Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

    Report Post
    Page 5 of 8 FirstFirst ... 34567 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 153
    1. #1
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,094
      Rep Power : 27014
      Likes Received
      8231
      Likes Given
      17325

      Default Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?


      Attachment 54031

      Attachment 54032


      Tukio lenyewe lilitokea hapo majira ya asubuhi mnamo Februari 21, 1978. Ni baada ya kuambiwa mumewe wakati anaenda kazini kwamba akirudi asimkute hapo nyumbani, na kama akimkuta, atamtoa hapo nyumbani kwake uchi. Alikuwa na watoto wao wanne hapo nyumbani. Baada ya mumewe kuondoka, na yeye aliondoka na gari kuelekea mjini ambapo alinunua chupa kadhaa za sumu ya kuulia wadudu.


      Alipofika nyumbani kwake, aliwaita watoto wake wote wanne chumbani kwake na kujifungia nao ndani, kisha akawaambia “tunaondoka” watoto wale walimuuliza, “tunakwenda wapi?” yeye akawajibu, “tunasafiri, lakini huko tunakokwenda hatupajui.” Aliwabusu watoto wale na wao wakambusu mama yao na kisha wakapeana mikono kama ishara ya kutakiana safari njema. Baada ya tukio hilo, aliwapa kila mmoja kikombe chenye mchanganyiko wa ile sumu na Orange Squash na yeye akachukua mchanganyiko huo uliokuwa kwenye kikombe na kunywa. Baada ya kunywa mchanganyiko huo wote walianza kutapika, kutokana na kutapika huko, aliamua kunywa Iodine. Pia alikunywa vipande vya chupa zilizosagwa na kujifungia katika chumba kingine.

      Mfanya kazi wake wa hapo nyumbani aitwae Ramadhan na mtu mwingne aliyetajwa kwa jina la Bibie waliwasikia watoto wakilia huko chumbani. Baadae kidogo alifungua mlango na kumwambia Bibie amuoshe mmoja wa watoto wale ambaye alikuwa ni mdogo kwa wenzie kwani alikuwa anatapika na kuharisha kisha akarudi ndani na kujifungia katika chumba hicho peke yake.

      Aliombwa na Ramadhan pamoja na Bibie watumie simu ya pale nyumbani kumjulisha mumewe juu ya tatizo lile lakini alikataa.

      Wale watoto wengine watatu nao walianza kutapika na kuharisha na hali zao zilibadilika na kuwa mbaya. Ramadhan aliwajulisha majirani na walipofika, yeye alikwenda hadi chumba cha pili alipokuwa amejifungia na kumuuliza kama ni kitu gani kimewatokea wale watoto. Alimwambia, “Ramadhan, naomba uniache nife na watoto wangu, kwa sababu baba Taji (yaani Mumewe) hanipendi.”

      Wote walikimbizwa hospitalini na watoto watatu waliripotiwa kufariki lakini yeye na mwanaye mkubwa madaktari walifanikiwa kuyanusuru maisha yao.

      Taarifa ya kitabibu ilithibitisha kwamba wale watoto watatu walifariki kutokana na kunywa sumu, ambayo walinywesha na mama yao.

      Kesi hii ni ya mwaka 1979 ya Agnes Doris Liundi, alishitakiwa na Jamhuri kwa kosa la kuwauwa watoto wake watatu kwa kuwanywesha sumu hapo mnamo tarehe 21 Februari 1978 nyumbani kwake. Kosa hilo la Kuua kwa kukusudia (Murder) limeainishwa kwenye kanuni ya adhabu (Penal Code) kifungu cha 196.

      Kwa mujibu wa maelezo yaliyosomwa pale mahakamani wakati wa kusikilizwa kwa kesi hii ilielezwa kwamba, Agnes Doris Liundi aliolewa na George Liundi mnamo Februari 1967.

      Baada ya miaka miwili ya maisha yao ya ndoa iliyokuwa na furaha na amani, ghafla kukazuka kutoelewana na ugomvi usiyoisha kati ya wanandoa hao. Sababu iliyoelezwa kusababisha kutokuelewana huko ni hofu aliyokuwa nayo mume kuwa huenda mkewe siyo muaminifu kwake.

      Kutokana na ugomvi huo, mtuhumiwa alifukuzwa hapo nyumbani kwao na mumewe.

      Kama wiki moja hivi kabla ya kutekeleza mauaaji hayo, Mtuhumiwa na mumewe walihudhuria sherehe fulani. Wakiwa hapo kwenye hiyo sherehe ndipo mumewe alipomuona mwanaume mmoja ambaye alimtuhumu kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe na ndipo ule uhasama wao ukaibuka upya na kukazuka ugomvi mkubwa kati yao, yaani mtuhumiwa na mumewe, na ndio ukapelekea mtuhumiwa kutekeleza mauaji hayo siku ya tarehe 21, Februari 1978.

      Ilielezwa pale mahakamni kwamba, kabla ya kutekeleza mauaji hayo, mtuhumiwa aliandika barua nne na zote zilikuwa na tarehe hiyo ya 21 Februari 1978, na barua hizo ziligunduliwa na Polisi na zilifikishwa pale mahakamani kama kidhibiti. Barua tatu zilikuwa zimendikwa kichwa cha habari kisemacho, “kwa yeyote anayehusika,” na moja ilikuwa inamuhusu mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la mama Gaudensia ambaye ni rafiki wa mtuhumiwa.

      Barua moja kati ya zile tatu zilizoandikwa kichwa cha habari kisemacho “Kwa yeyote anayehusika” ilisomwa pale mahakamani kama ifuatavyo:

      c/o Box 9050
      DAR ES SALAAM

      21/2/1978


      KWA YEYOTE ANAYEHUSIKA


      Uamuzi niliouchukuwa ni wa mwisho. George mume wangu naomba asisumbuliwe au kuteswa au kulazimishwa kwa namna yoyote kwa sababu nilikuwa nampenda.

      Nimewachukuwa wanangu kwa sababu sitaki wateseke kama nilivyoteseka katika upweke wa kutisha. George mume wangu, hukujua ni kiasi gani nilikupenda nilipokuwa hai. Lakini sasa unaelewa.

      KWA AFISA WA POLISI

      Tafadhali msimchukulie mume wangu hatua yoyote kwa sababu hana hatia.

      Kwa mujibu wa maelezo yake aliyoandikisha Polisi hapo mnamo 3 April 3, 1978, ikiwa ni miezi miwili baada ya tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa alieleza historia ya maisha yake tangu utotoni. Alieleza jinsi alivyoishi maisha ya tabu na mashaka baada ya mama yake kufariki ambapo alililelewa kwa mateso na upweke na mama yake wa kambo.

      Mtuhumiwa alielezea maisha yao ya ndoa na mumewe yalivyokuwa na furaha na amani kwa kipindi cha miaka miwili tangu waoane, na jinsi maisha yalivyobadilika na ndoa yake kukumbwa na misukosuko isiyoisha.

      Alisema kwamba, matatizo yalianza baada ya yeye kudai kwamba aliwahi kubakwa na kaka wa mmoja wa marafiki zake, na kutokana na kitendo hicho alimuambukiza mumewe maradhi ya zinaa. Hakuthubutu kumweleza mumewe kuhusu tukio hilo la kubakwa kwa muda mrefu alitunza siri hiyo, lakini baadae aliaamua kumweleza mumewe, jambo ambalo lilimletea matatizo makubwa katika ndoa yake mpaka kupelekea tukio hilo la tarehe 21 Februari 1978.

      Wakati mumewe anaondoa hapo nyumbani siku hiyo ya tarehe 21 Februari 1978, mtuhumiwa alichanganyikiwa na alianza kukumbuka maisha yake ya utotoni jinsi yalivyokuwa ya mateso na kujikuta akiwa hana pa kwenda. Alimuona mumewe kama mama yake, baba yake, kaka yake na dada yake na maisha yake yote alikuwa akimtegemea mume wake huyo.

      Aliamua kwenda kununua sumu na kurudi nayo nyumbani, alijaribu kulala lakini hakupata lepe la usingizi na hakupata suluhu, nini cha kufanya kuhusiana na jambo hilo, na ndipo alipoamua kunywa hiyo sumu.

      Kwa maelezo yake mwenyewe alisema:

      “Nilikuwa na hasira na wasiwasi kuhusiana na matatizo kati yangu na mume wangu. Nilijiuliza, ina maana matatizo haya yamefikia hatua ya kutisha kiasi cha mume wangu kufikia hatua ya kunifukuza. Nilijiwa na wazo kwamba, acha nijimalize (Kujiuwa) mwenyewe niwaache wanangu wakiwa hai. Lakini baadae nilianza kukumbuka maisha yangu ya utotoni jinsi yalivyokuwa ya mateso na upweke, na nilijiuliza kwamba huenda na wanangu nao wataishi maisha kama yangu kwa kuishi na mama wa kambo. Kwa kuwa mume wangu aliniambia nitakapoondoka nihakikishe siwaachi wanangu nyuma, niliamua kuwachukuwa na kuingia nao chumbani na kufunga mlango. kisha nikawaambia “tunaondoka” wakaniuliza, “tunakwenda wapi?” nikawajibu, “tunasafiri, lakini huko tunakokwenda hatupajui.” Kisha nikawabusu na wao wakanibusu, wakapeana mikono kama ishara ya kutakiana safari njema. niliwapa kila mmoja kikombe chenye mchanganyiko wa ile sumu na Orange Squash na mimi nikachukua mchanganyiko huo uliokuwa kwenye glasi na kunywa. Baada ya kunywa mchanganyiko huo wote tulianza kutapika, kutokana na kutapika huko, aliamua kunywa Iodine. Pia nilikunywa vipande vya chupa zilizosagwa na kujifungia katika chumba kingine. Kutoka muda huo, nilipoteza fahamu na sikuweza kutambua kilichotokea baada ya hapo”

      Wakati alipokamatwa mtuhumiwa alikuwa chini ya uangalizi wa daktari aliyejulikana kwa jina la Dk. Haule, huyu ni mtaalamu wa magonjwa ya akili aliyekuwa akifanya kazi katika Hospitali ya Muhimbili.

      Aliwasilisha ripoti yake pale mahakamani na pia alitoa ushahidi wake pale mahakamani. Kwa kifupi katika maoni yake Dk. Haule alisema kwamba, wakati akitekeleza tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya, alikuwa anajua kwamba anawauwa watoto wake kwa kuwalisha sumu, lakini hakujua kwamba kufanya kitendo hicho ni kosa.

      Kwa mujibu wa vifungu vya 12 na 13 vya sheria ya kanuni ya adhabu ambavyo vinahusika na swala hili la uwendawazimu vinaeleza kama ifuatavyo:

      Kifungu cha 12. Sheria inamchukulia mtu yeyote kuwa ni mwenye akili timamu kwa wakati wowote mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo.

      Kifungu cha 13. Mtu yeyote hawezi kuchukuliwa kuwa ametenda kosa kama kutenda kwake au kutokutenda kwake na katika muda wa kutenda au kutokutenda alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa na akili na hivyo kumfanya kutokutambua alichokuwa anakifanya.

      Dk. Haule katika ushahidi wake kwenye ripoti yake aliainisha vidokezo vifuatavyo,

      Kwa mara ya kwanza alipomuona mtuhumiwa muda mfupi baada ya tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa hakuwa katika hali ya kawaida na hakuonekana kujali. “nilikuwa kama vile naongea na mti.” Alisema Dk. Haule. Kwa maoni yake Dk. Haule alisema, inawezekana kwamba mtuhumiwa alikuwa katika hali ya isiyo ya kawaida kwa majuma mawili au zaidi kabla ya tukio hilo, na kwamba, mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya wakati alipokuwa akiwanywesha sumu wanae, lakini hakujua kwamba kitendo hicho ni kosa.

      Alielezea juu ya kipindi kigumu cha maisha ya ndoa ya mtuhumiwa alichopitia, jinsi maisha yake ya ndoa yalivyokumbwa na misukosuko ya kutoelewana na mumewe. Nafasi aliyokuwa nayo, maisha aliyopitia utotoni na jinsi alivyokuwa akimtegemea na kumtii mumewe. Dk. Haule, alikuwa na maoni kwamba, kitendo cha mtuhumiwa kuamua kujiuwa na kuwaua wanae, aliamini kwamba, alikuwa amemriwa na mumewe afanye hivyo. Alisema kwamba, alisoma barua zilizokuwa zimeandikwa na mtuhumiwa kabla ya kutekeleza mauaji hayo lakini barua hizo hazikuweza kubadili maoni yake juu ya jambo hilo.

      Wakati fulani Dk Haule alidai kwamba mtuhumiwa hakuwa na tatizo la kurukwa na akili lakini baadae alisema kwamba mtuhumiwa alikuwa na tatizo hilo.

      Kwaq mamneno yake mwenyewe Dk. Haule alisema. “Alikuwa amerukwa na akili, na aliona kitendo alichokifanya kilikuwa kinakubalika.”

      Dk. Haule alisema kwamba, mwaka mmoja baada ya tukio hilo hali ya mtuhumiwa iliimarika, kiasi cha kujua kwamba, kitendo alichokifanya kilikuwa ni kosa, lakini bado alikuwa kwenye matibabu.

      Katika kesi hii mwanasheria aliyekuwa akimtetea mtuhumiwa alikuwa ameegemea kwenye utetezi wa uwendawazimu.

      Akitoa utetezi wake wakili Jadeda alisema kwamba, wakati mtuhumiwa akitekeleza mauaji hayo, hakuwa akijua kwamba kitendo anachokifanya ni kosa. Wakili huyo alirejea maoni ya Dk. Haule.

      Wakili huyo alisema kwamba, mtu yeyote aliyerukwa na akili anaweza kupanga hatua kwa hatua kutekeleza mauaji kama aliavyofanya mtuhumiwa na asijue kama kitendo alichokifanya ni kosa.
      Wakili Jadeda alikuwa akipinga maoni ya upande wa mashitaka kwamba, mtuhumiwa alikuwa kijua kitendo anachokifanya ni kosa.

      Akisoma hukumu Mheshimiwa Jaji Makame alikubaliana na swala la mtuhumiwa kuwa na dhamira ovu (Malice aforethought), hasa kwa kuangalia vitendo vya mtuhumiwa tangu maandalizi, dhamira na akiwa na utambuzi kwamba, akiwanywesha wanae sumu itawasababishia kifo, na hiyo inadhihirisha kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya, na si lazima ajue kwamba kufanya hivyo ni kosa.

      Hata hivyo Mheshimiwa Jaji Makame alikuwa ameshawishika kuamini hivyo kutokana na barua nne alizoziandika mtuhumiwa kabla ya kutekeleza mauaji hayo, ambazo aliziandika sambamba na tendo alilofanya tarehe 21 Februari 1978. Barua hizo kwa uwazi zilionyesha kabisa kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua anachokifanya ni kosa.

      Kwa maneno yake Mwenyewe Mheshimiwa Jaji Makame alisema, “Katika barua ambayo ilisomwa hapa mahakamani wakati wa shauri hili, mtuhumiwa alisema wazi kwamba mumewe asije akaadhibiwa au kuteswa kwa kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa. Pia kulikuwa na ombi la mtuhumiwa kwa Polisi kwamba, wasije wakamchukulia hatua mumewe kwa sababu hana hatia.”

      Muheshimiwa Jaji Makame aliendelea kusema kwamba, wazo la kutokuwa na hatia na kutompa mumewe adhabu katika barua alizoandika mtuhumiwa, linadhihirisha wazi kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua kwamba kitendo anachokifanya ni kosa na alitaka kuweka wazi kuwa mumewe hahusiki kwa namna yoyote na kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa. Alijua kama mumewe akihusishwa na kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa, ataadhibiwa kwa kosa hilo.

      Mheshimiwa Jaji Makame aliendelea kusema,

      “Ni kweli Dk. Haule alisema kwamba, ukiachana na barua hizo alizoziandika mtuhumiwa, lakini yeye alikuwa na maoni kwamba, mtuhumiwa hakuwa anajua anachokifanya kuwa ni kosa. Alisema, barua zilimuonesha kwamba, mtuhumiwa alikuwa akimtegemea mumewe kwa kiasi kikubwa na hasa katika mahusiano yao. Kama tunamuelewa Dk. Hauli vizuri, alikuwa huenda anamaanisha kwamba, hizo barua zilikuwa na uhusiano na imani aliyokuwa nayo mtuhumiwa kwamba, alikuwa ameshurutishwa kujiuwa na kuwauwa watoto wake na mumewe. Kwa bahati mbaya barua haijaeleza kuwa mtuhumiwa alikuwa na imani ile. Ilikuwa ni ahuweni aliyoiweka Dk Hauli. Japokuwa barua ilieleza kuwa mtuhumiwa alikuwa anamtegemea sana mumewe, lakini bado zilikuwa zinathibitisha kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua kitendo anachokifanya ni kosa.
      Pia nashindwa kuunganisha maelezo ya barua hizo na maoni ya kurukwa na akili yaliyotolewa na Dk. Haule, aliposema kwamba, mtuhumiwa aliamini kuwa ameamriwa na mumewe ajiuwe na kuwauwa watoto wake.”

      Mheshimiwa Jaji aliendelea kusema,

      “Kwangu mimi, namuona Dr. Hauli kama mtaalamu mwenye uzoefu na ujuzi mkubwa wa magonjwa ya akili, pamoja na mambo mengine, pia ni mwanachama Royal College of Psychiatrists na anayo Diploma ya Psychiatric Medicine aliyoipata nchini Uingereza. Naheshimu sana maoni yake kulingana na utaalamu wake na ninashindwa kupinga ushahidi wake. Pia ninakubaliana na ukweli kwamba hata kama mtuhumiwa ataonyesha kurukwa lakini hiyo itakubalika iwapo kutakuwa na kipimo chenye uwelekeo (Balance of Probability).

      Mtuhumiwa lazima aoneshe ushahidi wote; kwamba kutokuwa na akili timamu ni zaidi ya kuwa timamu. Ingawa inawezekana ikawa chini ya tunachodhamiria. Katika kuliweka sawa hili mamlaka ya kuthibitisha inafananishwa na kesi ya Nyinge Siwato Vs Jamhuri 1959 East Africa 974 ikifuatiwa mara nyingi sana ikihusishwa na MbekuleV-R. 1971, East Africa 479. Jaji Enzi zake alielezea katika kesi ya Siwato “Mahakama haifungwi kukubaliana na ushahidi wa hospitalini (Medical Testimony) kama/endapo kuna sababu madhubuti ya kutofanya hivyo. mwisho wa siku ni kazi ya mahakama kutafuta ushahidi na viambatanisho katika kufanya hivyo, ni wajibu wangu kuangalia na kulipima na ushahidi uliotolewa kabla na ikiwemo utaalam wa Daktari.”

      Mheshimiwa Jaji Makame akihitimisha hukumu hiyo alisema:

      “Inawezekana hasa kwamba sheria yetu katika swala la kurukwa na akili imepitwa na wakati na ni ya zamani sana, Dk. Haule katika ushahidi alieleza kuwa katika utaalamu wa sasa, utofauti kati ya kurukwa na akili na kutojitambua katika utenedaji vinapingana. Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa hekima linaweza kulifanyia marekebisho hili sambamba na sheria ndogo ndogo na kulileta katika utandawazi wa kitabibu. Mipaka ya kimahakama, ikiwemo ya Afrika Mashariki wamefanya hivyo.”

      Mtuhumiwa katika kesi hii alihukumiwa kunyongwa.
      JokaKuu, RR, NATA and 26 others like this.

    2. #81
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,256
      Rep Power : 31392
      Likes Received
      9623
      Likes Given
      685

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By Mujumba
      nikicompare na hii ya lulu wa kanumba basi naona katoto kuachiwa na kenyewe!
      Ushahidi wa kumpata Lulu na hatia sidhani kama upo!!
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.
      CAMARADERIE is offlinestyle="display:none;visibility:hidden;" data-cfsrc="template/JamiV1/default/misc/progress.gif" alt="" /> Reply With Quote

    3. #82
      CAMARADERIE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd March 2011
      Location : 1 Luthuli Street
      Posts : 4,163
      Rep Power : 2720
      Likes Received
      1587
      Likes Given
      1145

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By NATA
      Huyu Dr. Haule huyu ndiye yule wa Asha Mkwizu?
      Yule ni Dr Hauli
      Mtambuzi likes this.
      A compliment is something like a kiss through a veil




    4. #83
      Mwita Maranya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2008
      Location : Ikorongo Game Reserve
      Posts : 7,989
      Rep Power : 12010
      Likes Received
      5314
      Likes Given
      5144

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Ahsante sana Mtambuzi kwa kutuwezesha kuifahamu kesi hii kwa undani kidogo, maana tulikuwa tunaisikia kwa masimulizi ya juu juu.
      Kitu ambacho sijakiona katika kesi hii ni mashahidi wa pande zote mbili kama ilivyokuwa katika kesi ya Asha Mkwizu ama zile kesi za wamarekani. Hapa unaonekiana ushahidi wa daktari Haule pekee.

      Btw, hivi huyu daktari Haule ndiye yule aliyekuwa mume wa Asha Mkwizu ama ni majina tu yamefanana?
      Mtambuzi likes this.
      Honesty is a very expensive GIFT. Do not expect it from cheap people.

    5. #84
      Companero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2008
      Posts : 4,755
      Rep Power : 6504
      Likes Received
      955
      Likes Given
      1107

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      "Each generation must, out of relative obscurity, discover its mission, fulfil it, or betray it"/Kila kizazi, katika utata wa kipindi chake, lazima kiutambue wajibu wake na kiutekeleze au kiusaliti - Frantz Fanon

    6. #85
      mkonomtupu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th July 2011
      Location : Peponi
      Posts : 263
      Rep Power : 342
      Likes Received
      58
      Likes Given
      33

      Default

      Quote By Limbani
      Duh, huyu Taji mtoto aliyebaki ndio huyu mtangazaji Taji Liundi?
      Haswaa ndio huyohuyo. Hii kesi mama yangu alishawahi kunisimulia mwaka 1993. Very touching kwa kweli.
      Mtambuzi likes this.

    7. Miaka 50

    8. #86
      B'REAL's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2010
      Location : streat
      Posts : 1,206
      Rep Power : 677
      Likes Received
      196
      Likes Given
      82

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By Mtambuzi
      Haya ni Ijumaa nyingine tena wasomaji wa JF, nimekuja na kesi hii iliyowahi kutokea hapa hapa nchini miaka ya mwishoni mwa 1970. Leo sina maneno mengi, nawaachie wenyewe msome na kuweka maoani yenu...........
      mkuu we mwanasheriaa hizi kesi zako zinanivutia sanaaa
      Mtambuzi likes this.

    9. #87
      Ennie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th January 2011
      Location : DAR ES SALAAAM
      Posts : 1,594
      Rep Power : 817
      Likes Received
      498
      Likes Given
      539

      Default

      Quote By Bishanga
      Kwanza wali commute to
      life sentence,kisha Mwalimu akamuachia after seven years,she is alive
      and well,yuko hapa dar maeneo ya keko.
      ndiyo hivyo mambo ya sheria ila huyo baba(GEORGE) ana share yake ya lawama.

    10. #88
      Tusker Bariiiidi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2007
      Location : Sinza Dar es Salaam.
      Posts : 3,234
      Rep Power : 1254
      Likes Received
      376
      Likes Given
      51

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Nashukuru sana Mtambuzi,Pole Taji Liundi.

    11. #89
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,094
      Rep Power : 27014
      Likes Received
      8231
      Likes Given
      17325

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By NATA
      Huyu Dr. Haule huyu ndiye yule wa Asha Mkwizu?
      Kuna mdau alijibu hili swali.............

      Quote By ntogwisangu
      Thanks Mtambuzi!kesi hii ni moja ya kesi zilizowahi kutikisa jiji la Dar,kamakesi ilivyofuata kwenye miaka ya 80 mwanzoni kesi iliyomuhusu Dr huyu huyu kwenye kesi hii.Jambo kubwa hapa,kesi zote zilihusisha mambo ya mapenzi,tena kwa vijana wasomi wa kipindi hicho!na zote zilipelekea mauaji ya kutisha!!!Jamo moja kubwa la kujifunza hapa kwetu sote,pamoja na madhaifu yetu kama binadamu,hakuna jambo linaloweza kuumiza nafsi ya mwenzio kama usaliti wa mapenzi.Na basi tunapoamua kuingia katika ndoa ni lazima uamuzi huo uwe umefanyika kwa dhati!!Leo mzee Liundi pamoja na heshima yake katika jamii nadhani ni jambo linalomuumiza mpaka siku mauti yatakampomkuta!!!TUPENDANE KWA DHATI!!!!NDOA SIO MAIGIZO AU MAKARATASI YA MAKANISANI,MSIKITINI AU KWA MKUU WA WILAYA!!

    12. #90
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,094
      Rep Power : 27014
      Likes Received
      8231
      Likes Given
      17325

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By Mwita Maranya
      Ahsante sana Mtambuzi kwa kutuwezesha kuifahamu kesi hii kwa undani kidogo, maana tulikuwa tunaisikia kwa masimulizi ya juu juu.
      Kitu ambacho sijakiona katika kesi hii ni mashahidi wa pande zote mbili kama ilivyokuwa katika kesi ya Asha Mkwizu ama zile kesi za wamarekani. Hapa unaonekiana ushahidi wa daktari Haule pekee.

      Btw, hivi huyu daktari Haule ndiye yule aliyekuwa mume wa Asha Mkwizu ama ni majina tu yamefanana?
      Kwenye Bold, swali hili lilijibiwa na mdau hapa chini...........
      Quote By ntogwisangu
      Thanks Mtambuzi!kesi hii ni moja ya kesi zilizowahi kutikisa jiji la Dar,kamakesi ilivyofuata kwenye miaka ya 80 mwanzoni kesi iliyomuhusu Dr huyu huyu kwenye kesi hii.Jambo kubwa hapa,kesi zote zilihusisha mambo ya mapenzi,tena kwa vijana wasomi wa kipindi hicho!na zote zilipelekea mauaji ya kutisha!!!Jamo moja kubwa la kujifunza hapa kwetu sote,pamoja na madhaifu yetu kama binadamu,hakuna jambo linaloweza kuumiza nafsi ya mwenzio kama usaliti wa mapenzi.Na basi tunapoamua kuingia katika ndoa ni lazima uamuzi huo uwe umefanyika kwa dhati!!Leo mzee Liundi pamoja na heshima yake katika jamii nadhani ni jambo linalomuumiza mpaka siku mauti yatakampomkuta!!!TUPENDANE KWA DHATI!!!!NDOA SIO MAIGIZO AU MAKARATASI YA MAKANISANI,MSIKITINI AU KWA MKUU WA WILAYA!!
      Kuhusu maelezo ya mashahidi naomba uniwie radhi, kwani nilipata kesi ya rufaa, na sikupata kesi ya mahakama kuu ambayo ina details zote...........Nasikitika kwamba juhudi zangu hazikuzaa matunda, lakini naamini sijawaangusha, nimejitahidi kuiandika kwa makini ili nisipoteze maana.

    13. #91
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,094
      Rep Power : 27014
      Likes Received
      8231
      Likes Given
      17325

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By Ronn M
      Doris alikuwa na state of mind which would be subjected to defence of diminishing responsibility. This defence is given when an accused mind was 'impaired' at the time of committing a crime. However it was not in our laws at the time. The judge could not read it in our laws or at invoke it as a new law
      Ronn M ..........Ahsante kwa maoni yako.......... Naomba usaidie kujibu baadhi ya maswali ya kisheria yatakayojitokeza humu, maana ki ukweli mimi sio mtaalamu wa sheria........................ !

    14. #92
      Ronn M's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Location : Moshi~Arusha
      Posts : 1,283
      Rep Power : 612
      Likes Received
      660
      Likes Given
      403

      Default

      Quote By Mujumba
      nikicompare na hii ya lulu wa kanumba basi naona katoto kuachiwa na kenyewe!
      Kezi za jinai huwa proved beyond reasonable doubt, yaani mtu mwenye akili timamu akiulizwa kuhusu hatia ya mtuhumiwa aseme bila shaka yoyote kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo! Sasa hii ya Lulu kila mwenye akili timamu anajiuliza 'ni kweli haka 'katoto' kalimwua kanumba? In absence of clear evidence this kid will be free, most likely
      Mtambuzi likes this.

    15. #93
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,094
      Rep Power : 27014
      Likes Received
      8231
      Likes Given
      17325

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By The Listener
      Thanx brother Mtambuzi. Nimekuja tena kwa mara nyingine mimi ex detective - the listener. Wakati naanza kusoma kisa hiki katika hatua za mwanzo mwanzo akilini ikawa inanijia picha ya kuwa huyu mama atashinda kesi kwani yaonekana kweli alipata rukwa na akili - temporary insanity'. Kama zisingekuwepo barua alizoandika na kuonyesha dhamira yake ya kufanya mauaji ya watotot wake, kuna kila dalili kuwa angeweza kuwa huru. Barua hizi zinaonyesha wazi kuwa alikuwa anajua fika ni nini alikuwa anakifanya wakati anawapa sumu wanae na suala hili hasa ndo lililopelekea kumtia hatiani

      Thanx again brother kwa visa hivi kwani naona narefresh kwa kazi nilizofanya miaka ya nyuma. I hope next friday utakuja na kitu kingine motomoto
      The Listener ...............Mkuu nautambua uwepo wako katika thread hii, leo mimi nimeamua nisiwe mchangiaji sana niwaachie wasomaji...................... .

    16. #94
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,636
      Rep Power : 16776
      Likes Received
      2514
      Likes Given
      1934

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Kwa hiyo mzee Liundi mwenyewe hakuingizwa katika kesi?

    17. #95
      Ronn M's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Location : Moshi~Arusha
      Posts : 1,283
      Rep Power : 612
      Likes Received
      660
      Likes Given
      403

      Default

      Quote By Mtambuzi
      Ronn M ..........Ahsante kwa maoni yako.......... Naomba usaidie kujibu baadhi ya mashali ya kisheria yatakayojitokeza humu, maana ki ukweli mimi sio mtaalamu wa sheria........................ !
      Bila shaka mkuu, nitajitahidi pale niwezapo na kupata muda

    18. #96
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,094
      Rep Power : 27014
      Likes Received
      8231
      Likes Given
      17325

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By Ronn M
      Kezi za jinai huwa proved beyond reasonable doubt, yaani mtu mwenye akili timamu akiulizwa kuhusu hatia ya mtuhumiwa aseme bila shaka yoyote kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo! Sasa hii ya Lulu kila mwenye akili timamu anajiuliza 'ni kweli haka 'katoto' kalimwua kanumba? In absence of clear evidence this kid will be free, most likely
      Ronn M ...............Nimekusoma mkuu..........Ahsante sana

    19. #97
      Ronn M's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Location : Moshi~Arusha
      Posts : 1,283
      Rep Power : 612
      Likes Received
      660
      Likes Given
      403

      Default

      Quote By Katavi
      Kwa hiyo mzee Liundi mwenyewe hakuingizwa katika kesi?
      Yeap, hakushtakiwa maana hakuhusika katika mauaji yale
      Mtambuzi likes this.

    20. #98
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,256
      Rep Power : 31392
      Likes Received
      9623
      Likes Given
      685

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By Ronn M
      Kezi za jinai huwa proved beyond reasonable doubt, yaani mtu mwenye akili timamu akiulizwa kuhusu hatia ya mtuhumiwa aseme bila shaka yoyote kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo! Sasa hii ya Lulu kila mwenye akili timamu anajiuliza 'ni kweli haka 'katoto' kalimwua kanumba? In absence of clear evidence this kid will be free, most likely
      Hiyo standard ya beyond a reasonable doubt nayo ni subjective vile vile. O.J. Simpson watu wengi waliona kuwa ana hatia. Ushahidi wa kisayansi pia ulionyesha hatia yake. Hata physical evidence pia zilionyesha ana hatia. Lakini jurors wakamuona hana hatia.

      The bottom line is law is maddeningly subjective because so much is usually left up to individual interpretation and that's why sometimes you have wrongful convictions and wrongful acquittals.
      Mtambuzi and Ronn M like this.
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    21. #99
      Ronn M's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Location : Moshi~Arusha
      Posts : 1,283
      Rep Power : 612
      Likes Received
      660
      Likes Given
      403

      Default

      Quote By Nyani Ngabu
      Hiyo standard ya beyond a reasonable doubt nayo ni subjective vile vile. O.J. Simpson watu wengi waliona kuwa ana hatia. Ushahidi wa kisayansi pia ulionyesha hatia yake. Hata physical evidence pia zilionyesha ana hatia. Lakini jurors wakamuona hana hatia.

      The bottom line is law is maddeningly subjective because so much is usually left up to individual interpretation and that's why sometimes you have wrongful convictions and wrongful acquittals.
      You are right, subjective interpretation is a problem. Just like many of Tanzanian judges do, especially where there are some interest involved. Likewise appealling system is there to make sure there is checks and balance, very unfortunately it doesnt work with our political courts here in Tanzania
      Mtambuzi likes this.

    22. #100
      Mwita Maranya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2008
      Location : Ikorongo Game Reserve
      Posts : 7,989
      Rep Power : 12010
      Likes Received
      5314
      Likes Given
      5144

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By Mtambuzi
      Kuhusu maelezo ya mashahidi naomba uniwie radhi, kwani nilipata kesi ya rufaa, na sikupata kesi ya mahakama kuu ambayo ina details zote...........Nasikitika kwamba juhudi zangu hazikuzaa matunda, lakini naamini sijawaangusha, nimejitahidi kuiandika kwa makini ili nisipoteze maana.
      Mkuu Mtambuzi nimekuelewa sana, najua utunzaji wa kumbukumbu katika taasisi zetu za umma bado ni tatizo na ukizingatia mahakama ndiyo kabisa, bado hawajaweza kuziweka kwenye electronics devices ili iwe rahisi kupata rejea.

      Bila shaka tumenufaika sana na maelezo haya uliyoyatoa hapa na ninakutakia tu afya njema ili uendelee kutupa darasa la maisha hapa JF. Naamini panapo majaliwa yake Mwenyezi Mungu utafikia lengo lako la kuwafikia watanzania wengi kupitia vyombo vingine vya habari mathalani magazeti, majarida na television.
      Mtambuzi likes this.
      Honesty is a very expensive GIFT. Do not expect it from cheap people.

    Page 5 of 8 FirstFirst ... 34567 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...