Buchanan, namkubali Prof. Mvingi kama msomi wa sheria aliyebobea kama ambavyo nitamkubali Prof. Mwakiembe, ila sizikubali comments zake kwenye baadhi ya issues kwa sababu yeye Mvungi, ameshajipambanua kushiriki siasa, na ndivyo ambavyo Prof. Mwakiembe atakavyo jipambanua kulinda mauza uza yote ya CCM.
Honest opinion kwenye hili, inatakiwa kutoka kwa wanasheria independent kama Prof. Shivji.
Kusu Zanzibar kuwa nchi ndani ya nchi, nilisema yafuatayo,
Zanzibar na Tanzania ni kama Baba na mwana. Wewe ndiye baba, unaitwa baba kwa sababu ndiye mkuu wa kaya, bread winner mwenye mamlaka yote.
Inapotokea mtoto wako umpendaye akaanza kulia kutwa kucha kwamba kwa nini ni wewe tuu unaitwa baba, na yeye anataka lazima aitwe baba, na kuendelea kulia kwa makelele mpaka unakosa amani, lakini wife alipomwambia 'nyamaza baba', ghafla alinyamaza na kuanza kufurahi sana, na yeye ameitwa Baba!, akamwambia mama na mimi ni baba. Jee wewe baba wa ukweli, utakasirika au kununa kuwa mwanao amechukua nafasi yako ya kuitwa baba, ama na yeye anataka kuitwa baba jina tuu lakini sio baba chochote, kwa vile powers za ubaba hana!.
Ndivyo ilivyo kwa JMT, Zanzibar kwanza walianza kwa kuomba bendera yao, wakapewa, kisha wakaomba wimbo wao wa taifa, wakapewa, kisha wale wagambo wao, (KMKM na JKU) kumpigia saluti rais wao, wakapewa, ndipo juzi wakajitwalia jina la 'nchi' na kuliingiza kwenye katiba ya Zanzibar ili hali kwenye katiba ya JMT, Zanzibar sio nchi ni sehemu tuu ya JMT. Jee JMT inasababu wa kuwakatalia kujiita majina yoyote inayoyataka hata wakiuita Falme za Zanzibar na kiongozi wao akawa Sultani Seif/Shein etc.
Zanzibar ni nchi kweli kama Zanzibar ndani ya Tanzania, kama mwanao atakavyoitwa baba ndani ya nyumba yenu, lakini nje ya nyumba, mwanao ni mtoto tuu, hana ubaba wowote mbale ya macho ya umma, ndivyo ilivyo nchi hii mpya ya Zanzibar, ni nchi jina tuu, haina uinchi yoyote mbele ya mataifa, ni nchi jina isiyo na nguvu zozote za dola. Sasa unamashaka na jina tuu?.
Zanzibar nchi jina!.
Follow Us Here