Source TBC1 news
"Ticha" Makamba amesema aliosema kuhusu Sumaye ni maoni yake.
Kuhusu mitandao na matumizi ya hela kwa ajili ya urais- CCM haina habari
Source TBC1 news
"Ticha" Makamba amesema aliosema kuhusu Sumaye ni maoni yake.
Kuhusu mitandao na matumizi ya hela kwa ajili ya urais- CCM haina habari
hakuna kazi ya kufanya maana ukuta umeamua kudondoka wenyewe kwa nyimbo zetu na zumari zuri tulilompigia muumba. Kaa tu kunja nne vita si vyetu acha wamalizane kwa mapanga yao kwanza wakisha jitumbukiza kwenye mashimo waliyojichimbia wakidhani sisi watanzania tungetumbukia; basi nyanyuka taratibu vyote walivyovikusanya for years tutatakiwa kuvibeba na kugawana kisha tuende kivulini tuanze kula taratibu kwa raha zetu.
FREDDY SUMAYE HEBU WAPELEKE NA HAWA HUKO ULIKOSOMA MAJUZI NAO WAPATE KUBADILIKA NDIPO URUDI TUKAJADILI WEWE KUTAMANI KUWA RAIS WANGU
Kwa watu makini, hata bila kumona uso kwa uso huyu aliyekua Fundi Mitrekta Freddy Sumaye aliyeishi siasa zetu chafu hapo kipindi cha nyuma na ukachukua wala dakika chache kumlinganisha na Mheshimiwa Fredrick Sumaye tuliemsoma moja kwa moja akiripotiwa na Invisible kwenye Press Conference aliyojiitishia pale Courtyard Hotel basi bila shaka utagundua kwamba kweli darasa bila DESA imetusaidia kwa kiasi kikubwa kupangusa uzuri kopo ambalo sie wengine tulishalitupa kwenye jalala la kule Vigunguti na sasa lafaa kuchotea tena maji ya kunywa kumpelekea mgeni rasmi (wapigakura) sebuleni!!
Kwa msingu huo nilitamani hata naye huyu Fisadi wa Kimaasai tukimpeleka tu shule huko ma-Ughaibuni mbona hizi siasa za fitina fitina na kutembeza senti tano mitaani ataziacha tu!!
Ila hili lingine ambalo akimuingiza mtu kwenye BLACK BOOK yake basi mpaki kifo ndicho kije kuwapatanisha nasema hata tungempeleka shule za kule nchi ya ya Mzee Shaaban Robert (Kusadikika) wala huo ukoko wa sias za Chuki, Visasi, Vinyongo, Umimi, Upwani, na mambo mengine kama hayo kamwe hayawezi kumtoka.
Shule hutakasha bwana usiombe; hebu muone yule Fundi Mekanika wa mitrekta aliyesome SUA, Freddy Sumaye, leo hii MBA ya ukweli ilivyompiga jiki kichwa na kuondoa yale mi-oili chafu yote ya mitrekta mbovu; hata anapozungumza siku hizi mtu unaweza ukapata cha kwenda kumsimulia mtu wa pili na wala hana tena ile LUGHA YA MAFUNDI tuliokua tumzoea nayo huko nyuma.
Mhe Sumaye, japo kwenye mahesabu yetu ya kuwa rais wa nchi hii na wewe wala haumo lakini hebu chonde mfanyie mpango huyu ndugu Eddu wa Monduli naye aende huko ulikoenda kula Kitabu walau akabadilike. Maana, kwa kusema ukweli, mtu ukimtazama kwa karibu Ndugu Lowasa, Mrema Augustino, Rostam Aziz, Seif Shariff Hamad, Nchimbi, Malisa, Ridhiwani Kikwete, Makamba Junior, Hussein Mwinyi, Julius Mtatiro, Zitto Kabwe ... na wengine wengi tu hapa nchini na kweli kabisa utakuta ni watu wenye uwezo mkubwa sana tu ambao taifa letu limebahatika kuwapata isipokua tu wanakosa sana kati ya mambo haya matatu:
(1) PERSONAL ETHICS AND LEADERSHIP INTEGRITY
(2) SOUND EDUCATION BACKGROUND, VISIONARY & READINESS TO LEARN AT ALL TIMES, and
(3) EXPOSURE FAR BEYOND THEIR OWN NEIGHBOURHOODS
Hivyo nasema hapa kwamba laiti viongozi wetu wangelikua ni watu wa kukosolewa wakakosoleka, wasikivu na wenye kujitathmini wenye tu japo hata mara moja katika ngazi ya nafsi yake mwenyewe, basi ni kwamba mtu utagundua kuna mikasoro ya kufanyia kazi. Lakini pale ambapo mwanasiasa ni ni Mbumbumbu (hata kama kapata vijidarasa vichache tena kwa KUDESA TU OPEN UNIVERSITY pale Kinondoni) na kwamba hana habari kama kweli yeye ni mbumbumbu, na kwamba bado yuko tayari hata kutafuta umbumbumbu wake huo kwa kutumia VIJISENTI MITAANI ili umbumbumbu wake huo uonekane kwamba ina mng'ao sawa tu na Almasi zetu toka kule Mwadui, basi hadi hapo ndipo taifa zima mjue kwamba tunalo MZIGO MKUBWA SANA TENA GUNIA LA MISUMARI YA MOTO kuubeba wakati wote mgongoni.
Ningeendelea sana kuomba Shule alikoenda yule Fundi Sumaye na lugha / fikra za kwenye mi-gereji tu kichwani hadi leo hii karudi nyumbali mtu ambaye si lazima akutangazie kama kaongeza darasa bali kwa nidhamu tu ya lugha yake, direction thabiti kwenye maelezo yake (japo mie sijayanunua bado) na kwenda kwa stepu bila uswahili na fitina mingi ni dalili tosha kwamba kweli mwenzetu huyu kapata shule BILA KU-DESA na kwamba shule hiyo hakika imemkomboa hivi sasa!!
Jamani kiongozi wa ngazi yoyote akiwa na walau sifa hizo tatu hapo juu basi kazi huwa ni nyepesi mno lakini the vice versa ni kiama. Ndio maana wataalam wetu wote wanaofanya kazi chini ya madiwani katika jiji, manispaa na halmashauri mbalimbali nchini KIKUKWELI NAWAHESHIMU MNO maana mazingira yao ya kazi ni ngumu kupita kiasi kwa sababu mabosi wao ambao ni madiwani waliowengi ni watu ambao ni MBUMBUMBUMBU WA KUDUMU KWA KUJICHAGULIA!!!
Na wala usiniulize kwa nini Mambumbumbu wa jiji la Dar es Salaam nao waliona kero sana baada ya CCM nacho kuligundua tatizo hili ninalolizungumzia na kuamua kuwaletea diwani PhD Masaburi na watu tukasikia in a chorus mambumbumbu wa jiji wakigoma kabisa kumkaribisha huyu mtu aliyeona mwanga, kusafiri sana ila kama anayo personal ethics na leadership integrity bado nasubiri kwa hamu kuona PRACTICAL RESULTS jijini na wala si mi-ripoti mizuri mizuri na takwimu yasio na maana yalioandaliwa kwa utaalam mkuba.
Mhe Sumaye, wahimize wanasiasa waende shule zisizoendekeza KUDESA, WACHANJE MBUGA MBALI NA VIJIJI WALIKOZALIWA ILI WAJUE KWAMBA KUMBE KWINGINEKO KUNA MPISHI MZURI ZAIDI AMBAYE WAZAZI WETU WANGEENDA NAO KUJIFUNZA. Chonde wasaidie maana katika hizo points tatu hapo juu viongozi wetu wamegawanyika katika mix ambazo ni so interesting.
Kwa mfano, na ninasema kwa nia njema kabisa, Zitto Kabwe anayo good education background bila DESA ila hana personal ethics wala leadership integrity.
Mheshimiwa Lowassa anayo very UNIQUE IN-BORN TALENT of both Social and Business Enterpreneurial Mind lakini hajaruhusu ikapigwa msasa hii talanta imekua naexcesses nyingi mno katika jamii. Jambo ambalo linatushawishi ku-question his genuine education background so far, na his personal ethics and leadership integrity is REALY WANTING.
Mheshimiwa Mrema ni mtu mmoja ambaye otherwise ni LULU KWA TAIFA LETU. Watu wa aina yake huwa hawazaliwi wengi sana ndani ya kipindi kifupi. Watu wa aina yake ambao nao ni lulu ni akina Mwalimu Nyerere, Dr Ali Mohamed Shein, Salim Ahmed Salim, Everist Kaigaruki, Magufuli, Moringe Sokoine, Mama Nkya ... lakini a mark of an UNTRACEABLE SOUND EDUCATION background inamuangusha sana ila Personal Ethics ni Average na Leadership Integrity imesimama mpake arudi kwa muumba wake.
Julius Mtatiro anayo personal ethics and leadership integrity ya hali ya juu (hata kama bado hajajaliwa fedha wala haonyesha uharaka wa kuzikimbilia), huyu bwana kwa UDSM pale wenzake waliosoma naye wanamheshimu kitaaluma ila dosari yake kubwa ni kwamba hajui lolote zaidi ya mipaka ya Tanzania basi!!
Mhe Sumaye wasaidie wenzio waenda NDANI YA DARASA ulikoenda wewe (japo swala la wewe kuwa rais wangu tutaujadili siku nyingine) ili wakome kuwa miziko yetu kifikra na matendo yao!!!
Originally Posted by Ntemi Kazwile
Dah kumbe shule nzuri bwana, tangu amalize MBA yake siku hizi Sumaye anaongea point, nimeshitushwa kidogo maana nilizoea kumsikia akitoa point zilizokuwa tata sana enzi za uwaziri mkuu wake.
Hongera Sumaye
Nilizidi kumtoa makamba maanani pale alipomjibu bhanji kihuni wakati hoja ilitolewa kimantiki
Mwenzenu niko nafanya Ibaada ya shukrani maana maombi yanajibiwa live never expected this; is the testimony in my life the reason I am to worship the Lordship of Jesus Christ for ever and ever! Gosh am very much excited!
mimi sikumwelewa shigela hata kidogo,kwanza ameongea kwa kupanic ajabu,utafikiri kalazimishwa!,kama hao ndiyo viongozi wa umoja wa vijana basi ni makopo kabisa,ningependa kujua elimu yake kwani maongezi yake hayana tofauti na makamba!,yaani anaongea kwa kuropoka!naomba kujua hivi ni makosa kukopa?ni dhambi kuwa na mashamba?,kwa kumbukumbu zangu sumaye aliwai kutuhumiwa akaenda mahakamani mwenyewe kufungua kesi na alishinda,naomba leo lowasa na swahiba wake rostam waende mahakamani wakajisafishe!!!!!!!!!!!!
Ninachoweza kusema ni kuwa vita vya panzi ni furaha ya kunguru. Hapa ndipo washindani na wapenzi wa kweli wa nchi yetu wanatakiwa kuchanja mbuga na kuwasambaratisha maadui wa nchi yetu na kutupatia ukombozi wa pili. Hivyo hakuna sababu ya kuwaingilia CCM kwani wakiparurana na kupofushana ndiyo furaha ya Mama Tanzania. Wakati wa CCM kutawala umekwisha kwani wao ni wajuzi na jana si wa leo wala kesho, kesho-kutwa ama mtondogoo.i
Hivi unategemea kuna namna ya kuwatenganisha CCM na ufisadi hasa hii CCM ya ******? Wao wenyewe wanasema CCM ina wenyewe nao ni mafisadi. Hii ina maana wanaonufaika na CCM ni mafisadi na familia zao, lakini wanachama wengi ni vipaza sauti tu na kazi yao ni kuvaa manguo ya kijani na kutumiwa tu! CCM wakubali tu kwamba mchawi wao mkubwa ni ufisadi wao!
Waacheni wafu wawazike wafu wao....!
CCM Kushnehi!
'' Mtu ni Utu sio Kitu''
Yaani huu mchezo unaochezwa na CCM wao kwa wao ni sawa na ile movie ya akina Kanumba! Safi sana tunataka sasa tushuhudie EKTA akifa kabla ya movie kuisha!CCM!
'' Mtu ni Utu sio Kitu''
TANESCO hawashindwi kununua mitambo yao Kama kweli Dowans siyo ya JK ataifishe mitambo hiyo kwa sheria ya uhujumu awafilisi RA, EL vile vile awachukulie hatua waliokwapua fedha BOT
Ni kama vile UVCCM na Makamba wamoja! au Wana-JF mnaonaje?
Siku tutakapoacha kuwa mashabiki wa wanasiasa ndio siku hatua ya kwanza ya kujikomboa itakapo anza
Kabla hii panic haijaisha mwezi wa nne phase nyingine ya maandamano ya CDM ikianza itasabisha watu wavue nguo hadharani nakukimbiana mchana kweupe. Match my beloved CHADEMA match never miss this golden opportunity na sisi tulio huku porini tuje out kusherehekea ushindi baada ya miaka mingi ya kusota na baridi na wanyama wa kali wa porini!
Follow Us Here