re: Jua haki yako unapokamatwa na Polisi
hii post imenifurahisaha sana, kwanini nilikuwa najiandaa kuandaa thread yenye madhumuni kama hayo..
kwa kifupi ni kwamba nyumbani kuna gari inayofanya biashara za usafiri, sasa jana askari akawa ameikamata na kuomba mmliki aende eti kosa ni kuwa hakuwa na insurance ya kufanyia biashara( sasa kwa kutokujua akajua kuwa labda kuna insurance nyingine tofauti na zile tunazonunua za kawaida) wakapewa faini ya tz elfu 20 , katika kujitetea yule traffic akamwambia alipe elfu kumi ili wamalizane( wakati huo mama akiwa kesha nitumia sms kunieleze kuhusu hilo swala), alipomaliza kumlipa Mama ikabidi afatilie kwenye vyombo husika ili kujua kama anatakiwa kulipa insurance nyingine, bahati nzuri kafika kule na kuelezwa kuwa hakuna bima nyingine zaidi ya hiyo uliyonayo, baada ya kama dk 45 mama akanitumia tena sms akisema "swala lile lilikuwa ni uonevu tu, wamechukua elfu kumi" . sio siri nilighadhabika sana na kumpigia simu na kumuuliza "kulikoni mtu umeshatambua kuwa ni uonevu bado unampa elfu kumi? kwa nini usirudi na kumwomba hiyo pesa yako? hivi ni kwa nini mnaruhusu kunyonywa wazi wazi kiasi hicho? akanijibu kuwa yaani huku Tanzania kila kitu ni rushwa tu iwe unataka au hutaki haki yako bila rushwa hakuna chochote..huku akiongezea kuwa sasa mimi nitafanyaje wakati sijui hata sheria zinasemaje? mmh hapo nikachoka kabisa
je ni wangapi wanaofanyiwa madudu kama haya? unajua matatizo mengine tunayasabisha sisi wenyewe wananchi kwa kupenda kufanya haraka haraka bila kufuata procedure..
Nimetafakari sana na kutambua kuwa wananchi wengi hawajui sheria na wanaendelea kunyonywa tena wakinyenyekea kutoa chochote ili wapate haki yao, hivi hawa matraffic wataacha huu ubabaishaji hadi lini? sio siri kama ningekuwa Tanzania ningehakikisha namfatilia huyu traffic hadi mwisho ili iwe funzo kwa wengine kama hao.
Ee Bwana uyasikilize maneno yangu, ukaangalie kutafakari kwangu.
Follow Us Here