Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mbowe kuanza kutoa shukrani kuanzia kesho

    Report Post
    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast
    Results 21 to 40 of 56
    1. #1
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,011
      Rep Power : 2560
      Likes Received
      784
      Likes Given
      28

      Default Mbowe kuanza kutoa shukrani kuanzia kesho

      Mbowe aanzisha safari ya 2010 kwa helikopta tena



      na Mwandishi Wetu


      MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, leo anaanza awamu ya kwanza ya ziara ya kuzunguka mikoa 10 nchini, akitumia helikopta, kwa malengo ambayo yanaonyesha kuanza maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.


      Habari kutoka Mwanza ambako ndiko ziara hiyo inakoanzia zinaeleza kwamba, helikopta ambayo Mbowe ataitumia, iliwasili katika jiji hilo jana jioni ikitokea nchini Kenya.


      Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zilithibitishwa na Mbowe mwenyewe, ajenda kuu ya ziara hiyo ni kuwashukuru wananchi kwa namna walivyokiunga mkono chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.


      Hata hivyo, alipotakiwa kueleza iwapo ziara yake hiyo ilikuwa ikilenga kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Mbowe hakuwa tayari kueleza moja kwa moja zaidi ya kusema tu kwamba; “lengo la chama chochote makini ni kuchukua madaraka ya dola.”


      Taarifa rasmi kuhusu ziara hiyo iliyotolewa Dar es Salaam jana jioni na kutiwa saini na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Shaib Akwilombe, ilisema dhumuni la kwanza la ziara hiyo ni kuwashukuru Watanzania waliokipigia kura chama hicho, kwenye uchaguzi wa mwaka jana.


      Pamoja na hilo, Akwilombe katika taarifa yake hiyo alisema pia kwamba, atakapokuwa katika ziara hiyo, Mbowe atawashukuru wananchi kwa kufanikisha uchaguzi huo kwa njia ya amani, pamoja na kuwapo kwa mazingira magumu waliyokuwa nayo, ambayo hata hivyo taarifa hiyo haikuyafafanua.


      Dhumuni jingine linalotajwa katika taarifa hiyo, ni kuwaandaa wananchi kujenga na kuimarisha chama hicho, kwa lengo la kuimarisha upinzani nchini, kama sehemu ya utekelezaji wa programu ya miaka mitano ya chama hicho yenye ujumbe unaosema ‘Tumaini Jipya’.


      Aidha, alisema ziara hiyo ina lengo la kuhamasisha uwajibikaji wa viongozi na wananchi katika ngazi mbalimbali baada ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Nne, ili kuchochea demokrasia na maendeleo nchini.


      Naibu huyo amesema, ziara ya mwenyekiti huyo itaanza leo wilayani Nansio kisiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Shirati, Tarime na Musoma mjini, mkoani Mara.


      Akiwa katika ziara hiyo ambayo itamchukua siku 10, Mbowe atakwenda pia katika mikoa ya Kagera, Mara, Kigoma, Shinyanga, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Dar es Salaam.


      Kwa mujibu wa taarifa hiyo, awamu ya pili ya ziara hiyo ya Mbowe ambaye hivi sasa anasoma masomo ya falsafa, siasa na historia katika Chuo Kikuu cha Hull nchini Uingereza na wakati huo huo akipata mafunzo mengine maalum ya uongozi huko huko Uingereza, itaanza katikati ya Mwezi Aprili mwakani.


      Katika uchaguzi mkuu uliopita, Mbowe ambaye aligombea urais kwa mara ya kwanza, alishika nafasi ya tatu, akitanguliwa na Rais Jakaya Kikwete (CCM) na Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), na chama chake kilipata viti vitano vya wabunge na kina wabunge sita wa viti maalum.

    2. Miaka 50

    3. #21
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default

      Tabasamu,
      sasa haya matusi!...
      Yaani umeziona vipi hizo wilaya kiasi kwamba magazeti na Luninga ni big deal!..kwani Freeman anakwenda miji mikuu ya wilaya hizi ama anaingia deep vijijini?.. Wee pale Nansio, Ukerewe pasikie tu...watu hawajachelewa kabisa...
      Exploration of reality

    4. #22
      Wacha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd November 2006
      Posts : 799
      Rep Power : 798
      Likes Received
      82
      Likes Given
      142

      Default

      Mkandara

      Wewe uko nje, hali ni mbaya sana Bongo sio huko tu alikosema kila mahali. hata pale Dar ni asilimia ngapi wenye uwezo wa kuwa na access ya computer. Usisahau ofisi nyingi TZ hazijawa computerised.

    5. #23
      S. S. Phares's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 3,041
      Rep Power : 1247
      Likes Received
      16
      Likes Given
      106

      Default

      Kwenda Vijijini ni muhimu sana...haya magazeti yenyewe yanaandikwa kwa matakwa ya serikali. Hivyo ni bora wananchi wa huko vijijini wakashangae helikopta anaweza akapanda mbegu ya mageuzi vizuri zaidi kuliko TV na Magazeti.

    6. #24
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default

      Lordtical_Jnr,
      Freeman hakwenda vijijini kaenda miji mikuu ya hizo wilaya!...

      Wacha,
      Umesema hali ni mbaya sana lakini kumbuka kitu kimoja kuwa huko ni kwangu mimi... Nyumbani. Nazipata latest na maendeleo ya pale kuliko wewe uliyepo Bongo. UK wananchi waliokuwa wengi wanaridhika na maendeleo ya CCM. Njaa kali sana lakini wengi wao hawajawahi kuona shibe ni kitu gani!..
      Mnachoshindwa kuelewa nyie ni kwamba sisi TZ tulikuwa washamba sanaaa!. Mwinyi alisifika kwa sababu wananchi waliweza kupata access ya TV na ununuzi wa magari ya anasa! huku akiendelea kuua kabisa viwanda. Asilimia kubwa ya wananchi vijijini hawafahamu tofauti ya maendeleo kati ya anasa, majumba, na ustawi wa jamiii. mwizi aliyejenga kwao hupewa sifa zote kuliko mzalendo mweye kutazama watu wote!..
      Jamani mweee!...Wananchi walio wengi wanachopima ni kule tulikotoka (kwa Nyerere) ambako hata sabuni ilikuwa shida... na ndio maana ile indicator inagonga 5 kila mwaka.. maanake tulitoka shule (no income) na kuanza kufanya kazi kwa utumwa. Pato lazima lionekane kubwa sana!
      Leo hii, hawa jamaa zangu ndio kwanza wamepata umeme baada ya mika 25 ya promise za wabunge wa CCM. Wameisha sahau kabisa uozo ule kinachotazamwa ni kile kilichopo mfukoni mwao leo hii.. Umeme.
      Kwa hiyo mwanaume hapa ni yule anayeleta gunia la mchele, kwa mdanganyika mwenye njaa, chakula adimu kupatikana.
      Chadema have to learn kwanza mila za Wadanganyika, kisha zichukulie hizo at your advantage pamoja na kwamba nia na lengo lako ni kubwa zaidi ya gunia la mchele...
      CCM wanaweza kuwa Uozo lakini nakwambieni hawa jamaa wanafikiri mbele ya vyama vingi katika swala hili la Kampeni. Nasikia kuwa wanafungua tawi la CCM hapo London...Mhhhhh! sijawahi kusikia hii maisha yangu lakini trust me hii mbinu kali sana!...mwenye upeo mdogo hataweza kuona kinachokusudiwa hapa.
      Pili,...sijasema Kompyuta!.. hata huku Ulaya asilimia kubwa ya wananchi hawana PC. Hao wenye PC asilimia 75, wanazitumia kwa kazi zao zaidi na sio maswala ya news ama Politics. Hakuna mtu anayesoma habari mpya ktk PC kama haihusiani na kazi yake ama hobby(michezo).

      Na kama maneno yako ni kweli kuhusu wilaya zetu kuwa nyuma kiasi kwamba hata radio 277 siku hizi ni deal basi Freeman angetumia nafasi hiyo kufungua matawi yake wilaya hizohizo... na kusambaza hizo 277 kwa wanachama wake, CCM (Nyerere) walifanya hivyo kutukamata wote hadi vijijini.
      Wacha, kwa sisi tulioko nje ukitembelea nyumbani bila zawadi basi mshikaji khukujenga kitu kabisa na utasemwa kuwa huyu na kukaa kote Ulaya kaja hana kitu?.. hao washikaji wako watakuja siku ya kwanza tu kwa vishindo na utalakiwa kama King!.. U must have something... zawadi yao!.. huna zawadi bob wanatakuacha wewe kizani, mbali na wewe kushuka na hilo dude la Swiss Air!..
      Kweli, watashangaa sana pale airport, lakini hata siku moja usije fikiria Mdanganyika kushangaa kwake airport (on his case helikopta) ndio kesha kupa kura zake. Bora yule asiyewatembelea lakini hutuma kitu kuliko uende mikono mitupu!...Sijui kama umenielewa.

      Freeman anatakiwa kwanza atujengee familia yake (sisi wananchi) hivyo vibanda hata akianza na vya uani!... Matawi ya Chadema.
      Last edited by Mkandara; 31st December 2006 at 16:12.
      Exploration of reality

    7. #25
      Wacha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd November 2006
      Posts : 799
      Rep Power : 798
      Likes Received
      82
      Likes Given
      142

      Default

      Mkandara

      Umesema hali ni mbaya sana lakini kumbuka kitu kimoja kuwa huko ni kwangu

      Je, Unapopata latest ndio maendeleo? Hata kama ni nyumbani?


      UK wananchi waliokuwa wengi wanaridhika na maendeleo ya CCM. Njaa kali sana lakini wengi wao hawajawahi kuona shibe ni kitu gani

      What do you mean here I don’t understand?

      Umeme siulikuwa wa mgao?

      Mkandara you are confusing yourself

      Mimi nimesema hali ni mbaya sana Bongo sio huko tu alikosema kila mahali. hata pale Dar ni asilimia ngapi wenye uwezo wa kuwa na access ya computer. Usisahau ofisi nyingi TZ hazijawa computerised.

      Hii inamaanisha ni percentage ndogo sana ambayo ina uwezo wa ku-access information. i.e. Umasikini bado ni mkubwa hata graduate ambaye amemaliza shule hawezi kununua compyuta yake nyumbani au laptop.

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default

      Wacha,
      Hiyo ni Lugha ya Michuziline ndugu yangu.. Newala ndio New York na UK ndio Ukerewe! hilo moja...Ama hata Michuziline itakuwa shida nyingine?...haya Michuziline ndiye mwana Blog wetu Issa Michuzi.

      Maendeleo unayoyafahamu wewe na mimi na wengine wote ktk kijiwe hiki sio maendeleo yanayotegemewa na wengi...
      Wadanganyika NJAA! njaa kali kiasi kwamba hawaoni tena kama kuna njia za kuondoa njaa hii isipokuwa miujiza ya Yesu (alipogawa samaki na wine). CCM leo wanachofanya ni mazingaombwe matupu jambo ambalo wewe, mimi na wengine ktk kijiwe hiki tunaelewa kuwa ni UONGO. Wadanganyika wengi wanaona kuwa CCM wanafanya miujiza ya Yesu ama Mussa toka nchi iliyokuwa haina sabuni hadi kufikia nchi imejaa wazungu na Wachina wanaouza ma -toys na vitu fake!...Asilimia 80 ya Wadanganyika hawafahamu tofauti kati ya Miujiza na mazingaombe!...yote NJAA!
      Hata huko mijini kwenyewe, watoto siku hizi hawaruki kamba, hawapandi miti kucheza - Nago, hawatengenezi magari ya visoda, bali kila kitu kinaletwa toka Ulaya.Wako hooked ktk PC kucheza games na matoy ya kizungu. Haya kwao ndio maendeleo na wazazi wao ndio wanaokumbatia maendeleo ya namna hii...
      Darasa hili la kumfahamisha Mdanganyika sio darasa la siku moja kwenda na helikopta huwezi kuwaeleza kitu Wakerewe ambao CCM imewaletea umeme baada ya miaka 25 ya ahadi, leo hii wote wameisha sahau na kusamehe kabisa...wala umeme sio big deal. Ukiuliza watasema UK imeendelea kishenzi, kila kitu kipo madukani, umeme ni secondary!..

      Rudia kusoma utanielewa.
      Last edited by Mkandara; 31st December 2006 at 17:07.
      Exploration of reality

    10. #27
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,619
      Rep Power : 2891
      Likes Received
      3837
      Likes Given
      12224

      Default

      Mkandara,
      Nimekuelewa tokea take one. Nakubaliana na mengi uliyosema. Kweli kuna kazi ya ziada kwa upinzani kuelimisha umma kwamba CCM ni wadanganyifu na hawana sera.

    11. #28
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,668
      Rep Power : 21814
      Likes Received
      735
      Likes Given
      3189

      Default

      Mkandara,

      Kama hata hapo kina Mbowe et al hawasikii, basi tena, ila tusichoke kuwakumbusha.

      wakati mwingine sioni tofauti kabisa kati ya CCM na wapinzani na hasa wakti wa kupewa ushauri wenye maslahi ya wananchi

    12. #29
      kichwamaji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2006
      Posts : 399
      Rep Power : 717
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default Why all this cynicism on Chadema?

      Quote By Ogah
      Mkandara,

      Kama hata hapo kina Mbowe et al hawasikii, basi tena, ila tusichoke kuwakumbusha.

      wakati mwingine sioni tofauti kabisa kati ya CCM na wapinzani na hasa wakti wa kupewa ushauri wenye maslahi ya wananchi
      Nadhani wengi wetu hapa tunaoijadili CHADEMA hatusomi vema majibu ya Mnyika, wala hatusomi tovuti yao. Baadhi ya hoja na maswali yanayoulizwa hapa yanaonyesha hivyo! Pili, hatutafiti kuhusu ziara za Mbowe, hasa kwa wale mlio ughaibuni.

      Kwanza, Mkandara na wenzako ni vema mjue kwamba siasa si za CCM tu. Wakifanya wao sawa, akifanya mwingine kosa! Pili, Chadema hawafuati mbinu za CCM.

      Tatu, kuhusu helikopta,, tumeshajibiwa. Huu ni usafiri tu. Hatuwezi kujiita wasomi kama bado nasi tunajenga hoja zinazoonyesha kwamba 'tunashangaa' helikopta ya Mbowe. Ni vema pia tujajua kwamba helikopta gharamam nafuu kukliko mashangingi 10 au 20 anayotumia JK na wenzie kufanya kazi ya siasa za CCM kwa pesa ya serikali! Na bado tunaona sawa!

      Nne, ziara hii ya Mbowe mikoani imetengwa katika awamu 2. Hii ni ya kwanza na ina-cover mikoa 10. Kila mkoa unapewa siku nzima. Mikutano inapangwa kila jimbo au kila wilaya, na inahitimishwa mkoani. Kazi mbaya hii?

      Tano, hotuba za Mbowe sizo pekee zinazpaswa kujenga Chadema. Wadau wanaendelea kuwasha moto kila anapotoka. Mbowe anajenga Chama. Badala ya kubezwa angesaidiwa nma kuungwa mkono. Hata Nyerere alibezwa hivi hivi...huku akiitwa mtoto huyu...huku akilinganishwa na wazungu!

      Kweli, Mbowe si scandal ya vijana wa leo. Ni shujaa anayepaswa kupewa kila aina ya neno la faraja. Anatoa changamoto tuliyoikosa kwa muda mrefu. Kuwa cynic hakutasaidia kujenga nchi. Chadema wanafanya kazi njema. Tatizo letu tunafikiri mno ki-CCM kwa kila kitu. Na CM kama wana lolote wanaloweza ni propaganda, uwongo, wizi na rushwa. Tuwasifu kwa hayo?

      Mbowe hana sababu ya kupeleka kitu kingine kwa wananchi, bali ujumbe mpya wa matumaini. Kauli inayojenga ujasiri. naona wengine hapa tunafikiria ki rushwa rushwa tu....kwamba angekwenda kuwahonga wananchi ndipo aonekane wa maana! TUnajadili mapinduzi hapa? Tumekata tamaa? Basi,, kama tumekata tamaa, si tuwaache wenye moyo wachape kazi? Why all this cynicism?

    13. #30
      Wacha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd November 2006
      Posts : 799
      Rep Power : 798
      Likes Received
      82
      Likes Given
      142

      Default

      Mkandara

      Ulisema ni matusi; naona umefuzu kutokujibu maswali kama JK, Richmonduli, Mbowe, Mnyika etc (politicians)

    14. #31
      Wacha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd November 2006
      Posts : 799
      Rep Power : 798
      Likes Received
      82
      Likes Given
      142

      Default

      Unafahamu nyinyi chadema mna dharau sana ndio maana hata mseme namna gani watu hawawezi kuwaamini. MNASEMA ATI HATA HAPA KWENYE MIJADALA WATU HAWASOMI MNAWEZA KUTHIBITISHA HAYO?

      ACHENI MBWEMBWE ZISIZOKUWA NA MSINGI. SISI TUNAELEWA FIKA HIKI KIJIWE NI CHA NANI NA MWELEKEO WAKE.

      Mkiulizwa maswali mpaka mkae kikao alafu jibu dogo tu mtaanza safiii sanaaa what a joke? Acheni umbeya mmekuwa kama vibaka.

      CCM wana makosa sana tu lakini watu inabidi waelimishwe hasa kule vijijini ambako ndio wapiga kura nyinyi. Cha msingi ambacho mmeona ni usafiri wa rahisi wa chopa kukodi kutoka Kenya. Kama chopa ingekuwa rahisi hivyo mbona msikodi kutoka Mwanza, Dodoma au Dar. Acheni madebe yasiyokuwa na maana.

      Hamuwezi hata kuonyesha matumizi ya pesa mnazopewa na conservative party ndio sababu watu wanasema ni cha ukabila. Wabunge wenu wanachojua ni kusinzia tu kule bungeni, mlijua CCM hawawezi kuuliza suala la umeme KWA NINI WABUNGE WENU WASIULIZE? HALAFU MNAKUJA HAPA NA UTAPELI WENU.

      NYIE NDIO MNGEWEZA KUWAFUKUZISHA WATU KAZI KWA KUFUATILIA MASUALI KULE BUNGENI – MATOKEO YAKE MNACHAGUANA KWA UPENDELEO NA KWENDA KULALA BUNGENI WHAT A JOKE?

      NAFIKIRI nyie Chadema anzani kuamka kabla ya kumwamsha aliye lala. Kwani mmelala na CCM wanalijua hilo mna kazi kubwa.

    15. #32
      Tabasamu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 279
      Rep Power : 694
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default

      Kichwamaji,
      Asante sana kwa ufafanuzi mwanana. Nimeipenda hiyo sehemu ya kufikiria ki CCM. Watu wanaamini mno kwenye pilau, kofia, tshirt na Kanga. Ukiwaeleza hali halisi hawataki ati wanataka ujenge madarasa na zahanati kwa hizo pesa. Utafikiri jengo ndiyo shule na zahanati.
      Mkandara,
      Hiyo Bongo unayoongelea wewe ni ipi? Magazeti ni kweli yanafika Nansio lakini ni watu wangapi wanaweza kumudu kutoa hiyo mia tatu? Nilikuwepo Nansio miezi mitano iliyopita magazeti yanafika pale baada ya siku mbili au tatu tangu yachapishwe halafu ni nakala chini ya ishirini kila gazeti na haziishi. Magazeti ya udaku au ukipenda ya mia mia ndio kidogo yanauzika sasa hapa utanambiaje watu wanapata habari? TV zinashika lakini ni watu wachache mno wanaoweza kumudu na kwa taarifa yako events kama kombe la dunia na mapambano ya ngumi au ligi ya Uingereza kuna watu wanaoweza kumudu satellite dishes ndio wanakamata na wanatoza sh. mia kwa mechi hebu sasa twambie nani anaweza toa mia kwenda kuangalia habari?
      Sijaona mpaka sasa tatizo la Mbowe kutumia chopa na tumeshaambiwa ni rahisi zaidi kuliko magari ambayo hata barabara hakuna. Kwa wasiokubaliana na Mbowe ni kuwa hafanyi chochote lakini hata CCM wenyewe wanajua he is a force to reckon.

    16. #33
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default

      Wacha na Tabasamu,

      Shukrani kwa mawazo yenu ambayo binafsi sioni kama yana tofauti na ushabiki wa Simba na Yanga.
      Ebu labda niwaamshe ktk harakati zangu za utoaji hoja zangu mimi.
      Nachojaribu kusema hapa ni mawazo ya mtu mwingine - Mdanganyika ambaye anachukua asilimia 80 ya wapiga kura wetu. Sii lazima mawazo nayoyaweka hapa ndio msimamo wangu.
      Inashangaza sana kila napojaribu kuwapeni mifano ndio kwanza nyie mnazidi kudidimia jangwani.. hamunielewi kabisa.
      Huu ni upande wa pili wa shilingi navyoutazama wala mimi sii mshiriki kabisa wa ushabiki wenu wa Yanga na Simba (CCM v/s Chadema). Nawatazama Chadema kama chama ambacho kinajaribu kupambana na CCM hali wachezaji wake bado wanayumba hawana formation.
      Ukisoma kwa makini hoja zangu, sijasema kabisa kuwa kutumia helikopta ni makosa ila makosa yanakuja ktk upangaji wa hizi safari!.. One day ktk mkoa yaani una cover wilaya zote kwa mikutano ndicho nachosema sidhani kuwa ni wazo zuri na sababu zangu nazitoa. Nimewapa hata viji -mila vyetu vilivyo hai ambavyo hakuna kati yenu anavipinga - yet, bado mnazungusha hoja zenu kuipamba safari ya Freeman mikoani na kumwona Mkandara kuwa ni mpinzani.
      CCM hawafanyi makosa ktk hili, wameisha jijenga miaka kibao, na nyote mnalikubali hili. leo hii Chadema mtoto anayetambaa kutaka kufanya mambo kwa ushindani na CCM ni makosa!...
      Nimesema Chadema inatakiwa kuchukua muda mrefu kuwaelimisha wananchi kwa lugha yao. Na Chadema lazima waelewe kuwa wananchi wana NJAA kali... Je jinsi gani ya kumvuta mtu mwenye NJAA akusikie kuwa wewe ni mwokozi wake dhidi ya mazingaombwe ya CCM.
      Nabii Mussa aliyafanya hayo kuwavuta wa Misri kutokana na Imani ya Mungu Jua..baada ya kugeuza fimbo yake kuwa nyoka na kummeza nyoka wa Mfalme sio joho alilovaa ama jinsi alivyoingia Misri. Yesu aliyafanya hayo baada ya njaa kali kuwapa wavuvi samaki na baadaye kawapa mvinyo kupoza roho zao... Hawa wote Manabii, lengo lao kubwa halikuwa kuondoa njaa za hawa watu ila kufundisha neno la Mungu na walikuja fanikiwa kwa ktumia mbinu na lugha inayofahamika kwa wenyeji.
      Hivyo basi, kwa mtazamo wa mlalahoi, Freeman kuingia na helikopta ni moja ya kivutio, hii haina ubishi isipokuwa kama Freeman anakwenda kutoa hotuba tu na kuondoka... sidhani kama ataweza kuzivuta nyoyo za Wadanganyika..trust me hata mimi leo hii siwezi kuja huko na kukaa siku mbili eti ndugu na marafiki zangu wananielewa!...zaidi nitawajaza maswali mengi kuhusu mimi badala ya kujenga mioyo yao ya matumaini.
      Haya ni mawazo yangu mimi sii lazima yawe ndio ukweli bali nafikiria kuwa is the only correct way to deal with Wadanganyika.
      Kama mnakumbuka November mwaka 2005, niliwambia haya haya kuhusu Freeman na hiyo helikopta!...
      Tabasamu, nimezipata salaam za Freeman kabla kabisa ya hiyo helikopta!..Niliambiwa na wazee tena watu wa CCM kuwa Freeman ni tishio kubwa kwa sababu Freeman kaweza kile walichoshindwa Mrema na Lipumba... Freeman ni mchanganyiko wa Mtikila, Mrema na hata Lipumba kwa mbinu zake kwani amekuwa karibu sana na wananchi...Na waliendelea kudai kuwa kama CCM itafanya makosa ya kumweka mtu ambaye hana nuru ya wananchi wameumia... Freeman is the man.
      Alipoanza tu safari za Helikopta... CCM walipata mwanya!... problem yenu nyie mnashindwa kuelewa kuwa Bakhresa (CCM) anaweza kusafiri kwa ndege na familia yake wakamwelewa lakini mimi hapa Mkandara nikisha anza usafiri wa ndege hali sina kibanda wataniona mwendawazimu...
      sasa hayo ya kusema why not!... tutasema sana lakini ukweli unasimama kila mtu huvaa koti linalomlingana.
      CCM wanazo fedha na wataendelea kuiba...kinachotakiwa ni nyie kuwahakikishia wananchi huu wizi wa mazingaombwe kuondoa hizo imani zao za kuwa Chadema wana wivu...
      Mimi, wewe na wanabodi wengi humu tunayaelewa yote haya.. hata hilo swala la umeme la Richmond!... unadhani wangapi kweli wanalifuatilia kwa makini nakujali matokeo yake!.. Umeme umesharudi kutokana na mvua nyingi wananchi wameanza kulisahau na kuliweka nyuma!...Hapa kijiweni tumelizungumzia hili kuliko bungeni mara kumi!... viongozi wa upinzani ndio wamejificha kabisaaa!.. haya Freeman ndio yuko shule wakati anapohitajika zaidi...
      Sasa kampeni zenu zinakuja wakati umeme umesha rudi na wadanganyika wengi hawataweza kuamini kabisa kuwa mnachosema ni kweli na sio mbinu zenu zilizojaa wivu na uroho wa madaraka. Hivi ndivyo mnavyopambwa huko nje!....
      CCM wanaendelea na mazingaombwe yao ya kumeza sindano zinatoka noti!
      Ni lazima Chadema mfahamu mentality ya Mdanganyika!.. sio mimi Mkandara ambaye najaribu kuwakilisha mawazo ya wadanganyika!...
      Last edited by Mkandara; 1st January 2007 at 02:17.
      Exploration of reality

    17. #34
      Wacha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd November 2006
      Posts : 799
      Rep Power : 798
      Likes Received
      82
      Likes Given
      142

      Default

      Mkandra

      Unajua zile mbio za olympic za kuruka viunzi.

    18. #35
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default

      Wacha,
      Walaa sina urukaji viunzi ktk uandishi wangu, labda sema mbio za marathon. utasomaaa weee mwisho unasahau ulikoanzia! heee! hee! heee!..hilo halina shaka kabisa kwani Ikangaa hata siku moja hawezi mbio za mita 100, ni adhabu!

      Wacha, sikuweza kujibu maswali yako kwa sababu wewe mwenyewe hukunielewa nilichosema. PC ni kitu adimu sana na sikuzungumzia hilo bali TV, redio na magazeti. Kisha naowazungumzia mimi ni walalahoi wasiokuwa na uwezo sio graduates!..
      kuhusu UK nimekujibu sijui wapi bado! hata siku moja sikimbii maswali ila yangu huwa hayajibiwi isipokuwa washiriki hupandisha hoja juu yake!
      Mnasoma nayoandika na kutafuta kosa la kimaandishi not the message!
      Exploration of reality

    19. #36
      Jafar's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2006
      Location : Msoga, Chalinze
      Posts : 1,249
      Rep Power : 895
      Likes Received
      13
      Likes Given
      0

      Default

      Nimesikiliza kipande cha hotuba ya Mbowe alipokuwa Kagera juzi. Amenifurahisha aliposema kuwa atawafuatilia CCM ili waweze kutimiza ahadi walizoahidi na kuchaguliwa ili zisije kuwa zilikuwa ahadi "feki".I realy give him a big-up for that, 'cause I did not expected more than that.

      Lakini aliposema kuwa ameibiwa kura ndio maana akashindwa "to me was a nonesense urgument one year after election results on which him (Mbowe) conceded defit", kama hiyo ndio madhumuni ya kuruka kwake then he is wasting his time. Alitakiwa kwenda mahakamani kabla ya kutangazwa matokeo. Hivi lini waaafrika tukawa na utamaduni wa kukubali matokeo na kuanza kufikiria mbinu mpya za kushinda hapo mbeleni. Kama ni hivyo "Democtrats" in 2006 wasingemshinda "Bush" maana na wao waliibiwa kura 2005.

    20. Ole
      #37
      Ole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th December 2006
      Posts : 1,114
      Rep Power : 862
      Likes Received
      10
      Likes Given
      7

      Default

      Huyu mbowe mbabaishaji tu kama wengine. Tanzania itapata mabadiliko ya kweli pale tu kiwango cha elimu ya juu kitakapopanda vinginevyo ni hadithi za paukwa pakawa.

    21. #38
      Kitila Mkumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2006
      Posts : 3,919
      Rep Power : 6962
      Likes Received
      1065
      Likes Given
      35

      Default

      Ole: kweli unaamini elimu ya juu ndio itasaidia. Hii inanipa shida kwani sasa hivi wengi wenye hiyo elimu ya juu ndo mashabiki wakubwa wa system na sisiemu. Ukifanya uchambuzi wa support ndogo walio nayo wapinzani ni katika maeneo waliopo walalahoi wasio na elimu hiyo juu uliyosema. Mifano kama Temeke, n.k. Kuleta mabadiliko kwa Tanzania is more complex than we may think. Inakuwa ngumu zaidi pale ambapo watu wengi wanaoelewa wanakaa pembeni wakisubiri vyama vya upinzani viwe perfect! Hivi ni lini tutaamua kuwa ni sehemu ya hayo mabadiliko badala ya kukaa pembeni na kuangalia tu tukiwalaumu akina Mbowe? Kwa nini basi wengine tusijiunge na hivyo vyama ili tuchangie kuvifanya viwe 'perfect' badala kuwashambulia akina Mbowe tu kila siku?
      A Struggle Without Casualties is No Struggle-Steve Biko

    22. Ole
      #39
      Ole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th December 2006
      Posts : 1,114
      Rep Power : 862
      Likes Received
      10
      Likes Given
      7

      Default

      Unafahamu ni kama wewe mzee ulikuwa pale UDSM sasa unafanya ka PHD kwa nini? acha na wenzio wasiokuwa na hata kadegree kamoja wasome kama wewe na wengineo ndio tunakuwa kwenye level ground. Hata huyo Mbowe si ameona watu hawamsikii ndio maana anataka awe na kamshiko.

      kwa hiyo kisomo tu kiwe cha maana ili tuweze kupambana na mafisadi.

    23. #40
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,502
      Rep Power : 46710
      Likes Received
      16360
      Likes Given
      8419

      Default

      Ole, usiingie kwenye huo mtego.. waliosoma ndio hao hao mafisadi!! Unafikiri wala rushwa wakubwa wameishia darasa la saba?
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast

    Similar Topics

    1. Mbunge anapotumia muda mwingi kutoa shukrani
      By Makene in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 18
      Last Post: 5th July 2011, 00:04
    2. Napenda kutoa shukrani kwa hawa wafuatao.
      By Slave in forum JF Doctor
      Replies: 4
      Last Post: 28th February 2011, 00:07
    3. Replies: 1
      Last Post: 8th November 2010, 14:13
    4. Eti soko la """kitimoto ""kuanza kupungua kuanzia kesho""
      By Pdidy in forum Celebrities Forum
      Replies: 2
      Last Post: 11th August 2010, 11:27
    5. Mashindano ya Umisseta kuanza kesho
      By Balantanda in forum Sports
      Replies: 0
      Last Post: 27th June 2009, 02:16

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...