Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Pinda na Makinda wameshindwa kutimiza wajibu wa waziri mkuu na Spika bungeni

    Report Post
    Results 1 to 5 of 5
    1. #1
      Watanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th July 2009
      Posts : 730
      Rep Power : 653
      Likes Received
      34
      Likes Given
      4

      Default Pinda na Makinda wameshindwa kutimiza wajibu wa waziri mkuu na Spika bungeni

      Kwa waliomwona na kumsikiliza Pinda akielezea kuhusu mauaji ya Arusha watahitimisha bila shaka yoyote kuwa ni mnafiki na ana tabia inayofanana na Paka. Anaoongea mambo yasiyothibitishwa huku amepindisha mwili na shingo upande mmoja na kuonyesha sura ya kutaka kuonewa huruma kama njia ya kuwahadaa watu wakubali anachoeleza. Chadema walimtega Pinda, kwa unafiki wake akalieleza bunge eti wenye makosa ni Chadema huku akijua kuwa kesi ya mauaji ya Arusha iko mahakamani. Kama Pinda asingekuwa mnafiki basi angeacha kujibu maswali kuhusu mauaji ya watu Arusha yaliyofanywa na Polisi kwa kuwa suala hilo liko mahakamani. Pinda alitakiwa akatae kama Makinda alivyokataa hoja ya Dowans kwa kisingizio cha eti kesi iko mahakamani. Ndiyo, ni visingizio tu vya kulinda mafisadi kwa sababu kamati ya wabunge wa CCM hivi karibuni ilijadili suala la Dowans na kuiambia serikali ya CCM isiilipe Dowans ya Rostam huku suala hilo likiwa mahakamani tayari. Kwa nini Makinda anakataa Dowans isijadiliwe bungeni wakati wao CCM wamelijadili katika kamati ya wabunge?

      Kwa upande wake Pinda anataka watanzania waamini kuwa Polisi wa CCM hawakuua raia wasiokuwa na makosa Arusha huku akijua kesi iko mahakani. Ni mara ngapi polisi wanaua raia na kushiriki katika ujambazi?. Je hajui kuwa hivi karibuni kwa mfano kuna askari Polisi aliyempiga risasi dereva wa teksi na kumnyanganya gari kisha kwenda kupora pesa kituo cha Mafuta huko Arusha?. Hajui kuwa Polisi wa CCM wanashiriki uhalifu kama walivyo majambazi? Kwa hiyo Pinda anaishawishi mahakama ihukumu kuwa Polisi hawakuua bali wenye makosa ni Chadema, je huku si kuingilia uhuru wa mahakama? Makinda naye anafoka na kuonyesha chuki kwa Chadema huku amekalia kiti cha uspika. Anahamaki kama mama anayemfokea mtumishi wa ndani kumbe anamtetea Pinda. Kwa hiyo Makinda anaungana na Pinda kuishawishi mahakama kuwa Chadema ndiyo wenye makosa. Hivi ni tabia gani ya spika kuhemkwa, kufura na kuwafokea Wabunge hasa wa Chadema kana kwamba anashughulika na mambo ya nyumbani kwake?. Kwa hakika tabia ya Makinda haiendani na cheo cha uspika na Watanzania tumshauri ajiuzuru uspika kabla hajaendelea kuliharibu zaidi bunge. Bunge la Sitta ndiyo lilikuwa bunge la maana kwa Watanzania, hili la Makinda naona ni la kutetea Mafisadi tu. Tabia mbaya ya Pinda na Makinda kutetea mafisadi na uovu wa serikali inatisha na inazidi kuota mizizi. Clip ya video yaweza kuthibitisha kuwa Pinda kweli ni mnafiki na anatabia ya paka, na kwamba Makinda ana chuki kwa Chadema na Watanzania, chuki iliyopitiliza na wanalinda mafisadi hata kushindwa kutimiza wajibu wao wa uwaziri mkuu na uspika.
      Last edited by Watanzania; 11th February 2011 at 08:44.

    2. #2
      Watanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th July 2009
      Posts : 730
      Rep Power : 653
      Likes Received
      34
      Likes Given
      4

      Default Re: Pinda na Makinda wameshindwa kutimiza wajibu wa waziri mkuu na Spika bungeni

      Quote By Watanzania View Post

      Mods naomba msaidie kuhariri aya ya pili ili herufi zifanane na za aya ya kwanza.

    3. #3
      Gad ONEYA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th October 2010
      Posts : 2,552
      Rep Power : 953
      Likes Received
      125
      Likes Given
      574

      Default Re: Pinda na Makinda wameshindwa kutimiza wajibu wa waziri mkuu na Spika bungeni

    4. #4
      DMussa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2007
      Location : Dar es salaam
      Posts : 931
      Rep Power : 786
      Likes Received
      27
      Likes Given
      19

      Default Re: Pinda na Makinda wameshindwa kutimiza wajibu wa waziri mkuu na Spika bungeni

      Hebu tupe kesi iliyoko mahakamani ni ipi? Je ni ile ya viongozi wa Chadema kushitakiwa kwa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano au ni kuhusiana na mauaji? au ni zote?
      It is not the strongest species that survive, nor the most intelligent, but the ones most responsive to change - Charles Darwin

    5. #5
      Mzalendo80's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2010
      Location : Magogoni, Tanganyika
      Posts : 2,280
      Rep Power : 964
      Likes Received
      822
      Likes Given
      1589

      Default Re: Pinda na Makinda wameshindwa kutimiza wajibu wa waziri mkuu na Spika bungeni

      Ikiwa chama chao kimeshindwa kuleta maendeleo ya nchi unategemea hao 2 wataweza tena wajeuri kama Fisadi Kikwete[/B]
      The CCM is a crime syndicate, Most members and MPs of CCM are corrupt. No conceince, No brains no nothing, just bunches of criminal and theft. Corruption cost mlalahoi in de street.

    Similar Topics

    1. Spika Amuonya Waziri Mkuu Bungeni
      By tatanyengo in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 54
      Last Post: 16th August 2011, 08:17
    2. Replies: 10
      Last Post: 2nd July 2011, 10:04
    3. Waziri akishaisoma hotuba bungeni, bunge haliwezi kubadilisha kitu-Spika makinda
      By tanga kwetu in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 10
      Last Post: 26th May 2011, 10:30
    4. Replies: 7
      Last Post: 23rd February 2011, 21:54

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...