Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

    Report Post
    Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 81
    1. #1
      MSEZA MKULU's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd July 2011
      Posts : 169
      Rep Power : 429
      Likes Received
      58
      Likes Given
      213

      Default Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      Ufafanuzi Kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhitibi wa Hifadhi ya Jamii

      UFAFANUZI KUHUS FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.

      Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

      1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

      2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

      3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

      4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

      5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

      6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

      7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu

      8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

      9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo. Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.

      Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

      Wenu.
      Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii

      Irene Isaka
      MKURUGENZI MKUU
      The most powerful moral influence is example

    2. Miaka 50

    3. CPA
      #21
      CPA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st March 2011
      Location : DAR ES SALAAM
      Posts : 491
      Rep Power : 515
      Likes Received
      106
      Likes Given
      25

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      Zito kabwe, mnyika, nchemba, kingwangala etc najua mpo humu? Hili mlipitisha? Tunaomba majibu?

    4. #22
      Lyceum's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2009
      Posts : 547
      Rep Power : 600
      Likes Received
      100
      Likes Given
      128

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      Duh watunga sheria wetu sijui wakoje. Life span yenyewe imepungua sana. Anyway ndo sheria zinazotungwa na watu kama nhemba, lusinde, maji marefu na kupigiwa chapuo na Werema. Tutegemee makubwa zaidi

    5. #23
      Scofied's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2012
      Location : A-City
      Posts : 1,279
      Rep Power : 606
      Likes Received
      332
      Likes Given
      58

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      hivi hnyama vya wafanyakazi vinatambua hili? Mbona avilizungumzii hiki? Kuna umuhimu wa kutokuchangia tena wakuu! Huu ni wizi wa waziwazi...

    6. #24
      MASIKITIKO's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th December 2011
      Posts : 205
      Rep Power : 478
      Likes Received
      28
      Likes Given
      2

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      Wanakopa hela za kuwalipa wafanyakazi wa Serikali Mishahara kwenye hii mifuko hadi inafilisika.

    7. #25
      Polisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2010
      Posts : 1,533
      Rep Power : 737
      Likes Received
      359
      Likes Given
      234

      Default

      Quote By mgodi
      Kuna mtu anakumbukumbu na hii sheria kuwa ilishapata baraka za bunge kweri? Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

      1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

      2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.
      Sijaona mtu akifariki inakuwaje au naye anasubiri 55 years? What a shame. Huu uwe mtaji kwa chadema kupata kura zaidi za wafanyakazi

    8. RukaaJuu Final

    9. #26
      Scofied's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2012
      Location : A-City
      Posts : 1,279
      Rep Power : 606
      Likes Received
      332
      Likes Given
      58

      Default

      Quote By Polisi
      Sijaona mtu akifariki inakuwaje au naye anasubiri 55 years? What a shame. Huu uwe mtaji kwa chadema kupata kura zaidi za wafanyakazi
      Walisimamie kulipinga hili kwa nguvu zote,wafanyakazi wote tuwaunge mkono...lakini wap vyama vya wafanyakazi? Hawajalijua hili?

    10. MTK
      #27
      MTK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th April 2012
      Posts : 936
      Rep Power : 4497
      Likes Received
      303
      Likes Given
      333

      Default Re: Waliotegeea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena baaasi!!!! Ufafanuzi kutoka kwa mamlaka ya

      Quote By Gurta
      Bila kuwa na sheria ya Unemployment Benefits (au inayofanana na hiyo) hili sio wazo zuri hata kidogo.
      Elimu ya umma kuhusu swala hili ni muhimu itolewe kwa haraka na kwa upana na uwazi sana haraka iwezekanavyo ili kuzuia taharuki na wasiwasi unaoweza kutokea kutokana na uelewa mdogo wa wananchi wa sera hii na athari za opportunists ambao watependa kupindisha ukweli kwa maslahi yao binafsi. Irene jenga imani kwa wananchi ili wakuamini; hili ni swala nyeti sana kwa sababu linagusa mafao ya wananchi hasa wale wa kipato cha chini. Historia haitakuonea huruma katika hili ikiwa utatumbukia katika mtego wa ujanja ujanja ambao kwa sasa it appears to be the practise rather than the exception in Tanzania, the public is watching!!
      Gurta likes this.

    11. #28
      kichwat's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th March 2010
      Posts : 1,044
      Rep Power : 692
      Likes Received
      215
      Likes Given
      24

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      Jambo moja muhimu hapa ni kwamba sheria ni MKATABA. Utaratibu huu ni mpya hivyoi ni lazima uhusike na michango ya kuanzia pale ulipotangazwa onwards. Kisheria kuna hoja hapo.
      Huwezi kuimpose new terms on existing contract UNILATERALLY. Wanasheria tutoeni kifungoni.

    12. #29
      Scofied's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2012
      Location : A-City
      Posts : 1,279
      Rep Power : 606
      Likes Received
      332
      Likes Given
      58

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      washaniaribia mipango yangu.......nasikia hasira mpaka basi,nachukia kuwa mtanzania kwa kweli....

    13. #30
      Wimana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th June 2012
      Posts : 1,047
      Rep Power : 557
      Likes Received
      281
      Likes Given
      180

      Default

      Quote By Tidito L
      Mi nashaang'aa hii nchi inavyoendeshwa...
      Hapa itakuwa hawa jamaa wa serikari wamechota hela kwenye hizo fund wakashindwa kurudisha wkt watu wanadai hela zao ndo wakaona waitungie sheria.
      Du!ama kweli hii nchi!
      Ripoti ya CAG ilisema wazi Serikali imeshindwa kulipa mabilio ya pesa ilokopa kutoka NSSF au pale ilipodhamini mikopo kutoka NSSF. Ni NSSF wamejenga Udom, wamekopesha Gen Tyre, Daraja la Kigamboni nk.
      Sasa mtu umeachishwa kazi, utasubiri 55 yrs
      ? Daini haki zenu.

    14. #31
      Wimana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th June 2012
      Posts : 1,047
      Rep Power : 557
      Likes Received
      281
      Likes Given
      180

      Default

      Quote By ITEGAMATWI
      Huu ni wizi wa mchana kweupee!!Yaani nikiacha kazi kabla ya miaka 55 hela mnayonikata kila mwezi mnaichukua nyie?Au labda sijaelewa vizuri?
      Miaka michache iliopita niliamua kufanya maamuzi magumu. Nilichukua balance yangu NSSF nikakuta nina 8m, riba wameweka elfu 8! Yaani interst hairudishi hata kushuka thamani kwa shilingi! Baada ya 2yrs nikaacha kazi nikazoa milioni zangu nikaziwekeza mahali ambapo napata laki 8 kila mwezi, si haba.
      MSEZA MKULU and ITEGAMATWI like this.

    15. #32
      Mtundu Kisu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th September 2011
      Posts : 676
      Rep Power : 524
      Likes Received
      147
      Likes Given
      9

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      Lakini kwa utaalam wangu wa sheria,hii sheria haipawi kuapply kwa wanyakazi waloajiriwa kabla ya kuanza kufanya kazi kwa sheria hii.

      Hii itakuwa retrospective,na sheria yoyote haipaswi kuapply retrospective.

      Hivyo basi,kwa maoni yangu tunaweza kuichallenge hii sheria mahakama kuu kwa ground kadhaa.kama ifuatavyo
      1. Kwanza ni hiyo ya retrospective
      2. Pili ni kuwa inahatarisha haki mbalimbali za msingi kikatiba,kwa mfano,right to life na hivyo ni unconstitutional.

      Remedy yake ni kuwa declared unconstitutional na kuwa nullified.

      Tundu lisu,LHRC mko wapi?

    16. #33
      Domhome's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th June 2010
      Location : Chimbo
      Posts : 703
      Rep Power : 592
      Likes Received
      182
      Likes Given
      142

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      Jana kumetokea mtafaruku mkubwa sana Mgodini Nzega. Kwani wafanyakazi wa Kampuni ya Caspian woote waliamua kuachakazi, kwa kuandika resignation ya 24hrs, wakarudisha mashine toka site na kurudi ofisini kumkabidhi mkuu wao hizo barua. Hii yote imetokana na taarifa hizi za SSRA, imesababisha Management ichanganyikiwe na Production ilisimama kwa masaa 3 hivi, na sasa Kampuni ya Resolute na Caspian zimetuma wawakilishi Dar ili Kupata ukweli juu ya hali halisi.

      Nasikia huko Nzega taarifa zinasema eti SSRA, itaanza kuitumia sheria hii kuanzia tarehe 1 Oktoba 2012 ndo maana wafanyakazi huko Mgodini wameamua kuacha kazi sasa na kwenda kuchukua mafao yao kabla ya Oktoba Mosi.
      “It’s now the moment for political baboons to see their backsides” - Time for politicians to look at themselves in the mirror! (Kenyan human right's activist)

    17. #34
      TANMO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Tanzagiza
      Posts : 5,046
      Rep Power : 7769
      Likes Received
      1808
      Likes Given
      3439

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      Basi wapunguze umri wa mtu kustaafu kwa hiari uwe miaka 35 manake life expectancy ya Mtanzania ni arround 40's..
      Do Something......

    18. #35
      Crashwise's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2007
      Location : Safarini
      Posts : 13,127
      Rep Power : 14289
      Likes Received
      4015
      Likes Given
      3273

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      hili nipigo kwangu na kwajamii kwa ujumla nilipanga kuacha kazi za kuajiriwa mwisho mwa mwaka huu ili vijisenti vyangu viniwezeshe kuendeleza kijikampuni changu..daah wabunge hili mlilipitisha kweli

    19. #36
      OLESAIDIMU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2011
      Posts : 1,242
      Rep Power : 733
      Likes Received
      494
      Likes Given
      470

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      [QUOTE=CPA;4288257]Zito kabwe, mnyika, nchemba, kingwangala etc najua mpo humu? Hili mlipitisha? Tunaomba majibu?

      Na wengine mnaoingia kwa hidden ID's kweli haya ndo mambo mlipisha huko???

      If yes it could be fair and balanced that you as well wait till that decaying age to rip the benefits associated with the expiry of tenure...........

      Sadist's era.....................!!!!!! !!!!!!!!!!!!!!!!!????????????? ????????
      Hegemony is unlikely ever to be complete (A. Gramsci)

    20. #37
      Rejao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2010
      Location : Long Street
      Posts : 8,756
      Rep Power : 25651
      Likes Received
      3344
      Likes Given
      2878

      Default

      Quote By Crashwise
      hili nipigo kwangu na kwajamii kwa ujumla nilipanga kuacha kazi za kuajiriwa mwisho mwa mwaka huu ili vijisenti vyangu viniwezeshe kuendeleza kijikampuni changu..daah wabunge hili mlilipitisha kweli
      Huu utakuwa ni ujinga. Unaacha kazi kwa kutegemea 20% ya contributions zako ndio uendelezee kampuni!!!

      Hii sheria ya SSRA nimeipenda. Itasaidia sustainability ya mifuko yetu na pia wanaweza kuplan vizuri especially kwenye long term investmennts.

    21. #38
      Polisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2010
      Posts : 1,533
      Rep Power : 737
      Likes Received
      359
      Likes Given
      234

      Default Re: Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

      Nimejaribu kuipitia hiyo sheria, sijaona hicho kipengele maana kipengele cha 37 bado kinazungumzia kuwepo kwa mafao ya muda mfupi na muda mrefu. Last week mimi nimepeleka madai yangu nssf ila hawajaniambia hicho kitu mbali ya kusema wameipokea na wataifanyia kazi. Kesho asubuhi naenda kuwaona

    22. #39
      Rejao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2010
      Location : Long Street
      Posts : 8,756
      Rep Power : 25651
      Likes Received
      3344
      Likes Given
      2878

      Default

      Quote By Domhome
      Jana kumetokea mtafaruku mkubwa sana Mgodini Nzega. Kwani wafanyakazi wa Kampuni ya Caspian woote waliamua kuachakazi, kwa kuandika resignation ya 24hrs, wakarudisha mashine toka site na kurudi ofisini kumkabidhi mkuu wao hizo barua. Hii yote imetokana na taarifa hizi za SSRA, imesababisha Management ichanganyikiwe na Production ilisimama kwa masaa 3 hivi, na sasa Kampuni ya Resolute na Caspian zimetuma wawakilishi Dar ili Kupata ukweli juu ya hali halisi.

      Nasikia huko Nzega taarifa zinasema eti SSRA, itaanza kuitumia sheria hii kuanzia tarehe 1 Oktoba 2012 ndo maana wafanyakazi huko Mgodini wameamua kuacha kazi sasa na kwenda kuchukua mafao yao kabla ya Oktoba Mosi.
      Sheria tayari imeshaanza kutumika. Wasubiri tu mpaka wafike 55 yrs voluntary au 60 yrs compulsary!
      Domhome likes this.

    23. #40
      Polisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2010
      Posts : 1,533
      Rep Power : 737
      Likes Received
      359
      Likes Given
      234

      Default

      Quote By Rejao
      Huu utakuwa ni ujinga. Unaacha kazi kwa kutegemea 20% ya contributions zako ndio uendelezee kampuni!!!

      Hii sheria ya SSRA nimeipenda. Itasaidia sustainability ya mifuko yetu na pia wanaweza kuplan vizuri especially kwenye long term investmennts.
      Aisee. Nimejaribu kama dakika 10 kutafuta maneno makali ya kukujibu nimekosa. Yote naona yatapelekea nilimwe kifungo
      Malila, Crashwise and MSEZA MKULU like this.

    Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...