Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: JK apata mshituko juu ya ongezeko la bei ya vyakula; aagiza serikali kuingilia kati

    Report Post
    Page 2 of 4 FirstFirst 1234 LastLast
    Results 21 to 40 of 72
    1. #1
      mchakachuaji192's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th October 2010
      Posts : 291
      Rep Power : 494
      Likes Received
      24
      Likes Given
      14

      Default JK apata mshituko juu ya ongezeko la bei ya vyakula; aagiza serikali kuingilia kati

      RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ameshtushwa kupanda kwa bei ya vyakula na gharama za maisha mijini.Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete ameagiza chakula cha akiba cha taifa kuingizwa katika masoko ya mijini hasa jiji la Dar es Salaam mara moja ili kupunguza bei ya chakula katika masoko ya miji na kupunguza makali na gharama ya maisha kwa wananchi.

      Rais Kikwete ameagiza kuwa kazi hiyo ya kuingilia soko na kupunguza bei ya chakula kwa wananchi iwe kazi ya nyongeza na ya kudumu ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na Wakala wa Akiba ya Chakula ya Taifa (NFRA).

      Amesema kuwa miji ya Tanzania ina masikini wengi na malalamiko makubwa ya masikini hao ni bei kubwa ya chakula na kuwa ni wajibu wa Serikali kuchukua hatua za makusudi kuwapunguzia wananchi gharama hizo za maisha kwa kuingiza chakula cha bei nafuu katika masoko ya mijini.

      Rais alitoa maagizo hayo wakati alipotembelea maghala ya NFRA mjini Dar es Salaam kama mwendelezo wa ziara zake na Wizara mbalimbali na taasisi za wizara hizo.

      Rais Kikwete amesema kuwa kama hatua za kuingilia soko zingechukuliwa tangu Oktoba mwaka jana wakati bei ya mahindi ilipokuwa sh. 300 kwa kilo mjini Dar es Salaam, bei hiyo isingepanda na kufikia sh. 430 kwa bei ya sasa.

      “Hii ndiyo kazi yetu kuanzia sasa yaani kuhakikisha kuwa tunaingilia soko, kuingiza chakula cha kutosha na hasa mahindi kwa sababu hiki ndicho chakula kikuu cha Watanzania na kuhakikisha kuwa tunaishusha bei hiyo ya mahindi hadi sh. 300 katika kipindi kifupi iwezekanavyo,” Rais amewaambia maofisa wa Wizara na Wakala huo.

      Amesema kuwa lazima viongozi waelewe kuwa hata mijini kuna upungufu wa chakula.

      “Tafsiri ya njaa ni kama mji haupati chakula cha kutosha basi kuna njaa, Hivyo tujipe mamlaka ya kuingiza haraka soko ili kuwalinda wananchi kwa sababu hatuwezi kuwaacha wananchi mikononi mwa wafanyabiashara binafsi wa chakula ambacho kichocheo chao kikubwa ni faida,” amesema Rais Kikwete.

      Amesema hiyo sasa ni kazi yao ya kila siku yaani kufuatilia masoko na kuhakikisha kuwa kinakuwepo chakula cha kutosha kupunguza bei.
      Amewaagiza viongozi kucheza na soko la Dar es Salaam ili kuhakikisha kuwa bei zinakwenda chini haraka iwezekanavyo.

      Amesema kuwa siyo busara kwa mahindi kubakia maghalani kusubiri njaa wakati bei za vyakula zinapanda sana. Nyie mna wajibu wa kulilisha taifa hili.

      Source: Dar leo
      My take ina maana yeye anakaa tu magogoni bila kujua changamoto zinazowakabili wananchi wake? huyu baba Rizione One day yes

    2. RukaaJuu Final

    3. #21
      Ba Martha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th August 2010
      Location : Nyarugusu
      Posts : 296
      Rep Power : 505
      Likes Received
      27
      Likes Given
      34

      Default Re: JK apata mshituko

      Hivi wachumi wanaomzunguka ****** pale magogoni wana kazi gan? Dah bora BEN kuliko huyu mtu...hata kiberiti kushusha bei hawawezi kweli?????????????

    4. #22
      mndeme's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2008
      Posts : 318
      Rep Power : 610
      Likes Received
      48
      Likes Given
      34

      Default Re: JK apata mshituko

      hana kipya kila siku yeye anashangaa tu

    5. #23
      MkamaP's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2007
      Posts : 4,675
      Rep Power : 1569
      Likes Received
      310
      Likes Given
      93

      Default Re: JK apata mshituko

      Walisimamishe bunge lisikae mda wa miaka 2 bila malipo, harafu fedha hizo ziingizwe sokoni. Hakuna wanachofanya wabunge hata bunge lisipokuwapo. Wabunge ni wezi na wizi uliopitishwa kisheria.

    6. #24
      mbogo31's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th November 2008
      Posts : 535
      Rep Power : 642
      Likes Received
      113
      Likes Given
      108

      Default Re: JK apata mshituko

      Quote By WildCard
      Hivi ule mradi wa kukataa mashangingi wa WM Pinda umeishia wapi?

      Pinda akatae mashangingi, hivi wewe unamfahamu vizuri Pinda!?, ukimuona wawezafikiri ni mtoto wa mkulima sivyo ndugu yangu.

      fanyia uchunguzi habari hii hapa chini, sijachunguza ila kama ni kweli nimesikitishwa nae sana!, tena nasisitiza kama ni kweli Waziri Mkuu hakuwatendea haki majirani zake ambao ni maskini na umeme wanausikia tu!

      Kama angekuwa mtoto wa mkulima na mpenda watz angekubali mpango wa kuwekewa umeme kwenye shamba lake kule mikwambe Kigamboni kwa milioni 300 na hivyo mradi ule ungesaidia hata wananchi wengine, ila yeye aliukataa mradi huu kuwa ni gharama na kuamua kununua generator ya milion 200 ( atatumia yeye tu, Fikiria mafuta ya huu mtambo kwa siku) pia kaangalie jinsi katapiller inavyochonga barabara ya kwenda huko shamba kila mwezi!

    7. #25
      Papizo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th February 2008
      Location : What for??
      Posts : 3,310
      Rep Power : 1236
      Likes Received
      406
      Likes Given
      2270

      Default Re: JK apata mshituko

      Kila siku huwa nasema kwamba viongozi wa hii nchi wapo madarakani kwa ajili ya maslahi yao na familia zao na sio maslahi ya wananchi ambao wanatoa kodi zao......inasikitisha sana kwa kweli kuona watu wanavujisha pesa bila mpango wowote inatia huruma sana tena sana.....yaani inaonekana sasa jinsi JK alivyokuwa na upeo mdogo wa kufikiria kwenye madaraka yake.......

    8. Miaka 50

    9. #26
      August's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2007
      Posts : 2,745
      Rep Power : 1163
      Likes Received
      251
      Likes Given
      2515

      Default Re: JK apata mshituko

      siku zote alikuwa wapi mpaka maji yamefika mdomoni ndio anaamkaa? kila miezi sita taarifa ya hali ya kiuchumi hutolewa na bank kuu, waziri wa fedha yupo nae mara kwa mara wakipata kikombe cha ghahawa, washauri wa kiuchumi anao kwenye ofisi yake binafsi etc etc lakini taaarifa hazipati za hali ilivyo

    10. #27
      August's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2007
      Posts : 2,745
      Rep Power : 1163
      Likes Received
      251
      Likes Given
      2515

      Default Re: JK apata mshituko

      mfumuko wa bei unaweza kupunguzwa kwa kuongeza vyanza vya uzalishaji wa chakula, kuwepo kwa miundo mbinu mizuri, kuongeza ushindani wa kibiashara, mamlaka zinazo simamia biashara iwe tra, trading standards , fair competition na uslama wa taifa wafanye kazi zao kwa uadilifu

    11. #28
      Ntandalilo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th March 2011
      Posts : 96
      Rep Power : 434
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: JK apata mshituko

      Nafikiri angekaa na jopo la washauri wake wa uchumi waone tatizo liko wapi kabla ya kutoa hili agizo kwa kutumia akili yake iliyo fupi kama mkia wa mbuzi akisaidiwa na Rijizi one na mkewe................!!!

    12. #29
      Mikael P Aweda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th December 2010
      Posts : 1,866
      Rep Power : 6555
      Likes Received
      2462
      Likes Given
      2266

      Default Re: JK apata mshituko

      Quote By taffu69
      Hivi huyu JK anaishi dunia gani. Kila kitu kwake ni kipya na anabaki kushangaa pasipo majibu. Hakuna tatizo hata moja ambalo ameweza kusimama na kutoa ufumbuzi wake. Anapozungumzia kupanda kwa bei ya vyakula halafu anasema fungueni maghala ambayo yamejaa mahindi pekee anamaanisha nini. Hivi anafikiri kwa kujaza mahindi kwenye soko ndiyo bei ya vyakula itapungua? Waliacha wajanja wachache wakaficha sukari kwa lengo la kupandisha bei lakini Serikali ilishindwa kufanya lolote. Sukari iliyokuwa inauzwa kati ya sh. 1400-1500 sasa inauzwa kwa sh. 1700-2000 kwa kilo. Mafuta ya kupikia lt 5 yalikuwa yanauzwa kati ya sh 14,000-16,000 kwa sasa mafuta hayo yanauzwa kati ya sh. 19,000-20,000. Kwa hali hii Mtanzania atawezaje kuyamudu maisha ilhal ongezeko hilo ni kwa kila kitu hadi nauli za daladala. Watu wakihoji Rais anasema wanataka kuangusha Serikali, anapoulizwa anabaki kushangaa na kipato cha Mtanzania kinazidi kuporomoka,

      Tufanye nini katika hali kama hii ama ndiyo kiama kwa wanyonge kinatimia?

      Mimi kweli namshangaa sana Rais wangu,
      Kwanza hizi staili za kupitia wizara aliyemshauri kampotosha Rais. Hayo anayoyashangaa hadharani alipaswa kuyajua mapema. Siyo mbele ya Kamera. Hii staili imepitwa na wakati. Kwani yeye ndiye anajua sana kuliko JK Nyerere, mwinyi na Mkapa ambao hawakufanya hivyo?
      Mfumuko wa bei haushuki kwa staili hiyo.Uchumi wa wapi huo?. Heri mimi ambaye sijawahi kumpigia kura.
      Mikael P Aweda 0784 583 330
      Elimu kwanza

    13. #30
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,091
      Rep Power : 12254
      Likes Received
      6015
      Likes Given
      6854

      Default Re: JK apata mshituko

      Quote By camaraderie
      hapana...unaposhusha kodi bei hupungua na watu hufanya manunuzi zaidi....kutokana na unafuu wa bei...watu watanunua zaidi(in terms of volumes) na wigo wa kodi kupanda....simple economics...kwa vile vat sio production cost
      kwa bongo wananufaika hawazidi laki

      teh list is the same, manji, rostam, mengi, el, mahoteli ya kitalii, kokakola, na makampuni ambayo main account ziko nje ya nchi

      hizo kodi kwenye daily life sisi wa chini mchango wetu ni chini mno, ukiondoa paye

      to me paye would have helped majority directly and indirectly
      .....Ana sifa zote, nzuri na mbaya!!!

    14. #31
      Joyum's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th October 2007
      Posts : 152
      Rep Power : 621
      Likes Received
      11
      Likes Given
      6

      Default Re: JK apata mshituko

      Makubwa haya. Kinachofuata ni uchapishaji wa hela nyingi pindi atakapopita wizara ya fedha na kuambiwa hali ya maisha ni ngumu na pato la mwanchi liko chini sana. Hahahahaaaa......i am so embarased to have a president like this!!!!?????!!!!!

    15. #32
      Mr. Zero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2007
      Posts : 4,076
      Rep Power : 1436
      Likes Received
      481
      Likes Given
      72

      Default Re: JK apata mshituko

      Sasa anapoamrisha kutoa chakula cha akiba, njaa ikija itakuwaje?? Wakati huo huo nasikia mvua mwaka huu si za kutosha hivyo mvuno hayategemewi kuwa mazuri!!
      "The Only Necessary for the Triumph of Evil is for Good Men to do Nothing" Edmund Burke (1729 - 97)

    16. #33
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,625
      Rep Power : 2894
      Likes Received
      3845
      Likes Given
      12250

      Default Re: JK apata mshituko

      Quote By MTM
      hIZI MOVES ZITALIPUNGUZIA TAIFA MAPATO
      Basi apunguze matumizi ya serikali. Be frugal.

    17. #34
      Radi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 22nd May 2010
      Posts : 94
      Rep Power : 480
      Likes Received
      15
      Likes Given
      0

      Default Re: JK apata mshituko

      Quote By WildCard
      Mchakachuaji,
      Rais wetu mgonjwa halafu unaweka heading hiyo. Umetushtua kidogo. Maagizo/ Ushauri wake huo una walakini. Haoni kutokuwa na kodi kwenye mafuta ya taa kunavyochangia uchakachuaji kwenye mafuta mengine?
      Hallo WildCard unanokosea kusema mgonjwa,sema alikuwa mgonjwa!!! lakini baada ya kupata kikombe kwa Babu ameshapona.

    18. #35
      ngwendu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2010
      Posts : 1,971
      Rep Power : 858
      Likes Received
      160
      Likes Given
      50

      Default Re: JK apata mshituko

      Quote By msafiri.razaro
      Usalama wa Taifa walipaswa kuna na wataalamu wa kuthibiti mfumuko wa bei, kwani umfumuko wa bei unachangia kukosekana na usalama. Hii ni Hatari ya kuwa na Cocktail ya waagizaji wa bidhaa Nchini (importers), wanauwezo wa kukaa meza moja na kupanga kupandisha bei za bidhaa, lakini kama kungelikuwa na kitengo cha kudhibiti mfumuko wa bei hali isingekuwa hivi ilivyo. Kulitakiwa kuwe na mfumo wa kibiashara unaothibiwa usalama wa nchi, yaani kutafuta, kununua, kuingiza bidhaa muhimu kama mafuta, nafaka, sukari n.k na kuziuza kwa bei poa ilikulazimisha kushusha bei. Kwa mfano TPDC, na Mashirika ya Umma, yakiongozwa na Usalama wa taifa kwa kificho au wazi wakatumia pesa za serikali kuagiza bidhaa na kuuza kwa bei poa wafanyabiashara nao watashusha. Sio sahihi kwa serikali kujitoa kufanyabiashara, asali zake ni hizi...
      you wrote sense mr/ms. Thank you important contribution. michango mingine ni yakivuvuvuvuvuzela tu. Hope they will lern from you. Tkanks again.
      we have to be focused!

    19. #36
      Sizinga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2007
      Location : Mars
      Posts : 3,953
      Rep Power : 1435
      Likes Received
      1515
      Likes Given
      1621

      Default Re: JK apata mshituko

      huyu nae jk akili zake fupi..yaani yeye anaona leo kupanda kwa gharama za maisha, wakati wenye akili waliliona hili mwaka mmoja tu tangu aupate urais(2006), licha ya CDM kumkumbusha lakini wapi....duh nimeamini jamaa alikuwa kwenye usingizi mzito, naona kaamshwa baada ya lile agizo la uingereza kwamba apunguze safari za nje....muheshiwa karibu nyumbani!!
      GESI KWANZA KOROSHO BAADAE!!

    20. #37
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default Re: JK apata mshituko

      hapa ndipo huwa nasema kuwa huyu jamaa sio kiongoz mzuri .......na haya mambo ya kipuuzi ndo unakuta mtu kama anthony lusekelo anapaza sauti na kusema rasi huyu ni mzuri...mara hivi mara vile....

      ajabu kweli....nilishasema we have a president who cannot think beyond the next meal.

    21. #38
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default Re: JK apata mshituko

      Quote By msafiri.razaro
      Usalama wa Taifa walipaswa kuna na wataalamu wa kuthibiti mfumuko wa bei, kwani umfumuko wa bei unachangia kukosekana na usalama. Hii ni Hatari ya kuwa na Cocktail ya waagizaji wa bidhaa Nchini (importers), wanauwezo wa kukaa meza moja na kupanga kupandisha bei za bidhaa, lakini kama kungelikuwa na kitengo cha kudhibiti mfumuko wa bei hali isingekuwa hivi ilivyo. Kulitakiwa kuwe na mfumo wa kibiashara unaothibiwa usalama wa nchi, yaani kutafuta, kununua, kuingiza bidhaa muhimu kama mafuta, nafaka, sukari n.k na kuziuza kwa bei poa ilikulazimisha kushusha bei. Kwa mfano TPDC, na Mashirika ya Umma, yakiongozwa na Usalama wa taifa kwa kificho au wazi wakatumia pesa za serikali kuagiza bidhaa na kuuza kwa bei poa wafanyabiashara nao watashusha. Sio sahihi kwa serikali kujitoa kufanyabiashara, asali zake ni hizi...
      usalama wa taifa wengi wao ni wezi wakiongozwa na kim mgaya.......hawa wakipewa rungu hilo nakwambia utakuwal nyasi kaka.....wamejikita katika biashara haram na za kipuuzi kuliko maelezo......ushauri ni kuwa tulipaswa kuwa na mamlaka ya kuthibiti mfumko wa bei. lakini ukiwapa hawa watu wa ikulu sijui usalama wa taifa....nakwambia tutakaanga hata nzi tule wacha kabisa wale hawafai kamanda


    22. #39
      Mateso's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th August 2008
      Location : Bongo
      Posts : 224
      Rep Power : 595
      Likes Received
      3
      Likes Given
      1

      Default Re: Baba Rizione apata mshituko

      Quote By housta
      hapo ndipo tunapoona upeo wake mdogo wa kufikiri.yeye anadhani tu kuingiza chakula cha akiba ndio kutapunguza mfumuko wa bei.kuna factors nyingi sana zinachangia,mfano bei ya mafuta.mfumuko wa bei unachangiwa zaidi na bei ya mafuta.akiweza kudhibiti bei ya mafuta,mfumuko na utapungua.lakini kwa sababu hana hata idea hizi,basi tujue tu inakula kwetu kwa sana tu mpaka 2015.inatia huruma kuwa na kiongozi ambaye ana mawazo duni kama huyu wa sasa.
      naona aibu kusema sana kwani jana nimelisemea sana hili. Naamini itafi8ka wakati ataagiza pesa zichapishwe nyingi ili kuondoa umaskini tanzania na kuwafurahisha wananchi wasiichukie serikali. Tufunge na kuomba wakati tunaisubiria 2015. Mungu ibariki tanzania mungu tubariki walala hoi tunaoendeshwa au kuvutwa kama mkokoteni. Wakulima wameletewa vi-tractor vinaitwa power tilla (sijui spelling zake) ambazo zinatoa moshi kwa mbele na kuingia puani kwa anayelisukuma moja kwa moja. Baada ya miaka mitano wote watakufa kwa tb. Hiyo ndiyo sera ya kilimo kwanza au kuua kwanza?

    23. #40
      Froida's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Posts : 3,754
      Rep Power : 1319
      Likes Received
      729
      Likes Given
      147

      Default Re: JK apata mshituko

      Hamna dogo anataka kuwaleteeni nafuu kelele kwa saaannnnnnnnnnnnnnnnnnnnna au hamumwamini,haya tungoje kushuka kwa hiyo bei yaa unga iwe ya kuridhisha basi

    Page 2 of 4 FirstFirst 1234 LastLast

    Similar Topics

    1. Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe
      By tibwilitibwili in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 211
      Last Post: 27th October 2012, 18:11
    2. Chadema:ni sahihi serikali kuingilia uhuru wa mahakama??
      By kulwa12 in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 4
      Last Post: 7th November 2011, 21:58
    3. Replies: 9
      Last Post: 7th November 2011, 11:58
    4. Tetesi: Rais aagiza Lema aachiwe kwa dhamana ya serikali
      By Kanigini in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 68
      Last Post: 2nd November 2011, 14:24
    5. Serikali yaombwa kuingilia mgogoro Bulyanhulu
      By BAK in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 1
      Last Post: 2nd November 2007, 15:05

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...