Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

    Report Post
    Results 1 to 12 of 12
    1. BAK is offline
      BAK
      #1
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,827
      Rep Power : 45014
      Likes Received
      8683
      Likes Given
      8666

      Default Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

      Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi
      Stella Nyemenohi, Dodoma
      Daily News; Sunday,June 15, 2008 @00:01

      Ofisi ya Spika imewasilisha taarifa kwa Polisi na Usalama wa Taifa ili washughulikie madai yaliyojitokeza hivi karibuni kuhusu Mbunge na Ofisa mmoja Mwandamizi wa Bunge kukutwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakifanya vitu vinavyodhaniwa kuwa ni ushirikina.

      Tukio hilo lililoripotiwa jana na baadhi ya vyombo vya habari, linadaiwa kufanyika Jumatatu wiki iliyopita likimhusisha Mbunge na Ofisa wa Bunge, ambao hata hivyo, hawakutajwa ni akina nani.

      Imedaiwa kuwa watu hao walinaswa wakinyunyizia vitu visivyojulikana katika kila kiti cha Mbunge na kuishia cha Spika. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuahirishwa semina ya

      Wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi mjini hapa, Spika Samuel Sitta alisema Kamanda wa Polisi mkoani hapa na Usalama wameanza kufuatilia zaidi tangu juzi ili kubaini ukweli wa suala hilo .

      Ingawa alisema bado suala hilo ni uvumi na kwamba halina budi kusubiri kukamilika uchunguzi wa vyombo hivyo vya usalama , Sitta alisema hata hivyo tahadhari zote zinachukuliwa katika Ukumbi wa Bunge.

      Hata hivyo, alisema kwa upande mwingine, tahadhari zinaweza kuwa ngumu ikizingatiwa kuwa wanaohusishwa ni watu ambao hawana kipingamizi cha kuingia katika ukumbi huo.

      Akizungumzia juu ya tukio hilo , Spika alisema, “Inashangaza. Lakini ni suala la uvumi, linachunguzwa. Tusubiri RPC na Usalama wa Taifa wakamilishe uchunguzi wao…tahadhari zote zinachukuliwa,” alisema.

      Kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa na baadhi ya magazeti, tukio hilo la ushirikina, linadaiwa kufanyika siku moja kabla ya kikao cha kwanza cha Mkutano wa 12 wa Bunge kuanza Jumanne iliyopita.

      Spika alisema wakati wa tukio hilo, kamera sita zilizokuwa katika ukumbi huo, hazikuwa zimewashwa. Isipokuwa inadaiwa, kamera moja ya studio ndiyo iliyoonyesha watu hao.

      Hata hivyo, Sitta alisema kamera hiyo ilionyesha picha iliyofifia ambayo ni vigumu kubaini wahusika. Hata hivyo, alisema anaamini kuwa ikifikishwa kwa wataalamu, ndiyo watakaoweza kubaini wahusika.

      Alipoulizwa na waandishi kuhusu mantiki ya kuhusisha tukio hilo la ushirikina na ugonjwa wa ghafla wa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), Spika alisema halihusishwi ikizingatiwa kuwa taarifa za daktari, zilionyesha kuwa alikuwa na uchovu.

      Kwa mujibu wa Spika, Dk. Mwakyembe alianza kujisikia anaishiwa nguvu Alhamisi dakika chache wakati akijaribu kuwasiliana na Spika ndani ya Bunge. Alitoka nje ya ukumbi kwa msaada wa Mbunge mwenzake na kupelekwa hospitalini.

      Baada ya Mwakyembe kukabiliwa na maradhi hayo ya ghafla, kesho yake (juzi) ulienea uvumi kuwa amefariki. Wakati Sitta alisisitiza jana kuwa afya yake inaendelea vizuri, HabariLeo ilimshuhudia Mbunge huyo jana akiwa katika viwanja vya Bunge katika hali ya kawaida.

      Wakati huohuo, semina ya NEC-CCM ilianza jana na inatarajiwa kumalizika leo mjini Dodoma. Kwa mujibu wa Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM John Chiligati alisema miongoni mwa waliotoa mada ni pamoja na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Beno Ndullu.

      "Hatujamaliza semina. Inaendelea hadi kesho (leo). Kwa hiyo, maazimio yote yatakayofikiwa, tutatoa taarifa kesho saa 11," Chiligati aliwaambia waandishi na kusisitiza kuwa lengo la semina hiyo ni kuhusu masuala ya uchumi, hususan kilimo.
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    2. Shy is offline
      Shy
      #2
      Shy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2006
      Posts : 4,922
      Rep Power : 0
      Likes Received
      76
      Likes Given
      0

      Default Re: Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

      Katika Usalama Wa Taifa Au Chochote Hatuamini Katika Uchawi Wala Imani Za Kishirikina Wala Chochote Kinachohusu Uficho Wa Kitu Fulani ,kazi Ni Mtindo Moja Tu ,kumlinda Mwananchi Na Mali Zake , Kupeana Na Kupashana Habari Kuhakikisha Nchi Inaendelea Kuwa Na Amani ,mshikamano ,undugu Na Upendo Kama Ilivyosiku Zote

    3. BAK is offline
      BAK
      #3
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,827
      Rep Power : 45014
      Likes Received
      8683
      Likes Given
      8666

      Default Re: Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

      Quote By shy View Post

      Kama ndiyo hivyo kulikuwa na haja gani hiyo ofisa ya spika kuwaambia Watanzania kwamba imewasilisha ripoti ya uchawi polisi ili waifanyie uchunguzi? Ofisi ya spika haiyajui hayo uliyoandika hapo juu au ni katika kudanganya wadanganyika?
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    4. Shy is offline
      Shy
      #4
      Shy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2006
      Posts : 4,922
      Rep Power : 0
      Likes Received
      76
      Likes Given
      0

      Default Re: Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

      Ndio Hivyo Umeshadanganywa Kama Ni Wewe Nenda Vituo Vyote Vya Polisi Uulize Kuhusu Uchawi Au Ushirikina Uone Utajibiwa Nini ,mada Zingine Hazina Masihali Kwa Jamii Forum

    5. #5
      Augustoons's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2007
      Posts : 409
      Rep Power : 675
      Likes Received
      3
      Likes Given
      1

      Kinachochunguzwa sio uchawi wenyewe bali ni nia ya mtu kufanya mambo ya kishirikina kama alivyoainishwa kwenye sheria ya mambo ya kishirikina(yaani witchcraft ordinance) kwa lengo la kuwadhuru watu hao ambao wewe na wenzio mmesema mnawalinda.Sasa unabisha nini?kama huyajui mambo si utulie ukalale?isitoshe wewe ni kama ni wale wa kuambiwa tu fanya hiki fanya kile.Iistoshe hata akijulikana muhusika sio lazima ashughulikiwe kijinai hiyo inaweza pia kumuwezesha spika kumshughulikia administratively(kimaadili na nidahmu ya bunge).

    6. BAK is offline
      BAK
      #6
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,827
      Rep Power : 45014
      Likes Received
      8683
      Likes Given
      8666

      Default Re: Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

      Quote By shy View Post
      Katika Usalama Wa Taifa Au Chochote Hatuamini Katika Uchawi Wala Imani Za Kishirikina Wala Chochote Kinachohusu Uficho Wa Kitu Fulani ,kazi Ni Mtindo Moja Tu ,kumlinda Mwananchi Na Mali Zake , Kupeana Na Kupashana Habari Kuhakikisha Nchi Inaendelea Kuwa Na Amani ,mshikamano ,undugu Na Upendo Kama Ilivyosiku Zote
      Yule mtoto aliyekutwa na kichwa cha mtoto na akaanza kukila pale Muhimbili polisi walimkamata na kumtia ndani ambako yuko hadi hii leo na huku kesi yake ikiendelea mahakamani. Sasa kama polisi ni sehemu ya usalama wa Taifa kulikoni mpaka wakamkamata yule kijana na kumuweka rumande hadi sasa kama wao hawaamini uchawi? Unapotaka kujadili hakikisha una facts za kusupport kile unachokisema vinginevyo utaonekana unabwabwaja tu!
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    7. #7
      yakhe's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 15th June 2008
      Posts : 3
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

      Jamani hili bunge lishughulikie mambo ya maana ya kuongoza nchi .tuwache itikadi .mjue tuu serekali hairogwi

    8. #8
      Mzozo wa Mizozo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th May 2008
      Posts : 428
      Rep Power : 650
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

      Quote By yakhe View Post
      Jamani hili bunge lishughulikie mambo ya maana ya kuongoza nchi .tuwache itikadi .mjue tuu serekali hairogwi
      Maneno mema...

      Moja: Serikali ni nini? na inajumuisha vitu vingapi ili iweze kuitwa serikali?

      Mbili: Baada ya kuacha itikadi tutafuata mwelekeo gani?

      Tatu: Je Tanzania tuna Witchcraft Act? Kama ndio ni ya nini na inaisaidiaje Serikali?

      Uchawi ni silaha muhimu sana ya Maangamizi sema tumeamua itumia vibaya na kujaribu itumia angamiza wale wema...Kungekuwa na chuo cha uchawi ningeenda nipate ujuzi kisha niwekane sawa na hawa mafisadi wanaodharau wapiga kura wao na kujivisha Umungu!
      Change will not come if we wait for some other person or some other time. We are the ones we've been waiting for. We are the change that we seek.

    9. #9
      Augustoons's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2007
      Posts : 409
      Rep Power : 675
      Likes Received
      3
      Likes Given
      1

      Default Re: Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

      Quote By Mzozo wa Mizozo View Post
      Maneno mema...

      Moja: Serikali ni nini? na inajumuisha vitu vingapi ili iweze kuitwa serikali?

      Mbili: Baada ya kuacha itikadi tutafuata mwelekeo gani?

      Tatu: Je Tanzania tuna Witchcraft Act? Kama ndio ni ya nini na inaisaidiaje Serikali?

      Uchawi ni silaha muhimu sana ya Maangamizi sema tumeamua itumia vibaya na kujaribu itumia angamiza wale wema...Kungekuwa na chuo cha uchawi ningeenda nipate ujuzi kisha niwekane sawa na hawa mafisadi wanaodharau wapiga kura wao na kujivisha Umungu!
      Dhana kwamba serikali hairogiw ni nadharia tu,ambayo ukweli wake ni kuwa serikali haiwezi anguka kwa kurogwa yaani viongozi wote wa serikali wafe siku moja,lakini cha kujiuliza?serikali inaundwa na nani?kama jibu ni watu je,watu wanarogeka?kama jibu ni ndiyo basi serikali inarogeka.Uchawi upo? je jibu ni ndiyo au hapana?kwa Tanzania jibu ni ndiyo na je,unatambulika na serikali kuwa upo?jibu ni ndiyo upo na ndiyo maana katika sheria za Tanzania kuna Witchcraft Act, iwapo serikali isingekuwa inaamini uchawi upo basi sheris hii ingefutwa zamaniiiiiiiiiiiii,kwani mbali ya kupigiwa kelele na wasomi na watetezi wa haki za binadamu kuwa ifutwe na imepitwa na wakati bado serikali inaikumbatia na imekuwepo tokea enzi za mkoloni.
      Uchawi na influence zake upo mahali pote ndiyo maana hata wenzetu waingereza wanaogopa na katu hawatalala kwenye chumba namba 13 na kutokana na hilo hoteli zote duniani za hadhi ya kitalii duniani hazina namba hiyo.Pili waingereza wenyewe wana sikukuu yao inaiwa haloween hii ni sherehe ya mizimu na kuna matambiko hufanyika ili wasidhurike na winta isiwe mbaya.Tatu wakati wa summer kama kipindi hiki ni imani ya waingereza kuwa kila ulapo nyama (barbeque) choma lazima uchomee nje ili moshi ufuke uende juu ukahanikize mizimu ili summer iwe nzuri na winta isiwe mbaya kwa upande wao. Hizizote ni imani za kishirikina na hazipo tz tu hata wenzetu waloendelee.

    10. #10
      hollo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st April 2008
      Posts : 739
      Rep Power : 717
      Likes Received
      38
      Likes Given
      13

      Default Re: Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

      Taifa linalozungumzia the so called uchawi!karne hii ya 21!kwa kweli lazima uboubt na uwezo wa wananchi pamoja na viongozi wake!Ndo maana mtu mweupe anawasiwasi na uwezo wa mtu mweusi!

    11. #11
      Yo Yo's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 31st May 2008
      Posts : 10,895
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1356
      Likes Given
      2594

      Default Re: Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

      Quote By shy View Post
      Katika Usalama Wa Taifa Au Chochote Hatuamini Katika Uchawi Wala Imani Za Kishirikina Wala Chochote Kinachohusu Uficho Wa Kitu Fulani ,kazi Ni Mtindo Moja Tu ,kumlinda Mwananchi Na Mali Zake , Kupeana Na Kupashana Habari Kuhakikisha Nchi Inaendelea Kuwa Na Amani ,mshikamano ,undugu Na Upendo Kama Ilivyosiku Zote
      .......???

    12. BAK is offline
      BAK
      #12
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,827
      Rep Power : 45014
      Likes Received
      8683
      Likes Given
      8666

      Default Re: Uchawi’ bungeni wafika Usalama wa Taifa, Polisi

      Voodoo, poison threats: Bunge still trembling under shadow of fear

      THISDAY REPORTER
      Dar es Salaam

      THE recently reported incident of witchcraft rituals allegedly performed by a senior MP and a parliament official inside the National Assembly (Bunge) Hall in Dodoma has sparked concern among other members of parliament over a possible poison attack targeted at certain legislators.

      The Kigoma North MP, Zitto Kabwe (CHADEMA), said yesterday that the incident could be more than just a simple matter of voodoo rituals, but possibly an outright attempt to poison someone or some people in the House.

      According to Zitto, the incident could even be directly linked to the sudden sickness that has apparently befallen Kyela legislator Dr Harrison Mwakyembe, who was abruptly taken ill while attending a parliamentary session last week.

      Mwakyembe was chairman of the Bunge committee that probed the Richmond power generation scandal and delivered a scathing report that led to the resignation of former prime minister Edward Lowassa and two senior cabinet ministers, Nazir Karamagi and Dr Ibrahim Msabaha.

      The Kyela MP and other members of the committee are already on record as having publicly declared that they received death threats during the course of the probe.

      In Zitto’s opinion, special medical tests need to be conducted on Mwakyembe to conclusively establish whether or not he might have been somehow poisoned in Dodoma.

      ’’I personally don’t believe that there are witchcraft rituals in parliament...It is possible we are deliberately being diverted from what might actually be the real issue, that some kind of poison could have been spilled inside the House,’’ he told THISDAY.

      Likewise, the Tarime legislator also on a CHADEMA ticket, Chacha Wangwe, described the reported Bunge vodoo rituals as ’’suspicious’’ and warranting a deeper investigation.

      Mwakyembe himself has been unreachable since last week’s reports that he had suddenly fallen ill after an alleged ’’witchcraft ritual’’ was performed on his seat inside the Bunge Hall, at a time when parliament was not in session.

      The Speaker of the National Assembly, Samwel Sitta, has said his office has already informed the police and security/intelligence authorities about the incident, and asked for a formal investigation into the matter.

      There were conflicting reports regarding whether or not the alleged perpetrators of the decidedly un-parliamentary behaviour were actually caught on the surveillance cameras installed in parliament.
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    Similar Topics

    1. Replies: 78
      Last Post: 12th April 2012, 08:10
    2. Wajeshi 300 waja juu ,wakiwemo usalama wa Taifa na polisi
      By Mwiba in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 1
      Last Post: 20th April 2009, 02:29
    3. Polisi yazima uchawi bungeni
      By Pdidy in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 0
      Last Post: 11th July 2008, 11:30

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...