Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

    Report Post
    Page 3 of 8 FirstFirst 12345 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 153
    1. #1
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8242
      Likes Given
      17377

      Default Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?


      Attachment 54031

      Attachment 54032


      Tukio lenyewe lilitokea hapo majira ya asubuhi mnamo Februari 21, 1978. Ni baada ya kuambiwa mumewe wakati anaenda kazini kwamba akirudi asimkute hapo nyumbani, na kama akimkuta, atamtoa hapo nyumbani kwake uchi. Alikuwa na watoto wao wanne hapo nyumbani. Baada ya mumewe kuondoka, na yeye aliondoka na gari kuelekea mjini ambapo alinunua chupa kadhaa za sumu ya kuulia wadudu.


      Alipofika nyumbani kwake, aliwaita watoto wake wote wanne chumbani kwake na kujifungia nao ndani, kisha akawaambia “tunaondoka” watoto wale walimuuliza, “tunakwenda wapi?” yeye akawajibu, “tunasafiri, lakini huko tunakokwenda hatupajui.” Aliwabusu watoto wale na wao wakambusu mama yao na kisha wakapeana mikono kama ishara ya kutakiana safari njema. Baada ya tukio hilo, aliwapa kila mmoja kikombe chenye mchanganyiko wa ile sumu na Orange Squash na yeye akachukua mchanganyiko huo uliokuwa kwenye kikombe na kunywa. Baada ya kunywa mchanganyiko huo wote walianza kutapika, kutokana na kutapika huko, aliamua kunywa Iodine. Pia alikunywa vipande vya chupa zilizosagwa na kujifungia katika chumba kingine.

      Mfanya kazi wake wa hapo nyumbani aitwae Ramadhan na mtu mwingne aliyetajwa kwa jina la Bibie waliwasikia watoto wakilia huko chumbani. Baadae kidogo alifungua mlango na kumwambia Bibie amuoshe mmoja wa watoto wale ambaye alikuwa ni mdogo kwa wenzie kwani alikuwa anatapika na kuharisha kisha akarudi ndani na kujifungia katika chumba hicho peke yake.

      Aliombwa na Ramadhan pamoja na Bibie watumie simu ya pale nyumbani kumjulisha mumewe juu ya tatizo lile lakini alikataa.

      Wale watoto wengine watatu nao walianza kutapika na kuharisha na hali zao zilibadilika na kuwa mbaya. Ramadhan aliwajulisha majirani na walipofika, yeye alikwenda hadi chumba cha pili alipokuwa amejifungia na kumuuliza kama ni kitu gani kimewatokea wale watoto. Alimwambia, “Ramadhan, naomba uniache nife na watoto wangu, kwa sababu baba Taji (yaani Mumewe) hanipendi.”

      Wote walikimbizwa hospitalini na watoto watatu waliripotiwa kufariki lakini yeye na mwanaye mkubwa madaktari walifanikiwa kuyanusuru maisha yao.

      Taarifa ya kitabibu ilithibitisha kwamba wale watoto watatu walifariki kutokana na kunywa sumu, ambayo walinywesha na mama yao.

      Kesi hii ni ya mwaka 1979 ya Agnes Doris Liundi, alishitakiwa na Jamhuri kwa kosa la kuwauwa watoto wake watatu kwa kuwanywesha sumu hapo mnamo tarehe 21 Februari 1978 nyumbani kwake. Kosa hilo la Kuua kwa kukusudia (Murder) limeainishwa kwenye kanuni ya adhabu (Penal Code) kifungu cha 196.

      Kwa mujibu wa maelezo yaliyosomwa pale mahakamani wakati wa kusikilizwa kwa kesi hii ilielezwa kwamba, Agnes Doris Liundi aliolewa na George Liundi mnamo Februari 1967.

      Baada ya miaka miwili ya maisha yao ya ndoa iliyokuwa na furaha na amani, ghafla kukazuka kutoelewana na ugomvi usiyoisha kati ya wanandoa hao. Sababu iliyoelezwa kusababisha kutokuelewana huko ni hofu aliyokuwa nayo mume kuwa huenda mkewe siyo muaminifu kwake.

      Kutokana na ugomvi huo, mtuhumiwa alifukuzwa hapo nyumbani kwao na mumewe.

      Kama wiki moja hivi kabla ya kutekeleza mauaaji hayo, Mtuhumiwa na mumewe walihudhuria sherehe fulani. Wakiwa hapo kwenye hiyo sherehe ndipo mumewe alipomuona mwanaume mmoja ambaye alimtuhumu kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe na ndipo ule uhasama wao ukaibuka upya na kukazuka ugomvi mkubwa kati yao, yaani mtuhumiwa na mumewe, na ndio ukapelekea mtuhumiwa kutekeleza mauaji hayo siku ya tarehe 21, Februari 1978.

      Ilielezwa pale mahakamni kwamba, kabla ya kutekeleza mauaji hayo, mtuhumiwa aliandika barua nne na zote zilikuwa na tarehe hiyo ya 21 Februari 1978, na barua hizo ziligunduliwa na Polisi na zilifikishwa pale mahakamani kama kidhibiti. Barua tatu zilikuwa zimendikwa kichwa cha habari kisemacho, “kwa yeyote anayehusika,” na moja ilikuwa inamuhusu mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la mama Gaudensia ambaye ni rafiki wa mtuhumiwa.

      Barua moja kati ya zile tatu zilizoandikwa kichwa cha habari kisemacho “Kwa yeyote anayehusika” ilisomwa pale mahakamani kama ifuatavyo:

      c/o Box 9050
      DAR ES SALAAM

      21/2/1978


      KWA YEYOTE ANAYEHUSIKA


      Uamuzi niliouchukuwa ni wa mwisho. George mume wangu naomba asisumbuliwe au kuteswa au kulazimishwa kwa namna yoyote kwa sababu nilikuwa nampenda.

      Nimewachukuwa wanangu kwa sababu sitaki wateseke kama nilivyoteseka katika upweke wa kutisha. George mume wangu, hukujua ni kiasi gani nilikupenda nilipokuwa hai. Lakini sasa unaelewa.

      KWA AFISA WA POLISI

      Tafadhali msimchukulie mume wangu hatua yoyote kwa sababu hana hatia.

      Kwa mujibu wa maelezo yake aliyoandikisha Polisi hapo mnamo 3 April 3, 1978, ikiwa ni miezi miwili baada ya tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa alieleza historia ya maisha yake tangu utotoni. Alieleza jinsi alivyoishi maisha ya tabu na mashaka baada ya mama yake kufariki ambapo alililelewa kwa mateso na upweke na mama yake wa kambo.

      Mtuhumiwa alielezea maisha yao ya ndoa na mumewe yalivyokuwa na furaha na amani kwa kipindi cha miaka miwili tangu waoane, na jinsi maisha yalivyobadilika na ndoa yake kukumbwa na misukosuko isiyoisha.

      Alisema kwamba, matatizo yalianza baada ya yeye kudai kwamba aliwahi kubakwa na kaka wa mmoja wa marafiki zake, na kutokana na kitendo hicho alimuambukiza mumewe maradhi ya zinaa. Hakuthubutu kumweleza mumewe kuhusu tukio hilo la kubakwa kwa muda mrefu alitunza siri hiyo, lakini baadae aliaamua kumweleza mumewe, jambo ambalo lilimletea matatizo makubwa katika ndoa yake mpaka kupelekea tukio hilo la tarehe 21 Februari 1978.

      Wakati mumewe anaondoa hapo nyumbani siku hiyo ya tarehe 21 Februari 1978, mtuhumiwa alichanganyikiwa na alianza kukumbuka maisha yake ya utotoni jinsi yalivyokuwa ya mateso na kujikuta akiwa hana pa kwenda. Alimuona mumewe kama mama yake, baba yake, kaka yake na dada yake na maisha yake yote alikuwa akimtegemea mume wake huyo.

      Aliamua kwenda kununua sumu na kurudi nayo nyumbani, alijaribu kulala lakini hakupata lepe la usingizi na hakupata suluhu, nini cha kufanya kuhusiana na jambo hilo, na ndipo alipoamua kunywa hiyo sumu.

      Kwa maelezo yake mwenyewe alisema:

      “Nilikuwa na hasira na wasiwasi kuhusiana na matatizo kati yangu na mume wangu. Nilijiuliza, ina maana matatizo haya yamefikia hatua ya kutisha kiasi cha mume wangu kufikia hatua ya kunifukuza. Nilijiwa na wazo kwamba, acha nijimalize (Kujiuwa) mwenyewe niwaache wanangu wakiwa hai. Lakini baadae nilianza kukumbuka maisha yangu ya utotoni jinsi yalivyokuwa ya mateso na upweke, na nilijiuliza kwamba huenda na wanangu nao wataishi maisha kama yangu kwa kuishi na mama wa kambo. Kwa kuwa mume wangu aliniambia nitakapoondoka nihakikishe siwaachi wanangu nyuma, niliamua kuwachukuwa na kuingia nao chumbani na kufunga mlango. kisha nikawaambia “tunaondoka” wakaniuliza, “tunakwenda wapi?” nikawajibu, “tunasafiri, lakini huko tunakokwenda hatupajui.” Kisha nikawabusu na wao wakanibusu, wakapeana mikono kama ishara ya kutakiana safari njema. niliwapa kila mmoja kikombe chenye mchanganyiko wa ile sumu na Orange Squash na mimi nikachukua mchanganyiko huo uliokuwa kwenye glasi na kunywa. Baada ya kunywa mchanganyiko huo wote tulianza kutapika, kutokana na kutapika huko, aliamua kunywa Iodine. Pia nilikunywa vipande vya chupa zilizosagwa na kujifungia katika chumba kingine. Kutoka muda huo, nilipoteza fahamu na sikuweza kutambua kilichotokea baada ya hapo”

      Wakati alipokamatwa mtuhumiwa alikuwa chini ya uangalizi wa daktari aliyejulikana kwa jina la Dk. Haule, huyu ni mtaalamu wa magonjwa ya akili aliyekuwa akifanya kazi katika Hospitali ya Muhimbili.

      Aliwasilisha ripoti yake pale mahakamani na pia alitoa ushahidi wake pale mahakamani. Kwa kifupi katika maoni yake Dk. Haule alisema kwamba, wakati akitekeleza tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya, alikuwa anajua kwamba anawauwa watoto wake kwa kuwalisha sumu, lakini hakujua kwamba kufanya kitendo hicho ni kosa.

      Kwa mujibu wa vifungu vya 12 na 13 vya sheria ya kanuni ya adhabu ambavyo vinahusika na swala hili la uwendawazimu vinaeleza kama ifuatavyo:

      Kifungu cha 12. Sheria inamchukulia mtu yeyote kuwa ni mwenye akili timamu kwa wakati wowote mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo.

      Kifungu cha 13. Mtu yeyote hawezi kuchukuliwa kuwa ametenda kosa kama kutenda kwake au kutokutenda kwake na katika muda wa kutenda au kutokutenda alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa na akili na hivyo kumfanya kutokutambua alichokuwa anakifanya.

      Dk. Haule katika ushahidi wake kwenye ripoti yake aliainisha vidokezo vifuatavyo,

      Kwa mara ya kwanza alipomuona mtuhumiwa muda mfupi baada ya tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa hakuwa katika hali ya kawaida na hakuonekana kujali. “nilikuwa kama vile naongea na mti.” Alisema Dk. Haule. Kwa maoni yake Dk. Haule alisema, inawezekana kwamba mtuhumiwa alikuwa katika hali ya isiyo ya kawaida kwa majuma mawili au zaidi kabla ya tukio hilo, na kwamba, mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya wakati alipokuwa akiwanywesha sumu wanae, lakini hakujua kwamba kitendo hicho ni kosa.

      Alielezea juu ya kipindi kigumu cha maisha ya ndoa ya mtuhumiwa alichopitia, jinsi maisha yake ya ndoa yalivyokumbwa na misukosuko ya kutoelewana na mumewe. Nafasi aliyokuwa nayo, maisha aliyopitia utotoni na jinsi alivyokuwa akimtegemea na kumtii mumewe. Dk. Haule, alikuwa na maoni kwamba, kitendo cha mtuhumiwa kuamua kujiuwa na kuwaua wanae, aliamini kwamba, alikuwa amemriwa na mumewe afanye hivyo. Alisema kwamba, alisoma barua zilizokuwa zimeandikwa na mtuhumiwa kabla ya kutekeleza mauaji hayo lakini barua hizo hazikuweza kubadili maoni yake juu ya jambo hilo.

      Wakati fulani Dk Haule alidai kwamba mtuhumiwa hakuwa na tatizo la kurukwa na akili lakini baadae alisema kwamba mtuhumiwa alikuwa na tatizo hilo.

      Kwaq mamneno yake mwenyewe Dk. Haule alisema. “Alikuwa amerukwa na akili, na aliona kitendo alichokifanya kilikuwa kinakubalika.”

      Dk. Haule alisema kwamba, mwaka mmoja baada ya tukio hilo hali ya mtuhumiwa iliimarika, kiasi cha kujua kwamba, kitendo alichokifanya kilikuwa ni kosa, lakini bado alikuwa kwenye matibabu.

      Katika kesi hii mwanasheria aliyekuwa akimtetea mtuhumiwa alikuwa ameegemea kwenye utetezi wa uwendawazimu.

      Akitoa utetezi wake wakili Jadeda alisema kwamba, wakati mtuhumiwa akitekeleza mauaji hayo, hakuwa akijua kwamba kitendo anachokifanya ni kosa. Wakili huyo alirejea maoni ya Dk. Haule.

      Wakili huyo alisema kwamba, mtu yeyote aliyerukwa na akili anaweza kupanga hatua kwa hatua kutekeleza mauaji kama aliavyofanya mtuhumiwa na asijue kama kitendo alichokifanya ni kosa.
      Wakili Jadeda alikuwa akipinga maoni ya upande wa mashitaka kwamba, mtuhumiwa alikuwa kijua kitendo anachokifanya ni kosa.

      Akisoma hukumu Mheshimiwa Jaji Makame alikubaliana na swala la mtuhumiwa kuwa na dhamira ovu (Malice aforethought), hasa kwa kuangalia vitendo vya mtuhumiwa tangu maandalizi, dhamira na akiwa na utambuzi kwamba, akiwanywesha wanae sumu itawasababishia kifo, na hiyo inadhihirisha kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya, na si lazima ajue kwamba kufanya hivyo ni kosa.

      Hata hivyo Mheshimiwa Jaji Makame alikuwa ameshawishika kuamini hivyo kutokana na barua nne alizoziandika mtuhumiwa kabla ya kutekeleza mauaji hayo, ambazo aliziandika sambamba na tendo alilofanya tarehe 21 Februari 1978. Barua hizo kwa uwazi zilionyesha kabisa kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua anachokifanya ni kosa.

      Kwa maneno yake Mwenyewe Mheshimiwa Jaji Makame alisema, “Katika barua ambayo ilisomwa hapa mahakamani wakati wa shauri hili, mtuhumiwa alisema wazi kwamba mumewe asije akaadhibiwa au kuteswa kwa kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa. Pia kulikuwa na ombi la mtuhumiwa kwa Polisi kwamba, wasije wakamchukulia hatua mumewe kwa sababu hana hatia.”

      Muheshimiwa Jaji Makame aliendelea kusema kwamba, wazo la kutokuwa na hatia na kutompa mumewe adhabu katika barua alizoandika mtuhumiwa, linadhihirisha wazi kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua kwamba kitendo anachokifanya ni kosa na alitaka kuweka wazi kuwa mumewe hahusiki kwa namna yoyote na kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa. Alijua kama mumewe akihusishwa na kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa, ataadhibiwa kwa kosa hilo.

      Mheshimiwa Jaji Makame aliendelea kusema,

      “Ni kweli Dk. Haule alisema kwamba, ukiachana na barua hizo alizoziandika mtuhumiwa, lakini yeye alikuwa na maoni kwamba, mtuhumiwa hakuwa anajua anachokifanya kuwa ni kosa. Alisema, barua zilimuonesha kwamba, mtuhumiwa alikuwa akimtegemea mumewe kwa kiasi kikubwa na hasa katika mahusiano yao. Kama tunamuelewa Dk. Hauli vizuri, alikuwa huenda anamaanisha kwamba, hizo barua zilikuwa na uhusiano na imani aliyokuwa nayo mtuhumiwa kwamba, alikuwa ameshurutishwa kujiuwa na kuwauwa watoto wake na mumewe. Kwa bahati mbaya barua haijaeleza kuwa mtuhumiwa alikuwa na imani ile. Ilikuwa ni ahuweni aliyoiweka Dk Hauli. Japokuwa barua ilieleza kuwa mtuhumiwa alikuwa anamtegemea sana mumewe, lakini bado zilikuwa zinathibitisha kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua kitendo anachokifanya ni kosa.
      Pia nashindwa kuunganisha maelezo ya barua hizo na maoni ya kurukwa na akili yaliyotolewa na Dk. Haule, aliposema kwamba, mtuhumiwa aliamini kuwa ameamriwa na mumewe ajiuwe na kuwauwa watoto wake.”

      Mheshimiwa Jaji aliendelea kusema,

      “Kwangu mimi, namuona Dr. Hauli kama mtaalamu mwenye uzoefu na ujuzi mkubwa wa magonjwa ya akili, pamoja na mambo mengine, pia ni mwanachama Royal College of Psychiatrists na anayo Diploma ya Psychiatric Medicine aliyoipata nchini Uingereza. Naheshimu sana maoni yake kulingana na utaalamu wake na ninashindwa kupinga ushahidi wake. Pia ninakubaliana na ukweli kwamba hata kama mtuhumiwa ataonyesha kurukwa lakini hiyo itakubalika iwapo kutakuwa na kipimo chenye uwelekeo (Balance of Probability).

      Mtuhumiwa lazima aoneshe ushahidi wote; kwamba kutokuwa na akili timamu ni zaidi ya kuwa timamu. Ingawa inawezekana ikawa chini ya tunachodhamiria. Katika kuliweka sawa hili mamlaka ya kuthibitisha inafananishwa na kesi ya Nyinge Siwato Vs Jamhuri 1959 East Africa 974 ikifuatiwa mara nyingi sana ikihusishwa na MbekuleV-R. 1971, East Africa 479. Jaji Enzi zake alielezea katika kesi ya Siwato “Mahakama haifungwi kukubaliana na ushahidi wa hospitalini (Medical Testimony) kama/endapo kuna sababu madhubuti ya kutofanya hivyo. mwisho wa siku ni kazi ya mahakama kutafuta ushahidi na viambatanisho katika kufanya hivyo, ni wajibu wangu kuangalia na kulipima na ushahidi uliotolewa kabla na ikiwemo utaalam wa Daktari.”

      Mheshimiwa Jaji Makame akihitimisha hukumu hiyo alisema:

      “Inawezekana hasa kwamba sheria yetu katika swala la kurukwa na akili imepitwa na wakati na ni ya zamani sana, Dk. Haule katika ushahidi alieleza kuwa katika utaalamu wa sasa, utofauti kati ya kurukwa na akili na kutojitambua katika utenedaji vinapingana. Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa hekima linaweza kulifanyia marekebisho hili sambamba na sheria ndogo ndogo na kulileta katika utandawazi wa kitabibu. Mipaka ya kimahakama, ikiwemo ya Afrika Mashariki wamefanya hivyo.”

      Mtuhumiwa katika kesi hii alihukumiwa kunyongwa.
      JokaKuu, RR, NATA and 26 others like this.

    2. RukaaJuu Final

    3. #41
      Bishanga's Avatar
      JF Tanzanite Member Array
      Join Date : 29th June 2008
      Location : SIRIUS
      Posts : 13,399
      Rep Power : 33554
      Likes Received
      8071
      Likes Given
      7565

      Default

      Quote By JOJEETA
      well said petcash,wanaume muache kuongozwa na hisia.ni vizuri kuthibitisha jambo kabla ya kutoa maamuzi.swali la kizushi hivi mtambuzi wewe mwanasheria?
      Joj usiseme wanaume bana,sema binadamu maana na nyie mna vituko.

    4. #42
      N-handsome's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd January 2008
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 1,859
      Rep Power : 950
      Likes Received
      91
      Likes Given
      478

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Too SAD, unajua sisi wanaume tuna tatizo kubwa sana la kutowaelewa wake zetu. Tukae chini na kuwasoma tutaacha kuwatesa.Maana kwa mwanamke maisha ya ndoa ndio baasi keshamaliza. Happy Mother's Day

    5. #43
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,647
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By ntogwisangu
      Thanks Mtambuzi!kesi hii ni moja ya kesi zilizowahi kutikisa jiji la Dar,kamakesi ilivyofuata kwenye miaka ya 80 mwanzoni kesi iliyomuhusu Dr huyu huyu kwenye kesi hii.Jambo kubwa hapa,kesi zote zilihusisha mambo ya mapenzi,tena kwa vijana wasomi wa kipindi hicho!na zote zilipelekea mauaji ya kutisha!!!Jamo moja kubwa la kujifunza hapa kwetu sote,pamoja na madhaifu yetu kama binadamu,hakuna jambo linaloweza kuumiza nafsi ya mwenzio kama usaliti wa mapenzi.Na basi tunapoamua kuingia katika ndoa ni lazima uamuzi huo uwe umefanyika kwa dhati!!Leo mzee Liundi pamoja na heshima yake katika jamii nadhani ni jambo linalomuumiza mpaka siku mauti yatakampomkuta!!!TUPENDANE KWA DHATI!!!!NDOA SIO MAIGIZO AU MAKARATASI YA MAKANISANI,MSIKITINI AU KWA MKUU WA WILAYA!!
      Well said mkuu...watu hawajui hilo. Matatizo kidogo yakitokea badala ya kushirikiana kama wana ndoa kuyatatua kila excuse inatumika kuhalalisha mambo tofauti yaendelee
      ntogwisangu likes this.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    6. #44
      Bishanga's Avatar
      JF Tanzanite Member Array
      Join Date : 29th June 2008
      Location : SIRIUS
      Posts : 13,399
      Rep Power : 33554
      Likes Received
      8071
      Likes Given
      7565

      Default

      Quote By Smile
      daaah poleni aisee huyo mama kaolewa tena@bishanga?
      ndo mama yake taji liundi?
      Nina muda sina mawasiliano,sina uhakika,ila ni mtu mzima sasa.

    7. #45
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,647
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Kweli kila siku tunajifunza kitu kipya...sikuwahi kujua wala kusikia hii kitu. But it is so painful na hata hiyo familia yenyewe nayo baada ya haya mambo kutokea sidhani kama iliendelea kuwa familia...mhh! Mungu apishe mbali
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    8. Miaka 50

    9. #46
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,647
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By Mtambuzi
      haya Bana...............
      Mkuu unatisha...ukiendelea kutuletea hizi za kibongo bongo tutajifunza mambo mengi sana. Ulaya achana nao..wanagombea uhalali au sio halali jinsia moja kufunga ndoa. Inatuhusu nini sisi kama wameamua hilo??
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    10. #47
      Bishanga's Avatar
      JF Tanzanite Member Array
      Join Date : 29th June 2008
      Location : SIRIUS
      Posts : 13,399
      Rep Power : 33554
      Likes Received
      8071
      Likes Given
      7565

      Default

      Quote By Ronn M
      Doris alikuwa na state of mind which would be subjected to defence of diminishing responsibility. This defence is given when an accused mind was 'impaired' at the time of committing a crime. However it was not in our laws at the time. The judge could not read it in our laws or at invoke it as a new law
      Mkuu hivi ukiwa 'impaired' unachukua hela na kwenda kununua thiodan (thats what she used) kwenye duka la dawa za mimea? I wonder.....tuyaache lakini yashapita.

    11. #48
      mzurimie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th October 2011
      Location : Mtaa Mmoja
      Posts : 818
      Rep Power : 547
      Likes Received
      361
      Likes Given
      87

      Default

      Quote By Mtumishi Wetu
      Mkuu umetoa darasa tosha kabisa tuwe makini kwenye family zetu; kwanza tujifunze kumjua mwenzi wako na back ground yake!! Kila tunapotoa tamko tuwe tunalipima tuache mfumo dume wa vitisho tutapata hasara kwenye miji yetu, kweli hiyo inatisha!!!!

      Hivi wewe ku quote story lote ili iweje? Ungekuwa unaweka ref. Eeh ningekuelewa just click reply inatosha as hii ni story ya kwanza. Na wote tunaisoma na ukijibu tunajua unajibia hii, labda ktk zingine ukiquote kinaeleweka.
      Kongosho and TaiJike like this.

    12. #49
      Asnam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th January 2012
      Location : Yutong
      Posts : 2,618
      Rep Power : 11181
      Likes Received
      1637
      Likes Given
      1170

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      o “Mahakama haifungwi kukubaliana na ushahidi wa hospitalini (Medical Testimony) kama/endapo kuna sababu madhubuti ya kutofanya hivyo. mwisho wa siku ni kazi ya mahakama kutafuta ushahidi na viambatanisho katika kufanya hivyo, ni wajibu wangu kuangalia na kulipima na ushahidi uliotolewa kabla na ikiwemo utaalam wa Daktari.
      hii inaitwa expert opinion in legal terms.Naendelea kukukubali mkuu unaelimisha ile mbaya tusiwe tunakurupuka kufanya maamuzi.
      Mwita Maranya likes this.
      "Quality is always better than quantity. That's why the people I call true are few."

    13. #50
      mzurimie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th October 2011
      Location : Mtaa Mmoja
      Posts : 818
      Rep Power : 547
      Likes Received
      361
      Likes Given
      87

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Mtambuzi shukurani kwa kutujuza tena ya mahakamani. Nyerere alitenda wema kumnusuru.

      Kesi bi kesi wandugu, lazima kuna kesi itakuhusu au haitakuhusu hapa duniani.

      Kama hautaki kujadili na kujifunza huna haja ya ku komenti humu.

      Haya Mtambuzi endelea kuchambua.

    14. #51
      AmaniGK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2008
      Location : MAHALI FLANI
      Posts : 827
      Rep Power : 746
      Likes Received
      64
      Likes Given
      150

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Quote By mtotowamjini
      aisee story ndefu sana nimeshindwa kuisoma yote...so kwa walioisoma yote huyo mama alifanywa nini na mahakama??

      Ndio maana Tanzania inabaki ilipo, kweli habari ya kurasa chache hivi umeshindwa kuisoma yote, ukija kuwa kiongozi ukapewa mkataba mfano wa Richmond for review si utasoma tu ile karatasi ya mwisho tu yenye kuonesha mahali pa kusaini?. Nchi isiyo na wasomaji ni nchi liyojifia.
      rosemarie likes this.

    15. #52
      Ronn M's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Location : Moshi~Arusha
      Posts : 1,283
      Rep Power : 612
      Likes Received
      660
      Likes Given
      403

      Default

      Quote By Bishanga
      Mkuu hivi ukiwa 'impaired' unachukua hela na kwenda kununua thiodan (thats what she used) kwenye duka la dawa za mimea? I wonder.....tuyaache lakini yashapita.
      Its fairly possible mkuu! Kilichofanyika kwa huyu mama ni piling up of bitter and negative issues in her life. Chukulia historia yake ya utoto, halafu akabakwa, kisha mateso daily toka kwa mtu unayempenda na kumtegemea in everything. In that situation unaona kama umebakia peke yako in the whole world, upweke usio na maelezo. Akili yako inakuwa haina alternative na chochote kile unaona ni sawa. Hapo unaweza kuua, ukafanya maandalizi yote ukifahamu unaua, lakini akili yako, kutokana na mlundikano wa bitterness, inaona its a right thing! There you are impaired!

    16. #53
      Bishanga's Avatar
      JF Tanzanite Member Array
      Join Date : 29th June 2008
      Location : SIRIUS
      Posts : 13,399
      Rep Power : 33554
      Likes Received
      8071
      Likes Given
      7565

      Default

      Quote By Ronn M
      Its fairly possible mkuu! Kilichofanyika kwa huyu mama ni piling up of bitter and negative issues in her life. Chukulia historia yake ya utoto, halafu akabakwa, kisha mateso daily toka kwa mtu unayempenda na kumtegemea in everything. In that situation unaona kama umebakia peke yako in the whole world, upweke usio na maelezo. Akili yako inakuwa haina alternative na chochote kile unaona ni sawa. Hapo unaweza kuua, ukafanya maandalizi yote ukifahamu unaua, lakini akili yako, kutokana na mlundikano wa bitterness, inaona its a right thing! There you are impaired!
      Wanasheria bana,hamkosagi maneno.Haya bana.

    17. #54
      Ronn M's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Location : Moshi~Arusha
      Posts : 1,283
      Rep Power : 612
      Likes Received
      660
      Likes Given
      403

      Default

      Quote By AmaniGK
      Ndio maana Tanzania inabaki ilipo, kweli habari ya kurasa chache hivi umeshindwa kuisoma yote, ukija kuwa kiongozi ukapewa mkataba mfano wa Richmond for review si utasoma tu ile karatasi ya mwisho tu yenye kuonesha mahali pa kusaini?. Nchi isiyo na wasomaji ni nchi liyojifia.
      Mtoto wa mjini huyo! Lol
      AmaniGK and Kidogo chetu like this.

    18. #55
      Ronn M's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Location : Moshi~Arusha
      Posts : 1,283
      Rep Power : 612
      Likes Received
      660
      Likes Given
      403

      Default

      Quote By Bishanga
      Wanasheria bana,hamkosagi maneno.Haya bana.
      Sio swala la maneno. There is a difference between law and justice. Not all laws leads to justice. Huyu mama, strictly according to law, she is murderer! But according to justice unaona kabisa she doesnt deserve death but special treatment as a human being! Thats where these principles are introduced in law so that justice is fairly done. Even Makame said he would love to acquit her but was tied by the law! Thats why she was later left free! Kuna kesi ukisoma utatamani ulie, na ukifuata sheria, kitanzi ndo only alternative! Rules of justice and fairness have to be invoked in
      Mwita Maranya likes this.

    19. #56
      Kongosho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Location : Location loading...
      Posts : 25,269
      Rep Power : 13086
      Likes Received
      14148
      Likes Given
      15016

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Duh, hii sio story ya Ijumaa kwa kweli
      Inanyonya nguvu zoote.

      Pole kwa Taji kwa kweli, so sad and so hard.

      Temporally Insanity labda
      mkomatembo likes this.
      No matter how hot your anger is, it can not cook yams-Nigeria

    20. #57
      NATA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th May 2007
      Posts : 4,255
      Rep Power : 8417
      Likes Received
      1134
      Likes Given
      390

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Thanks Gustavo you made my friday!
      Mh kwa kweli it is so sad,

      Mama alitegemea angeondoka na wanawe lakini akabaki na wanawe wakaenda najua niuchungu kiasi gani aliupata baada ya kupata akili timamu.

      Mungu awalaze pema peponi malaika wale.

      Hiki kisa kimenifundisha vitu vingi sana
      Je yule mbakaji alijisikiaje baada ya haya yote kutokea?

      Na huyu mzazi mwenzie wa Doris alijisikiaje na alijutaje?

      Na pia nadhani kipindi hiki nikile wanawake wengi walikuwa tegemezi au waliona maisha bila kuolewa ni hakuna.
      Laiti kama hiyo fukuza ingetokea leo miaka hii nadhani huyu mama angebeba wanawe na kuenda kuanza maisha.

      Pole zake nyingi kwani uwezo wake wakutatua jambo uliishia pale.

      Hivyo nyie watu wa inf. angalieni sana madhara yatokanayo na kuingilia ndoa za watu.

      Nanyi wanaume wapendeni wake zenu na kuwahurumia.

      Ingekuwa ni Mume kabaka I am very sure kwamba Doris angemsamehe na kumstili .

      Playboy and prostute hawa si wote sawa?

      But playboy inaonekana sifa wakati prostute ni aibu na uchafu!

    21. #58
      Cantalisia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2011
      Location : Dar es salaam
      Posts : 4,953
      Rep Power : 3054
      Likes Received
      2630
      Likes Given
      2829

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Mmm! inasikitisha sana jaman,pole sana TL,

      Tumuomben mungu atupe hekima na busara za kuishi maisha ya ndoa,na tupate ujasiri wa kubebeana mapungufu yetu.
      "Be good to the people on your way up,coz you might meet them on your way down"

    22. #59
      Purple's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th February 2012
      Location : mjini
      Posts : 1,795
      Rep Power : 727
      Likes Received
      607
      Likes Given
      415

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Inasikitisha sana jamani,kwa hiyo baada ya huyo mama kuachiwa waliendelea kuishi kama mke na mume??

    23. #60
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,652
      Rep Power : 16779
      Likes Received
      2519
      Likes Given
      1941

      Default Re: Kesi ya Agnes Doris Liundi - Nini hasa kilitokea................?

      Hiki kisa kinasikitisha aisee, haya mambo ya mapenzi yanahitaji umakini...
      Ndahani likes this.

    Page 3 of 8 FirstFirst 12345 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...