Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mbowe kuanza kutoa shukrani kuanzia kesho

    Report Post
    Page 1 of 3 123 LastLast
    Results 1 to 20 of 56
    1. #1
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,002
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      781
      Likes Given
      28

      Default Mbowe kuanza kutoa shukrani kuanzia kesho

      Mbowe aanzisha safari ya 2010 kwa helikopta tena



      na Mwandishi Wetu


      MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, leo anaanza awamu ya kwanza ya ziara ya kuzunguka mikoa 10 nchini, akitumia helikopta, kwa malengo ambayo yanaonyesha kuanza maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.


      Habari kutoka Mwanza ambako ndiko ziara hiyo inakoanzia zinaeleza kwamba, helikopta ambayo Mbowe ataitumia, iliwasili katika jiji hilo jana jioni ikitokea nchini Kenya.


      Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zilithibitishwa na Mbowe mwenyewe, ajenda kuu ya ziara hiyo ni kuwashukuru wananchi kwa namna walivyokiunga mkono chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.


      Hata hivyo, alipotakiwa kueleza iwapo ziara yake hiyo ilikuwa ikilenga kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Mbowe hakuwa tayari kueleza moja kwa moja zaidi ya kusema tu kwamba; “lengo la chama chochote makini ni kuchukua madaraka ya dola.”


      Taarifa rasmi kuhusu ziara hiyo iliyotolewa Dar es Salaam jana jioni na kutiwa saini na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Shaib Akwilombe, ilisema dhumuni la kwanza la ziara hiyo ni kuwashukuru Watanzania waliokipigia kura chama hicho, kwenye uchaguzi wa mwaka jana.


      Pamoja na hilo, Akwilombe katika taarifa yake hiyo alisema pia kwamba, atakapokuwa katika ziara hiyo, Mbowe atawashukuru wananchi kwa kufanikisha uchaguzi huo kwa njia ya amani, pamoja na kuwapo kwa mazingira magumu waliyokuwa nayo, ambayo hata hivyo taarifa hiyo haikuyafafanua.


      Dhumuni jingine linalotajwa katika taarifa hiyo, ni kuwaandaa wananchi kujenga na kuimarisha chama hicho, kwa lengo la kuimarisha upinzani nchini, kama sehemu ya utekelezaji wa programu ya miaka mitano ya chama hicho yenye ujumbe unaosema ‘Tumaini Jipya’.


      Aidha, alisema ziara hiyo ina lengo la kuhamasisha uwajibikaji wa viongozi na wananchi katika ngazi mbalimbali baada ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Nne, ili kuchochea demokrasia na maendeleo nchini.


      Naibu huyo amesema, ziara ya mwenyekiti huyo itaanza leo wilayani Nansio kisiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Shirati, Tarime na Musoma mjini, mkoani Mara.


      Akiwa katika ziara hiyo ambayo itamchukua siku 10, Mbowe atakwenda pia katika mikoa ya Kagera, Mara, Kigoma, Shinyanga, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Dar es Salaam.


      Kwa mujibu wa taarifa hiyo, awamu ya pili ya ziara hiyo ya Mbowe ambaye hivi sasa anasoma masomo ya falsafa, siasa na historia katika Chuo Kikuu cha Hull nchini Uingereza na wakati huo huo akipata mafunzo mengine maalum ya uongozi huko huko Uingereza, itaanza katikati ya Mwezi Aprili mwakani.


      Katika uchaguzi mkuu uliopita, Mbowe ambaye aligombea urais kwa mara ya kwanza, alishika nafasi ya tatu, akitanguliwa na Rais Jakaya Kikwete (CCM) na Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), na chama chake kilipata viti vitano vya wabunge na kina wabunge sita wa viti maalum.

    2. Study Abroad

    3. #2
      Jafar's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2006
      Location : Msoga, Chalinze
      Posts : 1,249
      Rep Power : 895
      Likes Received
      13
      Likes Given
      0

      Default

      Mhishimiwa Mbowe bora wewe unayekumbuka kutoa shukrani. Wenzako walituahidi hatuoni ahadi kutimizwa wala kuwaona wao wenyewe.

    4. #3
      Kulikoni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th August 2006
      Posts : 434
      Rep Power : 737
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Jafar
      Mhishimiwa Mbowe bora wewe unayekumbuka kutoa shukrani. Wenzako walituahidi hatuoni ahadi kutimizwa wala kuwaona wao wenyewe.
      Jafar,

      Huu ni uongo. Akina JK na EL wamepita sana tu... mpaka wameanza kusemwa kuwa kwanini hawakai ofisini. Tofauti iliyopo ni hayo makeke ya Mbowe ya helikopta.,.. a press release rasmi kuwa, according to Chinga, '..anakwenda kutoa shukrani kwa kutochaguliwa'!
      If you want to judge a leader, look at the organization ten years later.

    5. #4
      Mafuchila's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2006
      Posts : 915
      Rep Power : 852
      Likes Received
      13
      Likes Given
      6

      Default

      Mhmmm,
      Mwaka mmoja unamalizwa kwa ziara za shukrani je tutafika?

    6. #5
      kichwamaji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2006
      Posts : 399
      Rep Power : 717
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Mafuchila
      Mhmmm,
      Mwaka mmoja unamalizwa kwa ziara za shukrani je tutafika?
      Hivi kuna kibaya gani Mbowe kafanya sasa? Mbona wengine humu mna roho ya korosho? Kama angekuwa mzomokaji angekwisha kufanya hiki anachokifanya sasa. Lakini lazima awape walioshinda muda wa kutekeleza ahadi zao. Mwaka mmoja unatosha kufanyia tathmini ya kazi za serikali. Huu ndio upinzani makini.

    7. Miaka 50

    8. #6
      Mafuchila's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2006
      Posts : 915
      Rep Power : 852
      Likes Received
      13
      Likes Given
      6

      Default

      Kichwamaji usiwe kichwamaji kweli, hakuna mahala ambapo CHADEMA wamesema ni ziara ya kufanya tathmini, walichosema ni ziara ya kuwashukuru wananchi. So my point of departure was shukrani na sio tathmini kama unavyodai.

    9. #7
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,002
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      781
      Likes Given
      28

      Default

      Jina ama nia shukrani na mengine yatatokea. JK alifanya Ziara Mara kusemas asante na akaambiwa Mara CCM haiko ni ubabe umewaa ushindi . Akaenda Tarime akajionea akasema he was not happy . Akasema atarudi na kweli karudi na baadaye kamtuma Lowasa .Wote kwa ujumla Ziara 4 na wamevuna Uongozi wa Wilaya wa Chadema maana ni mwiba pale Tarime . Sasa Mbowe atasema asante na kuwakumbusha wananchi walivyo liwa na watakavyo liwa maana bado miaka 4.Atawaeleza juu ya Richmonds etc . Ndiyo mambo yalivyo kile ni Chama hakiweza kufanya mambo kwa mujibu matakwa yetu tusio wanachama wake no.

    10. mTz
      #8
      mTz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th August 2006
      Posts : 407
      Rep Power : 736
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      Hivi kwa nini CHADEMA wasitoe hiyo asante yao kwa kujenga madarasa au zahanati? au hata kutoa mikopo midogo midogo. To me that mekes more sense to an average mTz than just going to say asante empty handed!
      "Be not afraid of growing slowly, be only afraid of standing still." Old Chinese Proverb

    11. #9
      Aljazeera's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th June 2006
      Location : Likuli Rd
      Posts : 112
      Rep Power : 682
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      Siyo kwamba wanakwenda kutoa shukrani tu, bali wanakwenda pia kukitangaza na kuwaelezea wananchi sera zake.

      Kujenga shule au zahanati siyo jukumu la chama cha siasa na hata kama wangependa kufanya hivyo lazima wapate eneo, vibali vya kuendesha nk. Je kwa mawazo yako unadhani Serikali itao kibali cha shule au Zahanati itakoyukuwa inajengwa au kumilikiwa na wapinzani.

      Nadhani ni vizuri kwenda kutoa shukrani na kutangaza chama empty handed kuliko kwenda kuwadanganya watu na bahasha zenye mia tano tano au kamba na kofia.

      Je wakati Ndesamburo alitaka kukarabati barabara za moshi mjini hasa ile ya Swahili na Kiusa, mbona Serikali ilimkatalia.

      Wewe umeshawahi kujiuliza kwa nini watu wengi wakipenda kutoa misaada yao lazima wapitie kwenye taasisi za dini. Jibu ni kwamba ukijifanya wewe ni mjanja na unajali masilahi ya wananchi utayaona matokeo yake hasa kama ni mkereketwa wa sera mbadala na Serikali.

      Unahitaji kuishi Tanzania na kukaa ndani ya siasa kujua namna mambo yanavyofanyika.

      Watu wako radhi kuchangia sherehe kuliko kuchangia maendeleo kwani wataonekana kuikosoa serikali.
      --------------------------------------------
      Wananchi Tumechoka, Viongozi Hawajitambui

    12. #10
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,002
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      781
      Likes Given
      28

      Default

      Eljazeera
      Maneno mazito haya na mwenye masikio haambiwi bali asikie na mwenye macho asome na kutia akili .Mbowe na Chadema Hoyeeeeeeeeeeeeeee

    13. #11
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default

      Lakini,
      Ebu twende mbele turudi nyuma!
      Hivi kweli kuna haja ya kutumia Helikopta ktk kutoa shukrani...hali chama kina matatizo ya Kifedha! (kulingana na habari za wale waliokimbia).
      I mean, kwa nini Freeman asitangaze ktk TV ama Radio, kisha wajumbe wake waendelee kumwakilisha...
      Jamani swala tunalozungumzia kila siku ni matumizi makubwa ya fedha za Umma pasipo sababu muhimu..Yes tunakubali kuwa Freeman hana muda mrefu wa kukaa TZ inabidi arudi Uingereza mapema lakini ktk kipindi hiki kifupi ataweza kukamilisha mangapi muhimu ktk hotuba za masaa ambapo hawezi hata kulala ktk wilaya hizo ili apate kuzungumza na wananchi wa sehemu hizo (kubadilishana mawazo). Navyofikiri mimi, ni muhimu sana kwa Freeman kwenda mikoani na kuwa msikilizaji zaidi kuliko mhutubiaji...shukran ya mswahili sio maneno matupu.. wape ahadi za kweli kulingana na matatizo yao. Unapotembelea wilaya, mikoa ni bora upate muda wa kusikiliza matatizo ya wananchi, kuelewa vipaji vyao, kuona mapungufu ya serikali ktk sehemu hizo kisha kupanga mbinu ambazo zinaweza kuwapa ahadi za uhai hawa wananchi!..
      hayo ni mawazo yangu sielewi kwa nini Freeman kafanya haraka hivyo wakati mgumu kama huu ambao yeye mwenyewe hana nafasi ya kutosha na pia chama bado kinahitaji fedha zaidi kujijenga!...
      Unless, kuna mambo muhimu zaidi ya kutoa shukrani..
      Last edited by Mkandara; 30th December 2006 at 00:54.
      Exploration of reality

    14. Ole
      #12
      Ole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th December 2006
      Posts : 1,114
      Rep Power : 862
      Likes Received
      10
      Likes Given
      7

      Default

      Huko Bongo tuna kazi . sio CCM wala CHADEMA wenye uwezo wa kuwaondoa waTZ kwenye matatizo ya umasikini. Hawa wote wanaangalia mifuko yao.

      Tutafika tuu.

    15. #13
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,818
      Rep Power : 2965
      Likes Received
      2417
      Likes Given
      3484

      Default

      mwacheni akaibomoe CCM huko mikoani. tumechoka,tumechoka,nasema tumechoka!!

      viongozi wote wa vyama vya upinzani waende mikoani "kuwashukuru" wananchi.

    16. #14
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default

      Jokakuu,
      Ebu nifahamishe hapa! Itaibomoa vipi CCM kwa mkutano wa masaa kisha huyooo anaruka na dude!..Hizi shukrani za kitu gani hasa!..
      Exploration of reality

    17. #15
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,818
      Rep Power : 2965
      Likes Received
      2417
      Likes Given
      3484

      Default

      Mkandara,
      unachoogopa ni nini? mwache akafanye hilo alilodhamiria, matokeo tutayajua baadaye.

      shukurani za kumnyima kura, na sasa watanzania wanayaona wenyewe.

    18. #16
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,612
      Rep Power : 2890
      Likes Received
      3826
      Likes Given
      12202

      Default

      Mkandara,
      Freeman is a politician. Angetoa shukrani kwenye TV ni wangapi ambao wangemsikia? Lakini kwa helikopta ametembelea maeneo mengi zaidi in such a short time. He has to stay in the news by making news. Na si hilo tu kuna message anayotoa katika kila kituo. Alipokuwa Musoma nasikia amezungumzia suala la Richmond na kwamba atawaomba wabunge wa chama chake walizushe bungeni. That is good, I think.

    19. #17
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,002
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      781
      Likes Given
      28

      Default

      Mkandara
      JK na Lowasa na hata Viongozi wa CCM kama Makamba huwa mikoani na maeneo hayo na kukaa masaa na kutoa hotuba zao huwa zinasaidia nini maana huwa hawa lali huko . Mbowe anaweza kulala kituo cha mwisho kwa siku hiyo maana siamini kwamba anaweza kuwa Mara na ni jioni aamue kurudi Moshi no . The same kwa akina Lowasa na JK .Mwacheni atoe shukrani .Chadema imetulia wenye shida ni hao walio nunuliwa kwa gharama kubwa toka Tarime ni nguvu za JK na Lowasa na hawana impact kule Tarime ndani ya Chadema. Chadema ni watu wengi na viongozi ni wale wachache wameondoka na wengine wataziba nafasi yao .

    20. #18
      Kitila Mkumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2006
      Posts : 3,917
      Rep Power : 6962
      Likes Received
      1060
      Likes Given
      35

      Default

      Mkandara: Kumbuka kuwa siku zote wapinzani wamelaumiwa kwa kufanya press conference pale maelezo bila kuwafikia wananchi. Sasa CHADEMA wameamua kuwafuata wananchi huko walipo, hilo nalo ni nongwa. Kuhusu helicopter, hiki ni chombo cha usafiri. Wangeweza kwenda kwa miguu, kutumia punda, baiskeli, gari, meli, n.k. Ni swala la kuangalia ni usafiri gani utafanikisha malengo yako kwa muda unaotaka na kwa gharama unazozimudu. Kuhusu gharama, rejea uchambuzi wa Mnyika katika hili.

      Hata CHADEMA isingetumia helicopter hao waliohama wangekuja na sababu zingine. Ni swala la matarajio. Inategemea hawa bwana walitarajia nini katika kujiunga kwao na CHADEMA. Kwa kweli katika upinzani mtu ukiingia kwa matarajio ya kuneemeka kipesa, utasubiri sana na mwishoni itabidi urudi ccm kama walivyofanya hao ndugu zangu. Kwa hiyo mimi siamini kwamba ni helicopter ndiyo iliyowatoa chadema. Kumbuka tupo katika mapambano sio tu na ccm, lakini na dola. Ahadi moja ya JK ilikuwa ni kuisambaratisha CHADEMA na aliitoa hii ahadi waziwazi sio katika vikao vya siri. Sasa kazi yetu ni kupambana. Katika haya mapambano, tutapoteza baadhi ya wapiganaji, na tutapata wengine katika mchakato huo. Tunaamini JK hatoweza kuua upinzani Tanzania kwa mikakati ya kuua upinzani bali kwa kutekeleza matarajio ya maisha mema aliyowapa, kitu ambacho kuna kila dalili kuwa kinamshinda.
      A Struggle Without Casualties is No Struggle-Steve Biko

    21. #19
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default

      Wanabodi,
      Nadhani mmenijibu vya kutosha pamoja na kwamba mmekwenda nje kabisa ya makusudio yangu..
      Nitawaeleza kwa kirefu nilichokuwa nikiuliza.

      Lunyungu,
      Umezungumzia JK na Lowassa kutembelea mikoani..
      Hizi ndizo tofauti ambazo Chadema wanashindwa kuziona. JK na Lowassa ni CCM, Chama kilichokwisha jijenga kwa wananchi na hakihitaji intro!.. Tofauti na Chadema kabisa!
      Hikihiki CCM wakati kilipoanzishwa (Kupighania Uhuru) walitembelea mikoa kwa dhumuni maalum.. na walichukua muda wao kujitangaza kwa kila hali na mali. Chadema leo hii ipo stage ya CCM miaka 45 kama sii 50 iliyopita!..
      Mila yetu inatueleza kuwa mgeni asiyelala huwa na dharau fulani ya makazi yako!... lakini yule anayelala na wewe ktk zizi la ng'ombe ndiye mgeni anayeyakubali maisha yako na kuelewa machungu ya kulala ktk zizi la ng'ombe...Kwa mkerewe inabidi ulishwe samaki wetu furu na Ugali wa mhogo.. kisha lazima kinywa kiwe na uchambuzi wa nyama na mifupa bila kutumia mikono.. hapo wewe mwenzao! (Utani)
      Kuna tofauti kubwa sana kati ya yale ambayo JK na Lowassa wanatakiwa kuyafanya na Freeman.. lazima Chadema mfahamu culture za watu wengine hasa mikoa ya ziwa.

      Jasusi,
      Point yako nzuri sana lakini hukuelewa kuwa nachojaribu kusema mimi ni kuwa ipo tofauti kubwa ya JK kulitangazia taifa kwa dakika 10 na kuwepo kwa saa moja. Lowassa alipotembelea hapa alitufanya hivyo wananchi, na kusema kweli kajenga lugha mbaya sana midomoni mwa wananchi.- Bad moral character!...hilo ndio neno pekee linalozungumzwa hivi sasa wakati Lowassa hafikirii hivyo kabisa.

      Mwanasiasa,
      Nadhani swala langu kubwa sio gharama za utumiaji wa helikopta peke yake ila gharama zake zitakuwa pigo kwa Chadema kama hazitaweza ku-de-liver kitu. Kila kitu kina mazuri na mabaya yake.. na binafsi naona mabaya ya Helikopta ni mazito zaidi kulingana na mipangilio aliyopewa. Ni uwezo wa helikopta ambao utamfanya Freeman asiweze kukaa zaidi na wananchi kwa sababu atakuwa na mikutano sehemu nyingine... Watu hawatakuwa na muda wa kumfahamu Freeman na Chadema. Freeman ni mgeni ktk nyumba za hawa wananchi na anapokwenda huko kujitambulisha kwa kumponda JK ili yeye apewe mke inabidi achukue muda zaidi ya masaa. Lugha inayotumika hapa ni kupondana tu!.. Freeman will be a good husbad kuliko JK na asichokifahamu Freeman ni kwamba Wazazi wa JK (yaani CCM) wanafahamika vijijini humo na sii rahisi Mdanganyika kumpa mke (kura) mtu ambaye hawamfahamu vizuri...Na kikubwa zaidi familia ya JK wanazo fedha... magunia kwa magunia ya mchele humwagwa kila siku.

      Kwa hiyo hapa nazungumzia hizo technics ambazo Chadema wanazitumia kwa muda mfupi kama huu tena sehemu ambazo wananchi wake wana mila zao.
      Last edited by Mkandara; 30th December 2006 at 17:00.
      Exploration of reality

    22. #20
      Tabasamu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 279
      Rep Power : 693
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default

      Mkandara,
      Usikwazwe na neno Shukrani. Hakuna timing nzuri kama hii kwa CHADEMA hasa baada ya kuwa Makuwadi wa rushwa wamepitia huko Tarime. Bila shaka hata kama hao viongozi wamerudi kule wanakoamini kuna ulaji bado kuna wanachama na washabiki wao ambao sera za CCM bado hazijawashika. Ingekuwa ni kichekesho Mbowe kukaa maelezo na kuanza kuwaelezea watu hawa mikakati ya CHADEMA kupitia magazeti na runinga vitu ambavyo hata hivyo wenye access ni wachache mno.

    23. FemaTV & Radio
    Page 1 of 3 123 LastLast

    Similar Topics

    1. Mbunge anapotumia muda mwingi kutoa shukrani
      By Makene in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 18
      Last Post: 5th July 2011, 00:04
    2. Napenda kutoa shukrani kwa hawa wafuatao.
      By Slave in forum JF Doctor
      Replies: 4
      Last Post: 28th February 2011, 00:07
    3. Replies: 1
      Last Post: 8th November 2010, 14:13
    4. Eti soko la """kitimoto ""kuanza kupungua kuanzia kesho""
      By Pdidy in forum Celebrities Forum
      Replies: 2
      Last Post: 11th August 2010, 11:27
    5. Mashindano ya Umisseta kuanza kesho
      By Balantanda in forum Sports
      Replies: 0
      Last Post: 27th June 2009, 02:16

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...