JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

  Report Post
  Page 6 of 6 FirstFirst ... 456
  Results 101 to 119 of 119
  1. Mpaka Kieleweke's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th February 2007
   Posts : 4,388
   Rep Power : 337314
   Likes Received
   1483
   Likes Given
   47

   Default Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   Nawawekea taarifa ya Press Conference ya Mhe.Lissu leo kuhusiana na sakata la mauaji ya polisi Tarime....

   17 Juni, 2011

   SPIKA ANAPENDELEA MAWAZIRI, SERIKALI: ANAKIUKA KANUNI ZA BUNGE!

   TAARIFA KWA UMMA

   Dodoma, Juni 17, 2011

   Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeelezea kusikitishwa na namna ambavyo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano amekuwa akishughulikia mijadala ya masuala muhimu kwa umma na ambayo yanaelekea kuibua uozo katika utendaji wa Serikali na watendaji wake wakuu.

   Hii inafuatia uamuzi wa Spika kukataa maswali aliyoulizwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu mauaji ya wananchi wengi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime yaliyofanywa na Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Polisi ya Tarime na Rorya kwa vipindi tofauti tangu mwaka 2008.

   Maswali hayo yaliulizwa na Mheshimiwa Tundu Lissu (Singida Mashariki, CHADEMA) na Mheshimiwa Esther Matiko (Viti Maalum, CHADEMA) wakati wa Kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu katika Kikao cha Tisa cha Bunge la Jamhuri siku ya Alhamisi ya tarehe 16 Juni 2011.
   Hata hivyo, katika hatua ya kushangaza, Spika wa Bunge alikataza maswali hayo kujibiwa kwa hoja kwamba yalikuwa yanahusu mambo ambayo tayari yako mahakamani na kwa hiyo kuyajadili Bungeni itakuwa sawa na kuingilia uhuru na mamlaka ya Mahakama kinyume na kanuni 64(1)(c) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007.

   Alipoombwa mwongozo wake kutokana na ukweli kwamba hakuna kesi hata moja ambayo imefunguliwa au inayoendelea katika mahakama yoyote ya Tanzania inayohusu mauaji ya wananchi wa Nyamongo au yanayowahusu polisi wanaohusika na mauaji hayo, Spika Anna Makinda alidai kwamba wauliza maswali wenyewe walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya jinai katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime yanayotokana na matukio ya mauaji ya wananchi watano yaliyofanywa na polisi katika eneo la Mgodi wa North Mara tarehe 16 Mei mwaka huu na kwa hiyo hawakupaswa kuuliza maswali yao.

   Akizungumzia uamuzi huo wa Spika Makinda, Mbunge Lissu - ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni - alimtuhumu Spika Makinda kwa kumkingia kifua Waziri Mkuu na kukiuka Kanuni za Kudumu za Bunge. “Mimi sijashtakiwa mahakamani kwa kosa lolote linalohusu mauaji ya wananchi wa Nyamongo, Tarime na wala kesi yangu katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime haiuhusu matukio ya Nyamongo”, Lissu alisema.

   Aliongeza kwamba: “Wakati mauaji ya wananchi wa Nyamongo yalifanywa na Jeshi la Polisi tarehe 16 Mei, mimi na wenzangu wengine saba tumeshtakiwa kwa madai ya kuingia kijinai katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime; kwa kufanya mkusanyo haramu katika eneo hilo; na kwa kuwazuia mganga wa Hospitali hiyo na askari polisi kufanya uchunguzi wa miili ya marehemu Emmanuel Magige, Chacha Ngoka, Chawali Bhoke na Mwikwabe Marwa waliouawa na Jeshi la Polisi. Makosa yote matatu yanadaiwa kutokea mnamo majira ya saa nne usiku wa tarehe 23 Mei 2011.”

   Kuhusiana na Mbunge Matiko, Lissu alidai kwamba Mbunge huyo wa Viti Maalum hakabiliwi na mashtaka yoyote mahakamani kwa jambo au kosa lolote lile.

   “Inaelekea Spika wa Bunge alitoa uamuzi wake huo bila hata kuuliza au kupewa taarifa sahihi kuhusu masuala ya mauaji ya Tarime na kesi iliyofunguliwa dhidi yangu na wenzangu. Hii ni hatari sana kwa uendeshaji bora wa Bunge kama Spika ambaye ndiye kiongozi mkuu wa Bunge atakuwa anatoa maamuzi ambayo hana taarifa sahihi juu yake. Sio tu mijadala inayohusu masuala muhimu kwa umma na ambayo yanatakiwa kujadiliwa Bungeni itazuiliwa kwa hoja zisizozingatia Kanuni za Kudumu za Bunge, bali pia hadhi na heshima ya Bunge na ya Spika mwenyewe itashuka kwa vile wananchi wataona kwamba Spika anafanya maamuzi kwa lengo la kuwakingia kifua mawaziri na Serikali ili wasiwajibishwe Bungeni. Hii ikitokea itakuwa ni hatari sana kwa demokrasia yetu ya kibunge.”

   Mheshimiwa Lissu alidai kwamba hii si mara ya kwanza kwa Spika Makinda kutoa uamuzi ulioonekana kumkingia kifua Waziri Mkuu wakati wa Kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu. “Itakumbukwa kwamba wakati wa Mkutano wa Pili wa Bunge la Jamhuri uliofanyika mwezi Februari mwaka huu, Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema aliomba Mwongozo wa Spika kutokana na kauli ya uongo iliyotolewa na Waziri Mkuu kuhusu mauaji ya Arusha. Badala ya kutoa mwongozo alioombwa, Spika wa Bunge alimkemea Mheshimiwa Lema na kumtaka athibitishe kauli yake juu ya uongo wa Waziri Mkuu.

   Hata hivyo, Lema alipotoa uthibitisho wake Spika Makinda alizima mjadala huo kwa kukalia uthibitisho wa Mheshimiwa Lema. Hadi leo Watanzania hawajaambiwa chochote juu ya jambo hilo.”
   Mheshimiwa Lissu alisema kwamba vitendo hivi vya Spika vinakiuka Kanuni za Kudumu za Bunge.

   “Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Spika wa Bunge ana mamlaka makubwa sana kimaamuzi. Hata hivyo, Spika hawezi akaendesha Bunge kama anavyoona yeye binafsi. Anatakiwa kuzingatia kanuni. Na kanuni kuu anayotakiwa kuizingatia muda wote ni kanuni ya 8 inayomtaka kuendesha shughuli za Bunge na “kutoa maamuzi kwa haki, uadilifu na bila chuki wala upendeleo wowote, kwa kuongozwa na Katiba, Sheria za nchi, Kanuni hizi, Kanuni nyingine zilizopo, maamuzi ya maspika wa Bunge waliotangulia na pia kwa kuzingatia uzoefu pamoja na mila na desturi za mabunge mengine yanayofuata utaratibu wa kibunge unaofanana na unaofuatwa na Bunge la Tanzania.”

   Kuhusiana na hatua wanazotazamia kuchukua dhidi ya uamuzi wa Spika Makinda wa kukataza maswali yao, Mheshimiwa Lissu alisema kwamba watapeleka malalamiko yao kwa Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge ili uamuzi wa Spika uchunguzwe na Kamati hiyo na kutolewa uamuzi.

   “Kwa bahati nzuri, uamuzi Spika kuhusiana na jambo lolote sio wa mwisho kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge letu. Pamoja na kwamba tusingependa kufanya hivyo, lakini kuuachia uamuzi potofu wa Spika wa Bunge usimame itakuwa ni kuweka precedent ya hatari kwa Bunge letu kwani uamuzi huo ukiachwa bila kupingwa unaweza kutumiwa kwa mijadala mingine kwa siku zijazo. Ili kuepuka hili, inabidi tumpeleke Mheshimiwa Spika kwenye Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge ili uamuzi wake ukajadiliwe na kutolewa maamuzi ya haki. Kazi ya kuandaa malalamiko hayo itakamilika baada ya muda mfupi kwani vielelezo vyote muhimu tayari vimekwishapatikana.”

   --------------------------------------------------------------
   Tundu A.M. Lissu (MB.)
   MNADHIMU MKUU, KAMBI RASMI YA UPINZANI  2. nguvumali's Avatar
   JF Bronze Member Array
   Join Date : 3rd September 2009
   Location : nimerudi Mwanza
   Posts : 4,799
   Rep Power : 1584
   Likes Received
   1030
   Likes Given
   308

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge.

   Quote By FaizaFoxy View Post
   Lissu kama mwanasheria anashangaza sana. Sasa mara aseme yeye yuko mahakamani kwa kesi inayohusu hao waliouiliwa Nyamongo halafu alaume Spika hakutenda haki kuzuwia yasiongelewe. Hivi ananini huyu? Ili mradi alalamike tu?

   SI asuse kama anaona hatendewi haki? Asuse na kwenda mahakamani pia (Spika sikasema yuko nje kwa dhamana? Au alidanganya hapo Spika). Lissu susa kwenda mahakamani halafu muulize Mbowe zile siku mbili alilaa kitandani? Sakafuni au juu ya desk? Alipokaidi kwenda mahakamani?
   inaonekana hata mashabiki wao wameiga akili na uwezo duni wa kufikiri wa viongozi wao wa kitaifa, tizama ujumbe wa huyu foxy, utajua tu , ni aina gani ya watu wanaoipenda na kuishabikia ccm , anaongea porojo nyepesi sana, sijui labda kuna wagonjwa na afya ya akili mtandaoni sikuhizi, hiki ni kielelezo tosha, kuwa kuwa mwanaccm, ni lazima uwe na kaupungufu fulani......
   The most potent weapon of the oppressor is the mind of the oppressed

  3. Wacha1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st December 2009
   Posts : 10,917
   Rep Power : 429499222
   Likes Received
   4057
   Likes Given
   4221

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   Chama Cha Majambazi mwaka huu mtakoma ubishi mmezoea kula vya kunyonga khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   Baada ya kufanya kazi nzuri katika wizara ya Ujenzi, John Pombe Magufuli amepewa dhamana na Watanzania kushika hatamu kuliongoza taifa. Wakati umefika kusafisha Ikulu, kusafisha wizara na mashirika ya Umma kuwatumikia Watanzania. Kutokomeza ufisadi uliokubuhu na kukomesha mafisadi ambayo yamejikita kuwadhulumu walipa kodi wa nchi hii.

  4. fikramakini's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 27th November 2010
   Location : msoga
   Posts : 247
   Rep Power : 614
   Likes Received
   60
   Likes Given
   17

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge.

   Quote By Njowepo View Post
   Kwa raha zake Makinda ata mkimtoa keshaweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa speaker!
   Kwake yeye mission accomplished so tutabaki tunaumiza kichwa
   Mkubwa una uhakika hapo kwenye red? Mwanamke wa kwanza duniani, africa, east africa, tanzania au kijijini kwao?

  5. Josh Michael's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th June 2009
   Location : Kibandani
   Posts : 2,555
   Rep Power : 1148
   Likes Received
   59
   Likes Given
   378

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   Mama mwenyewe amejaa unazi tu maana toka mwanzo alikuwa katika hali kama hiyo maana alikuwa na upendeleo mkubwa sana
   Those who are too smart to engage in politics are punished by being governed by those who are dumber. ~Plato:D

  6. kusisimba's Avatar
   Member Array
   Join Date : 21st May 2011
   Posts : 37
   Rep Power : 543
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   Kiukweli mh. Lisu kasema ukweli mtupu, haiingii akilini madam spika anafanya maamuzi kwa jaziba halafu watu wakakaa kimya, kimsingi inaonekana anataka kufanya kazi kimazoea. Si rahisi sana.

  7. ESAM's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th March 2011
   Posts : 952
   Rep Power : 867
   Likes Received
   299
   Likes Given
   211

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge.

   Quote By FaizaFoxy View Post
   Lissu kama mwanasheria anashangaza sana. Sasa mara aseme yeye yuko mahakamani kwa kesi inayohusu hao waliouiliwa Nyamongo halafu alaume Spika hakutenda haki kuzuwia yasiongelewe. Hivi ananini huyu? Ili mradi alalamike tu?

   SI asuse kama anaona hatendewi haki? Asuse na kwenda mahakamani pia (Spika sikasema yuko nje kwa dhamana? Au alidanganya hapo Spika). Lissu susa kwenda mahakamani halafu muulize Mbowe zile siku mbili alilaa kitandani? Sakafuni au juu ya desk? Alipokaidi kwenda mahakamani?
   Dada yangu mbona kila jambo liko wazi, au hutaki tu kuelewa? Kesi iliyoko mahakamani haihusu mauaji ya Nyamongo hata kidogo, bali matukio yaliyofanyika Tarime mjini. Kwa hiyo mauaji ya Nyamongo hayana kesi yoyote kwa sasa, na kama unadhani Mheshimiwa Spika alikuwa sahihi na vipi kuhusu alivyosema Esther Matiko anakabiliwa na kesi wakati hana kesi yoyote katika mahakama ya Tarime? Jamani hata kama ni wafuasi au wapenzi wa chama tawala pale kwenye ukweli tuwe wakweli tu ndipo tutaweza kuiendeleza Tanzania.

   Halafu unamshauri Lissu asuse nini? Mbona njia aliyotumia ndiyo sahihi ambayo inaendana na kanuni za bunge? Hebu tuwe wazalendo kwa nchi yetu jamani.

  8. sulphadoxine's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st November 2010
   Posts : 2,269
   Rep Power : 1084
   Likes Received
   617
   Likes Given
   2124

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   FaizaFoxy
   JF Senior Expert Member
   This message has been deleted by Paw.

   ReasonNje ya mada
   CHUKI NA UADUI NI MATOKEO YA UPUMBAVU:

  9. Chesty's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2009
   Posts : 1,553
   Rep Power : 936
   Likes Received
   315
   Likes Given
   105

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge.

   Quote By lm317 View Post
   Magamba wa kujipanga na kujibu hoja kama hizo ni nani?

   Angalia hoja zao!   Hata Bungeni mambo ni hayohayo!
   Mkuu nimetafuta kitufe cha thanks mpaka kwa kumulika kwa tochi sijakiona, nimeona nikupe thanks LIVE!

  10. Mtu wa Pwani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th December 2006
   Posts : 4,747
   Rep Power : 1721
   Likes Received
   380
   Likes Given
   769

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   lissu muhuni tu

   kwani utaratibu ndio haujui? sasa kuzungumza na vombo va habari iwe nn? kama sio kutafuta misifa ya kijinga

   hawa chadema wanadhani kutengeneza mabifu ndio kutawapandisha?
   Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

  11. zamlock's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th December 2010
   Posts : 3,769
   Rep Power : 1310
   Likes Received
   579
   Likes Given
   1

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   jamani huyu mama juzi mimi nimemuona mambo aliyofanya siyo kabisa na kwwa hali hii anajichimbia kaburi hata kwenye jimbo lake na ajue iko siku hii nchi itashikwa na chadema sijui watarajie nini,

  12. Augustine Moshi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd April 2006
   Posts : 2,188
   Rep Power : 2051
   Likes Received
   441
   Likes Given
   139

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   Kama kuna mwenye update kwenye hii ishu naomba atupatie. It is a precedent setting undertaking. Shujaa wetu Lisu tunakuombea. Laiti ungekuwa na nafasi zaidi ya kuongoza taifa. Laiti ungekuwa AG wetu. Mabwanyeye kama ya Barrick yangekoma.
   Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

  13. Barubaru's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th April 2009
   Location : Doha, Qatar
   Posts : 7,203
   Rep Power : 2342
   Likes Received
   2264
   Likes Given
   2861

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   Spika hajapata utulivu huyo. Mpeni Mume ndio atatulia na kutoa maamuzi sahihi.

   Poleni sana
   Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

   Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

  14. mkali wa leo's Avatar
   Member Array
   Join Date : 27th May 2011
   Posts : 84
   Rep Power : 551
   Likes Received
   3
   Likes Given
   7

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   anna makinda nakufagilia sana mana hao wabunge wapumbavu walijua wanakuja bungeni kutawala ss wamepatikana wamelutana na chuma cha pua.

  15. Haki Yetu's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 28th April 2011
   Posts : 162
   Rep Power : 571
   Likes Received
   43
   Likes Given
   93

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   Mtu yeyote mwenye akili hawezi kushangaa utendaji wa huyu spika. Ukifuatilia kwa jinsi alivyoingia hadi kupata kiti hicho hutashangaa hata kidogo. Anachokifanya ni sawa na baadhi ya wana JF hapa jamvini, ambao wametumwa kwa ajili ya kupinga hoja za wapinzani na kutetea utumbo wa chama tawala. Nina hakika wote tunawajua watu hao.

   Huyu mama hana uwezo wa kuliendesha bunge. Anafanya msisimko wa bunge unapungua kabisa. Ameshindwa kujifunza kabisa kutoka kwa mtangulizi wake "mzee wa kasi na viwango". Bahati mbaya kwake ni kwamba wabunge wa upinzani hasa wa CDM sio watu wa kuburuzwa na akiendelea na mtindo wake huu mwisho wake utakua mbaya sana.

   Naona pia Serikali imeanza kutuhujumu kuhusiana na sisi wananchi kufuatilia vikao vya bunge. Kwani huu mgawo wa umeme usiokuwa na kichwa wala miguu unatukosesha raha wananchi. Wameamua wamuweke spika wao kilaza na kutukatia umeme ili tusifuatilie mijadala bungeni. Kweli Serikali yetu inaonyesha kila dalili ya kuchanganyikiwa na anguko hivi sasa ni dhahili. Wenye akili walisema huwezi kuwadanganya watu wote kwa wakati wote

  16. MVUMBUZI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th January 2011
   Posts : 4,337
   Rep Power : 8976
   Likes Received
   1296
   Likes Given
   509

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge.

   Quote By FaizaFoxy View Post
   Lissu kama mwanasheria anashangaza sana. Sasa mara aseme yeye yuko mahakamani kwa kesi inayohusu hao waliouiliwa Nyamongo halafu alaume Spika hakutenda haki kuzuwia yasiongelewe. Hivi ananini huyu? Ili mradi alalamike tu?

   SI asuse kama anaona hatendewi haki? Asuse na kwenda mahakamani pia (Spika sikasema yuko nje kwa dhamana? Au alidanganya hapo Spika). Lissu susa kwenda mahakamani halafu muulize Mbowe zile siku mbili alilaa kitandani? Sakafuni au juu ya desk? Alipokaidi kwenda mahakamani?
   Sio lazima kuchangia mambo yasiyokuhusu kwani hii ni sawa na kuingilia ugomvi wa wanandoa na kuanza kutoa Comments za nyumbani kwenu.
   Acha uzuzu na acha kukurupuka kilaza wa CC-Magamba mkubwa. hujui chochote nyamaza kimya kibaraka weee!!!!!!!!!!

  17. MVUMBUZI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th January 2011
   Posts : 4,337
   Rep Power : 8976
   Likes Received
   1296
   Likes Given
   509

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   Quote By mkali wa leo View Post
   anna makinda nakufagilia sana mana hao wabunge wapumbavu walijua wanakuja bungeni kutawala ss wamepatikana wamelutana na chuma cha pua.
   Hivi kwa akili yako duni unaweza mfananisha Anne makinda na chuma cha pua kama si kukosa uwezo wa ku-rate mambo? Kama huna point unaweza kusoma to comments za wenzako sio lazima utoe pumba humu.

  18. Haki Yetu's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 28th April 2011
   Posts : 162
   Rep Power : 571
   Likes Received
   43
   Likes Given
   93

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge.

   Quote By Eric Samba View Post
   Dada yangu mbona kila jambo liko wazi, au hutaki tu kuelewa? Kesi iliyoko mahakamani haihusu mauaji ya Nyamongo hata kidogo, bali matukio yaliyofanyika Tarime mjini. Kwa hiyo mauaji ya Nyamongo hayana kesi yoyote kwa sasa, na kama unadhani Mheshimiwa Spika alikuwa sahihi na vipi kuhusu alivyosema Esther Matiko anakabiliwa na kesi wakati hana kesi yoyote katika mahakama ya Tarime? Jamani hata kama ni wafuasi au wapenzi wa chama tawala pale kwenye ukweli tuwe wakweli tu ndipo tutaweza kuiendeleza Tanzania.

   Halafu unamshauri Lissu asuse nini? Mbona njia aliyotumia ndiyo sahihi ambayo inaendana na kanuni za bunge? Hebu tuwe wazalendo kwa nchi yetu jamani.
   Eric Samba huyo dada muache kama alivyo. Hayo aliyoyaandika anatimiza wajibu wake ili angalau watoto waende msalani. Hutashangaa ukisikia kuwa hata yeye haamini hayo aliyoyaandika. Tulishawahi kuaswa na wanajamvi wenzetu kuwa tuwapuuze hao. Sio yeye tu yuko na wenzie wakina maralia sugu. Ukikuta mada we changia tu usimfuate mwenzio katumwa huyo. Jaman na wanajamvi wengine hao watu tuwapotezee tu pamoja ya kuwa ni vigumu kufanya hivyo.

  19. HISIA KALI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th October 2010
   Location : Mjini kwa mjomba
   Posts : 695
   Rep Power : 705
   Likes Received
   107
   Likes Given
   1

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge

   Huyu spika mara nyingi anaongea kabla ya kutafakari. Kumbuka alivyowatukana watu wa Kariakoo.

  20. The GreatMwai's Avatar
   Member Array
   Join Date : 28th April 2011
   Posts : 43
   Rep Power : 547
   Likes Received
   2
   Likes Given
   0

   Default Re: Taarifa ya Lissu kwa vyombo vya habari kuhusu Spika wa Bunge.

   Quote By FaizaFoxy View Post
   Lissu kama mwanasheria anashangaza sana. Sasa mara aseme yeye yuko mahakamani kwa kesi inayohusu hao waliouiliwa Nyamongo halafu alaume Spika hakutenda haki kuzuwia yasiongelewe. Hivi ananini huyu? Ili mradi alalamike tu?

   SI asuse kama anaona hatendewi haki? Asuse na kwenda mahakamani pia (Spika sikasema yuko nje kwa dhamana? Au alidanganya hapo Spika). Lissu susa kwenda mahakamani halafu muulize Mbowe zile siku mbili alilaa kitandani? Sakafuni au juu ya desk? Alipokaidi kwenda mahakamani?
   Kuwa na kesi mahakamani hakumaanishi mtu huyo haruhusiwi kushiriki maendeleo ya taifa kama mtu huru. Sheria ya Tanzania inatambua haki hiyo na ndiyo maana mtuhumiwa yeyote anahesabiwa hana kosa mpaka mahakama itakapotoa uamuzi kama ana kosa. Kuhusu spika wetu, ni dada yetu na wengine mama yetu, uongozi umemshinda na anaharibu Bunge linakosa ladha machoni pa jamii. Si kwa kuwa anatuhumiwa kuwalinda 'CCM' bali hafuati kanuni anafuata hisia zake. Hata hivyo naona wewe unashindwa kuwianisha mambo, suala la yeye kukataa kuhudhuria mahakamani na maswali ya Bungeni sioni uhusiano labda lengo lako ni kupoteza mantiki ya hoja iliyopo.

  Page 6 of 6 FirstFirst ... 456

  Similar Topics

  1. Hii Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Kaimu Mkuu Nishati na Madini
   By MaxShimba in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 1
   Last Post: 25th July 2011, 01:18
  2. Replies: 23
   Last Post: 4th July 2011, 02:12

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...