Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Madaktari wanalilia kuondokana na hiki....

    Report Post
    Results 1 to 7 of 7
    1. #1
      Dopas's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th August 2010
      Posts : 595
      Rep Power : 564
      Likes Received
      85
      Likes Given
      82

      Default Madaktari wanalilia kuondokana na hiki....

      Kilio.docx
      Madaktari wanalilia kuondokana na hali hii. Utashangaa wengine wanang'ang'ania kuwa eti Madaktari wanataka mishahara minono.
      Ikiwa hii ndiyo hali ya hospitali zetu nyingi, kuna tofauti gani ya hali hii na kifo? Ona tu mwenyewe.. afu uendelee kulalama kuwa madaktari wanataka mishahara minono..
      source ya picha Wavuti.com

    2. Miaka 50

    3. #2
      Bi. Mkora's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th October 2010
      Posts : 349
      Rep Power : 503
      Likes Received
      43
      Likes Given
      80

      Default Re: Madaktari wanalilia kuondokana na hiki....

      Sasa hata huyo daktari atapita vipi kuwahudumia hao wagonjwa katika hali kama hiyo? Mweh!!
      Mtoto ni mtoto kwa mama hakui

    4. #3
      Mokerema's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th November 2011
      Posts : 236
      Rep Power : 427
      Likes Received
      117
      Likes Given
      84

      Default Re: Madaktari wanalilia kuondokana na hiki....

      Quote By Dopas
      Kilio.docx
      Madaktari wanalilia kuondokana na hali hii. Utashangaa wengine wanang'ang'ania kuwa eti Madaktari wanataka mishahara minono.
      Ikiwa hii ndiyo hali ya hospitali zetu nyingi, kuna tofauti gani ya hali hii na kifo? Ona tu mwenyewe.. afu uendelee kulalama kuwa madaktari wanataka mishahara minono..
      source ya picha Wavuti.com
      Dopas,

      Hii clip ingeunganishwa Kama attachment kwenye barua iliyopelekwa UN kuomba ulinzi wa Madaktari, Wako wapi akina Makinda, UWT,Tamwa na wengineo hata akina mama wa Mewata? Huu ni udhalilishaji mkubwa wa akina mama.

      Ningekuwa na Vijisenti ningeungana na Mtikila kuishitaki serikali. Kuanzia Waziri wa Afya Waziri Mkuu Pinda halafu Dhaifu.

      Hawa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania bora wasepe?

    5. #4
      bullof's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 8th July 2012
      Posts : 4
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      3

      Default Re: Madaktari wanalilia kuondokana na hiki....

      Kwakweli nimekuwa nikifuatilia sakata la madaktari na serikali kwa huzuni sana. Tangu mgogoro huu uanze maisha ya watu wasio na hatia yamepotea. Swali ni nani alaumiwe, madaktari au serikali? Kwa wananchi wengi, ukisikiliza redio, lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa madaktari. Inawezekana lawama hizo kwa madaktari zinatokana na kauli za kupotosha za wanasiasa kwamba madaktari wanataka mshahara wa milioni tatu. Lakini ikumbukwe serikali hii hiii iliwahi kutamka kwamba haina uwezo wa kulipa kima cha chini cha mishahara shs 300,000? Aibu!!

      Niliwahi kukutana na mzungu mmoja kwenye ndege akaniambia tatizo la serikali ya tanzania ni kwamba inapesa kwa ajili ya mambo ya kipuuzi si mambo ya maendeleo. Mzungu akaponda angalia huu uwanja wa ndege wa mwanza ni kweli serikali ya tanzania haina uwezo wa kujenga uwanja wa kisasa? aliuliza huyo mzungu. Ukweli usiopingika ni kwamba Serikali inayo pesa kwa ajili anasa si maendeleo mfano, pesa kwa ajili ya chai, posho, magari ya kifahari, safari za viongozi za nje ya nchi zisizo na tija (mfano ni aibu kubwa kwa serikali kusamehe kodi ya matrilioni ya shilingi lakini kiongozi anatumia mabilioni ya fedha kwenda nchi za nje kuomba bilioni 10 au 20), pesa kwa ajili ya mishahara na posho za wanasiasa mfano wabunge. Hapo ndipo tatizo linapoanzia, wananchi wameelimika wanaona na kusikia jinsi viongozi wao wanavyo tumbua pesa, hakuna uwiano sawa katika mgao wa keki ya taifa. Wananchi hawakubaliani na viongozi wao kwamba pesa za kuboresha mishahara yao na huduma za jamii hazipo. Hiyo picha inaonesha hali halisi kwenye hospitali zetu, anzia muhimbili kwenyewe, halafu mwanasiasa anatoa majibu mepesi tu kwamba madaktari wanagoma kwa sababu wanadai milioni 3. Na kama ni kweli kuna ubaya gani kwa daktari kudai milioni tatu 3 wakati kuna watu bungeni wanapokea zaidi ya milini 10 kwa kwenda kuchapa usingizi bungeni na kuunga mkono kila utumbo unaoletwa na serikali!! Vio vikuu hamna vitendea kazi kama vitabu wanafunzi wanategemea notes za wenzao waliomaliza zamani ambazo nazo zimepitwa na wakati na hata mishahara ya walimu wa chuo kikuu inasikitisha ndiyo maana wake wengi wa walimu wanauza mpaka barafu lakini yuko mtu bungeni shule hana lakini anakomba zaidi ya milioni 10. Walimu wamekata tamaa hawafundishi (mgomo baridi) wanahangaika kutafuta pesa kwingine kiwango cha elimu kinazidi kuporomoka mwaka hadi mwaka

      Madaktari wanafahamu kuwa kisheria hawaruhusiwi kugoma kwa sababu wao wako kwenye essential service kama ilivyo kwa wafanyakazi wa zima moto na airport. Hao wakigoma madhara kwa wananchi ni makubwa sana, kama vile vifo kwa wananchi ambao uwezo wa kukimbili Appollo India haupo. Lakini wangefanyaje ikiwa serikali inapuuzia madai yao ya msingi ikiwemo mishahara na vitendea kazi, wakati uwezo wa kutimiza madai yao serikali inayo. Ukienda Muhimbili una ambiwa nenda kapige X-ray Aga khan au Regency kwakuwa mashine zao zimechoka na zimepitwa na wakati, Aibu!!

      kwa tabia hii ya serikali ya tanzania vitendo vya rushwa havita isha kamwe, jiulize mtu anawezaje kuishi kwa mshahara wa 100,000 au 300,000 kwa hali hii ya mfumuko wa bei, kila kitu kipo juu? Ukifika mahospitalini leo kama huna chochote utashuhudia mgonjwa wako anakata roho mbele ya macho yako

      Mungu aingilie kati

    6. #5
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Madaktari wanalilia kuondokana na hiki....

      Quote By Dopas
      Kilio.docx
      Madaktari wanalilia kuondokana na hali hii. Utashangaa wengine wanang'ang'ania kuwa eti Madaktari wanataka mishahara minono.
      Ikiwa hii ndiyo hali ya hospitali zetu nyingi, kuna tofauti gani ya hali hii na kifo? Ona tu mwenyewe.. afu uendelee kulalama kuwa madaktari wanataka mishahara minono..
      source ya picha Wavuti.com
      Weka madai yao hapa usitake kuchakachuwa. Hao madaktari wa agenda za siri na zimekwisha kujulikana na sasa si mjadala tena wameambiwa amma wafanye kazi amma wawache kazi, mjadala wa nini? mgomo wa nini? Rais kisha tangaza kinaga ubaga.

      Waende wakafanye wanapoona watahudumia vizuri zaidi kwani hospitali ni za Serikali tu hapa tanzania? zipo za binafsi, hao madaktari wanazo zao (mfano tumaini), zipo za kanisa (MoU), zipo za mashirika, Malumbano yanini si waondoke tu?
      Ndumbayeye likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      mwakaboko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th September 2010
      Posts : 633
      Rep Power : 566
      Likes Received
      140
      Likes Given
      858

      Default Re: Madaktari wanalilia kuondokana na hiki....

      uko sawa kabisa,LAKINI CHA MUHIMU NI KUWA MADAKTARI WETU NI WABINAFSI, wanataka 3,500,000/, madai mengine hayo ni blabla tu, tusidanganyane hapa. MIE NINGEwaunga mkono kama wangekuwa kweli wanamtetea mtanzania ambaye kima chake cha chini ni 135000 kupanda, lkn wao wanakuwa kama wanasiasa kwa ubinafsi, du
      Ndumbayeye likes this.

    9. #7
      Mfamaji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th November 2007
      Posts : 2,884
      Rep Power : 1161
      Likes Received
      285
      Likes Given
      158

      Default Re: Madaktari wanalilia kuondokana na hiki....

      Quote By mwakaboko
      uko sawa kabisa,LAKINI CHA MUHIMU NI KUWA MADAKTARI WETU NI WABINAFSI, wanataka 3,500,000/, madai mengine hayo ni blabla tu, tusidanganyane hapa. MIE NINGEwaunga mkono kama wangekuwa kweli wanamtetea mtanzania ambaye kima chake cha chini ni 135000 kupanda, lkn wao wanakuwa kama wanasiasa kwa ubinafsi, du
      Ungekuwa wewe Doc. wa wanawake ungedai sh. Ngapi kuhudumia hao akina mama hapo pichani kwa siku moja tu?
      ''The most pathetic person in the world is someone who has sight, but has no vision''

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...