| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
|
#1 | |||||||||||
|
||||||||||||
|
Views: 4540
|
||||||||||||
|
#2
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Ndg Mkono,
Pongezi, umeongea vema sana, however, ulikuwa wapi siku Bi Maua Daftari aliposema mikataba ni SIRI?, tulitegemea watu Wanasheria kama ninyi (Mliobobea + Mbunge) kupiga sana kelele kuhusu kauli ya Daftari,............. wanasheria mna usemi wenu "silence means YES" sasa naona UNAPIGIA KELELE END RESULT baada ya kukubali kilichosemwa bungeni!!!. mimi nikiwa mmoja wa wanachi wako tuliokupa kura nachelea kuona unachosema ni honest! Kama unasoma hii forum, tafadhali panga mikakati ya kupeleka hoja Bungeni ili wabunge kama ninyi muwa na nafasi ya kui-review mikataba kw amanufaa ya sisi wananchi |
|
#3
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Huyo Mbunge ambaye ni mwizi mkubwa wa mali ya serikali anapaswa kuwa mtu wa mwisho duniani kuongelea mambo ya wizi, huyu ambaye kila siku anafanya mipango ya ujanja kupewa tenda za serikali za sheria na kui-over charge serikali kwa kugawana na mawaziri leo anaweza kuthubutu kuwatukana viongozi wa manispaa? Ama kweli nyani haoni his behind?
Hela za kuilipia ile ndege aliyomkodishia mgombea mmoja wa urais wa CCM kuzunguka bongo nzima kutafuta signatures, alizipata wapi? Kama kawaida wananchi wa bongo wataendelea kudanganywa tu na waizi kama huyu! |
|
#4
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mzee Es,
Samahani mkuu lakini, kuna kuna wakati nashindwa kuelewa kama kweli wewe ndiye Mzee Es aama kuna mtu anatumia jina lako. Nakuona umepooza sana kwa hoja mzee vipi umeishiwa? Swala hapa ni hili la Barricks Gold na uhalali wa viongozi wetu kukubali kupokea hizo dola laki 2 kama ruzuku kwa halmashauri hali fedha hizi hazikupigiwa hesabu ya kimapato kama inavyotakiwa. Huyu mbunge hata kama anayo mabaya yake hii ni kesi nyingine kabisa na unaweza kuiweka hapa tukaijadili kwa mapana lakini kuchukua hoja kwa kutazama nani kasema sidhani kama ni mwendo mzuri. Labda mwenzetu unakubaliana na mikataba ya madini na vizuri utuambie hayo mazuri yake nasi tupate kuona ukichaa wa huyu mbunge.
__________________
Exploration of reality |
|
#5
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mzee ES, Mkono ni tajiri toka siku nyingi ana kesi ntinyi za kimataifa ana hela siyo kwa kuibia nchi. Ni kweli kama alivyosema Mkandara wakati mwingine unamchesha siyo kwa kutojua ila tu kwa chuki zako binfasi na kundi la mwalimu!
sijui mwl na kundi lake walikukosena nini?? Hivi kweli mambo anayaofanya mkono jaribu kwenda uone katika jimbo lake ! ni mkono huhyu huyu alieyatamka wazi bungeni waktai wa awamu ya Mkapa na kukemea kuhusu uuzwaji wa nyumba za serkali lakini wabunge wengine wote wlaikaa kimya! ninamnukuu" alisema mimi siyo mjamaa lakinini kwa hili la uuzinaji wa nyumba za serkali kana kwamba baadaya ya hii serkali hakutakuwa na serkali nyingine au tunaenda mbinguni ni ajabu kubwa na inatia shaka kama kweli nyie ni wajamaa!! Mzee ES tunaheshimu michango yako lakini jaribu tu kidogo kupunguza upenze na chuki zisiso za maana utakuwa kiongozi mzuri hapa kazi yetu ni kufundishana na kukosoana! Mimi Mkwa sasa nimeongia kwa nguvu mpya katika hii Formu ninaipenda kwa sasabu nimeona kuna watu wenye tofauti katika mitizamo na michango yao wote ni mizuri. |
|
#6
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mwakapungi unasema kweli? au na wewe ni mmoja wao!
http://www.ippmedia.com/ipp/guardian.../03/69547.html Huyo Mkono tumeskia kazi zake, sasa hilo la deal za kupata kesi mimi silijui ila tu kama alivyosema Mkwawa insemekana jamaa anapta international case. Hilo la kutoa la kutoa hela wakati wa Kampeni tukianza kuulizana hapa itakuwa kazi wenye katika CC ya CCM liliwashinda! Kikwete alitumia Kiasi gani alipta wapi? Malecela alikodi ndge alipoulizwa alisema rafikia yake alimlipia! hilo ninadhani tuliache kampeni zimeisha na makundi yaishe taratibu japo walioshindwa itawachukua miaka 20 kukubali!
__________________
"True peace is not merely the absence of tension, it is the presence of justice'' Dr.Martin Luther King Jr |
|
#7
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Hebu nijaribu kuwaelewa wazee,
Mwizi mmoja kwa sababu akiiba anawasaidia wananchi, na kwamba anapewa njia za kuiba mpaka nje ya nchi kwa kuwatumia viongozi wetu wa nchi na kugawana nao, na kwamba ameanza kuiba siku nyingi, basi it is ok kwake kuwatukana wezi wengine wa serikali wadogo wadogo! Mkandara ni kweli bro kuwa sasa wewe ndiye bingwa wa issues na maneno yako humu kwenye hii forum ndio ukweli wenyewe, lakini samahani, ninamjua Mkono tena na deal zake zote, Mkono ni another bongo Mafiya kama Mtandao nilishamzungumza toka BCS, na sikukusikia ukisema kitu, two wrongs haziwezi ku-make right, Mkono ni mwizi kama hao anaowapigia kelele na anapaswa kuwa mtu wa mwisho kuwauliza wezi wenziwe nuless kama hakupata mgawo kwenye hayto madini! Hayo maneno mengine nimeyazoea that is why I am ES! |
|
#8
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mzee ES,
Be that it may that Mkono is a thief. Does that take away anything in his message? Should he just keep quiet and watch these foreigners continue to plunder our wealth. Like Mkandara says we can debate Mkono's thievery in another forum. Let us focus on his message for now. |
|
#9
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mzee Es,
Siku zote wewe bingwa ktk kuendesha hoja ndani ya mada. Na mara kadhaa nimeona watu wakitaka kutafsiri hoja zako nje ya mada kwa sababu umehusisha mtu wasiomtegemea ndani ya mada husika. Kwa mtazamo huo nimekuwa nikikubaliana nawe kwa sababu walitaka kukutoa nje ya mada. Kwa hiyo binafsi huangalia mada yenyewe, hoja inayohusika kisha huitazama shilingi yangu kwa malengo ya kutafuta reality ama correct way ya ku-deal na swala hilo. Mara nyingi nimejikuta nakubaliana na wewe kwa sababu hizo hizo na sio swala la Right or Wrong! kwani hatupo kanisani wala msikitini hapa. Lakini hapa Mzee Es kidogo umetoka nje. Wana mtandao umewasema sana kwa mabaya na mazuri yanayotokea ndani ya hoja ama mada yenyewe. Wengine tumeshindwa kuamini hadi yalipotokea kweli. Kwa mfano hapo zamani ungesema mambo kibao ya MKONO yanayohusu yeye na madini na jinsi alivyotaka kuwafanyizia watu wa Mara. Ama uhusiano wa Mkono na Jambazi fulani la madini.
__________________
Exploration of reality |
|
#10
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
WanaTEF,
Nionavyo afadhali ya huyu Mkono anayeiba kisha kurudisha baadhi kwa wananchi kuliko hao manyang'au mengine kama Mahalu. Alichokemea ni sahihi na hili alilianzia toka siku ya kukabidhiwa hizo hela. ES kutofautiana ni jambo la kawaida miongoni mwa watu, Unaweza kuwa upo sahihi lakini sio kwenye hii mada. Nami naungana na wengine kusema umeteleza kidogo na kutoka nje ya mada. FD
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 01:29 AM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||