Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

    Report Post
    Page 4 of 5 FirstFirst ... 2345 LastLast
    Results 61 to 80 of 99
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,266
      Rep Power : 3568
      Likes Received
      3074
      Likes Given
      464

      Default Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli










      Stori: Makongoro Oging'

      SERIKALI imethibitisha kuwa kitendo alichokuwa akifanya babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Masapile, cha kutoa dawa ya kutibu magonjwa, ukiwemo Ukimwi aliyokuwa amedai kuwa ameoteshwa na Mungu ni cha kitapeli.


      Utafiti umebaini kwamba dawa hiyo ya babu wa Loliondo ni feki na kwamba haina uwezo wa kutibu Ukimwi wala kisukari.


      Kwa mujibu wa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (pichani), utafiti wa kulinganisha wagonjwa wa Ukimwi na kisukari waliokunywa dawa hiyo na wale ambao hawakunywa, umebaini kwamba hakuna utofauti wa afya ya mgonjwa.


      Alisema utafiti huo unafanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), ulianza Machi mwaka huu na kwamba unahusisha wagonjwa 200 wanaofuatiliwa kwa kupimwa damu, kinga ya mwili (CD4) na uzito wa mgonjwa, ambao ulifanyika tangu mgonjwa alipokunywa kikombe cha babu.


      “Matokeo ya awali ya utafiti yameonyesha kuwa hakuna utofauti katika vipimo vya kimaabara pamoja na damu, CD4, uzito na ubora wa afya ya wagonjwa kati ya waliokunywa na wale ambao hawakunywa dawa ya mchungaji,” alisema Dk. Mwinyi.


      Alisema lengo la utafiti huo ni kubaini uwezo wa dawa hiyo katika kutibu magonjwa aliyosema dawa yake inayatibu ili kuona kama kuna utofauti wowote baada ya mgonjwa kutumia dawa.


      Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini limesema kwamba linafuatilia kwa makini sakata la Mchungaji Masapile anayeishi katika kijiji cha Samunge mkoani Arusha kufuatia malalamiko ya wananchi kuwa licha ya dawa yake kuonekana haitibu, bado watu wanakwenda na kunywa.


      Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni ofisini kwake makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso, amesema kwamba kutokana na malalamiko hayo polisi watawasiliana na wizara ya afya ili kuchukua hatua stahiki.


      Msemaji huyo amesema kwamba wanataka kujua kama wizara ya afya imepiga marufuku dawa hiyo au inasema nini baada ya kubainika kuwa haitibu na amewataka wananchi kutoenda huko.


      Wananchi wengi waliozungumza na gazeti hili wamedai kwamba Babu amewatapeli wananchi na kinachowauma ni kuona kuwa kuna watu wanaendelea kwenda kunywa kikombe japokuwa hawatangazwi.


      “Wananchi wengi waliuza mali zao na kukimbilia kwa babu kupata tiba, kumbe ulikuwa ni utapeli, ukweli ni kwamba serikali imechelewa mno kutoa tangazo hili,” alisema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la John.


      Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyama vya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini (TAMOPHA), Julius Kaaya, ameitupia serikali lawama kwa kuipigia debe dawa ya Babu na kuwafanya wagonjwa kutoroka hospitali huku wengi wao wakiacha kuendelea na dawa wakiamini wangepona baada ya kunywa kikombe kimoja .


      “Huyu Babu inatakiwa ashitakiwe apelekwe mahakamani afilisiwe mali zake zote alizochuma toka kwa wagonjwa na ikiwezekana afungwe ili iwe fundisho kwa watu wengine,” alisema Kaaya na kuongeza kuwa wao wanajiandaa kumfungulia kesi.


      Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste (TAG) Mkoani Arusha, Steve Wambura, amemtaka babu huyo amrudie Mungu kwa kutubu kuwa aliwatapeli wananchi.


      Naye Mwenyekiti wa Waganga wa Tiba Asili Mkoa wa Dar es Saalam, Maneno Tamba, amesema babu huyo siyo mwanachama wao na walishangazwa na serikali kumpigia debe, hali iliyosababisha vifo vya watu wengi waliomkimbilia na kuacha tiba sahihi.


      Baadhi ya mawakili, akiwemo Mabere Marando wamesema kwamba wapo tayari kumfikisha mahakamani babu huyo wakijitokeza waliotapeliwa na watamfungulia kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
      Losomich likes this.

    2. RukaaJuu Final

    3. #61
      Mu-Israeli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2012
      Location : Jerusalem
      Posts : 1,197
      Rep Power : 601
      Likes Received
      427
      Likes Given
      187

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Vyombo vya habari navyo havikuwa nyuma kupigia debe 'dawa' hiyo ya kitapeli ...

      Angalia article hii kwenye Guardian la 29th march 2011.

      'Babu' cupful gets initial nod

      By Patrick Kisembo


      29th March 2011




      The concoction has no harm on human beings - researchers
      PM: Govt to create conducive environment for pastor`s services




      Retired pastor Ambilikile Masapile


      Ministry of Health and Social Welfare has endorsed the “miracle cure” administered by retired pastor Ambilikile Masapila (his proper names) as fit for human consumption, adding however that efficacy tests were going on.
      “It is a long process which cannot be completed in a short period of time,” said Tanzania Food and Drugs Authority Acting Director General Charys Ugullum when unveiling results of the laboratory analysis on the sample of the “miracle cure” to journalists in Dar es Salaam yesterday.
      “The investigation which has been conducted so far has yielded satisfactory results that the measurement used by “Babu” in dispensing the concoction is not harmful to human beings,” she said, adding: “So far we are satisfied by its safety.”

      She however said that the researchers were continuing with investigation into whether the herbal medicine can cure the five diseases as claimed by pastor Masapila.
      “This task, implemented according to world scientific rules and regulations, takes a long time to achieve acceptable national and international standards,” Ugullum said.
      She said the researchers were also following up on the health of some 200 patients who have taken the herbal medicine.
      “These patients have volunteered to be involved in the investigation to know their health status after taking the medication,” Ugullum said.
      She said the government was planning to make a follow up on the use of the “treatment tree” in other parts of the country because there were reports that it has been used by other tribes like Wagogo, Maasai, Wabarbaig and Wasonjo.
      The investigation team included people from TFDA, Muhimbili University for Health and Allied Sciences, Government Chemist and National Institute for Medical Research (NIMR).
      "Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi. " - Yakobo 04:17

    4. #62
      mito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th June 2011
      Posts : 1,051
      Rep Power : 611
      Likes Received
      445
      Likes Given
      1354

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Quote By Tram Almasi
      Hapo kwenye red hapoo, ina maana hata watafiti wa NIMRI na wengine wamepata false results kwa kuwa wameipeleka dawa nje ya eneo husika. Na je, walipoichukua kwa ajili ya utafiti walipata ruhusa ya babu?
      We umenichekesha sana ndg yangu, loh!
      Haki ya mtu haipotei, inacheleweshwa tu!

    5. #63
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7663
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Nchi ya Wajinga huongozwa na wajinga na hutapeliwa viile vile.. Tuliyasema haya toka mzee huyu alipojitokeza watu wakatuona wajinga.

      Sasa ebu jiulizeni ni viongozi wangapi walienda Loliondo wakapa kikombe, halafu mnataka kuongozwa na kundi la watu wanaoamini sana uchawi na Utapeli wa watu wanaodai kwamba wao wako karibu sana na Mungu na mkawaamini..

      Umaskini wetu sio bure, sisi kichwani hamna kitu..
      Ruge Opinion likes this.
      Exploration of reality

    6. #64
      mito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th June 2011
      Posts : 1,051
      Rep Power : 611
      Likes Received
      445
      Likes Given
      1354

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Quote By distazo
      Afadhali imedhihirika hivo,nilikosana na jamaa zangu kwa kuwaambia huu ni utapeli tu.
      mi nusra nikosane na mama yangu kwa kumnyima nauli ya kwenda kwa babu, sema baadae nilikubali yaishe nikampa
      Haki ya mtu haipotei, inacheleweshwa tu!

    7. #65
      majorbanks's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd February 2012
      Posts : 148
      Rep Power : 398
      Likes Received
      37
      Likes Given
      3

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Serikali inakumbuka styles za kucheza muziki wakati disco linaisha na kufungwa...!!

    8. Miaka 50

    9. #66
      Tram Almasi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 26th February 2009
      Location : Marsabit
      Posts : 753
      Rep Power : 672
      Likes Received
      217
      Likes Given
      92

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Quote By mito
      We umenichekesha sana ndg yangu, loh!
      Mkuu Mito,Manake tulishaambiwa kwamba dawa ikitoka nje tu, batili!Kwa hyo hata utafiti ilibidi ufanyikie palepale eneo la tukio tu! hahahaha
      mito likes this.
      "YouR MoST UNhaPPy CuSToMers ArE YoUr GREateST SOurCE Of LEarNInG"- BiLL GaTEs

    10. #67
      Tram Almasi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 26th February 2009
      Location : Marsabit
      Posts : 753
      Rep Power : 672
      Likes Received
      217
      Likes Given
      92

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Quote By Mu-Israeli
      Hilo sharti la 'kutotoka na dawa nje ya Loliondo' ndio lilikuwa sharti kuu la kuwezesha wagonjwa 'kupona'.
      Hapo ndio uongo wake ulipokuwa wazi kabisa.
      Watu ilibidi washtuke hapo, maana, haiingii akilini kusema kuwa 'dawa' haifanyi kazi nje ya Loliondo, halafu dawa hiyo-hiyo ichukuliwe ikachunguzwe nje ya Loliondo !!
      Hatimaye, NIMR wakatoa tamko kuwa 'dawa' haina madhara !!
      NIMRI na hata TFDA were right kusema dawa haina madhara kwa sababu haidhuru. lakini uwezo wa kutibu (pharmacological efficacy) ndio ''zero'' Mkuu.
      "YouR MoST UNhaPPy CuSToMers ArE YoUr GREateST SOurCE Of LEarNInG"- BiLL GaTEs

    11. #68
      Tikerra's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd September 2008
      Location : Morogoro
      Posts : 1,588
      Rep Power : 864
      Likes Received
      100
      Likes Given
      3

      Default

      Quote By Kakulwa P
      Huyo mchungaji aliwatahadharisha wananchi kuwa wasiache kutumia madawa yao ya hospitali. Kwa uzembe wa Serikali na wakapuuza ushauri wake wa katazo wakaenda kwa kasi kubwa. Leo wasimulaumu kwa kuwa alitoa tahadhali sisi watu makini hatukwenda, lakini pia bei ya dawa yenyewe ilitia mashaka. Wamuache babu wasimuletee shida, maana hata Prof. Maji Marefu baada ya kutapeli watu sasa hivi ni Mbunge mbona hamjapiga kelele. Serikali DHAIFU.
      Wajinga ndio waliwao.
      Mkandara likes this.

    12. #69
      Ruge Opinion's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd March 2006
      Location : DAR ES SALAAM
      Posts : 1,058
      Rep Power : 890
      Likes Received
      149
      Likes Given
      79

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Bado upumbavu anaendelea.

      Hivi Babu alikuwa anatoa risiti kwa waliokunywa 'Kikombe' chake? Unawezaje kuthibitisha kuwa ulikuwa mteja wake?

      Pili, kuna aliyelazimishwa kwenda Loliondo? Babu wala hakutoa matangazo mahali popote. Watu walimfuata nyumbani kwake kwa hiari zao. Na aliwaonya kuwa dawa yake inaendana na imani. Sasa kama hamkupona kwa kukosa imani yeye angefanyeje?

      Waliokwenda kwa Babu nyote mgeona aibu, kufunga midomo yenu na kuficha nyuso zenu kwa sababu ni wapumbavu. Sina nia ya kutukana mtu ila ni kuelezea hali.

      Wa kushitakiwa ni watu wakubwa kama mawaziri, wakuu wa mikoa hata maaskofu, ambao walishabikia na kwenda huko bila kuwa na ushahidi wowote kuhusu hiyo dawa. Wao ndiyo walitoa mfano mbaya na kuzidi kuhamasisha watu.
      Mkandara likes this.
      Loosing is a starting point to success

    13. #70
      kichomiz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 4,053
      Rep Power : 1232
      Likes Received
      652
      Likes Given
      80

      Default

      Quote By Ritz
      Mkuu Babu wa Loliondo ni Tapeli hakuna mtu aliyepona.
      "Ni vihele hele vyao tu viliwapeleka"

    14. #71
      Cynic's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th January 2009
      Location : Around
      Posts : 2,153
      Rep Power : 967
      Likes Received
      317
      Likes Given
      186

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      wa kulaumu ni pamoja na viongozi wa serikali na wa ccm (jk, salma, el, lusinde, makamba, kandoro, mwigulu, etc. ) ambao pamoja na wake zao walishiriki ktk kufanikisha huu utapeli kwa kunywa `uchafu ` huo. inasemekana lengo lilikuwa ni kuondoa habari za cdm kwa muda kwenye media outlets zetu
      '... Knowledge is good, but wisdom is even better ...'

    15. #72
      egbert44's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th March 2006
      Location : city center
      Posts : 334
      Rep Power : 742
      Likes Received
      26
      Likes Given
      12

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Babu kateseka sana maisha haya, katuliza kichwa kaja na mchongo wake makini wa uzeeni mnaanza kumletea gozigozi acheni zenu kwani Hosea yeye sie polisi mbona kalambishwa kikombe, nasikia mpaka mkuu wa kaya kalamba na hajadondoka tena jukwaani........ yaoneni kwanza!
      Jmpambije likes this.

    16. #73
      Smallfish's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th February 2012
      Posts : 112
      Rep Power : 389
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      maarifa ya Mungu huanzia kwenye upumbavu wa mwanadamu. Swala la imani lilithibitishwaje maabara?siku za kuishi za watu waliokunywa dawa je, zilirekodiwa kabla ya kunywa dawa ili zilinganishwe kama ziliongezeka ama kupungua?

    17. #74
      Moitalel's Avatar
      Member Array
      Join Date : 8th May 2010
      Posts : 60
      Rep Power : 471
      Likes Received
      2
      Likes Given
      1

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Hahahaha!!! babu katoka

    18. #75
      Ndogue Ndogue's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th July 2012
      Posts : 14
      Rep Power : 348
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By FJM
      Ingekuwa kwa wenzetu serikali nzima ingeachia ngazi. Huwezi kuachia watu watumia dawa then baadae ndio unasema ni utapeli!
      Ni kweli ndugu.Viongozi wangapi wa serikali walienda kunywa dawa hiyo na wakaipigia debe,leo babu ndio mwenye makosa.SERIKALI HII YAANI NI DHAIFU SANA.Hawataki kuboresha huduma za afya ili kuhalalisha watu wakaliwe na waganga wa kienyeji.

    19. #76
      Jmpambije's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th April 2008
      Posts : 85
      Rep Power : 583
      Likes Received
      12
      Likes Given
      30

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Quote By egbert44
      Babu kateseka sana maisha haya, katuliza kichwa kaja na mchongo wake makini wa uzeeni mnaanza kumletea gozigozi acheni zenu kwani Hosea yeye sie polisi mbona kalambishwa kikombe, nasikia mpaka mkuu wa kaya kalamba na hajadondoka tena jukwaani........ yaoneni kwanza!
      Mkuu hapo nakubaliana nawewe, sioni kosa la Babu, hakulazimisha mtu yeyote kumfuata na bado waliomfuata aliwataadhalisha. katusaidia kutuelewesha aina ya watu tulionao katika nchi yetu.

    20. #77
      Ernesto Che's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th January 2011
      Posts : 566
      Rep Power : 538
      Likes Received
      94
      Likes Given
      21

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Quote By Ritz
      Mkuu mbona ueleweki kwa hiyo Babu wa Loliondo ni Chadema...unapinga kuwa sio tapeli?
      utapeli si tapeli ila watu walikurupuka alisema ni imani. Hata kanisani kuna maji ya baraka kwani na hayo tyanatibu? ila kwa imani mtu apona
      "If there is no struggle, there is no progress.”

    21. #78
      Mwanaweja's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th February 2011
      Posts : 3,483
      Rep Power : 1116
      Likes Received
      470
      Likes Given
      962

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      serikali ndio ilifanya makosa na ndio imesababisha watu wengi wafe kutokana na dawa ya babu maana mpaka mawaziri walienda kupata kikombe na pengine hata jk aliletewa ikulu kwa siri siri

    22. #79
      kibogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Location : MBEYA
      Posts : 1,717
      Rep Power : 701
      Likes Received
      432
      Likes Given
      320

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Mambo yanayokwenda kiimani ni vigumu kuchukuliwa hatua za kisheria wengi wanadanganya au kwa kuwa hawatoi dawa mfano Kakobe, Lusekelo na wengineo kwa nini nao wasichukuliwe hatua kwa kutapeli juu ya kutibu watu UKIMWI kwa maombezi wakati sio? Mzee wa Gombe, Nkono na viongozi wengi sana wa Taifa hili walikunywa dawa hiyo tunasikia na mkuu wa kaya pia sasa isiwe wanataka kumuadhibu babu wa watu kwa sababu ya uzembe wao wenyewe wa kujipeleka na kunywa hiyo dawa.

    23. #80
      kaangwa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th January 2011
      Posts : 121
      Rep Power : 445
      Likes Received
      39
      Likes Given
      37

      Default re: Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

      Quote By Amiliki
      Kweli hapa Serikali Hatuna. Yaani kama ingekuwa ni sumu mpaka leo ndio serikali inastuka, je wangekuwa watu wangapi wamepoteza maisha?
      Mkuu malizia tu kwamba viongozi wetu walikunywa sumu,maana karibia serikali yote ilikwenda huko na kupata kikombe kwa uthibitisho huo wa serikali inamaanisha viongozi wetu wa nchi walitapeliwa.Kweli serikali DHAIFU haina maono,waziri wa afya hata kama utafiti wake ni kweli angekaa kimya kumtunzia heshima mkubwa wake wa kazi.

    Page 4 of 5 FirstFirst ... 2345 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...