TMF|JamiiForums Blog
  • Member Login:
http://www.jamiiforums.com/zain.jpg

Poll: TUVUNJE MUUNGANO?

+ Reply to Topic
Page 194 of 194 FirstFirst ... 94 144 184 192 193 194
Results 3,861 to 3,871 of 3871
  1. #1
    Sam
    Sam is offline
    JF Senior Expert Member Sam will become famous soon enough Sam will become famous soon enough Sam will become famous soon enough Sam will become famous soon enough Sam will become famous soon enough Sam will become famous soon enough Sam will become famous soon enough Sam will become famous soon enough
    Join Date
    Tue Jun 2006
    Posts
    595
    Thanks : 0
    Thanked 3 Times in 2 Posts
    Rep Power
    26

    Default Muungano na kero zake: Tuuvunje?

    Nimevumilia vya kutosha nikidhani kama kuna mtu anayekerwa na fumbuzi wa matatizo ya muungano yaliyotolea kwenye kikao cha pamoja kati ya Mh. Lowassa na Mh. Nahodha.

    Kitu kinachonitisha ni kwamba yale mambo waliowaamulia wananchi yatapelekwa bungeni october kwa ajili ya "constitutional reforms".
    Kwa upande wangu sikubaliana na ufumbuzi waliofikia kwa 100%
    Check this out:

    1) mineral and oil exploration be co-opted into the national debate on the future of the political federation.

    -debate is good but mineral and oil exploration should not be political.

    2)Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) should have an equal number of representatives from either side.

    -Equal number kwa vigezo gani? Idadi ya watu? Tuelezene mlivyokuja na hiyo soultion equal number of people.

    3)consultant on the distribution of wealth generated through mining and oil extraction be hired to advise the Union government on how it can be shared equitably.

    -Please kama ni hivyo na huo muungano hatuutaki. For what?

    4)It was decided that 50 per cent of the income would be used to finance the operations of the authority and the other 50 per cent be distributed on the basis of 60 per cent for the Mainland and 40 per cent for Zanzibar.

    -Hivi hizo hesabu mnafanyaje? How did you come up with 60%, ardhi, watu,?????

    Najua watanzania hawataki kuongelea muungano wakiogopa mizimu ya Mwalimu. Kwa upande wangu kuna mambo mawili tu hapa ambayo yanaweza kuleta ufumbuzi wa kudumu kwanza kuuvunja muungana na Zanzibar ikawa nchi kama ilivyo Kenya na tutaendelea kushirikian nao kama tunavyoshirikiana na Kenya, au Zanzibar uwe mkoa. zanzibar kuna watu wasiozidi 3 mil wakati mkoa wa Dar tu una watu 4 mil. Hapo utajiuliza ni kivitu tugawane nusu kwa nusu?

    Kama watu hamtaki kuongela hili sual basi mwezi October linaingia kwenye katiba.



    Mkataba wa makubaliano ya kuanzisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukisainiwa mwaka 1964.

    Mkataba wenyewe (uliosainiwa) umeambatanishwa kama attachment.
    Attached Files
    Last edited by Silencer; 29th January 2010 at 08:50 PM. Reason: Title from Tuvunje Muungano to new one!

  2. The Following 2 Users Say Thank You to Sam For This Useful Post:

    Mdondoaji (15th February 2010), Recta (28th January 2010)

  3. #3861
    JF Premium Member Kilasara will become famous soon enough Kilasara will become famous soon enough Kilasara will become famous soon enough Kilasara will become famous soon enough Kilasara will become famous soon enough Kilasara will become famous soon enough Kilasara will become famous soon enough Kilasara will become famous soon enough
    Join Date
    Sun Dec 2008
    Posts
    212
    Thanks : 130
    Thanked 43 Times in 25 Posts
    Rep Power
    22

    Red face Re: Muungano na kero zake: Tuuvunje?

    Wazanzibari hawatosheki licha ya kwamba Wabara have bent backwards ili kuwaridhisha. Unguja na Pemba hata hawanaukubwa kama mkoa mmoja wa Tanzania Bara.

    Pendekezo langu ni kwamba Muungano uvunjwe au Katiba ibadilishwe ili tuwe na Serikali moja itakayotambua Unguja kama mkoa na Pemba kama mkoa.

    Kupokezana kwa zamu u-Rais kama Mhe. Khatib anavyopendekeza ni kichekesho. Labda kila Mkoa Tanzania upewe zamu ya kutoa Rais. Zanzibar wameshapata zamu yao. Wangoje mpaka Rais wa 24!

    Kilasara

  4. #3862
    Junior Member Gasisi will become famous soon enough Gasisi will become famous soon enough Gasisi will become famous soon enough Gasisi will become famous soon enough Gasisi will become famous soon enough Gasisi will become famous soon enough Gasisi will become famous soon enough Gasisi will become famous soon enough
    Join Date
    Wed Apr 2010
    Posts
    1
    Thanks : 0
    Thanked 0 Times in 0 Posts
    Rep Power
    0

    Default Re: Dk. Mvungi aeleza sababu za mabadiliko Baraza la Mawaziri

    Quote Originally Posted by Unregistered View Post
    MABADILIKO ya baadhi ya mawaziri yaliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki yametokana na mawaziri hao kushindwa kufanya kazi kwa kasi.

    Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha ‘Sema Usikike’ kinachorushwa na televisheni ya ITV.

    "Mabadiliko hayo ninaweza kusema yametokana na baadhi ya viongozi kushindwa kufanya kazi. Mfano, bado kuna kero zinazowasumbua wananchi kwa kipindi cha miezi kumi, lakini hazijapatiwa ufumbuzi, hivyo anahofia imani kwa wananchi, kuwa serikali itawaletea maisha bora itapungua," alisema.

    Alizitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni matatizo ya umeme, maji, njaa na ajira.

    "Baada ya matatizo kuendelea kuwa ni kero kwa wananchi, tulitegemea kuona uwajibikaji kwa viongozi husika, kwani kipindi cha miezi kumi kinatosha kutatua matatizo, lakini wameonekana kushindwa kwenda na kasi, ingetakiwa kuwajibishwa, si kuwapangua," alisema.

    Dk. Mvungi pia alidai kuwa Rais aliwateua mawaziri hao bila kuangalia taaluma zao.
    nakubALIANA NA UNACHOSEMA

  5. #3863
    Senior Member jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari's Avatar
    Join Date
    Sat Feb 2010
    Posts
    122
    Thanks : 40
    Thanked 42 Times in 31 Posts
    Rep Power
    21

    Default Viongozi SMZ, Muungano hawaaminiani, asema Jussa

    WAKATI Watanzania wanaadhimisha ya miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, imeelezwa kuwa kuna hali ya kutoaminiana kati ya viongozi wa serikali za pande mbili. Aidha, imeelezwa kuwa wakati umefika sasa wa kuandikwa kwa katiba mpya na mkataba mpya wa Muungano kwa kuwa ndiyo msingi wa matatizo. Mbunge wa kuteuliwa, Ismail Jussa Ladhu alisema hayo katika mahojiano maalum na Mwananchi mjini Dodoma wakati alipoungana na wabunge wengine kueleza kuwa Muungano huo mkongwe una mafanikio ya kuigwa barani Afrika, lakini wakasema una kasoro ambazo ni lazima ziondolewe ili uwe imara zaidi. “Katika miaka 46 ya uhai wa Muungano huu, kuna hali ya kutoamiana kati ya viongozi wa serikali za pande mbili,” alisema Jussa. Alisema hali hiyo inadhihirishwa na mivutano baina ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Muungano, mivutano ambayo alisema imedumu kwa wakati wote tangu nchi hizo zilipoungana Aprili 26 mwaka1964 wakati rais wa serikali ya awamu ya kwanza, Julius Nyerere na rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume. Alisema ingawa wapo viongozi wachache wa SMZ waliomaliza muda wao bila kukwaruzana, upo ushahidi wa wazi wa kukwaruzana na kutoaminiana na kutaka kurekebishwa kwa hali hiyo. Alisema hayo yalisababishwa na tofauti ya mitazamo ya uendeshaji Muungano baina ya viongozi hao. “... ni wachache walioongoza Zanzibar bila kukwaruzana na Serikali ya Muungano. Upo ushahidi wa wazi wa mivutano na kukwaruzana... hata (rais wa pili wa Zanzibar) Aboud Jumbe, katika kitabu chake kuhusu Muungano, ameonyesha kuwa Nyerere na Karume walikwaruzana na hawakuzungumza katika mwaka wa mwisho wa uhai wa Karume,” alisema Jussa. Alibainisha kuwa katika kitabu hicho Jumbe, ambaye pia aliwahi kuwa makamu wa rais, ameonyesha kuwa kwa muda huo wa mkwaruzano Karume na Nyerere walizungumza kupitia yeye (Jumbe) na marehemu Bhoke Munanka. Alisema anachokiona yeye ni kuwa Muungano huo ulikuwa wa kisiasa zaidi na haukuwa na msingi mzuri wa katiba na sheria, jambo alilosema ndiyo msingi wa matatizo yake. “Muungano ulikuwa wa kushtukiza, ni wa kisiasa, hauna msingi mzuri wa katiba na sheria. Wakati umefika sasa ‘kufanyike solution’ (suluhisho) kwa kuandikwa kwa katiba mpya na mkataba mpya wa Muungano,” Jussa alisema. Katika hatua nyingine, Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha amesema kuwa kuvunja Muungano si njia ya kutatua kero zinazoukabili, bali ni kusababisha matatizo. Akizungumza na waandishi wa habari juzi wakati wa hafla ya miaka 46 ya Muungano Ikulu jijini Dar es Salaam, Nahodha alisema kutokana na kutambua kuwepo matatizo ndani ya Muungano, pande zinazohusika ziliamua kuunda kamati inayoshughulikia masuala hayo peke yake. Alisema kamati hiyo yenye wajumbe kutoka Tanzania Bara na Visiwani tayari imetatua kero ya kwanza iliyokuwa ni kutozwa ushuru wa kusafirisha mizigo kwa wananchi wa Zanzibara na imemalizia na kero ya ukusanyaji wa kodi ya mapato ya kibiashara pande hizo za muungano. “Kuvunja muungano si njia ya kutatua matatizo, bali njia sahihi ni kukaa pamoja na kuangalia chanzo cha matatizo ili kuweza kulipatia ufumbuzi. Jambo hili litatuongoza kwenye makubaliano yetu, lakini watu mkianza kugombana mnaweza kufikishana pabaya wakati ni ndugu,” alisema Nahodha. http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-...ni-asema-jussa

  6. #3864
    Senior Member jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari's Avatar
    Join Date
    Sat Feb 2010
    Posts
    122
    Thanks : 40
    Thanked 42 Times in 31 Posts
    Rep Power
    21

    Default Kauli ya Waziri Khatib yawakera Wazanzibari

    SIKU moja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mohammed Seif Khatib kupendekeza mrithi wa Rais Jakaya Kikwete atoke Zanzibar, wanasiasa wamemjibu kuwa fursa ya Mzanzibari kuongoza Serikali ya Muungano kwa sasa haipo baada ya Dk Salim Ahmed Salim kukumbana na vikwazo mwaka 2005. Juzi Waziri Khatib, ambaye amekuwa akitajwa kuwemo kwenye kinyang'anyiro cha urais wa Zanzibar, alipendekeza kuanzishwa kwa utaratibu wa kupokezana urais kwa zamu baina ya Wazanzibari na Wabara ili kuimarisha Muungano, ambao juzi ulitimiza miaka 46 tangu ulipoasisiwa. Hadi sasa Ali Hassan Mwinyi ndiye Mzanzibari pekee aliyewahi kuongoza Serikali ya Muungano baada ya kuongoza serikali ya awamu ya pili kuanzia mwaka 1985 hadi 1995, lakini wanasiasa wanaona kuwa wazo la Khatib halifai. Juma Dun Haji, mwanasiasa machachari visiwani na ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na rais, alipingana na kauli ya Khatibu akidiriki kuiita kuwa ya kinafiki, akimtuhumu waziri huyo kuwa alikuwa miongoni mwa watu waliofanya propaganda chafu dhidi ya Dk Salim alipogombea urais mwaka 2005. “... ni unafiki; 2005 ilikuwa fursa na nafasi ya Mzanzibari kuongoza Tanzania, lakini Seif Khatib na kundi lake wakamtuma bibi mmoja wa Kikwajuni, Zanzibar ambaye alililewa katika familia ya Dk Salim aende kusema Dk Salim ni mmanga, Hizbu,” alidai Duni. “Kauli hii ilimfanya Dk Salim karibu kuzimia katika mkutano mkuu wa CCM Chimwaga. Leo miaka minne baadaye Seif anataka aonekane mwema kwa Wazanzibari; haiwezekani, ni mnafiki tu,” alidai Duni. Alidai kuwa hata Mzee Nassor Moyo aliwaeleza kuwa wamefanya jambo baya sana kwa Wazanzibari kwa kuvunja utaratibu aliouweka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wa kupokezana urais. “Nafasi ya wazanzibari kuongoza Tanzania ilikuwa mwaka 2005... sasa tunaitaka haipo tena, Seif aache unafiki,” alisema Duni. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema fursa ya Wazanzibari kwa nafasi ya urais wa Muungano kwa sasa haipo kwa kuwa hamna mwanasiasa ambaye anaweza kutoa changamoto hiyo, ndani ya CCM. “Kwa chaguzi zijazo na mwelekeo unavyoonyesha ndani ya CCM, fursa ya Wazanzibari kuongoza urais wa Muungano haipo. Ni vigumu sana kwa Mzanzibari kuwa rais wa Muungano,” alisema Profesa Lipumba. “Fursa pekee ya Wazanzibari kuongoza urais wa muungano ilikuwa mwaka 2005, baada ya Rais Benjamin Mkapa ambapo mzanzibari pekee ndani ya CCM mwenye kila sifa ya kuongoza Tanzania anayekubalika kitaifa na kimataifa alikuwa Dk Salim Ahmed Salim, lakini alitengenezewa fitna na kuangushwa,” aliongeza Lipumba. Alisema hoja ya Waziri Khatib ni ya msingi, lakini imeegemea zaidi katika mgogoro wa kikatiba na sehemu ya kero ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964. “Kama Waziri Khatibu anajiamini kisawasawa basi hoja hiyo inapaswa kutolewa katika vikao halali vya chama chake na sio kuitoa katika vyombo vya habari,” alisema Profesa Lipumba. “Hoja hii imegemea zaidi katika mgogoro wa kikatiba na kero ya Muungano, kwa hiyo CCM wenyewe ambao ndio wapo madarakani kwa sasa ndio wanajua namna ya kulishughulikia,” aliongeza Lipumba, ambaye ameshagombea urais mara tatu. Hata hivyo, alisema ni vigumu kutekelezeka kwa Tanzania kwa kuwa inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa na rais wake anapatikana kupitia kura anazopigiwa moja kwa moja na wananchi. “Maana ingekuwa rais hana mamlaka makubwa (ceremonial), ambaye anapatikana kwa kupigiwa kura na wabunge, basi ingekuwa rahisi lakini kwa mfumo huu tunaofuata sisi utaratibu huo hautekelezeki,” alisema Profesa Lipumba. http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-...ra-wazanzibari

  7. #3865
    Senior Member jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari will become famous soon enough jamadari's Avatar
    Join Date
    Sat Feb 2010
    Posts
    122
    Thanks : 40
    Thanked 42 Times in 31 Posts
    Rep Power
    21

    Exclamation Lini tutamaliza kabisa kero za Muungano?


    Maoni ya katuni.



    Kinachofurahisha ni kwamba Watanzania wengi hawaongelei kuhusu kuvunja Muungano na kama wapo basi wanayasema hayo kichini chini, isipokuwa kinacholalamikiwa na wengi ni kero katika Muungano huo unaotumiza miaka 46 leo. Ni kero, kero kila siku kero.
    Kwamba muungano wetu huu wa damu, licha ya kuwa wa aina yake duniani, unatoa fursa kibao zenye manufaa kwa wananchi wa pande zote mbili ni ukweli usiokuwa na pingamizi. Pengine ndio maana tunadhani kwamba mwenye mawazo ya kutaka uvunjike ana matatizo kichwani ama ana lake jambo.
    Mwishoni mwa wiki iliyopita, wasomi na wanasiasa wa hapa nchini na wenzao kutoka nchini jirani zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, walikutana jijini Dar es Salaam, nao wakaishauri Tanzania kutatua kwanza kero zilizoko katika Muungano kabla ya kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC) miaka miwili ijayo.
    Baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa yakitajwa kuwa na kero ni pamoja na uendeshaji wa nchi, masuala ya kodi na biashara pamoja na rasilimali kama vile za mafuta na gesi. Yamekuwepo pia malalamiko kuhusu ukiukwaji ama uongezwaji wa mambo ya Muungano bila wananchi kushirikishwa, na pia Wazanzibari wamekuwa wakilalamika kwamba hawanufaiki sana na Muungano kama wenzao wa Bara. Suala la Rais wa Zanzibari kuwa waziri katika baraza la mawaziri, nalo limekuwa likitajwa kama kitu kinachowachefua Wazanzibari wakiona kama linampunguzia hadhi raisa huyo. Haya yote ni mambo yanayoweza kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi.
    Licha ya kuwepo kwa wizara maalum inayoshughulikia masuala ya Muungano iliyo chini ya ofisi ya Makamu wa Rais, kinachoonekana ni kwamba kero hizi zimeendelea kuwepo. Ni vigumu pia mtu leo hii kusimama akaona waziwazi namna wizara hii ilivyotatua kero za Muungano kwa muda wa takriban miaka mitano toka Rais Jakaya Kikwete aiunde.
    Lakini, kwa mujibu wa wasomi na wanasiasa waliokutana mwishoni mwa wiki, msingi wa kero hizi uko kwenye sheria za nchi yetu, hususan sheria mama, yaani Katiba.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Utafiti wa masuala ya siasa kutoka Uganda, Agustine Ruzindana, alitoa taarifa ya utafiti wao ikionyesha kwamba matatizo ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar yanatokana na baadhi ya vipengele vya Katiba kushindwa kueleweka kwa pande hizi mbili za muungano.
    Alisema ili kumaliza dosari hizo ni lazima katiba ya nchi ifanyiwe marekebisho ili pande zote za Muungano ziweze kuamini kwamba zinanufaika nao.
    Alisema licha ya utafiti kuonyesha kwamba Wazanzibari wanaupenda Muungano, lakini wengi wanaona kama hauwanufaishi sana. Hata hivyo, alisema wenzao wa Bara walio wengi hawaamini kama Wazanzibari wana kero ambazo pengine bila Muungano wasingekuwa nazo.
    Katika mkutano huo wa wasomi na wanasiasa, Dk. Sengondo Mvungi alifafanua kwamba wakati wa kuunda Muungano, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume, walikubaliana vipengele vinane, lakini kwa sasa vimeongezwa na kufikia 11.
    Lakini akasema, kwa bahati mbaya sana, wananchi wa pande mbili hizi hawajui vipengele vya zamani vinasemaje na vilivyoongezwa vinazungumzia nini.
    Kitu kingine ambacho kimeanza kujitokeza ni Wazanzibari, tena kupitia baraza la wawakilishi kuhoji mambo mengi ya Muungano na mwisho wa siku kupitisha maamuzi ambayo taratibu yanaonekana kama yatarudia ama yanapunguza nguvu za Muungano wetu.
    Tunadhani kwamba lazima tuwe na dhamira ya kweli katika kutatua kero za Muungano kwa kukaa pamoja na kuzungumzia ikiwa ni pamoja na kupitia upya katiba na sheria za nchi yetu zinazoonekana kuwakwaza wananchi wa pande hizi mbili.
    Ingawa hili linawakera baadhi ya watu, lakini si vibaya tena ukaanzishwa mjadala wa nchi nzima kuhusu aina ya Muungano ambayo wananchi wanaitaka likiwemo suala la serikali tatu.
    Kitu kingine muhimu ni kutoa elimu kwa wananchi wa pande hizi mbili kuhusu mambo muhimu ya Muungano, yaani wayajue yale yaliyokuwepo na yaliyoongezwa na umuhimu wake.
    Tunaamini viongozi wetu wakiamua kuweka nguvu katika eneo hilo, kero za Muungano zinaweza kuisha kabisa kabla hatujaingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.



    CHANZO: NIPASHE

  8. #3866
    JF Premium Member Nyani Ngabu will become famous soon enough Nyani Ngabu will become famous soon enough Nyani Ngabu will become famous soon enough Nyani Ngabu will become famous soon enough Nyani Ngabu will become famous soon enough Nyani Ngabu will become famous soon enough Nyani Ngabu will become famous soon enough Nyani Ngabu will become famous soon enough Nyani Ngabu's Avatar
    Join Date
    Mon May 2006
    Location
    Ikungulyabashashi
    Posts
    17,812
    Thanks : 400
    Thanked 2,577 Times in 1,421 Posts
    Rep Power
    60

    Default Re: Lini tutamaliza kabisa kero za Muungano?

    Kero za muungano zitaisha pale huo muungano utakapovunjwa.
    Miafrika Ndivyo Tulivyo - "Though this be madness, yet there is method in it." - From Shakespeare's Hamlet

    To be frugal is sexy; to be cheap is tacky

  9. #3867
    ODD
    ODD is offline
    Member ODD will become famous soon enough ODD will become famous soon enough ODD will become famous soon enough ODD will become famous soon enough ODD will become famous soon enough ODD will become famous soon enough ODD will become famous soon enough ODD will become famous soon enough
    Join Date
    Thu Mar 2010
    Posts
    13
    Thanks : 0
    Thanked 1 Time in 1 Post
    Rep Power
    0

    Smile Mhe Nahodha usichaganye mambo ya muungano na vitabu vya dini

    Nilkuwa namisiliza Mhe Nahodha kwa kwenye TV akihojiwa nashangaa majibu au maelezo aliyokuwa anatoa yanasikitishwa. yeye kama mmoja wa waheshimiwa ambao wanazipitia kero za muungano.asinge pashwa kusema kero zitakuwa zinztatuliwa kidogo kidogo kama vile mtoto anavyo kuwa. leo ni miaka 46 huyu mtoto hajakuwa tu. umri wa kuishi sasa tz chini ya miaka 50 ...
    halafu kilichonifanye niandike ni kwa changa moto kwenye muungano hazina budi kuwepo , ansema pamoja na vitabu vya dini kuwa baada mtu kufa huenda ahera , lakini yeye haamini kama huko ahera hakuna changa moto lakini kuna changa moto. .Kwa maoni yangu hii sasa nikufika mbali.

    bibilia inasema huko mbinguni watu wanafurahi na kuimba nakumshanglia na kusifu Mungu , hakuna changamoto hata moja. Ni kweli sasa viongozi watu wamelewa madaraka !!!

  10. #3868
    JF Senior Expert Member Tindikali will become famous soon enough Tindikali will become famous soon enough Tindikali will become famous soon enough Tindikali will become famous soon enough Tindikali will become famous soon enough Tindikali will become famous soon enough Tindikali will become famous soon enough Tindikali will become famous soon enough
    Join Date
    Fri Mar 2010
    Posts
    271
    Thanks : 28
    Thanked 120 Times in 78 Posts
    Rep Power
    21

    Default Re: Mhe Nahodha usichaganye mambo ya muungano na vitabu vya dini

    Quote Originally Posted by ODD View Post

    bibilia inasema huko mbinguni watu wanafurahi na kuimba nakumshanglia na kusifu Mungu , hakuna changamoto hata moja. Ni kweli sasa viongozi watu wamelewa madaraka !!!

    Hii mada ni dini, sio siasa, au?

    Changamoto mbinguni zipo, Mkuu Nahodha kapatia. Shetani aliingia vishawishi vya kupindua utawala wa Ulimwengu, akazua sokomoko Mungu akamtupa duniani. Kuna changamoto ya kushikilia imani yako ya uaminifu ukiwa ahera.

    (Ni taarifa ya tukio kutoka upande mmoja, wa Mungu, shetani yeye hatujamsikia kuhusu kilichojili huko Mbinguni, usikute wakati wa uchaguzi ulifika Mungu akawa anaendelea kubadilisha Katiba ya Mbingu kusitiri himaya yake tena na tena. Shetani akaona isiwe tabu.)

  11. #3869
    JF Senior Expert Member saitama_kein will become famous soon enough saitama_kein will become famous soon enough saitama_kein will become famous soon enough saitama_kein will become famous soon enough saitama_kein will become famous soon enough saitama_kein will become famous soon enough saitama_kein will become famous soon enough saitama_kein will become famous soon enough saitama_kein's Avatar
    Join Date
    Thu Oct 2009
    Location
    TMK
    Posts
    404
    Thanks : 62
    Thanked 95 Times in 75 Posts
    Rep Power
    21

    Default Re: Mhe Nahodha usichaganye mambo ya muungano na vitabu vya dini

    Quote Originally Posted by ODD View Post
    Nilkuwa namisiliza Mhe Nahodha kwa kwenye TV akihojiwa nashangaa majibu au maelezo aliyokuwa anatoa yanasikitishwa. yeye kama mmoja wa waheshimiwa ambao wanazipitia kero za muungano.asinge pashwa kusema kero zitakuwa zinztatuliwa kidogo kidogo kama vile mtoto anavyo kuwa. leo ni miaka 46 huyu mtoto hajakuwa tu. umri wa kuishi sasa tz chini ya miaka 50 ... halafu kilichonifanye niandike ni kwa changa moto kwenye muungano hazina budi kuwepo , ansema pamoja na vitabu vya dini kuwa baada mtu kufa huenda ahera , lakini yeye haamini kama huko ahera hakuna changa moto lakini kuna changa moto. .Kwa maoni yangu hii sasa nikufika mbali. bibilia inasema huko mbinguni watu wanafurahi na kuimba nakumshanglia na kusifu Mungu , hakuna changamoto hata moja. Ni kweli sasa viongozi watu wamelewa madaraka !!!
    Mnh hapa sina comments....................
    We can't solve problems by using the same kind of thinking we used when we created them

  12. #3870
    Senior Member MLEKWA will become famous soon enough MLEKWA will become famous soon enough MLEKWA will become famous soon enough MLEKWA will become famous soon enough MLEKWA will become famous soon enough MLEKWA will become famous soon enough MLEKWA will become famous soon enough MLEKWA will become famous soon enough
    Join Date
    Sat Aug 2007
    Posts
    60
    Thanks : 0
    Thanked 12 Times in 7 Posts
    Rep Power
    24

    Default Re: Mhe Nahodha usichaganye mambo ya muungano na vitabu vya dini

    []
    Inabidi tujiulize huyu Nahodha mwenye kutaka Urais ndio alihusika kuwauzia Uraia wa Tanzania na ukaazi wa Zanzibar kwa lengo la kupata kura wale Wakimbizi wa Msumbiji huko Zanzibar.
    for more information see this link below.

    http://www.mzalendo.net/ushahidi-wa-...wa-wa-zanzibar

  13. #3871
    JF Senior Expert Member Buchanan will become famous soon enough Buchanan will become famous soon enough Buchanan will become famous soon enough Buchanan will become famous soon enough Buchanan will become famous soon enough Buchanan will become famous soon enough Buchanan will become famous soon enough Buchanan will become famous soon enough Buchanan's Avatar
    Join Date
    Tue May 2009
    Posts
    4,530
    Thanks : 1,119
    Thanked 1,744 Times in 1,074 Posts
    Rep Power
    31

    Default Re: Mhe Nahodha usichaganye mambo ya muungano na vitabu vya dini

    Quote Originally Posted by ODD View Post
    Nilkuwa namisiliza Mhe Nahodha kwa kwenye TV akihojiwa nashangaa majibu au maelezo aliyokuwa anatoa yanasikitishwa. yeye kama mmoja wa waheshimiwa ambao wanazipitia kero za muungano.asinge pashwa kusema kero zitakuwa zinztatuliwa kidogo kidogo kama vile mtoto anavyo kuwa. leo ni miaka 46 huyu mtoto hajakuwa tu. umri wa kuishi sasa tz chini ya miaka 50 ...
    halafu kilichonifanye niandike ni kwa changa moto kwenye muungano hazina budi kuwepo , ansema pamoja na vitabu vya dini kuwa baada mtu kufa huenda ahera , lakini yeye haamini kama huko ahera hakuna changa moto lakini kuna changa moto. .Kwa maoni yangu hii sasa nikufika mbali.

    bibilia inasema huko mbinguni watu wanafurahi na kuimba nakumshanglia na kusifu Mungu , hakuna changamoto hata moja. Ni kweli sasa viongozi watu wamelewa madaraka !!!
    Wewe tatizo lako ni nini? Unataka Nahodha aongee yaliyo kichwani mwako ndio tuseme kaongea vizuri?
    "Neither is there salvation in any other: for there is none other name under heaven (except the name of Jesus Christ of Nazareth) given among men, whereby we must be saved!" (Acts 4:12).


 

Topic Information

Users Browsing this Topic

There are currently 1 users browsing this thread. (0 members and 1 guests)

     

Tags for this Topic

Bookmarks

Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts