Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

    Report Post
    Page 2 of 14 FirstFirst 123412 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 261
    1. #1
      Quinine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th July 2010
      Posts : 3,704
      Rep Power : 1205
      Likes Received
      383
      Likes Given
      116

      Default Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      • Wasubiri barua zao kujibu mapigo, CCM yawaita Mapacha Watatu

      WAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijipanga kuwaandikia barua makada wake watatu wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Edward Lowassa (Monduli), Rostam Aziz (Igunga) na Andrew Chenge (Bariadi Mashariki), makada hao wanasubiri kukabidhiwa barua hizo ili watoe kile waliochokiita maamuzi mazito dhidi ya CCM, Tanzania Daima Jumatano limejulishwa.

      Makada hao maarufu kwa jina la Mapacha Watatu, wanasubiri kukabidhiwa barua hizo ili wavunje ukimya na kueleza upande wa pili wa shilingi kwa madai kuwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), hakukuwa na azimio lolote lililopitishwa la kuwataka wapewe siku 90 za kujiengua na pia hakukuwa na azimio la kuandikiwa barua.

      Mmoja wa makada hao, aliliambia Tanzania Daima Jumatano mjini Dodoma kuwa Rais Jakaya Kikwete na chama chake wamefanya jambo la hatari dhidi yao pengine kwa kujua au kutokujua lakini lazima wajibu mapigo ili jamii ielewe.

      “Sitaki kuzungumza sasa hivi na huo ndio msimamo wetu. Waswahili wanasema akutukanaye hakuchagulii tusi, tunaangalia, tunafuatilia kwa karibu mambo yote kuanzia ndani ya vikao hadi sasa kinachoendelea kwenye mikutano ya hadhara hakika ni udhalilishaji wa hali ya juu. Tusubiri barua, tutajua la kufanya,” alisema kada huyo, mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi.

      Aidha, baadhi ya watu wa karibu walidokeza kuwa kitu cha kwanza kinachotarajiwa kufanywa na makada hao mara tu baada ya kukabidhiwa barua zao, ni kurejesha kadi za CCM, hatua itakayofanya wapoteze majimbo yao ya uchaguzi, lakini watahakikisha lazima chama kithibitishe ufisadi wao.

      Kada huyo hakutaka kuzungumza kwa undani jinsi walivyopokea maamuzi ya NEC na hatua inayoendelea kwenye mikutano ya hadhara inayohutubiwa na Katibu Mkuu, Willson Mkama, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, na viongozi wengine wa sekretarieti mpya ambao jana walitua mkoani Iringa.

      Katika mikutano ya hadhara inayodaiwa kuwa ni ya kujitambulisha, Nape amekuwa akiwataja Mapacha Watatu: Lowassa, Rostam na Chenge kwamba wametakiwa kujiondoa kwenye ujumbe wa NEC ndani ya siku 90, vinginevyo watang’olewa kwa nguvu.

      Nape ambaye hadi sasa bado ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi, alienda mbali kwa kusema watuhumiwa hao hivi karibuni wataandikiwa barua na kuorodhesha tuhuma zao; na kusisitiza azimio la NEC la kuwataka wang’oke vinginevyo wataenguliwa na chama.

      Hata hivyo, katika hatua nyingine, azimio la kutoa siku 90 kwa watuhumiwa hao wa ufisadi limeibua vita ya kisiasa kati ya mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, na makada hao.

      Wadadisi wa mambo ya siasa, wanaona kuwa kilichotokea mjini Dodoma ni muendelezo wa minyukano ndani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2015 na siku za baadaye pia kwani mkakati wa kujivua gamba, ulipangwa makhsusi kwa ajili ya kuwaengua wao wakati orodha ya mafisadi ndani ya chama hicho ni ndefu.

      Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa na mmoja wa wajumbe wa NEC wanaodaiwa kupanga kusuka mpango huo, umethibitisha pasipo shaka kwamba Rais Kikwete, aliendesha vikao kwa kupanga wajumbe kutoa hoja za kuwang’oa Chenge, Lowassa na Rostam.

      Kiongozi mmoja wa siku nyingi wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima Jumatano anasema hoja ya kutaka Kamati Kuu na sekretarieti nzima kujiuzulu, ililenga kuwatema Mapacha Watatu, ndani ya vikao hivyo vyenye nguvu kwa njia ambayo ingemuepusha Rais Kikwete katika lawama za moja kwa moja.

      “Chama chenye maadili, falsafa, mwongozo na itikadi, hakiwezi kuwapigia kampeni watu wanaohusishwa na ufisadi kwamba wanafaa huku kikisema hakuna ushahidi, halafu baada ya kupata ubunge na wengine hata kuongoza kamati nyeti za Bunge, chama hichohicho kinawataka watoke kwa madai kuwa hawafai. Ushahidi wa sasa kwamba hawafai, wameupata wapi?” alihoji mjumbe mmoja wa NEC.

      Wadadisi wa mambo ya siasa wanaohoji hatua hiyo, wanasema uongozi mpya wa CCM ulipaswa kujikita kueleza matarajio ya chama siku zijazo na mikakati ya kujiimarisha na kueleza maazimio mengine ya NEC.

      “Nape na wenzake hapaswi kuendelea kumzungumzia Lowassa na wenzake; haya mambo wameyamaliza kwenye vikao. Wanapaswa kueleza matatizo ya msingi ya chama na taifa kwa ujumla, hasa utekelezaji wa Ilani ya CCM,” alisema.

      Anasema ingawa wanakubaliana kimsingi na hatua ambazo CCM inatakiwa kuzichukua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi, wanashangazwa na hatua ya Nape kutangaza azimio ambalo si sehemu ya mambo yaliyojadiliwa na kukubalika ama kwa kura au kwa kauli moja na wajumbe wote.

      Hatua ya Nape inafananishwa na matukio ya hivi karibuni hususan wakati John Chiligati akiwa Mkuu wa Idara ya Uenezi na Itikadi kwamba amepata kutaja mara kadhaa taarifa isiyo sahihi ya maazimio ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu tofauti na kile kilichojadiliwa ndani ya vikao hivyo.

      Chiligati alipata kulalamikiwa kwa kutoa taarifa potofu kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu kuhusu uamuzi wa ama kuilipa au kutoilipa fidia kampuni ya uzalishaji umeme ya Dowans ambayo inaidai Tanzania karibu shilingi bilioni 100.

      Chiligati anatajwa pia kupata kutoa maazimio ya kupotosha wakati aliposoma maazimio ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu utata ulioibuka baada ya kukatwa kwa jina la Hussein Bashe katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM kwa jimbo la Nzega katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
      Walianza na ukabila haukulipa wakaja na ukanda haukulipa, wakaleta singo ya udini imewarudi, mwisho wameibuka na ugaidi wamechanganyikiwa.


    2. #21
      gongolamboto's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 21st February 2011
      Posts : 153
      Rep Power : 452
      Likes Received
      26
      Likes Given
      36

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      Quote By kush afrika View Post
      huu ni mwisho wa mafisadi na chama chao
      Hakuna lolote hapo. CCM inawapiga changa la jicho tu. Sibirini muone
      A Conference is a gathering of important people who individually can't do
      anything but together can decide that nothing can be done

    3. #22
      Teamo's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 9th January 2009
      Location : KIJIWE SAMRI-BOM BOM
      Posts : 12,168
      Rep Power : 11902
      Likes Received
      806
      Likes Given
      635

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      hahaha!
      chenge-JOSEE MARA MUTOTO YA KIMARA

      rostitamu-HAMZA KALALA JUNIOR

      eddo-KHALEED CHOKORAA
      '!....Wakatafuta Namna Nzuuuuuuuuriiiiii.....WAKASHUG HULIKA....!'

    4. #23
      Polisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2010
      Posts : 1,574
      Rep Power : 749
      Likes Received
      382
      Likes Given
      238

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      Mwacheni Mwalimu aitwe Mwalimu. Naona yule mzee alipozungumzia suala la ubaguzi watu wengi hawakumwelewa. CCM wanawabagua CHADEMA kwa kusema wao chadema sisi CCM. Wamemaliza hapo, wamegundua ala kumbe kumbe tuna magamba. Watavua magamba yote na mwisho wa siku watagundua kuwa wana UPELE. Sasa hapo ndo ngoma itakapokuwa inogile. Jamani kutoa upele kazi sana, hiyo nadhani mpaka m/kiti atalia
      ''Taabu Huisha Bali Ujinga Hudumu''

    5. #24
      Ronal Reagan's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 2,722
      Rep Power : 981
      Likes Received
      641
      Likes Given
      262

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      Picha hizi ni ushahidi mzuri sana kuwa Kikwete ni mnafiki sana.

      Nasikia wakati wa kampeni za uchaguzi 2010 hukuo Rombo, Kikwete alisema mtuhumiwa anabaki hana hatia mpaka ithibitishwe vingnevyo na mahakama. Akimaanisha Mramba ni shoka la zamani lenye haki sawa kupata ridhaa ya kuongoza jimbo hilo. Fast foward miezi minne baadaye kwa nini huyu mnafiki asiwe na consitency?

      Sasa basi ni wajibu na dhamana yake sasa kutoa ushahidi hadharani wa hao pacha watatu. Lazima Kikwete na CCM (maana ndio waliowapitisha hao kwa majimbo yao) wawajibishwe sawa sawa. Chadema walishasema zamani hao ni mafisadi, wananchi walijua kitambo hao ni mafisadi lakini Kikwete alisimama mbele kuwatetea. Naamini alijua wazi kuwa hao na mafisadi. Huo ni ubadhirifu wa fedha na rasilimali ya umma, kwani hiyyo gharama ya kurudia uchaguzi katika majiombo hayo inapaswa ilipwe na Kikwete na CCM. Ni usanii. Ni ushenzi wa hali ya juu.

      Mwisho, hili igiz/filamu ni ya kustaajabisha kwa mengi. Kwani kiuhalisia Kikwete ni mtuhumiwa mkuu namba moja wa ufisadi. Jiulize mwisho wake ukoje!

    6. #25
      hmethod's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th February 2008
      Posts : 1,737
      Rep Power : 936
      Likes Received
      116
      Likes Given
      131

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      Chama Cha Misukule hicho hakuna haja ya kuhangaika nao....watamalizana karibuni maana wote ni misukule tu haina akili hiyo!
      Salus Populi Suprema Lex Esto

      Salva Veritate


    7. #26
      wakusoma's Avatar
      Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Posts : 37
      Rep Power : 585
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      mimi niliuliza mwaka 2005 kuwa tunampa nchi mkwereeeee???????ndiyo faida yake sasa hii.hawa watu wanaotoka mikoa ya pwani ni watu wa masihara masihara.si watu makini.huyu bwna sijui alifikaje chuo kikuu.uwezo wake wa kufikiri ni sawa na kijana wa form 4 mwenye division 3 labda.

    8. #27
      Chamkoroma's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th September 2010
      Posts : 187
      Rep Power : 483
      Likes Received
      6
      Likes Given
      1

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      Quote By Lukansola View Post
      I say thanks for this useful post, sijui prezidaa alikuwa anafikiri nini hapo, hii ni kuwafanya watanzania wajinga wasio na uwezo wa kifikiri, ni bora hata jk angeacha wakajipigia kampeni wenyewe, sidhani kama wangeshindwa bila kikwete, pili kwani jk aliwapigia kampeni wagombea wote wa ccm, sasa kwa nini hawa. This was a big mis-calculation.
      Na asiye na dhambi na awe wa kwanza kumpiga jiwe, Yesu akatazama chini na kuandika ardhini alipoinua macho wakawa wameondoka wote, nasema, JK umejipalia makaa, ndugu yangu, unawatosa watatu, wakati kunawengi, umeshau aliyekuwa MP wwa Rombo? hukumtosa, unajua ufisadi unaofanywa Maliasili umeamua vp?

      Unajua nini kunaendelea TRA, bandarini, viwanja vya ndege, mipakani umechukua juhudi gani? hawa ni wa bunge watatu, je unadhani ndiyo mianya pekee inayosababisha ufisadi kukua? Unakumbuka Azimio la Arusha sababu yake kuu nini? Siyo ufisadi? japo wengine tulikuwa bado au wadogo sn, lkn hatua ya Moringe sokoine kukomaa na mafisadi kuanzia wahindi mpaka wafanya kazi wa serikali ndiyo ulikuwa msingi pekee wakuiponya nchi, lkn hii hatua ni kuosha kikombe nje ndani kuna mende japo niwadogo lkn maji hayanyweki.

      Hakika nasema akina kabwela walala hoi tunakuambia kuwa ukitaka kuiponya nchi jukumu kubwa nikuwafilisi watendaji wakuu waserikali ambao unadhani au unauhakika na uporaji wamaliasili za nchi, nadhani siku hizi usalama wa taifa wamekuwa si watunza siri, hata ukiwatuma kwenye viwanja vya ndege kuwa wafanya kazi badala yake wataanza kufanya ufisadi.

      Mawaziri husika hawafanyi kushtukiza kukagua utendaji wa mipaka yetu, nakumbuka kufanyiwa rusha hapo nyerere airport, lkn leo ukisema unageukiwa wewe, ndug, dhambi hii japo umesema kwa kuponya kidonda cha kujikwaa kisiasa km ulipomwambia EL, unasababisha jipu ambalo kweli kupona kwake ni kulitumbua kwa kisu na usaha ukitoka watu wote watasema haaa! kumbe ccm wako hivi!

      Laiti ungesema yaliyopita si ndwele wa TZ kwaniaba ya wote tunaomba msamaha, halafu huko chinichini uchukuwe hatua ya kumwaga mboga, wao wangekula ugali bila kujua mboga inakuja hau imemwagwa, lkn unasema namwaga, wao wanasema cc ugali hatuli tunamwaga, wote mnalala njaa, ccm siyo mama, siyo baba, wakijitoa nakusema wakotayari kuwaomba msamaha wa TZ na wakakubaliwa wakirudi ulingoni kivinge, ww utakuwa unajipumnzisha ndipo watakuambia ukakalale lupango kwani hukusema ukweli kuhusu mali zako, nasema ukimaliza muhula wako ck zinaendelea, nakusikitikia hukuona mbali, utajiamaliza mwenyewe, hawa watuwakitubu nakurudisha mali walizochukua nakuomba msamaha kwa wanachi je utasmeaje?

      Amani ya kweli huja kwa kusameheana nakuomba yalopita yasirudiwe, na utendaji wa serikali uboreshwe.

    9. #28
      mzambia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Location : BHULAMBYA MALAWI
      Posts : 820
      Rep Power : 593
      Likes Received
      19
      Likes Given
      4

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      Waache waipige mkwara ccm maana jana nimesoma tazama tanzania wanasema kuwa ugomvi wa lowassa na jk ni kama wa kambona na nyerere au wa jenerali na mkapa kweli hiyooo!!!
      "HE WHO BUILD ON PEOPLE, BUILDS ON MAD" DON VITO CORLEONE AND " KEEP YOUR FRIEND CLOSE BUT YOUR ENEMY CLOSER"

    10. #29
      Duduwasha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Posts : 2,630
      Rep Power : 6254
      Likes Received
      526
      Likes Given
      421

      Default Re: Lowasa na Rostam wajiandaa kumuangamiza Kikwete.

      Nilipe Ng'ombe wangu....! Puta na mimi nipute...! Thubutu!!!!! Niguse uone!!!
      Tusubiri Suparing Ngumi za Majeba!!!!
      saragossa likes this.

    11. #30
      Sikonge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2008
      Location : Sikonge, Tabora
      Posts : 7,986
      Rep Power : 2362
      Likes Received
      2945
      Likes Given
      5799

      Default Re: Lowasa na Rostam wajiandaa kumuangamiza Kikwete.

      Duduwasha,

      Hiki Mami ni Kinyamwezi na si Kiswahili na naona umefanya direct translation tu hahahahaaa

      Umenirudisha utotoni wakati watu wanachonganisha wenzao wazipige " ....Nnepile ng'ombe zyane." Hahahaa ...

      Safi sana. Kuna ile ya kuchora mstari na ukiuvuka tu...... au sema Zuu!!!!
      Quote By Duduwasha View Post
      Nilipe Ng'ombe wangu....! Puta na mimi nipute...! Thubutu!!!!! Niguse uone!!!
      Tusubiri Suparing Ngumi za Majeba!!!!
      Nguruwe pita leo sina Mkuki(By Malila wa JF).

    12. #31
      ALI KIBERENGO's Avatar
      Member Array
      Join Date : 20th June 2009
      Posts : 73
      Rep Power : 523
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      Quote By Mpevu View Post
      Hatma ya CCM imefika ukingoni, kwa hatua ya kuwavua EL, AC & RA ni sawa na laana kwa chama. JK katu hatoweza kuitawala nchi hii na atapata laana kali ya muumba toka kwa watanzania wote (waislamu & wakristo), nayasema haya kwani ni jambo ambalo...WAMEKUWA PAMOJA, WAMEPANGA MIPANGO PAMOJA, WAMEFAULU PAMOJA, WAMEINGIA IKULU PAMOJA leo hii uwashushie dhambi kama hii wao tu?

      Ni uonevu usio kifani, mkuu wa nchi anapaswa kutazama mara mbili hayo aliyoongoza NEC kuamua kwani hata (hao watatu) wakipotezwa bado laana itaendelea kuwepo.

      MY TAKE:

      Ilipaswa wote wajiuzulu kuanzia mkuu wa nchi ambapo makamu wake ashike hatamu...NDIPO SALAMA ITAKUWEPO.

      Mola hawezi kuwaacha viumbe wake waliokuwa pamoja na sasa wanadhulumiana ilhali walisaidiana wakiwa ni 'boyz 2 men', kwa sasa kuwatupa tena kwa kashfa nzito shauri ya fahari hizi fupi za dunia ni uonevu na kukithiri kwa kupokea majungu toka kwa wapambe,, HAPANA;JK ANAPASWA AJITAZAME NA ATAZAME HATMA YAKE IKOJE, atakuwa hatarini abadan.
      TOBAAA, Hivi wewe unamshirikisha mungu kusaidia MAFISADIII, Umechanganyikiwa mwenzetu wewe tafuta mtu akuzinguwe

    13. #32
      samora10's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st July 2010
      Location : Kwa-Gude
      Posts : 3,271
      Rep Power : 1111
      Likes Received
      732
      Likes Given
      1170

      Default Re: Lowasa na Rostam wajiandaa kumuangamiza Kikwete.

      ..ukimwaga ugali nami namwaga mboga, sisi ngoja tukae pembeni tuangalie chezo zima linavyochezwa

      halafu hao wabunge wa ccm,mwenyekiti, spika na wengine ni vilaza wa ajabu.. sasa kama EL alikua anajulikana hata ndani ya chama kama fisadi? walimpigiaje kura ya kuwa mwenyekiti kamati ya mambo ya nje na usalama?
      ''Mipango na Mikakati imekamilika na sasa tuko kwenye mchakato wa mazungumzo na wafadhili"- M Pinda

    14. #33
      Idimi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2007
      Location : Ikwiriri
      Posts : 4,816
      Rep Power : 13657
      Likes Received
      934
      Likes Given
      345

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      Quote By kwempa View Post
      Oneni...nani gamba kubwa
      Huyo aliye kwenye mic
      A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man!
      [email protected]

    15. #34
      PrN-kazi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2011
      Posts : 2,246
      Rep Power : 5370
      Likes Received
      307
      Likes Given
      4

      Default Re: Lowasa na Rostam wajiandaa kumuangamiza Kikwete.

      Wakirudisha kadi za CCM-Original wataenda CUF au NCCR-mageuzi(CCM-B), hakuna jipya hapo lao moja wanatuzuga tu.

    16. #35
      samora10's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st July 2010
      Location : Kwa-Gude
      Posts : 3,271
      Rep Power : 1111
      Likes Received
      732
      Likes Given
      1170

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      chezo ndio kwanza limeanza hilo..
      ''Mipango na Mikakati imekamilika na sasa tuko kwenye mchakato wa mazungumzo na wafadhili"- M Pinda

    17. #36
      MAMENGAZI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 718
      Rep Power : 572
      Likes Received
      104
      Likes Given
      89

      Default Re: Lowasa na Rostam wajiandaa kumuangamiza Kikwete.

      Mambo baaaado!!!, fungukeni "mapacha watatu" tupate uhondo sie, tumeshategesha satelites tunasubiri kunasa mambo.
      Mhh TZ!!! toka boyz 2 men mpaka mapacha watatu!!!!

    18. #37
      MAMENGAZI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 718
      Rep Power : 572
      Likes Received
      104
      Likes Given
      89

      Default Re: Lowasa na Rostam wajiandaa kumuangamiza Kikwete.

      Quote By samora10 View Post
      ..ukimwaga ugali nami namwaga mboga, sisi ngoja tukae pembeni tuangalie chezo zima linavyochezwa

      halafu hao wabunge wa ccm,mwenyekiti, spika na wengine ni vilaza wa ajabu.. sasa kama EL alikua anajulikana hata ndani ya chama kama fisadi? walimpigiaje kura ya kuwa mwenyekiti kamati ya mambo ya nje na usalama?
      Sasa wewe umesahau mnene mwenyewe alimshika mkono akasema huyu saaaafiiiiiii!!!! leo imegeuka imekua chafuuuu!!!

    19. #38
      Muro's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th October 2010
      Posts : 168
      Rep Power : 471
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Lowassa, Rostam sasa kuwasha moto

      Huu ni kama mchezo wa kuigiza,hawa mapacha watatu ndiyo waliobeba siri zote za chama ufisadi wote waliofanya ni kwa ajili ya chama kupata fedha za kuendesha uchaguzi kuimarisha chama n.k,hawa wakiondoka tu na CCM ndiyo mwisho wake tena utakuwa mbaya sana,kwani wana watu wengi sana walio nyuma yao,na uwezo mkubwa sana wa kujieleza.siamini kabisa kuwa CCM wana nia ya dhati kuwaondoa ila wanatumia majina yao kujisafisa tu.LAKINI HAGUSWI MTU ITAKIGHARIMU CHAMA KULIKO KAWAIDA.INATISHA VIBAYA.
      Kichaa hapewi rungu

    20. #39
      Mlengo wa Kati's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 16th February 2011
      Posts : 1,382
      Rep Power : 0
      Likes Received
      197
      Likes Given
      11

      Default Re: Lowasa na Rostam wajiandaa kumuangamiza Kikwete.

      Tuwapokee tu Chadema naona wanasingiziwa! Lowassa atakua mgombea wa Urais Kupitia Chadema!

    21. #40
      Matola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2010
      Posts : 12,857
      Rep Power : 19823
      Likes Received
      5653
      Likes Given
      3875

      Default Re: Lowasa na Rostam wajiandaa kumuangamiza Kikwete.

      kwa Anaeweza kuconnect the dots ni kwamba kwenye siasa hakuna adui wa kudumu, hawa mapacha watatu wakiamuwa kwa dhati kwamba anaemwaga mboga wao watamwaga ugali, ni kwamba serikali nzima ya ccm haitobaki salama, kwanza kwenye list of shame mtuhumiwa namba moja ni JK, na kuna kashfa hiyo aliosaini mkataba wa madini akiwa kwenye wizara husika, na bomu la nyuklia ni EPA, maana EPA ndio iliyomweka madarakani JK. hii ni zaidi ya movie za hollywood. watch it very closely.
      Chadema hapa watapata mtaji mwingine wa dezo Rostam na Lowasa mwishowe wataamuwa kuwakabidhi CHADEMA document zote za wizi wa kimfumo ambao si kikwete wala nani atakaetoka salama kwenye mtego huo na katika movie hii starling ni Dr Slaa, ndio maana wanasema Dr Slaa anatetea mafisadi," kichekesho" leo hii muhasisi wa vita ya mafisadi eti anatuhumiwa kuwatetea mafisadi! hii si kweli, wanachokiogopa hapa Hawa magamba kinyesi ni Lowasa na Rostam wasije wakasurrender all criminal evidence kwa Dr Slaa. kwani huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa serikali hii kinajimu, na tutaingia kwenye uchaguzi mpya kabla hata ya 2015.
      N-handsome and wasaimon like this.
      Division four point 29 = Masters Mzumbe University. Nape Nnauye is my role model.

    Page 2 of 14 FirstFirst 123412 ... LastLast

    Similar Topics

    1. CHADEMA kuwasha moto Arusha leo 25 May, 2011
      By ngurati in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 26
      Last Post: 25th May 2011, 14:41
    2. Chadema kuwasha moto Tabora
      By Zak Malang in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 28
      Last Post: 16th April 2011, 01:37
    3. chadema kuwasha moto udsm kesho.
      By menyidyo in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 5
      Last Post: 22nd January 2011, 11:41
    4. Shivji, Ulimwengu kuwasha moto wa Katiba Dar
      By Rutashubanyuma in forum KATIBA Mpya
      Replies: 2
      Last Post: 13th January 2011, 07:55
    5. Replies: 25
      Last Post: 25th April 2008, 03:51

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...