Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Nimeshtushwa Polisi kutishia uhai wa watoto kwa silaha za kivita

    Report Post
    Page 3 of 3 FirstFirst 123
    Results 41 to 41 of 41
    1. #1
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,606
      Rep Power : 15261
      Likes Received
      3731
      Likes Given
      2867

      Default Nimeshtushwa Polisi kutishia uhai wa watoto kwa silaha za kivita




      Hii ni dalili kwamba Tanzania hatuna sheria ya kutetea haki za watoto. Maandamano ya hawa watoto au wanafunzi hayakuwa uvujaji wa amani au sheria, bali kuisaidia serikali kufungua zaidi na kuona madai ya walimu yafikiwe mwafaka ili wasiendelee kukosa vipindi madarasani sababu ya mgomo wa walimu.

      Askari polisi kutumia silaha za kivita kutishia uhai wa wanafunzi ni jambo hatari kabisa kwa malezi ya watoto hawa, la ajabu, na lisilo la kistaarbu kabisa, na kabisa kisaikolojia ni kuwaharibu hawa watoto. Athari za matukio ya polisi kutishia watoto kwa silaha kali za kivita ni kubwa katika maisha yao, na hapo ndipo busara inapokosekana kwa serikali na jeshi la polisi nchini ni kielelezo tosha.




      Tanzania hatuna wanasaikolojia wanaoweza kuwasaidia hawa watoto kuongea nao wakaelewa na pengine wakachukua mawazo ya watoto hawa na kuyafanyia kazi, na badala ya watoto hawa kuwatisha wanafunzi uhai wao ka mitutu ya bunguki na mabomu ya machozi, je walikuwa na silaha gani kama si mikono mitupu kudai haki yao ya kupata elimu jambo ambalo linaeleweka kwa kila mmoja? Wizara ya jamii na watoto kazi yao nini , na wanafanya nini kutetea hawa watoto?



      Hawa watoto ni haki yao kudai muda unaopotezwa na walimu wanapodai haki zao wakati wanakosa masomo madarasani. Binafsi sioni kosa la watoto kama maandamano yao yalikuwa ya amani, na kama waliziba njia ni bora kutumia njia za kisaikolojia kuwatuliza wanafunzi kuliko tishio la silaha za kivita.

      Serikali iko tayari kusikiliza kilio cha wanasiasa wabunge kuwaongezea mishahara na malupulupu, lakini wanaosota maisha yao yote kuandaa hili taifa la kesho wamewapiga danadana siku nyingi na leo wanapochukua hatua serikali inaamua kumalizia hasira kwa hawa malaika wasio na makosa, waadhiriwa na mgomo wa walimu.

      Je, serikali inapotumia jeshi la polisi kutishia watoto hawa ambao ni waadhirika wa kukosa masomo bila ridhaa yao kwa uzembe wa serikali yenyewe, je inajengwa taswira gani katika maisha, malezi na future ya watoto hawa?

      Hili ndilo tatizo la vyombo vya dola vinapotumika zaidi kisiasa.
      Ogah, Davie and kofiliko like this.

    2. RukaaJuu Final

    3. #41
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,606
      Rep Power : 15261
      Likes Received
      3731
      Likes Given
      2867

      Default Re: Nimeshtushwa Polisi kutishia uhai wa watoto kwa silaha za kivita

      Quote By TIMING
      THE SADDEST PART NI PALE WAKUBWA WANAPOKUA WAPOFU WA MATENDO DHALIMU KAMA KUOKOTA VITOTO VYA PRIMARY NA KARANDINGA, WATOTO WA KIKE WAMENYANYASWA ZAIDI KIJINSIA NA NI LAANA isiyoepukika
      Ni jambo ambalo haliwezi kuingia akilini mwangu kabisa, ila ipo siku watakuwa na la kuwajibika kwa haya.

    Page 3 of 3 FirstFirst 123

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...