Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kipigo cha Dk. Ulimboka chazua balaa tiGO

    Report Post
    Page 6 of 7 FirstFirst ... 4567 LastLast
    Results 101 to 120 of 127
    1. #1
      King Kong III's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Enaboishu-Umenyeni
      Posts : 11,929
      Rep Power : 5064
      Likes Received
      3203
      Likes Given
      2661

      Default Kipigo cha Dk. Ulimboka chazua balaa tiGO

      • Wafanyakazi 30 watimuliwa wakidaiwa kutoa mawasiliano ya siri kwa Gazeti la MwanaHalisi



      KUTEKWA, kupigwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama cha Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka na hatimaye kufungiwa kwa Gazeti la MwanaHalisi kwa muda usiojulikana, kumeleta kizaazaa katika kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

      Habari kutoka ndani ya kampuni hiyo ya simu yenye mtandao mpana nchini, zinasema kuwa zaidi ya wafanyakazi 30 wamefukuzwa kazi na wengine wako kwenye uchunguzi wakituhumiwa kuvujisha mawasilino ya siri ya simu za wateja kwa Gazeti la MwanaHalisi.

      Kwa mujibu wa habari hizo, taarifa za mawasiliano za simu zinazodaiwa kuvujishwa na wafanyakazi hao, zilikuwa kati ya Dk. Ulimboka, Afisa Usalama wa Ikulu na watu aliowasiliana nao kabla ya kutekwa.

      Rais Jakaya Kikwete amepata kuliambia taifa mara mbili kwa njia ya televisheni, mwishoni mwa Juni na alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari wiki iliyopita, kwamba serikali yake haihusiki kuteka, kutesa na kumtupa daktari huyo porini.

      Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda amepata kuliambia Bunge kuwa, serikali yake haihusiki na utekaji, utesaji na kuhoji, “...serikali imteke ili iweje?”

      Hivi karibuni serikali ililifungia Gazeti la MwanaHalisi baada ya kuandika habari iliyomtaja ofisa mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu (TISS), kuwa ndiye aliyetekeleza mpango wa kumteka, kumpiga na kumtesa hadi kumjeruhi Dk. Ulimboka, ambaye kwa sasa anaendelea na matibabu kwenye hospitali moja nchini Afrika Kusini.

      Kwa mujibu wa habari hiyo ambayo serikali inadai kuwa ni ya uchochezi, MwanaHalisi ilianika namba ya simu ya ofisa huyo pamoja na watu wengine wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo linaloendelea kuchunguzwa na kamati maalumu iliyoundwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI).

      Vyanzo vya habari kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi waliokumbwa na sekeseke hilo, zinasema kuwa waliofukuzwa wengi ni wafanyakazi wa kitengo cha IT ambao wanadaiwa kuhusika kutoa taarifa za siri ya mawasilino kati ya Dk. Ulimboka na watu wanaoaminika kuwa ni wabaya wake.

      Mmoja wa wafanyakazi kutoka Kampuni ya Tigo, aliliambia gazeti hili kuwa mbali na kutuhumiwa kutoa siri kwa Gazeti la MwanaHalisi, wafanyakazi wengine wametimuliwa kwa madai ya kufanya udanganyifu kwenye huduma za Tigo Pesa na kujipatia fedha.

      “Kweli watu wengi wamefukuzwa wakituhumiwa kutoa siri kwa Gazeti la MwanaHalisi, lakini wengine walikuwa wakishirikiana na mawakala wa Tigo Pesa kuiibia kampuni.

      “Kwa mfano mfanyakazi alikuwa anakubaliana na wakala kumwingizia kiasi kama cha sh milioni moja, lakini anaweza kuingiza hadi sh milioni 1.5 na kati ya hizo sh 500,000 ni mali yake,” alisema mfanyakazi huyo.

      Akizungumzia na Tanzania Daima Jumatano, Mhariri Mkuu wa Gazeti la MwanaHalisi, Jabir Idrissa alishangazwa na taarifa za Tigo kuwafukuza wafanyakazi wake kwa sababu ya habari iliyochapishwa na gazeti lake.

      “Chanzo chetu cha habari hakikutoka kwa wafanyakazi wa Tigo. Kama wamefukuzwa kwa sababu ya MwanaHalisi, wamewaonea bure. Kama Tigo ndio waliotupa taarifa na zile za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilitoka wapi?” alihoji Jabir na kusisitiza wafanyakazi hao wameonewa bure.

      Ofisa Uhusiano wa Tigo, Edward Shila, alipohojiwa kuzungumzia tukio hilo, hakukubali wala kukataa madai hayo na kumtaka mwandishi kumtumia maswali kupitia e-mail yake ili aweze kuyatolea majibu kiofisi.

      “Kama una maswali naomba uniandikie kupitia e-mail yangu ambayo nakutumia sasa hivi…maana siko tayari kutoa kauli yoyote isiyokuwa ya kiofisi,” alisema.

      Naye Omary Matulla ambaye amejitambulisha kuwa ni ofisa wa kitengo cha kumbukumbu katika kampuni hiyo, alikanusha kuwapo kwa taarifa za kufukuzwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

      Alisema kuwa kila mfanyakazi ana mipaka ya kufanya kazi katika kampuni hiyo, na pia ni wajibu wa kila mtumishi kutunza siri kubwa.

      “MwanaHalisi ana mbinu zake za kupata habari wala haiwezekani kupata habari kupitia kampuni yetu na hata hivyo jambo hilo si rahisi hata kidogo kutokea,” alikanusha Omary.

      Dk. Ulimboka alitekwa usiku wa Juni 26, kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

      Tangu kutokea kwa tukio la kutekwa kwa Dk. Ulimboka, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wamekuwa wakiinyoshea kidole serikali kwamba ndiyo iliyohusika.

      Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi mkoani Dar es Salaam, Suleiman Kova, hivi karibuni alitangaza kumfikisha mahakamani mtu mmoja aliyedai kukiri kuhusika na utekaji wa Dk. Ulimboka.

      Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa, polisi wamekamata mtu aitwaye Joshua Malundi kutoka Kenya ambaye amekiri kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka.

      Alidai kuwa mtuhumiwa alikwenda kutubu katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe, Dar es Salaam.

      Lakini hata hivyo, mchungaji wa kanisa hilo, Josephat Gwajima alikana kauli ya Kova juu ya mtuhumiwa huyo, akisema hajakwenda kutubu kwao.


      Source: Tanzania Daima
      mizambwa and kakobe junior like this.

    2. RukaaJuu Final

    3. #101
      Singo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th October 2010
      Posts : 297
      Rep Power : 603
      Likes Received
      42
      Likes Given
      213

      Default Re: Kipigo cha Dk. Ulimboka chazua balaa tiGO

      kama wamedhani siri imevujishwa na wafanyakazi wa tigo hiyo ni akili ndogo.Kuna watu kwa nafasi zao za kazi serikalini(USLAMA)wanaweza kuihitaji taarifa za mtu yeyote za mawasilino yake,na hao kwa utashi wao wameona ni vyema wanachi wajue pitia mwanahalisi, na isitoshe wataendelea hivyo kwa wasivyo viafiki.

    4. #102
      busara moco's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 23rd June 2012
      Posts : 4
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By tamuchungu
      Huyu jamaa amesingiziwa.haiwezekani mtu atumie jina lake halisi na namba alizosajili kumpigia mtu then amteke.huu ni uzushi mtupu
      mnakera na comments zenu,si mkae kimya tu,tunajua mpo kazini na huyo E.Coli...hamna jipya!!

    5. #103
      Mwanamayu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th May 2010
      Location : Manzese
      Posts : 3,049
      Rep Power : 1069
      Likes Received
      240
      Likes Given
      112

      Default tiGO kufukuza wafanyakazi ni ushahidi tosha?

      tiGO imefukuza karibu wafanyakazi wake 30 kutokana na kile kuwa wamefanikisha Kubenea au MwanaHalisi kupata mlolongo wa mawasiliano ya simu kati ya yule mfanyakazi wa ikulu, Ramadhani, na Dr. Ulimboka. Je, hii ni sababu au ushahidi tosha ya kuthibitisha kuwa serikali inahusika na mkasa wa Dr. Ulimboka?

      Source: TanzaniaDaima 8/8/2012, toleo namba 2805, Wednesday

    6. #104
      UPOPO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th December 2010
      Posts : 343
      Rep Power : 456
      Likes Received
      104
      Likes Given
      45

      Default Re: tiGO kufukuza wafanyakazi ni ushahidi tosha?

      Kazi ipo!mbona mpaka 2015 watafukuza wengi sana

    7. #105
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,647
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: tiGO kufukuza wafanyakazi ni ushahidi tosha?

      Kumbe wamefukuzwa! Ina maana Kubenea ndiye aliyefanya au ni baadhi ya watu ndani ya system yenyewe ambao wana access na mitandao yetu ya simu?
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    8. Miaka 50

    9. #106
      Crashwise's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2007
      Location : Safarini
      Posts : 13,141
      Rep Power : 14292
      Likes Received
      4021
      Likes Given
      3287

      Default Re: tiGO kufukuza wafanyakazi ni ushahidi tosha?

      hivi kuna mwehu mpaka leo hajaamini kuwa serikali ili husika kwa asilimia 100, au kuna mwehu anasubiri serikali ya chama cha mambwepande isimamame jukwaani na kukiri kuwa ilihusika..
      SMU likes this.

    10. #107
      Sibhonike's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th April 2011
      Posts : 87
      Rep Power : 428
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default Re: tiGO kufukuza wafanyakazi ni ushahidi tosha?

      Hizi zama ni zaidi ya zama za UWAZI NA UKWELI.

    11. #108
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,057
      Rep Power : 0
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1

      Default Re: Kipigo cha Dk. Ulimboka chazua balaa tiGO

      breaking News.

      Dr ulimboka kutua nchini wakati wowote akitokea af kusini kwenye matibabu.
      wanaharakati,madokta wenzake na vyama kadhaa vya siasa vinaandaa na kuratibu mapokezi yake yatakayofanyika kuanzia uwanja wa ndege jijini dsm.

      wanasiasa wakisaidiana na mwanahalisi inasemekana wanamlisha maneno ili aje ayaseme kuonyesha kwamba serikali ndio inahusika na kwamba mkenya ametengenezwa. namtakia afya njema dr ulimboka na ninamshauri asiendeleze malumbano,aendelee kupigania uhai wake kwanza kwani jamii ya watanzania bado inamhitaji na maadui zake bado wanamuwinda.



    12. #109
      Dumelang's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th August 2011
      Location : Dar es salaam
      Posts : 311
      Rep Power : 456
      Likes Received
      179
      Likes Given
      144

      Default Re: tiGO kufukuza wafanyakazi ni ushahidi tosha?

      Confirmed! Kikwe ana husika...na jumba lake la magogoni. Siku moja tukiwa katika mkutano wa ndani wa Chama (Sio wa Hadhara) Mh. Mbowe, alisema kuna watu wakati wa kufa hurusha miguu sana na usipokuwa makini uliye pembeni utapigwa mateke,alikuwa akitoa Angalizo kuhusu chama cha Majambazi kuwa kinapoelekea kufa KINAKUFA NA WENGI, kila mtu awe makini, wakati tunakifunika sanda NYEKUNDU,mtu akae upande wa kichwani, ukikaa miguuni tu, umekula teke.
      BURIANI CCM
      Never say more than is necessary.

    13. #110
      Ulimakafu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2011
      Location : Itabanya Balasi
      Posts : 10,968
      Rep Power : 2608
      Likes Received
      690
      Likes Given
      1615

      Default Re: Kipigo cha Dk. Ulimboka chazua balaa tiGO

      Japo wamefukuzwa wametusaidia kidogo kuujua ukweli.

    14. #111
      yaser's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd January 2012
      Posts : 953
      Rep Power : 635
      Likes Received
      137
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By Dumelang
      Confirmed! Kikwe ana husika...na jumba lake la magogoni. Siku moja tukiwa katika mkutano wa ndani wa Chama (Sio wa Hadhara) Mh. Mbowe, alisema kuna watu wakati wa kufa hurusha miguu sana na usipokuwa makini uliye pembeni utapigwa mateke,alikuwa akitoa Angalizo kuhusu chama cha Majambazi kuwa kinapoelekea kufa KINAKUFA NA WENGI, kila mtu awe makini, wakati tunakifunika sanda NYEKUNDU,mtu akae upande wa kichwani, ukikaa miguuni tu, umekula teke.
      BURIANI CCM
      khaaa sasa ww unaamin maneno ya DJ
      mkomatembo likes this.

    15. #112
      PrN-kazi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2011
      Posts : 2,213
      Rep Power : 5360
      Likes Received
      293
      Likes Given
      4

      Default

      Quote By Mwanamayu
      tiGO imefukuza karibu wafanyakazi wake 30 kutokana na kile kuwa wamefanikisha Kubenea au MwanaHalisi kupata mlolongo wa mawasiliano ya simu kati ya yule mfanyakazi wa ikulu, Ramadhani, na Dr. Ulimboka. Je, hii ni sababu au ushahidi tosha ya kuthibitisha kuwa serikali inahusika na mkasa wa Dr. Ulimboka?

      Source: TanzaniaDaima 8/8/2012, toleo namba 2805, Wednesday
      Kumbe tiGO imewafukuza wafanyakazi wake???, CMA iko wazi inawasubiri hao wafanyakazi ndani ya muda walete malalamiko yao suluhu itapatikana.

    16. #113
      ha ha ha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th December 2011
      Location : Hapahapa
      Posts : 456
      Rep Power : 466
      Likes Received
      45
      Likes Given
      71

      Default Re: tiGO kufukuza wafanyakazi ni ushahidi tosha?

      Haki ya mtu haichukuliwi,ila inaweza kucheleweshwa ata kama ni miaka mia ipo siku ataipata.

    17. #114
      Heri's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th August 2007
      Posts : 199
      Rep Power : 639
      Likes Received
      19
      Likes Given
      30

      Default Re: Kipigo cha Dk. Ulimboka chazua balaa tiGO

      Kila kazi ina ethics zake. Haijalishi hata kama kuna kitu kina kukera ,uende kutoa siri. Hii ni moja za sababu ya employers kutokuwa na imani na Watanzania.

    18. #115
      Nduka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd December 2008
      Posts : 5,593
      Rep Power : 1636
      Likes Received
      383
      Likes Given
      553

      Default

      Quote By Ulimakafu
      Japo wamefukuzwa wametusaidia kidogo kuujua ukweli.
      Kwa nini msiwachangie mishahara yao kila mwezi, kuna hatari vijana wakaanzm kudonolewa.

    19. #116
      mopaozi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2010
      Posts : 2,446
      Rep Power : 758
      Likes Received
      258
      Likes Given
      49

      Default Re: Kipigo cha Dk. Ulimboka chazua balaa tiGO

      Wafukuzwe tu kiherehere chao kimewaponza

    20. #117
      luckman's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2010
      Posts : 945
      Rep Power : 631
      Likes Received
      151
      Likes Given
      20

      Default Sakata la ulimboka na gazeti la mwanaharisi vyaitafuna tigo

      Habari za kuaminika toka ndani ya uvungu wa kampuni ya simu ya tigo, limeingia hatua nyingine baada ya wafanyakazi wake wanasadikika kufukuzwa wakidaiwa kutoa information za mawasiliano aliyoyafanya Dr Ulimboka na watekaji wake kwa Saed Kubenea, kazi hii imefanywa kwa ufasaha mkubwa sana na makachero nchi wanaofanya kazi ndani ya kampuni na wengine walionje ya kampuni, hii inasikitisha sana,

      serikali inahusika moja kwa moja juu ya hili sakata! lakin naomba mtambue mwisho wa haya yote u karibu sana!

    21. #118
      Mzalendo JR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th June 2012
      Posts : 908
      Rep Power : 532
      Likes Received
      277
      Likes Given
      213

      Default Re: Sakata la ulimboka na gazeti la mwanaharisi vyaitafuna tigo

      Hii kampuni nishasepa kitambo, wababaishaji kama serikali ya TZ.
      "Happiness is what you think, what you say, and what you do are in harmony"

    22. #119
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2885
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default Re: Sakata la ulimboka na gazeti la mwanaharisi vyaitafuna tigo

      Eh,haya mambo bado yanaendelea,,,tigo wenyewe hata siku nzima huwa wako off-air,washatuchosha,hapa nipo maeneo ya mikochen industrial arean,netweki inasumbua ajabu

    23. #120
      Nyalotsi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th July 2011
      Posts : 2,657
      Rep Power : 928
      Likes Received
      589
      Likes Given
      96

      Default

      Quote By Mzalendo JR
      Hii kampuni nishasepa kitambo, wababaishaji kama serikali ya TZ.
      mi mwenyewe line yao niliivunja vunja. Hii habari ni ya kitambo lakini!

    Page 6 of 7 FirstFirst ... 4567 LastLast

    LinkBacks (?)


    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...