Nyuzi kama hii ndipo nnapopata fursa ya kumsifu Kikwete, kabla
Invisible hajatuwekea humu hiki kitabu, Kikwete kaanza kulifanyia kazi zamani sana na nivyema mpaka leo (2008) elimu imewafikia kina
Invisible na wanaanza kuwatanabahisha na wengine, ingawa
Invisible yupo miaka miwili nuyma lakini hii ni kazi ya kuendelea na nampongeza kwa kuiunga mkono kwa kutowa elimu kama hii aliyotuwekea.
Kikwete hii kazi aliianza na kuifanya kwa kubadilisha sheria humu ndani ya nchi zinazohusiana na utoroshaji wa fedha na rushwa, hakuishia hapo akakazania sana kuhusu sheria ya Umoja wa Mataifa itakaruhusu fedha zilizopo nje ya Afrika za Waafrika ziwekwe wazi na kurudishwa ikigundulika hazijapatikana kihalali, hata juzi juzi alilisemea sana alipokuwa Arusha kwenye mkutano wa majaji wa jumuiya madola.
Alilitilia mkazo pia walipokutana na wakuu wa kuzuia rushwa afrika mashariki.
Sasa japo tunaona manufaa ya kazi yake, angalau tunajuwa ziko ngapi hapo Uswisi tu na bado zipo nje kwingine kwingi na nyingi tu nna uhakika Kikwete haziachi hizo, kama alivyorudisha fedha za rada na hizi zitarudi tu.
Hapo ndipo nnapompendea Kikwete, nyie semeni yeye anafanya.
Kuwakumbusha tu kuwa kazi hii kaianza zamani na leo mna matunda yake nimewawekea links tofauti hapa chini mjikumbushe:
http://www.google.com/url?sa=t&rct=j...vFP36w&cad=rj a
Kenya: Kikwete calls for uniform tax system in East Africa
Zimefichuka » Blog Archive » KIKWETE’S CAMPAIGN AGAINST CORRUPTION PROMISING
Kikwete on money laundering and corruption - Google Search[+Arusha
Follow Us Here