TiGo Internet
    Show/Hide This

    Topic: Muokoeni mama yangu

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 31 to 37 of 37
    1. #1
      Mazeejoh's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 15th January 2011
      Posts : 8
      Rep Power : 372
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Muokoeni mama yangu

      Ahsante kwa kufungua hii mail. Nimatumaini yangu utapata muda wa kunisikiliza na kuguswa kiasi cha kunishauri haraka iwezekanavyo kwani hali ni mbaya...

      Nalazimika kuanza kwa maelezo yafuatayo ili base of argument and the problem itself ieleweke.

      Sisi tumezaliwa watatu wote wakiwa ni wannaume (1978,1980,1985), Baba ni Mtanzania na Mama ni mtanzania. Tulilelewa kenya wote baada ya kuwa mama alikuwa ana fanya kazi kama mwalimu wa HIgh School kule. Baba alikuwa anafanya kazi kama mwalimu pia lakini 1985 aliachishwa kazi baada ya kuwa mlevi na mgomvi mgomvi tofauti na nidhamu ya taaluma inavyotaka. Alipoachishwa kazi mama akawa yeye ndiyo bread winner wa familia. In 1987 baba alituaga kwamba anakwenda nyumbani (TZ) atakuja baada ya wiki moja huyo ukawa mwanzo wa story iliyojaa Hasira, maudhi, kilio, hofu, upweke n.k. maishani mwa kila mmoja wetu.

      Wiki moja ikazaa mwezi, mwaka, miaka 2,5, 10 hadi 13.

      Ndani ya maika hii yote mateso mama aliyopitia sipati maneno ya kutosha kuelezea, maana hata niandikapo hii post roho inauma sana. Alifanya kila awezalo kutuelimisha, kutulisha, kutuvisha na kutulea katika maadili mema. Alijinyima kila aina ya starehe ili tupate mahitaji yetu, alijituma hadi kununua ngombe wa maziwa ili kujiongezea kipato cha kuendesha familia huku gharama zingine zikimuelemea, kidogo kidogo akapata shamba la eka mbili hili likawa tulizo kwani tulilima vyakula na kahawa ambayo ilimsaidia kulipa ada za shule kwa sisi wote. Yalikuwa ni maisha ya taabu sana, Namshukuru mungu hamna kati yetu aliyemuongezea maudhi kwa kuhitaji kisichowezekana. Raha nyingi za ujanani tulizikosa kwani hela ya kuvaa vizuri, kusoma shule bora, kula vizuri, na vitu vingine vizuri vizuri ambavyo wenzetu walikuwa wakivipata hatukapata, T.V. yenyewe hatukuwa nayo, radio ilikuwa ni hadi betri zipatikane sana sana mwisho wa mwezi. Hali iliendelea hivyo hadi mimi nilipomaliza Form 4 ilibidi nimpumzishe mama kwa kualisha miaka miwili ili wadogo zangu wapate ada ya kumalizia masomo yao. Nilibaki nyumbani na mama yangu nikiwa kama house boy sasa kwani kazi zote zilikuwa zangu mama akienda shule. Hapo ndo mama hata afya yake ikiwa afadhali kwani alipata mda wa kupumzika. Baada ya miaka miwili nikapata nafasi ya kujiunga na college ya Printing and Press Operation, mama akauza ngombe mmoja ilinipate fees ya kujiunga, kweli nikajitahidi kadri ya uwezo wangu na baada ya miaka miwili nikahitimu kwa CREDIT jambo ambalo lilimtia mama furaha sana.

      Mapenzi kama upofu fulani

      Katika kupekua barua zake, mama akakuta barua ya zamani sana ikitokea Tanzania. Mama akapata wazo la kufatilia senders postal address ili kujua hatma ya Baba kwani kwa kipindi chote hichi hatujawahi kusikia lolote kutoka kwake. Mara nyingi tulifikir kwamba kafa. Akakusanya hela ya kutosha na kutuaga kwamba anakwenda kumtafuta baba. Alifanikiwa kuja hadi Dar es Salaam na baada ya kufuatilia mwenye anuani ya barua akabahatika kufika kwa Baba Mkubwa wangu. Baba alipatwa na shock ya kufa mtu baada ya kumkuta mama kule jioni aliporudi. Alishindwa cha kusema na kujielezea ikabaki ameduwaa. Baada ya maongezi na mealewano ikaeleweka kwamba lazima sisi (watoto) turudi kwenye chimbuko letu (TANZANIA) ukizingatia wote ni wakiume. Basi mama akarudi na kutupa habari yote, ilikuwa vingumu kuamini na kuelewa eti baada ya miaka Ishirini na Miwili tungeweza kuondoka na kuacha kila kitu lakini kutokana na kuweka furaha ya mama mbele ikabidi tukubaliane nalo.

      BABA ANARUDI
      Baada ya mwezi mmoja toka mama arudi toka Dar es salaam. Baba akawasili, lakini tofauti na mategemeo yetu alikuwa hafanani na mafanikio ambayo tulidhani angekuwa nayo baada ya miaka yote hiyo. Tukampokea na kuamini huu ndo mwanzo mpya wa maisha na familia kwa ujumla. Cha kushangaza wote wawili waliamua kuuza kila kitu ambacho mama yangu alikuwa nacho ilikuja Tanzania waanze upya. Hiyo kwangu ilikuwa dalili ya baba hayupo hali njema ki fedha. Tukauza kila kitu na kuhamia Tanzania. Fedha iliyopatikana ndiyo ikawa kianzio, ikumbukwe mama hajastaafu hivyo ukasukwa mpango ahamishiwe shule jirani na mpaka wa TARIME na KENYA ili aweze kumalizia miaka yake na kupata pension yake. Mama akawa anakwenda asubuhi Kenya anafundisha na jioni anarejea Tanzania. Mshahara wake ukawa unalisha familia kwa sababu Baba hana kazi, mshahara huo huo ukawa unatumika kuwalipia wadogo zangu shule za sekondari hapa Tanzania. Baada ya miaka miwili mama akaja na idea ya kuanzisha shule, ikabidi baba atumie uwenyeji wake na wakapata eneo, mama akatoa hela ikawa kodi ya jengo na baby care class ikaanzishwa. Mama akalazimika kupata mkopo ilikuwezesha Baby Class itabuke ikiwa pamoja na huduma zake, waalimu wawili, uji na chakula cha mchana vikawa vivutio vvya vya wanafunzi kuongezeka. Pakawa na ongezeko kubwa la wanafunzi hadi wazo likawa kuanzisha shule kubwa. Basi Mama aakarudi benki tena na kuchukua mkopo mkubwa zaidi, likapatikana eneo kubwa na majengo matatu yakajengwa.

      Wazazi wangu walienda hatua moja mbele wakafunga ndoa kanisani, hili lilitokea baada ya kubaini baba anawatoto wengine hapa Dar es salaam. (3 watatu wakike 1 dume) baba alibisha sana na kumshawishi mama kwamba ili aamini yupo naye tu na hana mpango wa kado basi wafunge ndoa.. Mama alipostaafu pension yake ilikuwa nzuri sana kiasi kwamba Baba akawa anaitamani. Akaanza visa kwamba haheshimiki kwenye familia kwa sababu hana kazi maalum, akaanza kumlaumu mama eti ndiye anayeharibu familia, eti anatushawishi sisi watoto tudharau baba. Haya yote kwa sababu baba anapenda sana pombe, mara kadhaa amekutwa na vimwana akijirusha, hadi disko, aibu kweli kwa mama na familia kwani wote ni watu wazima na mama ni mzee wa kanisa. Sasa sisi hatukulelewa katika misingi ya ulevi na kujirusha kiasi hicho lazim tutofautiane naye. Lakini hili likawa chanzop cha kuleta vurugu za kumnyima mama usingizi. Ili kumtuliza mama akamnunulia Canter ambayo angeweza kufanyia biashara ya kusafirisha samaki na mazao, yeye akawa akipata hela haonekani nyumbani analewa hadi mtaji, zikiisha analianzisha nyumbani ili apate hela na kuendelea na ufuska wake. Upande wa pili shule imehsakuwa ngumzo katika wilaya ya MARA, kwani hivi sasa ina Boarding na DAY hadi darasa la SABA, ina magari matatu ya kusafirisha watoto na zaidi ya yote matokeo yake yamekuwa ngumzo MARA nzima. Kwa miaka miwili mfululizo imekuwa imeshikilia nafasi ya kwanza wilayani na kufaulisha wanafunzi asilimia 85%. Credit zote ni kwa mama kwa sababu she has been behind the steering all the way. Baba kazi kubwa bi kunywa na kuspend. Anaiba hadi ATM kadi ya account ya shule na ku draw hela bila ridhaa ya mtu yeyote an kuspend anavyotaka.

      Sasa ametangaza kwamba vyote ni vyake, nyumba, magari shule kila kitu ni chake. Anauwezo wa kufanya chochote awezalo bila ushauri wa yeyote yule. Mimi nimeoa na nina motto mmoja hapa DAR, mdogo wangu ameoa ni mwalimu na ana mtoto mmoja anaishi nyumbani tarime, mdogo wetu wa mwisho yupo SAUT Mwanza mwaka wa tatu. Kwangu na wote tunaamini huku nikumuonea mama kwani jasho lote ni lake.

      SWALI LANGU NI JINSI GANI NITAMUOKOA MAMA ILI?

      Kumuajibisha baba kwani ni dhahili siyo responsible but in human?

      Mali ziwe salama?

      Baba asiweze kuuza au kuingia mkataba wowote bila kuhusisha familia yote.?

      Kumdhibiti baba asifanye vurugu?

      Kuhakikisha nia ya mama kwamba vyote vifaidi watoto wa tumbo lake tu litimie.?

    2. #31
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 5,179
      Rep Power : 6147
      Likes Received
      323
      Likes Given
      252

      Default Re: Muokoeni mama yangu

      Kisa kirefu sana mpaka nimeshindwa kukisoma, "summarize". Unajuwa kila kisa kinapokuwa kirefu uongo unakuwa mwingi. Unatuandikia novo nzima, kisa na mkasa?

      Weka mistari mitatu minne yenye nguvu to the point.
      System At Work

    3. #32
      Wingu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2012
      Posts : 352
      Rep Power : 390
      Likes Received
      37
      Likes Given
      40

      Default Re: Muokoeni mama yangu

      Wanasheria jamani msaidieni kijana huyu

    4. #33
      Bondpost's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 16th October 2011
      Posts : 569
      Rep Power : 0
      Likes Received
      108
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By L'AMOUR View Post
      Mmhh tunakoelekea hapa TZ kuna haja ya kuanzisha family Courts
      Ni kweli kabisa mkuu.

    5. #34
      Bondpost's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 16th October 2011
      Posts : 569
      Rep Power : 0
      Likes Received
      108
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By zomba View Post
      Kisa kirefu sana mpaka nimeshindwa kukisoma, "summarize". Unajuwa kila kisa kinapokuwa kirefu uongo unakuwa mwingi. Unatuandikia novo nzima, kisa na mkasa?

      Weka mistari mitatu minne yenye nguvu to the point.
      Dah! Nahisi wewe unataka kujidai ni mathematician! Ila kama umeshindwa kusoma vimistari vichache hivyo sijui wewe upo katika kundi gani!
      Labda uwe unaenda kwenye jamii photo panakufaa! Huku ni maelezo kwa wingi mkuu!
      Ila na wewe yakikukuta utasimulia tu, ngoja tusubiri.

    6. #35
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 5,179
      Rep Power : 6147
      Likes Received
      323
      Likes Given
      252

      Default Re: Muokoeni mama yangu

      Quote By Bondpost View Post
      Dah! Nahisi wewe unataka kujidai ni mathematician! Ila kama umeshindwa kusoma vimistari vichache hivyo sijui wewe upo katika kundi gani!
      Labda uwe unaenda kwenye jamii photo panakufaa! Huku ni maelezo kwa wingi mkuu!
      Ila na wewe yakikukuta utasimulia tu, ngoja tusubiri.
      Si andika novo uuze.

      Hapa unaweka summary tu. Mimi nipo katika kundi wasilopenda uongo wa hadithi ndefu ndefu, huko kwenye picha ndio napapenda sana, unaweka mistari kidogo inayoelezea wazi kabisa. Nadhani hujui kuwa picha moja inaelezea maneno elfu moja. Kama unabishaa muulize Kipanya, yake moja inaelezea maneno laki moja.
      System At Work

    7. #36
      cute beiby's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 12th February 2012
      Posts : 7
      Rep Power : 316
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      Time will tell,

    8. #37
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 5,179
      Rep Power : 6147
      Likes Received
      323
      Likes Given
      252

      Default Re: Muokoeni mama yangu

      Baada ya kupata nafasi na kuipitia tena stori yako, naona hapo tatizo ni tamaa yako. Mwache baba afaidi. Wacha na hao wanawe wengine wafaidi. Mama hajaja na mali yake hapa duniani na anaondoka yeye tu, hivyo-hivyo kwako wewe, kwa baba yako, kwangu mimi na mwingine yeyote yule.

      Kama umewahi kuona raha kupokea, basi jaribu kutoa, si kutoa nauli, si kutoa kilo ya sukari, kutoa kitu ambacho unakipenda kama vile nusu ya mali yako, ukampe mwenye kuihitaji, raha yake haina mfano.

      Wacha ubahili na roho mbaya, umetoka kwa udongo utarudi kwa udondo, Hizi mali zipo na zitaendelea kuwepo milele na milele. Wewe Jee?
      System At Work

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...