Re: Diplomatic passports za Tanzania zinatolewa kama njugu
sasa kipi cha kustajaabisha hapo?
Kinje ana diplomatic passport ndio itakuwa huyo PRESHA INAPANDA, PRESHA INASHUKA
Mie sikuhizi huwa hata sishangai nikisoma habari kama hizi
sitoshangaa kama yule bosi (mYemen) wa Home Shopping Centre naye ana diplomatic passport na hasa baada ya kumwona Mange Kimambi anatumia VIP pale airport.
hii ndio nchi ya kufikirika iliyokosa ADILI NA NDUGUZE
Re: Diplomatic passports za Tanzania zinatolewa kama njugu
By Don Draper
Hivi mnaweza kuamini kuwa wabunge wote (inluding wale wa kuteuliwa ambao idadi yao inafika almost 150) wanatembea na pasi za kiplomasia?
Lakini kilichonistajaabisha ni kuwa wabunge wa nchi zingine wanatembea na passports za kawaida tuuu
Can you imagine mtu kama kepteni John Komba eti naye anatembea na diplomatic passport
Hivi wizara husika kwa nini haitoi mwongozo wa mambo haya?
Mkuu,
Miongozo ipo tena iliyoshiba tu na nafikiri watu wa Foreign Affairs wanaona hii.
Diplomatic passport hutolewa kwa watu ambao husafiri mara kwa mara kwenda nje ya nchi kwa safari ambazo zinahusiana na shughuli za kiserikali wakiwemo wabunge.
Pia kulingana na mazingira fulanifulani watu wengine ambao wanahusiana na hao unaowasema wanaweza kupatiwa passports hizo, watu kama ndugu wa karibu au familia.
Ila ikumbukwe kwamba diplomatic psssport haisaidii kila mbebaji wake kupewa kinga (immunity) dhidi ya madai yoyote yake yahusianayo na uvunjwaji wa sheria.
Wabebaji wa passports hizo wanaweza kuomba viza kabla ya kusafiri au kusafiri moja kwa moja na kupewa viza hizo mara wanapowasili katika nchi wenyeji.
Kuna baadhi ya watu wanabeba passport mbili yaani ile ya kijani na ile nyeusi ya diplomatic nafikir hapo ndipo mwanya (loophole) wa kuchezewa passports hizi unapojitokeza kwani watu wanaweza kuwa wanaziuza hizi passports na mtu akitaka kufanya mambo yake ya ajabuajabu anakuwa akiwachanganya maofisa wa uhamiaji.
Kuna watu wanauza pasi za kusafiria na hili ni kosa la jinai, endapo una taarifa zozote zitakazowezesha kupatikana kwa watu hawa una budi kutoa taarifa kwa vyombo husika.
When thinking about my risk assessment, I always remember: HAZARD and the RISK .
Follow Us Here