utasema imeandikwa wapi, fuatilia sasa baada ya kukupa huu mwanga, siyo ujiko ni responsibility---kwa maana ya liability!
      mbuva likes this.
      Hakuna msafi CCM, hakuna hata mmoja,..wote wamepotea hivyo wamepoteza utukufu wa uzalendo na upendo kwa taifa hili, na kupoteza sifa ya uraia

    4. #33
      Waberoya's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,773
      Rep Power : 1655
      Likes Received
      1372
      Likes Given
      2560

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      jamani hakuna jipya hapa; madai yote mawili yanayotolewa dhidi ya Nyerere hana ya ukweli:

      a. Upande wa Pili wa Nyerere (mapungufu) yameandikwa kwa kirefu kuanzia miaka ya sitini. Hakuna kiongozi wa Tanzania aliyekosolewa na kubainishwa mapungufu yake ya kisera na kiuongozi kama Nyerere. None.

      b. Nyerere hakufanya makosa; hakuna mtetezi yeyote wa Nyerere mwenye akili timamu ambaye amewahi kudai kuwa Nyerere hakufanya makosa. Hata yeye mwenyewe hakuwahi kudai kuwa hajakosea (ushahidi umewekwa hapa wa kutosha) na siyo leo tu, ndiye kiongozi pekee wa TAnzania aliyeandika kitu kinachoitwa "Tujisahihishe" wakati mwingine natamani niiweke hapa ili watu wajue kuwa Nyerere hakuwa na mashaka na kukosolewa wala kujikosoa as a leader!

      So.. hizi myths za kuwa Nyerere hakupenda kukosolewa au Nyerere alitukuzwa sana hazina msingi katika historia.
      Hapa mkuu you are dead wrong!!

      Mimini mwalimu wa chipukizi, nikiwa iringa mwaka 1969-1976, kwa kifupi ninamfahamu Nyerere kwa kumuona, kumgusa, kukaa naye..Nyerere was something else, alikuwa anatisha yet alikuwa anapendwa

      issue za ukimsema vibaya unaishia kubaya was not a myth was real........mkuu unapenda mno!!!!
      The Boss and KAMBOTA like this.
      Hakuna msafi CCM, hakuna hata mmoja,..wote wamepotea hivyo wamepoteza utukufu wa uzalendo na upendo kwa taifa hili, na kupoteza sifa ya uraia

    5. #34
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 26,634
      Rep Power : 22539
      Likes Received
      8482
      Likes Given
      4308

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By Eng. Burton A. Bukuku View Post
      Hapa mkuu you are dead wrong!!

      Mimini mwalimu wa chipukizi, nikiwa iringa mwaka 1969-1976, kwa kifupi ninamfahamu Nyerere kwa kumuona, kumgusa, kukaa naye..Nyerere was something else, alikuwa anatisha yet alikuwa anapendwa

      issue za ukimsema vibaya unaishia kubaya was not a myth was real........mkuu unapenda mno!!!!
      sasa si tuna rahisi anayependwa na anayesikiliza sana tena ana sura nzuri kweli dr. so and so?; hatishi? are we happy?
      Revolutionalist and KAMBOTA like this.
      mwanakijiji@jamiiforums.com
      Binafsi NAKERWA, NAKASIRISHWA, NA KUCHUKIZWA sana na haya mambo kwamba eti "ameshauriwa vibaya na wasaidizi wake!" Huwa mara zote najiuliza ikiwa anashauriwa vibaya ni kwanini basi kila wakati awe anachukua huo ushauri mbaya!! - NasDaz

    6. #35
      Waberoya's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,773
      Rep Power : 1655
      Likes Received
      1372
      Likes Given
      2560

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By KAMBOTA View Post

      Siku za hivi karibuni kumekuwa na kundi kubwa la watu waliojipambanua kuwa wao ni wakosoaji wa Nyerere na hata baadhi yao wamethubutu kumwita dikteta ingawaje kwa miaka mingi Nyerere amekuwa akiheshimiwa sana miongoni mwa wananchi wa kawaida wa Tanzania.

      Mara nyingi ukosoaji huwa umekuwa ukifanywa na vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na magazeti, blogs na wakati mwingine wanasiasa na watu binafsi mpaka sasa sitakosea nikisema ukosoaji dhidi ya Nyerere umekithiri kwa siku za karibuni.

      Kwa bahati mbaya mimi nimezaliwa miaka ambayo Nyerere ameshastaafu ingawaje nilifanikiwa kusoma vitabu vyake na hata kumwona. Kupitia maandiko yake sijaona jambo baya lakini bado sishawishiki kuwa alikuwa anapatia kila kitu.

      Hivyo ndugu wadau naomba kufahamu juu ya Nyerere, sihitaji sifa zake tu abadani sihitaji udhaifu wake pekee bali nahitaji kumfahamu Nyerere zaidi ya yale yaliyoandikwa vitabuni, nataka kumjua kiundani ili mwisho wa siku nifahamu je wanaompinga Nyerere wana hoja za msingi au wanatafuta umaarufu ama kutoka?

      NAWASILISHA
      Mdogo wangu, kama umesoma vitabu vya Nyerere na article zake zoote, lazima umjue, nenda soma kazi za wasomi na analysts mbali, watakuja na kukupa kila mtu view yake na utaona.

      View za udikteta hazijasemwahapa tu JF, zimesemwa kila kona ya dunia hii, inategemea nani anasema, na kwa nini anasema. watu wasiopenda ujamaa, they will surely call you dictator because to implement socialism ypu need to be a dictator nothing else, china, warusi, cuba ni mifano mizuri

      Kwa hiyo logically kama ujamaa ulifeli...Nyerere hakuwa dikteta! kama alikuwa dikteta basi hakuwa yule dikteta mzuri kwa hiyo alifeli katika udikteta wake!!! fikiri wewe

      Personally nimewafuatilia sana hawa jamaa http://digital.films.com/play/V4PPVM ambao ukisoma wansema kabisa bila kuuma maneno kuwa Nyerere alikuwa diktator!!! wala hajawakopesha!!! nimewafuatilia nikagundua ni watu fulani walikosa mambo fulani, lakini wamesema.

      Fuatilia mijadala ya Nyerere humu, ziko thread nyingi sana, sana

      Kwa kifupi wakosoaji wa Nyerere wamegawanyika sehemu kubwa

      1. wako ambao anaona ni sahihi kumkosoa mtu yeyote kwa nafasi yake-kwa makosa ambayo yanaendana na ufahamu wao, kwangu mimi hawa ni genuine criticiser
      2. wako wanaomkosoa kwa sababu ya misingi ya dini yao ( na hawa wamelishwa sumu na wazazi wao au jamii wanayotoka)
      3. wako wanaomkosoa Nyerere kwa sababu leo hii wameshindwa kufikia rank yake, ubora wake, na wameshindwa kuwaongoza watanzania leo hii na wanatupa mawe kwa Nyerere!

      Sasa ni wakati gani utamjua yupi ni yupi ni ngumu!
      kuwa unaweza kuwazuia ni ngumu!
      kuwa unarusha thread kila siku kumpamba Nyerere ni ngumu!
      Kuwa kila thread ya ubayawa Nyerere ikianza utetea ni ngumu!

      kwani wakosaji hawa wengi hawako JF, wako makwao, wanakutana vilabuni na baa, wanakutana kwenye harusi....hawako humu tu!

      Juzi nilikuwa na mzee mmoja wa miaka 70, akaelezea kwa nini ufisadi ulianza Tanzania, akarudi na kumkosoa sana Nyerere...sana, kuna siku ilirushwa thread hapa ya Nyerere kupunguza mshahara wake, nikaanza kuuliza wazee wawili watatu, ambao nao walikuwepo, nilikuwepo kwenye ile incident, lakini nikataka kuona wazee wale hasa walioiweka TANU na CCM moyoni wanasemaje...wote (4) walisema negative, mmoja (1) alisema positive, wakati yule mmoja aliyesema positive alisema kwa hisia kali kuliko wale wanne! u see!!

      Kwa hiyo ni view za watu

      I once said, HAKUNA MTU YEYOTE LEO HII, ALIYE HAI ambaye anaweza kumtetea Nyerere! hayupo wako lovers tu, lakini si watetezi!!

      Nyerere atajitetea kwa kazi zake, zitasimama vizazi vyote vijavyo, wakati wengine wamekufa, yeye jina lake litakuwepo, miaka 300 kutoka sasa sura ya Nyerere itakuwa kwenye fedha (kama zitaendelea kutumika) na kipindi hicho vitukuu vya vitukuu vyetu vitaulizana " aka kababu ndio kanani kwenye fedha' WATAJIBIZANA NDIO BABA WA TAIFA LA TANZANIA!!!

      Lakini atasemwa, atadhihakiwa, atatukanwa, atasifiwa, atapendwa, kwa sababu ni nyota ni kiongozi ndio gharama zake!!!! is natural is common!! leo hii washington kosa lake la kusema vi uongo uongo vingi, vinasemwa mpaka leo mpaka kesho.

      Ukinipa nafasi ya kumkosoa Nyerere, nitamkosoa kwa siku nzima, ukinipa nafasi ya kumsifia Nyerere nitamsifia nusu siku!
      KAMBOTA likes this.
      Hakuna msafi CCM, hakuna hata mmoja,..wote wamepotea hivyo wamepoteza utukufu wa uzalendo na upendo kwa taifa hili, na kupoteza sifa ya uraia

    7. #36
      Waberoya's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,773
      Rep Power : 1655
      Likes Received
      1372
      Likes Given
      2560

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      sasa si tuna rahisi anayependwa na anayesikiliza sana tena ana sura nzuri kweli dr. so and so?; hatishi? are we happy?
      Nafikiri bado assumptions zako ziko wrong! -unarudia rudia sana kosa hili soma post yangu ya juu!!

      Haina maana nikimkosoa Nyerere basi nampenda Kikwete!!!!!!!!!!!!!! is not like that,

      Niki-declare sehemu kuwa simpendi A kwa sababu nampenda B, ningesema hivyo nayo si dhambi-ila siyo akili!

      Kwa hiyo wewe uko kwenye group zuri sana la mpenzi wa Nyerere , sina tatizo unampenda Nyerere kwa ule upendo wa dhati kabisa, ..ila usitupe au kutulazimisha wengine tuwapende wengine kwa sababu ya kuwa tunamsema vibaya Nyerere..naweza kuwa nampenda ila kivingine sana!!!

      Said this I dont like Kikwete in many ways and I dont like Nyerere in many ways...to be fair, they all have weakness and strengths...Nyerere's quality of leadership ziko juu sana ya Kikwete (mawazo yangu)..happy now??? lakini hainizuii kumkosoa Nyerere...what??? sad now?

      Review your assumptions au hypotheses!
      mbuva and The Boss like this.
      Hakuna msafi CCM, hakuna hata mmoja,..wote wamepotea hivyo wamepoteza utukufu wa uzalendo na upendo kwa taifa hili, na kupoteza sifa ya uraia

    8. #37
      The Boss's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 18th August 2009
      Location : DARESALAAM
      Posts : 12,679
      Rep Power : 10005
      Likes Received
      7391
      Likes Given
      10219

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By eng. Burton a. Bukuku View Post
      nafikiri bado assumptions zako ziko wrong! -unarudia rudia sana kosa hili soma post yangu ya juu!!

      Haina maana nikomkosa nyerere basi nampenda kikwete!!!!!!!!!!!!!! Is not like that,

      niki-diclare sehemu kuwa simpendi a kwa sababu nampenda b, ningesema nayo si dhambi-ila siyo akili!

      Kwa hiyo wewe ukokwenye group zuri sana la mpenzi wa nyerere , sina tatizo unampenda nyerere kwa ule upendo wa dhati kabisa, ..ila usitupe wengine tuwapende wengine kwa sababu ya kuwa tunamsema vibaya nyerere..naweza kuwa nampenda ila kivingine sana!!!

      Review your assumptions au hypotheses!
      ha ha haaaaa
      i cant add a word here ..lol
      Waberoya likes this.
      SO MANY RELATIONSHIPS, YET SO LITTLE LOVE.....

    9. #38
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 26,634
      Rep Power : 22539
      Likes Received
      8482
      Likes Given
      4308

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By Eng. Burton A. Bukuku View Post
      Nafikiri bado assumptions zako ziko wrong! -unarudia rudia sana kosa hili soma post yangu ya juu!!

      Haina maana nikimkosoa Nyerere basi nampenda Kikwete!!!!!!!!!!!!!! is not like that,

      Niki-declare sehemu kuwa simpendi A kwa sababu nampenda B, ningesema hivyo nayo si dhambi-ila siyo akili!

      Kwa hiyo wewe uko kwenye group zuri sana la mpenzi wa Nyerere , sina tatizo unampenda Nyerere kwa ule upendo wa dhati kabisa, ..ila usitupe au kutulazimisha wengine tuwapende wengine kwa sababu ya kuwa tunamsema vibaya Nyerere..naweza kuwa nampenda ila kivingine sana!!!

      Said this I dont like Kikwete in many ways and I dont like Nyerere in many ways...to be fair, they all have weakness and strengths...Nyerere's quality of leadership ziko juu sana ya Kikwete (mawazo yangu)..happy now??? lakini hainizuii kumkosoa Nyerere...what??? sad now?

      Review your assumptions au hypotheses!
      ooh noo inabidi unisome vizuri; sijasema unampenda Kikwete; nimesema Kikwete si anapendwa na hatishi kama Nyerere (ambacho ni kipimo chako wewe kuwa alikuwa anatisha!). Sasa nimesema kama Nyerere kwa maelezo yako alikuwa anatisha na kupendwa kwa wakati mmoja alikuwa mbaya kwa sababu hiyo basi Kikwete lazima awe bora kwa sababu hatishi na anapendwa. Kikwete ana tabasamu zuri, haogopwi kama alivyokuwa anaogopwa Nyerere. Ndio swali, je tumefurahi na Kikwete asiyetisha na anayependwa?
      KAMBOTA likes this.
      mwanakijiji@jamiiforums.com
      Binafsi NAKERWA, NAKASIRISHWA, NA KUCHUKIZWA sana na haya mambo kwamba eti "ameshauriwa vibaya na wasaidizi wake!" Huwa mara zote najiuliza ikiwa anashauriwa vibaya ni kwanini basi kila wakati awe anachukua huo ushauri mbaya!! - NasDaz

    10. #39
      The Boss's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 18th August 2009
      Location : DARESALAAM
      Posts : 12,679
      Rep Power : 10005
      Likes Received
      7391
      Likes Given
      10219

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By mzee mwanakijiji View Post
      ooh noo inabidi unisome vizuri; sijasema unampenda kikwete; nimesema kikwete si anapendwa na hatishi kama nyerere (ambacho ni kipimo chako wewe kuwa alikuwa anatisha!). Sasa nimesema kama nyerere kwa maelezo yako alikuwa anatisha na kupendwa kwa wakati mmoja alikuwa mbaya kwa sababu hiyo basi kikwete lazima awe bora kwa sababu hatishi na anapendwa. Kikwete ana tabasamu zuri, haogopwi kama alivyokuwa anaogopwa nyerere. Ndio swali, je tumefurahi na kikwete asiyetisha na anayependwa?
      nafikiri wamasema two wrongs do not make it right lol
      SO MANY RELATIONSHIPS, YET SO LITTLE LOVE.....

    11. #40
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 26,634
      Rep Power : 22539
      Likes Received
      8482
      Likes Given
      4308

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By The Boss View Post
      nafikiri wamasema two wrongs do not make it right lol
      duh hii lugha kwa kweli ngumu. I'm trying kwa kweli.
      The Boss likes this.
      mwanakijiji@jamiiforums.com
      Binafsi NAKERWA, NAKASIRISHWA, NA KUCHUKIZWA sana na haya mambo kwamba eti "ameshauriwa vibaya na wasaidizi wake!" Huwa mara zote najiuliza ikiwa anashauriwa vibaya ni kwanini basi kila wakati awe anachukua huo ushauri mbaya!! - NasDaz

    12. #41
      The Boss's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 18th August 2009
      Location : DARESALAAM
      Posts : 12,679
      Rep Power : 10005
      Likes Received
      7391
      Likes Given
      10219

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By mzee mwanakijiji View Post
      duh hii lugha kwa kweli ngumu. I'm trying kwa kweli.

      ha ha haaaa
      actually nimeanza hata kujua nini utaandika next lol
      since engineer bukuku alivyosema tatizo lako ni kuwa
      you love nyerere too much....its love......
      Naelewa usichokielewa
      SO MANY RELATIONSHIPS, YET SO LITTLE LOVE.....

    13. #42
      Waberoya's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,773
      Rep Power : 1655
      Likes Received
      1372
      Likes Given
      2560

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      ooh noo inabidi unisome vizuri; sijasema unampenda Kikwete; nimesema Kikwete si anapendwa na hatishi kama Nyerere (ambacho ni kipimo chako wewe kuwa alikuwa anatisha!). Sasa nimesema kama Nyerere kwa maelezo yako alikuwa anatisha na kupendwa kwa wakati mmoja alikuwa mbaya kwa sababu hiyo basi Kikwete lazima awe bora kwa sababu hatishi na anapendwa. Kikwete ana tabasamu zuri, haogopwi kama alivyokuwa anaogopwa Nyerere. Ndio swali, je tumefurahi na Kikwete asiyetisha na anayependwa?
      Acha spinning we mzee wangu!

      unataka view zangu? Kikwete naye anatisha!

      Jaribu kuandamana uone, jaribu kudai haki uone....tisho lakikwete liko so openly! anatumia mtutu kutawala na anaua na usalama wa taifa kutisha watu.

      Nyerere alikuwa anatumia usalama wa taifa na anakupoteza kabisa

      hawa wote mambo yao yataandikwa tu vizazi vyote
      Hakuna msafi CCM, hakuna hata mmoja,..wote wamepotea hivyo wamepoteza utukufu wa uzalendo na upendo kwa taifa hili, na kupoteza sifa ya uraia

    14. #43
      Waberoya's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,773
      Rep Power : 1655
      Likes Received
      1372
      Likes Given
      2560

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      duh hii lugha kwa kweli ngumu. I'm trying kwa kweli.
      Kweli mzee hasa pale unavyotaka iandikwe kama unavyotaka wewe!
      Hakuna msafi CCM, hakuna hata mmoja,..wote wamepotea hivyo wamepoteza utukufu wa uzalendo na upendo kwa taifa hili, na kupoteza sifa ya uraia

    15. #44
      ritz's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 6,752
      Rep Power : 6879
      Likes Received
      1506
      Likes Given
      105

      Default

      Quote By OneManArmyMan View Post
      Eti "Emotional Intelligence-Groups EI", "Visionary", "Integrity"??? Duuh! Hayo maelezo uliyotoa yaani hayaendani kabisa na maana halisi ya dhana hizo za kiingereza na tena za kigeni. Mswahili bana akijifanya naye kaenda shule, inakuwa taabu tupu!
      Mkuu acha utumwa wa kiakili, wewe ukiona mtu anajua kiingereza au kuandika basi wewe unaona eti kaenda shule! wewe ukifika Uingereza utasema Waingereza wote ni Wasomi, Kiingereza ni lugha kama kichagga tu, jibu hoja kwa wanaomkosoa Nyerere

    16. #45
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 26,634
      Rep Power : 22539
      Likes Received
      8482
      Likes Given
      4308

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By Eng. Burton A. Bukuku View Post
      Acha spinning we mzee wangu!

      unataka view zangu? Kikwete naye anatisha!

      Jaribu kuandamana uone, jaribu kudai haki uone....tisho lakikwete liko so openly! anatumia mtutu kutawala na anaua na usalama wa taifa kutisha watu.

      Nyerere alikuwa anatumia usalama wa taifa na anakupoteza kabisa

      hawa wote mambo yao yataandikwa tu vizazi vyote
      Kikwete anafanana sana na Nyerere then. Ni Dikteta naye?
      mwanakijiji@jamiiforums.com
      Binafsi NAKERWA, NAKASIRISHWA, NA KUCHUKIZWA sana na haya mambo kwamba eti "ameshauriwa vibaya na wasaidizi wake!" Huwa mara zote najiuliza ikiwa anashauriwa vibaya ni kwanini basi kila wakati awe anachukua huo ushauri mbaya!! - NasDaz

    17. #46
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 26,634
      Rep Power : 22539
      Likes Received
      8482
      Likes Given
      4308

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By The Boss View Post
      ha ha haaaa
      actually nimeanza hata kujua nini utaandika next lol
      since engineer bukuku alivyosema tatizo lako ni kuwa
      you love nyerere too much....its love......
      Naelewa usichokielewa
      the opposite could be true kwako na kwa wanaomchukia Nyerere. They hate him too much.
      KAMBOTA likes this.
      mwanakijiji@jamiiforums.com
      Binafsi NAKERWA, NAKASIRISHWA, NA KUCHUKIZWA sana na haya mambo kwamba eti "ameshauriwa vibaya na wasaidizi wake!" Huwa mara zote najiuliza ikiwa anashauriwa vibaya ni kwanini basi kila wakati awe anachukua huo ushauri mbaya!! - NasDaz

    18. #47
      SaidAlly's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd January 2011
      Posts : 683
      Rep Power : 506
      Likes Received
      180
      Likes Given
      22

      Default

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      sasa si tuna rahisi anayependwa na anayesikiliza sana tena ana sura nzuri kweli dr. so and so?; hatishi? are we happy?
      Hahahahah.....wakanywe nae kahawa sasa!Mzee Mwanakijiji! Kwakweli mie ninapoona watu wanajaribu kutafuta vijisababu vya nguvu kuthibitisha Nyerere alikua Mtu mbaya sijui hata wanataka nini?? Hatukatai kuna aliyokosea, haya watupe basi alikuja akapatia?? Kama alikua hafai angalia leo hii vitu vyote alivyotuasa tusivifanye waliomfuata wakafanya-nini kinatokea?? Alituasa khs JK, nini kinatokea? Azimio la Arusha kwanini baadhi ya viongozi wanadai lirudi? Uongozi wa Umma alifanya ni kazi ya kutojirimbikizia mali, angalia leo marumbano ya posho-wote wanaotaka ziendelee hamna hata anaetoa mashiko ya maana zaidi ya kusingizia ni sheria, mara tuzitumia kuwasaidia wananchi, je, ndio maelekezo ya matumizi ya hizo posho mliyopewa?? Basi badilisheni jina, ili mzifanyie retirements na kuwe na justification inayokubalika kwy auditing. Katika mambo ya maendeleo, angalia kwa uchache tu vitu alivyoanzisha kama vingeendelezwa vizuri leo hii tungekua wapi? Sidhani hata kama tungehitaji vyama vingi.

    19. #48
      Waberoya's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,773
      Rep Power : 1655
      Likes Received
      1372
      Likes Given
      2560

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      Kikwete anafanana sana na Nyerere then. Ni Dikteta naye?
      Uko huru kusema dikteta au la, definition ya u-dikteta iko kwenye mawazo na standard ya mtu personally! is not universal and it will never be!!

      nadhani nimeishawahi kukujibu kama hivi mkuu!! sijawahi kusema Nyerere dikteta, ila sitampinga mtu anayemwita Nyerere dikteta, wala simtampinga wanaomwita Kikwete dikteta (lawyers wa kanada wamesema Kikwete anatawala kidikteta kwa mauaji ya Nyamongo)!

      MKJJ neno dikteta wanapewa mpaka akina baba majumbani, walimu wakuu wa mashuleni...mpak wachungaji.....Kakobe juzi zmeitwa dikteta!!

      sasa hizi ligi zako za kusema ikiwa A iwe B, siziwezi hizi ligi mkuu!!

      pole mkuu!
      Hakuna msafi CCM, hakuna hata mmoja,..wote wamepotea hivyo wamepoteza utukufu wa uzalendo na upendo kwa taifa hili, na kupoteza sifa ya uraia

    20. #49
      matunge's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 189
      Rep Power : 410
      Likes Received
      32
      Likes Given
      10

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By Malaria Sugu View Post
      aliwanyima watu wa pwani elimu, na kuwekeza sana arusha na kuitwa azimio la kuijenga arusha
      unasikitisha ndugu!! ulitaka awashike kwa nguvu na kuwapeleka shule? pwani? hujui kama kwa sehemu kubwa (pwani) ilikaliwa na waarabu ambao hawakujali elimu dunia.Arusha hujui ni moja ya maeneo (pamoja na kilimanjaro) yaliyokaliwa na wazungu waliowekeza katika elimu kwa kujenga shule, na hospitali. Pia ujue kama Nyerere asingelitaifisha shule za wazungu kuwa za umma sijui leo ungelisema nini? maana hata hao wakazi wa pwani wachache waliosoma sijui wangelisomea wapi??? funguka na uweze kuchambua mambo kwa mapana yake na si kuingiza udini hapa.
      mbuva likes this.

    21. #50
      KAMBOTA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Posts : 151
      Rep Power : 392
      Likes Received
      55
      Likes Given
      69

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      the opposite could be true kwako na kwa wanaomchukia Nyerere. They hate him too much.
      Hapa ndiyo ninapoanza kushawishika kuwa Nyerere hahitaji kujitetea bali maisha yake mwenyewe yanajenga utetezi mkubwa, sasa ndugu yangu Mwanakijiji sijakupata vizuri ama sijakuelewa kwa hivyo ni swala la opposite tu? kwa maana mimi siamini kuwa unampenda NYERERE nachojua unaandika ukweli kuhusu mawazo, sera na fikra za NYERERE au nimekosea mkuu?

    22. #51
      mwanaharakat's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2011
      Posts : 405
      Rep Power : 444
      Likes Received
      64
      Likes Given
      0

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Ni bora utawala Dikteta Nyerere watz maskini walienda shule bure kwa uchumi uliotegemea pamba, mkonge na mazao mengine ya kilimo kuliko leo tunategemea dhahabu, Tanzanite, Almasi, Mito na maziwa, mbuga za wanyama etc. Ni bora utawala wa Kimaskini wa Dikteta Nyerere viongozi wake hawakuwa mafisadi, wabaguzi wa dini na kabila, wabadhirifu, matajiri, waroho, wachumia tumbo, waongo kama hawa wa leo wa kidemokrasia. Nyeree was the best than Ever.
      Mzee Mwanakijiji and mbuva like this.

    23. #52
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 1,658
      Rep Power : 755
      Likes Received
      1507
      Likes Given
      955

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Nafuatilia mijadala mingi kuhusu Nyerere. Kuna kitu watu wanakiificha au hawataki kukikubali. Nyerere kama mwanadamu hakosi sura mbili . Sura hizi ni ya yale mema aliyofanya na yale mabaya aliyofanya. Mema yana sura moja ya wema, mabaya yan sura mbili za ubaya, kwanza ni je, ubaya ulikuwa wa dhamira na pili, ni kwa makosa ya kibinadamu!

      Wengi ambao kwa kusema ukweli hawasomi au hawakuwahi kuishi nyakati za Nyerere wanadiriki kuongelea ya Nyerere bila kuwa na reference kwasababu tu wanahubiriwa au kufundishwa. Mapungufu haya ambayo ni sehemu kubwa ya udhahifu wetu watanzania ndiyo chanzo cha watu kuanzisha topic ile ile kila kukicha. Inashangaza wasio Watanzania wanaweza kuandika na wanaufahamu mkubwa sana kuliko sisi kuhusu Nyerere ambaye tuna access na nyaraka zote ikiwa ni pamoja na majarida, vitabu na hata watu waliofanya kazi naye kwa ukaribu sana.

      Matokeo ya kusikia au kusimuliwa yanadhihirika kwa watu kushindwa kutetea hoja zao kwa ushahidi. Wengi wanapenda kujadili kwa hisia tu ili waweke nadharia zao lakini inapowekwa nyaraka ya kuthibitisha hawana uwezo wa kuitetea.
      Tumeona hapa JF kila ikiwekwa nyaraka inayomhusu Nyerere watu wanakimbia na kesho yake unakuta Thread mpya iliyoanzishwa kwa nadharia. Fikiria mtu anaposema Nyerere aling'oa reli ya Dar -Mtwara hapa ni nini kama si masimulizi bila ya utafiti au uthibitisho wa aina yoyote.

      Nyerere kama Icon na Beacon anachambuliwa kuliko viongozi wengine na hiyo ndiyo privilege ya great personality. Nina mambo ninayoyaeleza kila siku kuhusu mapungufu ya mwalimu, lakini hayo siwezi kuyatumia kuficha mema aliyoyafanya. Hakuna ushindani bali ni ushindanishi wa hoja.

      Lile kundi linalomtetea Mwalimu, sio lazima kuwa linampenda bali linatetea rekodi yake inayoharibiwa makusudi ili kuunda rekodi iliyokusudiwa na si iliyopo. Kundi linalomchukia Nyerere linaongozwa na chuki na linatumia mbinu za kutafuta makosa ya kweli na ya uongo ili kujenga hoja zinazoshabihiana na lengo hilo. Tofauti ya makundi haya mawili ni kuwa kundi la kwanza lipo tayari kusimama na ushahidi kutetea hoja. Kundi la pili kwa bahati mbaya halipendi mjadala wenye data, takwimu au ushahidi, bali kujenga nadharia ambayo mara nyingi haiwezi kuitetea.

      Mfano, mtu atasema Nyerere alikuwa dikteta, well and good! prove it, no answer. Yaani tuamini tu kwasababu imesemwa.
      Nyerere alikuwa mdini, hapa amekuja Mohamed Said mwenye takwimu, hakuweza kuthibitisha zaidi ya kudai wazee wake wengine walifariki siku moja kabla hajawahoji. Mohamed said ameshindwa, kama wasivyoweza kutetea wanao amini nadharia ya udini wa Nyerere.

      Nyerere alikuwa mkabali, inawezekana!!!, prove it, hakuna jibu, ila tuamini tu kwasababu fulani kasema.
      Nyerere ndio chanzo cha mgao wa umeme, ok! prove it, ah ooh unajua ujamaa, kambona etc, ili mradi tu hakuna hoja bali kumsingizia.
      Hakujenga viwanda, then prove vilivyojengwa baada yake, aahh aoooh unajua may be, hakuna jibu.

      Kumewekwa nyaraka ya mpango wa maendeleo 1963.... wote wanaomchukia mwalimu wameingia mitini. Hakuna hata mmoja aliyethubutu kuonyesha, ukanda, ukabila au udini wa mwalimu.

      Makosa ya mwalimu yasemwe, mazuri yasemwe na ikibidi yawekwe kwenye mizani, lakini tungo, mashairi yenye vibwagizo hayatusaidiii hata kidogo.
      Tuangalie hoja bila kuongozwa na chuki zetu za kibinadamu au kufundishwa. Tuangalie kazi yake na tuichambue bila kuangali umbo lake.
      Tujadili hoja kwa ushahidi si kusadikika, nadharia, majungu, ngano, mashairi au simulizi.
      I have a simple philosophy: Fill what's empty. Empty what's full. Scratch where it itches-- Alice

    24. #53
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 26,634
      Rep Power : 22539
      Likes Received
      8482
      Likes Given
      4308

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Nguruvi, umesema kweli kwa mfano Bukuku hapo juu kasema ati ukimpinga Nyerere "anakupotezea" tukimbana atoe mfano ataanza kutukwepesha maana ya neno "kupotezea" kwa sababu hakutaka kutumia neno "kuua!". Amesema Kikwete anatawala kwa mtutu wa Bunduki na "anaua" yaani anamtuhumi Rais wa Tanzania kuwa ni muuaji; akiambiwa atoe ushahidi wa maneno hayo makali - ambayo sisi wengine wakosoaji wakubwa wa Kikwete hatuthubutu kuyatumia kwa sababu ni charge ambayo ina criminal element - kwa maneno mengine anasema Kikwete ni mhalifu. Tukimuuliza ataanza kufafanua maana ya "kutawala kwa mtutu wa bunduki na kuua" nje ya maana ambayo hata mtoto mdogo anaelewa.

      Wanasema Nyerere aliua "watu wengi" hadi leo hakuna mtu aliyekuja na idadi au mifano ya watu waliouawa na Nyerere! Wengine wanasema wakati wa Operesheni Vijijini "Maelfu ya watu waliuawa" lakini hakuna mtu ambaye amewahi kutuonesha japo orodha ya watu kumi - zaidi ya kutuambia "nilisimuliwa na baba yangu au bibi"! Na tukiwabana sana usije ukashangaa mtu anakuja na stori kuwa Nyerere "alikuwa na gas chambers huko Mtwara!"; Leo hii wapo wanaeneza kabisa kuwa Nyerere alikuwa na chuki na Waislamu, na ukiwaletea ushahidi wa kiakili na kuwahoji wanaanza -hamtaki kukubali kwa sababu mnafanya Nyerere Mungu!

      Halafu cha kuudhi wenye kuendesha fikra hizo wanaamini kabisa wao ni miongoni mwa wasomi. Hii inashangaza. Sasa hawa kama wangekuwa wakati wa Mwalimu wangeweza hata kujenga hoja ikaeleweka? Wangeweza kujibu maswali ambayo wanaulizwa au watakaa kimya na kufanya kama walivyofanya wale jamaa - wakamuita Nyerere "haambiliki" kumbe sasa tunajua kwanini alikuwa haambiliki! hawakuwa na cha kumwambia zaidi ya kunung'unika. Watu wanataka kusikilizwa si kwa sababu ya uzito wa hoja zao bali uzito wa vyeo vyao, majina au nafasi zao.
      mwanakijiji@jamiiforums.com
      Binafsi NAKERWA, NAKASIRISHWA, NA KUCHUKIZWA sana na haya mambo kwamba eti "ameshauriwa vibaya na wasaidizi wake!" Huwa mara zote najiuliza ikiwa anashauriwa vibaya ni kwanini basi kila wakati awe anachukua huo ushauri mbaya!! - NasDaz

    25. #54
      NATA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th May 2007
      Posts : 2,190
      Rep Power : 7951
      Likes Received
      228
      Likes Given
      180

      Default Re: Kwanini mwalimu nyerere alitunyima mambo haya ya msingi?

      Quote By Malaria Sugu View Post
      Kupata habari kupitia TV. kwani Tv ya mwanzo ilianza wakati wa mwinyi
      Chakula cha kutosha. kwani tukipanga foleni hadi za mawe.
      Sabuni na bidhaa muhumi kuadimika
      Uvivu wenu mlitaka aje awalimie.
      mbuva likes this.

    26. FJM is offline
      FJM
      #55
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 3,581
      Rep Power : 1258
      Likes Received
      2623
      Likes Given
      2259

      Default Re: Kwanini mwalimu nyerere alitunyima mambo haya ya msingi?

      Quote By Malaria Sugu View Post
      Kupata habari kupitia TV. kwani Tv ya mwanzo ilianza wakati wa mwinyi
      Chakula cha kutosha. kwani tukipanga foleni hadi za mawe.
      Sabuni na bidhaa muhumi kuadimika
      Hata sasa hivi watu wanakula mizizi, mbona huulizi? Mwl. RIP
      mbuva likes this.

    27. #56
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 26,634
      Rep Power : 22539
      Likes Received
      8482
      Likes Given
      4308

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By KAMBOTA View Post
      Hapa ndiyo ninapoanza kushawishika kuwa Nyerere hahitaji kujitetea bali maisha yake mwenyewe yanajenga utetezi mkubwa, sasa ndugu yangu Mwanakijiji sijakupata vizuri ama sijakuelewa kwa hivyo ni swala la opposite tu? kwa maana mimi siamini kuwa unampenda NYERERE nachojua unaandika ukweli kuhusu mawazo, sera na fikra za NYERERE au nimekosea mkuu?
      Nampenda Nyerere
      Namheshimu Nyerere
      Namsoma Nyerere
      Napata hekima kutoka kwake
      Nimejifunza mengi kuhusu yeye, udhaifu wake, mapungufu yake na makosa yake
      Nimejifunza maana ya uongozi, falsafa yake, maono yake n.k

      I am un-apologetically Nyerereist. Sijaanza leo, kinyume na watu wengine, sijajifunza walichoandika kina Smith na Johnson; nimefunza kwanza kabisa alichoandika na kusema yeye mwenewe Nyerere, nimejifunza vilivyoandikwa na watu wenyewe - maandishi ya Prof. Maina kuhusu Detention act, masimulizi ya watu engine mbalimbali - kama kina Prof Njozi (ambaye nilifanya naye mahojiano ya kina miaka minne iliyopita) na kina Mohammed Said ambaye tumejadiliana mengi. Badala ya kusikiliza watu tu nimekusanya vitabu vingi vya wakati wa Nyerere, hotuba zake zote muhimu, maandishi ya watu kama kina Dr. Kleruu (sijui kama kuna watu wanajua aliwahi kuandika kitu!)

      Njia pekee ya kutafuta ukweli ni kuusaka, na kuwa tayari kuufuata kokote utakakokuongoza. Mapenzi yangu kwa Nyerere hayakuja hivi hivi tu. Ninaamini katika maabdiliko, aliposimama Mwanza (pale Nyamagana) kumpigia kampeni Mkapa, nilimsikiliza na nilisikiliza hoja zake lakini sikukubaliana na chaguo la Mkapa - nilimpigia kura Mrema! Ndio mbegu ya mageuzi ndani yangu ilivyowashwa. Lakini ni katika kuzidi kujua zaidi ya nchi yangu ndio nikaamua kwa makusudi kujifunza juu ya Nyerere na kuachana na masimulizi ya mitaani. Ukianza na chuki huwezi kujua uzuri wa mtu.

      Ni sawasawa na mtu akaja na kukuambia "unamuona yule kijana, ni mwizi sana akiingia kwako uwe mwangalifu kweli". Sasa kijana wa watu akija nyumbani kwako utafanya nini? Utaanza kuwa mwangalifu, ukimwacha ndani ukirudi unaanza kuangalia kama kila kitu kipo. Baada ya muda unakuja kugundua kuwa yule jamaa kumbe alikuwa amegombana na huyo kijana na akataka amharibie tu ili asiaminiwe. Unamuuliza kijana anakupa stori yote na unakuja kugundua ni kijana muaminifu kweli kwani uliposahau wallet yako aliokota na kukurudishia na kila senti nawe ukashangaa - kwanini ulishangaa? kwa sababu uliamini alikuwa mwizi! kisa? uliambiwa.

      So wakati mwingine kama msomi, take time to read Nyerere usitusikilize tu humu tunavyolumbana.
      mwanakijiji@jamiiforums.com
      Binafsi NAKERWA, NAKASIRISHWA, NA KUCHUKIZWA sana na haya mambo kwamba eti "ameshauriwa vibaya na wasaidizi wake!" Huwa mara zote najiuliza ikiwa anashauriwa vibaya ni kwanini basi kila wakati awe anachukua huo ushauri mbaya!! - NasDaz

    28. #57
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 6,465
      Rep Power : 1782
      Likes Received
      537
      Likes Given
      0

      Default Re: Kwanini mwalimu nyerere alitunyima mambo haya ya msingi?

      Chakula hadi sasa ni tatizo,watu wanashinda na kulala bila kula,habari hadi leo si wote wanaopata habari,tena kwa makusudi ya serikali,maana wanapoish hakuna umeme,hivyo redio na t,v ni anasa,lakini pia hata magazeti hawapati maana njia ni mbovu.......intaneti ndio anasa kabisaaaaa,kwani weeeeng wa watanzania hawazmudu gharama za kompyuta,intaneti.........

    29. #58
      macho_mdiliko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2008
      Posts : 1,153
      Rep Power : 755
      Likes Received
      104
      Likes Given
      43

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Hi sasa ni balaaa! Nimesoma makala moja ya gazeti la raia mwema ... mwandishi anataka kuhusisha udhaifu wa uongozi wa serikali ya awamu ya nne na Nyerere. Raia Mwema

    30. #59
      Mwalimu's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 21st August 2008
      Posts : 990
      Rep Power : 694
      Likes Received
      126
      Likes Given
      363

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By macho_mdiliko View Post
      Hi sasa ni balaaa! Nimesoma makala moja ya gazeti la raia mwema ... mwandishi anataka kuhusisha udhaifu wa uongozi wa serikali ya awamu ya nne na Nyerere. Raia Mwema
      Na hii ndio sababu kubwa ya kushamiri kwa mijadala kuhusu failures za Nyerere sasa hivi....Kwamba matatizo yaliyopo hayakuanza sasa, hata wakati wa Nyerere yalikuwepo na akashindwa kuyamaliza! Watawala wetu wanaficha madhaifu yao kwa kuonyesha madhaifu ya wengine....
      I'm teaching fools some basic rules...

    31. #60
      ukwelikitugani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th October 2010
      Posts : 374
      Rep Power : 458
      Likes Received
      72
      Likes Given
      218

      Default Re: Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?

      Quote By KULIKONI UGHAIB View Post
      Agreed,but two wrongs do not make a right.Ubabaishaji na upuuzi mwingine wa Kikwete hauwezi kuhalalisha kufunika mapungufu aliyokuwa nayo Nyerere.Na JK anaweza kujitetea (katika kuficha udhaifu wake) kuwa alirithishwa nchi iliyokwishakongoroka.With exception of madhara ya the 1978-9 Kagera war,Nyerere angeweza kutupa sababu zipi za msingi za kuliacha taifa likiwa hoi bin taaban wakati anastaafu 1985?
      Ndugu, Kikwete hapaswi kujitetea kwa kusema hata Mwl,Baba wa taifa aliliacha taifa likiwa hohe hahe,..arudi nyuma kidogo kwa Mkapa,aliye mtangulia. hali haikuwa mbaya kama tuliyonayo sasa.
      Ukweli unabaki pale,kuwa Mwl alikosea mambo kadha wa kadha,na mwenyewe alikili hilo. Kinachonipa shida ni criticism hizo with respect to Mkweree..
      mbuva likes this.

    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Hoja ya Madaraka Nyerere kuhusu barabara ya Serengeti
      By Saint Ivuga in forum Jamii Intelligence
      Replies: 26
      Last Post: 28th June 2011, 18:03
    2. Hoja za mwalimu nyerere kupinga serikali tatu
      By Gamba la Nyoka in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 0
      Last Post: 6th March 2011, 09:06
    3. Wengi wasiojua au wachache wenye hoja:Nyerere
      By fige in forum KATIBA Mpya
      Replies: 0
      Last Post: 22nd January 2011, 11:58
    4. Kwa Hoja CDM ni Kama Kambarage Nyerere
      By RealMan in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 0
      Last Post: 30th November 2010, 00:14
    5. Replies: 6
      Last Post: 28th September 2010, 20:54

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...