JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Kardinali Pengo: Watawala siyo miungu; Maandamano hayana tatizo so far..

  Report Post
  Page 4 of 7 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
  Results 61 to 80 of 134
  1. Shinto's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th December 2010
   Posts : 1,782
   Rep Power : 810
   Likes Received
   80
   Likes Given
   10

   Default Kardinali Pengo: Watawala siyo miungu; Maandamano hayana tatizo so far..

   ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema haoni tatizo katika maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

   Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi jana, Kardinali Pengo alisema badala yake Serikali: “Ichimbue mizizi ya matatizo badala ya kukimbilia kukata matawi.”

   Kauli ya Pengo ni kama inaunga mkono matamshi yaliyotolewa juzi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliishauri Serikali kutotumia vyombo vya dola dhidi ya Chadema na badala yake ijirekebishe kwa kuwa na wepesi wa kukabiliana na matatizo yaliyopo nchini.

   Kadhalika, kauli hiyo ya Pengo imekuja wakati Serikali ikiendelea kulaani maandamano hayo ya Chadema na kutaka yasitishwe kwa madai kuwa yanaweza kuleta machafuko nchini.

   Katika mahojiano hayo Kardinali Pengo alisema haoni kama Chadema kinafanya vurugu katika maandamano yake kama baadhi ya watu wanavyodai: “Sioni ‘point’ ya kusema maandamano ya Chadema yanaweza kusababisha vurugu,” alisema Kardinali Pengo na kuongeza:

   Alisema ikiwa kuna tatizo katika maandamano hayo kama inavyoelezwa na serikali, ni bora hali hiyo ikafafanuliwa mapema na kukiambia Chadema kisitishe kuandamana.

   “Lakini serikali isichukulie ‘comment’ (maoni) ya mtu mmoja mmoja na kusema kwamba Chadema inasababisha vurugu, bila kusikiliza na kuchambua kwa undani,” alisema.

   Aliongeza kuwa endapo serikali imechunguza na kubaini ukweli kwamba maandamano hayo yanaweza kuleta vurugu za kisiasa, basi iyasitishe badala ya kutoa kauli tu kwamba yanahatarisha amani.

   Pengo alisema huenda uamuzi wa Chadema kufanya maandamano unatokana na madai yao dhidi ya kupanda kwa gharama za maisha, umeme na malipo kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans kwamba hayakusikilizwa.

   Alisema Serikali haitakiwi kuyafumbia macho matatizo ya kisiasa nchini badala yake itafute kiini chake na namna ya kuyatatua.

   “Serikali ianze kuchimbua mizizi ya matatizo ya kisiasa yaliyopo ndani ya Taifa, badala ya kukimbilia kukata matawi. Kwa sababu kuanza kukata matawi ni kuzidi kuipeleka nchi katika machafuko ya kisisasa na matokeo yake ni kuleta madhara kwa wananchi,” alisema.

   Askofu huyo mkuu pia alisisitiza kuwa Serikali inatakiwa kuhakikisha inafuatilia matatizo yanayowakabili wananchi kwa sasa, ambayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka ili watu wasipate fursa ya kudai mambo hayo kwa maandamano.

   Kwa mujibu wa Kardinali Pengo, Serikali pia haipaswi kutoa vipaumbele kwenye masuala ya siasa na kusahau matatizo ya wananchi kwani hilo linaweza kuwa kiini cha vurugu... "Serikali iguswe kama ilivyoguswa na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotoka mwaka huu."

   Baadaye akihubiri katika Misa ya Jumatano ya Majivu kuashiria kuanza kwa siku 40 za Mfungo wa Kwaresma ambao Wakristo hukumbuka mateso ya Bwana wao, Yesu Kristo kabla ya Pasaka zaidi ya miaka 2000 iliyopita, Kardinali Pengo alikemea tabia ya viongozi kung'ang'ania madaraka na kudhani kuwa bila wao nchi zao haziwezi kuwepo au kusonga mbele.

   "Yapo matatizo katika viongozi wanaong'ang'ania madaraka wakiwa tayari hata kumwaga damu ya wengine ili wao wabaki madarakani. Hawa ni viongozi wanaofikiri uwezo unaweza kuwa ndani yao, wanajifanya wao Mungu," alisema Pengo.

   Alisema viongozi hao wanatazama fadhila za kibinadamu wakiacha upungufu wao na kudhani kuwa wasipokuwa na madaraka basi nchi zao hazitakuwepo jambo ambalo si sahihi na halifai katika jamii.

   "Viongozi hao wanajifanya wao ndiyo miungu, wanatazama fadhila za kibinadamu, wakiacha mapungufu yao. Hicho ni kiburi, wakumbuke kuwa Mungu aliwaumba kwa vumbi na watarudi kuwa vumbi, sasa kwa nini mnakuwa na kiburi?," Alihoji Kardinali Pengo na kuongeza;

   "Mungu aliwaumba kwa vumbi kwa nini wawe na kiburi? Unadhani ukifa na nchi itakufa, kwani kabla yako nchi haikuwepo? Kumbuka wewe ni uvumbi na utarudi mavumbini."

   Alisema thamani ya mtu haitokani na anavyojiona, bali nguvu ya Mungu akiwakumbusha Wakristo kutubu na kumrudia Mungu katika kipindi hiki cha Kwaresma.

   Wakati huohuo; Festo Polea anaripoti kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambao wapo katika taasisi isiyo ya kiserikali ya Truya wamesema ili kuondokana na machafuko yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, viongozi wanaokiuka matakwa ya uongozi, uvunjaji wa Katiba na sheria za nchi wanapaswa kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

   Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Helman Sheluleta alisema Ibara ya 18 ya Katiba ya nchi inatambua haki ya mtu kutoa maoni, kusikilizwa na kuandamana kwa amani na kwa mujibu wa sheria lakini sheria inapovunjwa kwa ajili ya kupata haki ndiko kuhatarisha amani ya nchi.

   Source: Mwananchi March 10, 2011
   ============================== ============================== =====
   Hatukutarajii uone tatizo ndani ya Chadema!
   Ila unadhihirisha kile ambacho wengi humu wanakificha kwamba Mkulu unashabikia na ulishawishi watu washabikie Chama chetu kileeee!

  2. Mungi's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 23rd September 2010
   Location : JF
   Posts : 16,733
   Rep Power : 201413717
   Likes Received
   9023
   Likes Given
   5180

   Default Re: Kardinali Pengo: Watawala siyo miungu; Maandamano hayana tatizo so far..

   Kuna watu humu wanaupinga ukweli badala yake wanageuza maneno eti udini!

   Hakuna udini hapa, very credible point! maisha yamepanda kupindukia, thamani ya hela imeshuka ajabu, ufisadi umekithiri yote haya ni ya ukweli kabisa! big up Pengo!
   God will not permit any troubles to come upon us, unless He has a specific plan by which great blessing can come out of the difficulty..

  3. Maishamapya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd November 2010
   Location : Dar, Tanzania
   Posts : 1,279
   Rep Power : 820
   Likes Received
   373
   Likes Given
   339

   Default Re: Kardinali Pengo: Watawala siyo miungu; Maandamano hayana tatizo so far..

   Quote By zubeda View Post
   Nchi hii imejiwekea utaratibu usio rasmi wa kubadilisha Rais kutokana na Dini mbili kubwa Uislam na Ukristo! utaratibu huu aliuasisi Nyerere ndio maana baada yake aliingia Mwinyi, Mkapa na sasa Khalfani Mrisho!!! sasa mwaka 2005 CCM hawakuwa na hiyari iliwalazimu kumpitisha JK kwa sababu 3:
   1) Alijijengea Mtandao mkubwa ndani na hata nje ya CCM zaidi Umoja wa Vijana wa CCM ambao una ushawishi mkubwa ktk CCM!
   2) Alikusanya Fedha nyingi zaidi za kampeni kuliko mgombea wowote!
   3) Dini yake ya Uislamu kwani ilikuwa ni zamu ya Waislamu baada ya Mkristo Mkapa ingawaje JK hakuwa RELIGIOUS kama alivyokuwa Mkapa ambae alikuwa mtiifu kwa Kanisa lake kinyume na JK aliyekuwa zaidi handsome boy, chekbob, Kanali mstaafu na Chipukizi wa mafundisho ya Uliberali!! na wala hakuwa akionekana sana Misikitini kama alivyokuwa Sheikh Ali Hassan Mwinyi!!!
   Hoja hii kwenye red ni ya udini pia. Kwa kusema nchi imejiwekea utaratibu usio rasmi ni kuanza kuwaangalia watu kutokana na dini zao. Sidhani hiyo ni sawa. Kigezo kikubwa ni uwezo wa mtu, dhamira thabiti ya kutatua matatizo ya watz inayoweza kuthibitishwa kwa track record yake, na ufahamu wake juu ya mambo ya kimataifa (globalization) na jinsi anavyoweza kuyaoanisha na hali halisi nchini kwa manufaa ya watz. Hii haitajalisha ametoka katika hizo dini mbili kubwa kama ulivyozitaja au la. Tukijiangalia ktk mtazamo huo tutakuwa tunajali maslahi ya nchi zaidi kuliko maslahi ya kundi au vikundi fulani vya watu.
   Ninajua hapo mwanzo tulijiwekea utaratibu kuwa rais akitoka sehemu moja ya muungano basi makamu atoke upande mwingine. Utaratibu huo ulikuwa unafaa kwa wakati huo. Watawala wetu wenyewe wameutupilia mbali mfumo huo kwa kuona hautafaa katika mazingira ya vyama vingi na badala yake wakaangalia uwezo wa mtu mmoja mmoja bila kujali anatoka upande uleule aliotoka mtangulizi wake.

  4. The Finest's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th July 2010
   Posts : 21,719
   Rep Power : 6262
   Likes Received
   5950
   Likes Given
   5020

   Default Re: Kardinali Pengo: Watawala siyo miungu; Maandamano hayana tatizo so far..

   Quote By Pepombili View Post
   Padri SLAA na Padri Pengo wote lao moja wasitusitushughulishe hapawote wanafiki hawana lao wameanzisha chama wakadhani watashinda maana padri slaa alikuwa ndio chaguo lao .sasa kaanguka ndio wameanzisha USAVIMBI hata kumkemea alipoiba mke wa mtu walishindwa viongozi gani wa kiroho wanatetea ZINAA
   Pepombili unahitaji utolewe hayo mapepo mawili uliyonayo
   "What is legal, but not logical, logical, but not legal, and neither logical, nor legal?"

  5. Mujumba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th January 2011
   Location : Soweto
   Posts : 856
   Rep Power : 725
   Likes Received
   290
   Likes Given
   117

   Default Pengo: Sioni tatizo la maandamano ya CHADEMA   Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Kadinali Polycarp Pengo (kushoto), akimpaka majivu mmoja wa waamini wa kanisa hilo wakati wa misa ya Jumatano ya majivu kwenye kanisa Kuu la Mt Joseph jana. Picha na Salhim Shao

   ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema haoni tatizo katika maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

   Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi jana, Kardinali Pengo alisema badala yake Serikali: “Ichimbue mizizi ya matatizo badala ya kukimbilia kukata matawi.”

   Kauli ya Pengo ni kama inaunga mkono matamshi yaliyotolewa juzi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliishauri Serikali kutotumia vyombo vya dola dhidi ya Chadema na badala yake ijirekebishe kwa kuwa na wepesi wa kukabiliana na matatizo yaliyopo nchini.

   Kadhalika, kauli hiyo ya Pengo imekuja wakati Serikali ikiendelea kulaani maandamano hayo ya Chadema na kutaka yasitishwe kwa madai kuwa yanaweza kuleta machafuko nchini.

   Katika mahojiano hayo Kardinali Pengo alisema haoni kama Chadema kinafanya vurugu katika maandamano yake kama baadhi ya watu wanavyodai: “Sioni ‘point’ ya kusema maandamano ya Chadema yanaweza kusababisha vurugu,” alisema Kardinali Pengo na kuongeza:

   Alisema ikiwa kuna tatizo katika maandamano hayo kama inavyoelezwa na serikali, ni bora hali hiyo ikafafanuliwa mapema na kukiambia Chadema kisitishe kuandamana.

   “Lakini serikali isichukulie ‘comment’ (maoni) ya mtu mmoja mmoja na kusema kwamba Chadema inasababisha vurugu, bila kusikiliza na kuchambua kwa undani,” alisema.

   Aliongeza kuwa endapo serikali imechunguza na kubaini ukweli kwamba maandamano hayo yanaweza kuleta vurugu za kisiasa, basi iyasitishe badala ya kutoa kauli tu kwamba yanahatarisha amani.

   Pengo alisema huenda uamuzi wa Chadema kufanya maandamano unatokana na madai yao dhidi ya kupanda kwa gharama za maisha, umeme na malipo kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans kwamba hayakusikilizwa.

   Alisema Serikali haitakiwi kuyafumbia macho matatizo ya kisiasa nchini badala yake itafute kiini chake na namna ya kuyatatua.

   “Serikali ianze kuchimbua mizizi ya matatizo ya kisiasa yaliyopo ndani ya Taifa, badala ya kukimbilia kukata matawi. Kwa sababu kuanza kukata matawi ni kuzidi kuipeleka nchi katika machafuko ya kisisasa na matokeo yake ni kuleta madhara kwa wananchi,” alisema.

   Askofu huyo mkuu pia alisisitiza kuwa Serikali inatakiwa kuhakikisha inafuatilia matatizo yanayowakabili wananchi kwa sasa, ambayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka ili watu wasipate fursa ya kudai mambo hayo kwa maandamano.

   Kwa mujibu wa Kardinali Pengo, Serikali pia haipaswi kutoa vipaumbele kwenye masuala ya siasa na kusahau matatizo ya wananchi kwani hilo linaweza kuwa kiini cha vurugu... "Serikali iguswe kama ilivyoguswa na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotoka mwaka huu."

   Baadaye akihubiri katika Misa ya Jumatano ya Majivu kuashiria kuanza kwa siku 40 za Mfungo wa Kwaresma ambao Wakristo hukumbuka mateso ya Bwana wao, Yesu Kristo kabla ya Pasaka zaidi ya miaka 2000 iliyopita, Kardinali Pengo alikemea tabia ya viongozi kung'ang'ania madaraka na kudhani kuwa bila wao nchi zao haziwezi kuwepo au kusonga mbele.

   "Yapo matatizo katika viongozi wanaong'ang'ania madaraka wakiwa tayari hata kumwaga damu ya wengine ili wao wabaki madarakani. Hawa ni viongozi wanaofikiri uwezo unaweza kuwa ndani yao, wanajifanya wao Mungu," alisema Pengo.

   Alisema viongozi hao wanatazama fadhila za kibinadamu wakiacha upungufu wao na kudhani kuwa wasipokuwa na madaraka basi nchi zao hazitakuwepo jambo ambalo si sahihi na halifai katika jamii.

   "Viongozi hao wanajifanya wao ndiyo miungu, wanatazama fadhila za kibinadamu, wakiacha mapungufu yao. Hicho ni kiburi, wakumbuke kuwa Mungu aliwaumba kwa vumbi na watarudi kuwa vumbi, sasa kwa nini mnakuwa na kiburi?," Alihoji Kardinali Pengo na kuongeza;

   "Mungu aliwaumba kwa vumbi kwa nini wawe na kiburi? Unadhani ukifa na nchi itakufa, kwani kabla yako nchi haikuwepo? Kumbuka wewe ni uvumbi na utarudi mavumbini."

   Alisema thamani ya mtu haitokani na anavyojiona, bali nguvu ya Mungu akiwakumbusha Wakristo kutubu na kumrudia Mungu katika kipindi hiki cha Kwaresma.
   Last edited by Invisible; 12th March 2011 at 09:33.

  6. Smartboy's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th November 2010
   Posts : 1,109
   Rep Power : 789
   Likes Received
   121
   Likes Given
   4

   Default Re: sioni tatizo la maandamano ya chadema-kardinali Pengo

   Duh! Ujumbe mzito, ila serikali itasema anaingilia siasa.

  7. Mujumba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th January 2011
   Location : Soweto
   Posts : 856
   Rep Power : 725
   Likes Received
   290
   Likes Given
   117

   Default Re: sioni tatizo la maandamano ya chadema-kardinali Pengo

   Quote By Smartboy View Post
   Duh! Ujumbe mzito, ila serikali itasema anaingilia siasa.
   umeona eeh?

  8. Juaangavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd November 2009
   Posts : 867
   Rep Power : 791
   Likes Received
   88
   Likes Given
   22

   Default Re: Pengo: Sioni tatizo la maandamano ya CHADEMA

   Ninatamani kam Mungu mwenye wivu angeshusha rungu lake ili atuondelee hawa wtz wenzentu wanaojifanya miungu watu. Ni amri ya kutosema uongo, lakini wao wameng'ang'ana kudanganya watu bila hata ya kutoa udhibitisho. Tumeshuhudia maandamano ya kanda ya ziwa yakiwa hayana Zecomedy, wananchi wakijitokeza kwa hiari yao na kupokea elimu ya urai kisha wakirejea majumbani mwao salama. Ushahidi wa uvunjifu wa amani inayopigiwa kelele ni nani aliyenao. Na ni kwa nini asiutoe adharani.

   Eeh! Mungu ndani ya taifa hili ambalo umetujalia utajiri wa kila namna, wabaka uchumi wamejigeuza miungu wanataka kutulazimisha kuwaabudu, tafadhali shuka utung'olee hivi visiki

  9. kilimasera's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd December 2009
   Posts : 3,073
   Rep Power : 1236
   Likes Received
   212
   Likes Given
   261

   Default Re: sioni tatizo la maandamano ya chadema-kardinali Pengo

   serikali ya kihuni hii ndio maana watasema hivyo ila ni wajibu wake Pengo kuwaambia wakristo hivyo
   Quote By Smartboy View Post
   Duh! Ujumbe mzito, ila serikali itasema anaingilia siasa.

  10. bulunga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th October 2010
   Posts : 257
   Rep Power : 618
   Likes Received
   25
   Likes Given
   29

   Default Re: sioni tatizo la maandamano ya chadema-kardinali Pengo

   Quote By Smartboy View Post
   Duh! Ujumbe mzito, ila serikali itasema anaingilia siasa.
   Ni kweli kabisa, lakini ukiangalia kwa undani utaona kuwa waziri Nchimbi alipokuwa Songea kwenye sherehe za wanawake wa Kanisa Katoliki alitumia fursa hiyo akiwa mgeni mualikwa kutaka kushawishi umma kuwa maandamano ya chadema yalikuwa ya kutaka kuleta vurugu nchini , TBC kama kwaida na propaganda za chama tawala walitoa airtime kubwa for no reason , nafikiri Pengo ameliona hilo na hii ni kama jibu kwa CCM na kanisa lisitumiwe na watu type ya Nchimbi

  11. Gerald's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th November 2007
   Posts : 272
   Rep Power : 774
   Likes Received
   39
   Likes Given
   32

   Default Re: Pengo: Sioni tatizo la maandamano ya CHADEMA

   Quote By Kashaga View Post

   Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Kadinali Polycarp Pengo (kushoto), akimpaka majivu mmoja wa waamini wa kanisa hilo wakati wa misa ya Jumatano ya majivu kwenye kanisa Kuu la Mt Joseph jana. Picha na Salhim Shao

   ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema haoni tatizo katika maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

   Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi jana, Kardinali Pengo alisema badala yake Serikali: “Ichimbue mizizi ya matatizo badala ya kukimbilia kukata matawi.”

   Kauli ya Pengo ni kama inaunga mkono matamshi yaliyotolewa juzi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliishauri Serikali kutotumia vyombo vya dola dhidi ya Chadema na badala yake ijirekebishe kwa kuwa na wepesi wa kukabiliana na matatizo yaliyopo nchini.

   Kadhalika, kauli hiyo ya Pengo imekuja wakati Serikali ikiendelea kulaani maandamano hayo ya Chadema na kutaka yasitishwe kwa madai kuwa yanaweza kuleta machafuko nchini.

   Katika mahojiano hayo Kardinali Pengo alisema haoni kama Chadema kinafanya vurugu katika maandamano yake kama baadhi ya watu wanavyodai: “Sioni ‘point’ ya kusema maandamano ya Chadema yanaweza kusababisha vurugu,” alisema Kardinali Pengo na kuongeza:

   Alisema ikiwa kuna tatizo katika maandamano hayo kama inavyoelezwa na serikali, ni bora hali hiyo ikafafanuliwa mapema na kukiambia Chadema kisitishe kuandamana.

   “Lakini serikali isichukulie ‘comment’ (maoni) ya mtu mmoja mmoja na kusema kwamba Chadema inasababisha vurugu, bila kusikiliza na kuchambua kwa undani,” alisema.

   Aliongeza kuwa endapo serikali imechunguza na kubaini ukweli kwamba maandamano hayo yanaweza kuleta vurugu za kisiasa, basi iyasitishe badala ya kutoa kauli tu kwamba yanahatarisha amani.

   Pengo alisema huenda uamuzi wa Chadema kufanya maandamano unatokana na madai yao dhidi ya kupanda kwa gharama za maisha, umeme na malipo kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans kwamba hayakusikilizwa.

   Alisema Serikali haitakiwi kuyafumbia macho matatizo ya kisiasa nchini badala yake itafute kiini chake na namna ya kuyatatua.

   “Serikali ianze kuchimbua mizizi ya matatizo ya kisiasa yaliyopo ndani ya Taifa, badala ya kukimbilia kukata matawi. Kwa sababu kuanza kukata matawi ni kuzidi kuipeleka nchi katika machafuko ya kisisasa na matokeo yake ni kuleta madhara kwa wananchi,” alisema.

   Askofu huyo mkuu pia alisisitiza kuwa Serikali inatakiwa kuhakikisha inafuatilia matatizo yanayowakabili wananchi kwa sasa, ambayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka ili watu wasipate fursa ya kudai mambo hayo kwa maandamano.

   Kwa mujibu wa Kardinali Pengo, Serikali pia haipaswi kutoa vipaumbele kwenye masuala ya siasa na kusahau matatizo ya wananchi kwani hilo linaweza kuwa kiini cha vurugu... "Serikali iguswe kama ilivyoguswa na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotoka mwaka huu."

   Baadaye akihubiri katika Misa ya Jumatano ya Majivu kuashiria kuanza kwa siku 40 za Mfungo wa Kwaresma ambao Wakristo hukumbuka mateso ya Bwana wao, Yesu Kristo kabla ya Pasaka zaidi ya miaka 2000 iliyopita, Kardinali Pengo alikemea tabia ya viongozi kung'ang'ania madaraka na kudhani kuwa bila wao nchi zao haziwezi kuwepo au kusonga mbele.

   "Yapo matatizo katika viongozi wanaong'ang'ania madaraka wakiwa tayari hata kumwaga damu ya wengine ili wao wabaki madarakani. Hawa ni viongozi wanaofikiri uwezo unaweza kuwa ndani yao, wanajifanya wao Mungu," alisema Pengo.

   Alisema viongozi hao wanatazama fadhila za kibinadamu wakiacha upungufu wao na kudhani kuwa wasipokuwa na madaraka basi nchi zao hazitakuwepo jambo ambalo si sahihi na halifai katika jamii.

   "Viongozi hao wanajifanya wao ndiyo miungu, wanatazama fadhila za kibinadamu, wakiacha mapungufu yao. Hicho ni kiburi, wakumbuke kuwa Mungu aliwaumba kwa vumbi na watarudi kuwa vumbi, sasa kwa nini mnakuwa na kiburi?," Alihoji Kardinali Pengo na kuongeza;

   "Mungu aliwaumba kwa vumbi kwa nini wawe na kiburi? Unadhani ukifa na nchi itakufa, kwani kabla yako nchi haikuwepo? Kumbuka wewe ni uvumbi na utarudi mavumbini."

   Alisema thamani ya mtu haitokani na anavyojiona, bali nguvu ya Mungu akiwakumbusha Wakristo kutubu na kumrudia Mungu katika kipindi hiki cha Kwaresma.

   Du lelo imekuaje kutoa mada isiyokua na itikadi? endelea hivyo hivyo

  12. RealMan's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th November 2010
   Location : Daslam
   Posts : 2,257
   Rep Power : 17399073
   Likes Received
   1141
   Likes Given
   573

   Default Re: sioni tatizo la maandamano ya chadema-kardinali Pengo

   Quote By Smartboy View Post
   Duh! Ujumbe mzito, ila serikali itasema anaingilia siasa.
   Mbaya zaidi watasema Chadema ya wakristo ndio maana Pengo anaitetea.

   Yaani hii nchi viongozi walishatufanya sisi mandondocha/mazezeta ili wao waneemeke.!!!!!!!!!
   -- Ukichanganya Akili yako na ile ya kuambiwa...inamaanisha una Akili--

  13. Mujumba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th January 2011
   Location : Soweto
   Posts : 856
   Rep Power : 725
   Likes Received
   290
   Likes Given
   117

   Default Re: Pengo: Sioni tatizo la maandamano ya CHADEMA

   Quote By Gerald View Post
   Du lelo imekuaje kutoa mada isiyokua na itikadi? endelea hivyo hivyo
   i always follow my instincts

  14. Sizinga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th October 2007
   Location : Mars
   Posts : 7,455
   Rep Power : 3673119
   Likes Received
   2960
   Likes Given
   3437

   Default Re: Pengo: Sioni tatizo la maandamano ya CHADEMA

   kashaga upo kama kinyonga....
   GESI KWANZA KOROSHO BAADAE!!

  15. genekai's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th February 2010
   Location : Loitering!
   Posts : 10,531
   Rep Power : 248805509
   Likes Received
   2520
   Likes Given
   2850

   Default Re: sioni tatizo la maandamano ya chadema-kardinali Pengo

   Kwa yeyeote asiyyekuwa biased atakubaliana na Pengo! Nimeipenda mkuu!
   "The people who cast votes decide nothing, the people who count the votes decide everything" - Joseph Stallin

  16. Ng'wanangwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th August 2010
   Posts : 9,171
   Rep Power : 18071471
   Likes Received
   2220
   Likes Given
   1528

   Default Kardinali Pengo: hata CCM wakanyamazisha vyombo vyote vya habari mawe yatasema

   MAisha yangu yamo mikononi mwenu, lakini mjue ni Mungu amenituma hayo (Nabii Yeremia).kama kuniuwa muniue, kwani ninajali?mnasikia hamtaki kusikia shauri yenu.mkiniua mjua munamwaga damu isiyo na hatia na itawaangiukia wenywe.nasema hivi si kama mtu anayeropokaropoka tu, ninasema nikiwa na akili timamu.

   asema serekal inalazimisha kuliapa mdeni wya Dowanzan wakat ata umeme hatuutumii.

   alaani waandishi waliopindisha habari kuhusu mkutabnow wa Bunda

   sosi: Tumaini Radio
   UNITED WE STAND  17. Societa Jesuit's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 1st February 2011
   Posts : 200
   Rep Power : 593
   Likes Received
   4
   Likes Given
   0

   Default Re: Kardinali Pengo: hata CCM wakanyamazisha vyombo vyote vya habari mawe yatasema

   alichosema pengo ni sahihi kama raia wa tanzania na si kama kiongozi wa dini ...hapa watu msilete udini.

   ''i was born with it and not without it, to whom should i leave it''.

  18. theophilius's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 19th November 2010
   Posts : 151
   Rep Power : 597
   Likes Received
   49
   Likes Given
   24

   Default Re: Kardinali Pengo: hata CCM wakanyamazisha vyombo vyote vya habari mawe yatasema

   Kweli hasa! wenye masikio wamesikia

  19. samirnasri's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th November 2010
   Posts : 1,370
   Rep Power : 839
   Likes Received
   198
   Likes Given
   73

   Default Re: Kardinali Pengo: hata CCM wakanyamazisha vyombo vyote vya habari mawe yatasema

   Title na content haviendani, pengo kayasema hayo lini. Mbona maneno hayo yanakaribiana na ya privatus karugendo alipokuwa akimjibu wasira kwenye gazeti la raia mwema. Karugendo alisema, nanukuu "hata chadema ikifutwa na dr slaa kuwekwa ndani, miti na mawe yatasimama na kuandamana" (raia mwema, 9 march, 011 pg.18) mwisho wa kunukuu.

  20. plawala's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th January 2011
   Posts : 627
   Rep Power : 681
   Likes Received
   59
   Likes Given
   1

   Default Re: Kardinali Pengo: Watawala siyo miungu; Maandamano hayana tatizo so far..

   Pengo mkali,waliopewa mamlaka kwa uhalali ndiyo wanaoweza kuwasemea wnanchi
   Kumbuka alioyosema katika ibada ya mazishi ya askofu wa jimbo la mwanza miaka ya nyuma
   Aliiambia serikali haiwezi kuchagulia viongozi wa kanisa mambo ya kusema,uzuri ni kwamba noti za mafisadi haiwezi kupenyeza kwake

  21. Nditu's Avatar
   Member Array
   Join Date : 12th March 2011
   Posts : 84
   Rep Power : 567
   Likes Received
   26
   Likes Given
   32

   Default Re: Kardinali Pengo: Watawala siyo miungu; Maandamano hayana tatizo so far..

   Quote By Jesuit View Post
   ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema haoni tatizo katika maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

   Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi jana, Kardinali Pengo alisema badala yake Serikali: “Ichimbue mizizi ya matatizo badala ya kukimbilia kukata matawi.”

   Kauli ya Pengo ni kama inaunga mkono matamshi yaliyotolewa juzi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliishauri Serikali kutotumia vyombo vya dola dhidi ya Chadema na badala yake ijirekebishe kwa kuwa na wepesi wa kukabiliana na matatizo yaliyopo nchini.

   Kadhalika, kauli hiyo ya Pengo imekuja wakati Serikali ikiendelea kulaani maandamano hayo ya Chadema na kutaka yasitishwe kwa madai kuwa yanaweza kuleta machafuko nchini.

   Katika mahojiano hayo Kardinali Pengo alisema haoni kama Chadema kinafanya vurugu katika maandamano yake kama baadhi ya watu wanavyodai: “Sioni ‘point’ ya kusema maandamano ya Chadema yanaweza kusababisha vurugu,” alisema Kardinali Pengo na kuongeza:

   Alisema ikiwa kuna tatizo katika maandamano hayo kama inavyoelezwa na serikali, ni bora hali hiyo ikafafanuliwa mapema na kukiambia Chadema kisitishe kuandamana.

   “Lakini serikali isichukulie ‘comment’ (maoni) ya mtu mmoja mmoja na kusema kwamba Chadema inasababisha vurugu, bila kusikiliza na kuchambua kwa undani,” alisema.

   Aliongeza kuwa endapo serikali imechunguza na kubaini ukweli kwamba maandamano hayo yanaweza kuleta vurugu za kisiasa, basi iyasitishe badala ya kutoa kauli tu kwamba yanahatarisha amani.

   Pengo alisema huenda uamuzi wa Chadema kufanya maandamano unatokana na madai yao dhidi ya kupanda kwa gharama za maisha, umeme na malipo kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans kwamba hayakusikilizwa.

   Alisema Serikali haitakiwi kuyafumbia macho matatizo ya kisiasa nchini badala yake itafute kiini chake na namna ya kuyatatua.

   “Serikali ianze kuchimbua mizizi ya matatizo ya kisiasa yaliyopo ndani ya Taifa, badala ya kukimbilia kukata matawi. Kwa sababu kuanza kukata matawi ni kuzidi kuipeleka nchi katika machafuko ya kisisasa na matokeo yake ni kuleta madhara kwa wananchi,” alisema.

   Askofu huyo mkuu pia alisisitiza kuwa Serikali inatakiwa kuhakikisha inafuatilia matatizo yanayowakabili wananchi kwa sasa, ambayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka ili watu wasipate fursa ya kudai mambo hayo kwa maandamano.

   Kwa mujibu wa Kardinali Pengo, Serikali pia haipaswi kutoa vipaumbele kwenye masuala ya siasa na kusahau matatizo ya wananchi kwani hilo linaweza kuwa kiini cha vurugu... "Serikali iguswe kama ilivyoguswa na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotoka mwaka huu."

   Baadaye akihubiri katika Misa ya Jumatano ya Majivu kuashiria kuanza kwa siku 40 za Mfungo wa Kwaresma ambao Wakristo hukumbuka mateso ya Bwana wao, Yesu Kristo kabla ya Pasaka zaidi ya miaka 2000 iliyopita, Kardinali Pengo alikemea tabia ya viongozi kung'ang'ania madaraka na kudhani kuwa bila wao nchi zao haziwezi kuwepo au kusonga mbele.

   "Yapo matatizo katika viongozi wanaong'ang'ania madaraka wakiwa tayari hata kumwaga damu ya wengine ili wao wabaki madarakani. Hawa ni viongozi wanaofikiri uwezo unaweza kuwa ndani yao, wanajifanya wao Mungu," alisema Pengo.

   Alisema viongozi hao wanatazama fadhila za kibinadamu wakiacha upungufu wao na kudhani kuwa wasipokuwa na madaraka basi nchi zao hazitakuwepo jambo ambalo si sahihi na halifai katika jamii.

   "Viongozi hao wanajifanya wao ndiyo miungu, wanatazama fadhila za kibinadamu, wakiacha mapungufu yao. Hicho ni kiburi, wakumbuke kuwa Mungu aliwaumba kwa vumbi na watarudi kuwa vumbi, sasa kwa nini mnakuwa na kiburi?," Alihoji Kardinali Pengo na kuongeza;

   "Mungu aliwaumba kwa vumbi kwa nini wawe na kiburi? Unadhani ukifa na nchi itakufa, kwani kabla yako nchi haikuwepo? Kumbuka wewe ni uvumbi na utarudi mavumbini."

   Alisema thamani ya mtu haitokani na anavyojiona, bali nguvu ya Mungu akiwakumbusha Wakristo kutubu na kumrudia Mungu katika kipindi hiki cha Kwaresma.

   Wakati huohuo; Festo Polea anaripoti kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambao wapo katika taasisi isiyo ya kiserikali ya Truya wamesema ili kuondokana na machafuko yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, viongozi wanaokiuka matakwa ya uongozi, uvunjaji wa Katiba na sheria za nchi wanapaswa kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

   Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Helman Sheluleta alisema Ibara ya 18 ya Katiba ya nchi inatambua haki ya mtu kutoa maoni, kusikilizwa na kuandamana kwa amani na kwa mujibu wa sheria lakini sheria inapovunjwa kwa ajili ya kupata haki ndiko kuhatarisha amani ya nchi.

   Source: Mwananchi March 10, 2011
   ============================== ============================== =====
   Hatukutarajii uone tatizo ndani ya Chadema!
   Ila unadhihirisha kile ambacho wengi humu wanakificha kwamba Mkulu unashabikia na ulishawishi watu washabikie Chama chetu kileeee!
   Nafurahi hata Kardinali Pengo ameliona hilo. Mimi kwa upande wangu nilikuwa nashindwa kabisa kuelewa maana ya tuhuma za makada wa CCM kwamba ati CHADEMA wanafanya "Vurugu" kwa lengo la kuiangusha serikali iliyoko madarakani.
   Ukweli kwa kadiri ninavyofahamu ni kwamba CHADEMA wanatekeleza jukumu lao kama chama pinzani kuikosoa serikali na kuwaonyesha wananchi kile kinachokosewa na serikali ili waihukumu. Serikali yenyewe kwa uzembe wake imeipa umaarufu mkubwa pengine zaidi hata inavyostaili CHADEMA kwa maamuzi yake tata na mara kadhaa ya ya kishabiki na ya kukurupuka kama pale ilipoamuru kishabiki kuuwawa na kujeruhiwa kwa waandamanaji kule Arusha. Kibaya kabisa ni ushabiki ulioonyeshwa na makada wa CCM pamoja na Mwenyekiti wao wa eti waliouwawa na kujeruhiwa "Walijitakia". Tukio la kijinga lile litaitafuna CCM kwa muda mrefu ujao na huenda likawa ndiyo mwanzo wa kuanguka vibaya kwa chama hiki ambacho kwa dalili zote kimedhoofishwa na kutekwa nyara na mafisadi.
   Mchawi wa CCM yupo ndani ya CCM yenyewe na kamwe si CHADEMA inayotimiza wajibu wake kikamilifu na kwa uadilifu. Tatizo hapa ni kwamba CHADEMA wanazungumza lugha inayoeleweka vyema na wananchi wa kawaida wanaposema maisha ni magumu, serikali ni legelege na imeshindwa kazi kiasi cha kushindwa hata kuwasha umeme nchi nzima, serikali na chama kimesheheni wezi, vibaka, mafisadi na matapeli..... Hebu niambie ni nani atakataa? Hata wana CCM wenyewe kwa pembeni wanaafikiana na hoja za CHADEMA ingawa hadharani wanajifanya kuilaani.

  Page 4 of 7 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Mukama akutana na Kardinali Pengo
   By Miruko in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 28
   Last Post: 1st July 2014, 17:27
  2. Kardinali Pengo: Kanisa litasema kweli bila kuogopa gharama!
   By Candid Scope in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 97
   Last Post: 19th March 2014, 09:41
  3. Replies: 32
   Last Post: 16th December 2011, 01:37
  4. Replies: 10
   Last Post: 13th June 2011, 19:50
  5. Replies: 39
   Last Post: 10th November 2010, 02:30

  Tags for this Topic

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...