WanaJF hususani jamvi la Sheria naomba msaada wenu. Ndugu yangu alishitakiwa kwa kosa la jinai, kesi imekuwa ikisomwa mara kwa mara kwa muda usiopungua siku tisini (90) baada ya hapo mahakama ikaamua kufuta kesi hiyo kwa kuwa shahidi (mshitaki) hajawahi tokea mahakamani toka shauri lianze. Baada ya kesi kufutwa, washitakiwa wamekamatwa tena na kufunguliwa mashitaka yale yale waliyofutiwa na mahakama. Sasa je ni halali kushitakiwa kwa kosa ulilofutiwa na mahakama katika mahakama hiyo hiyo? Nisaidieni ndugu zangu.

Reply With Quote
Follow Us Here