Heshima zenu wakuu, na poleni na majukumu ya wiki nzima.
Kuna jambo naomba kujuzwa kuhusu kubadili jina. Hii inatokana na ukweli huu "nilipokuwa std 4 tz nilihamishiwa shule huko kenya ambapo nilisoma miaka miwili ( std 4 &5) kisha nikarudi tz, ile shule niliyokuwa mwanzoni nikakuta jina langu kuna mtu analitumia naye yupo std 7. Nikahamia shule ya jirani mwalimu mkuu akanipa jina la mwanafunzi mwingine ambaye alirudia std 6 nikawa nalitumia hadi sasa nipo chuo mwaka wa 2.
Kuna tetesi nimepata kwamba mtu unaweza kubadili jina. Wajuzi naomba mnijuze, je ni hatua gani natakiwa kuzifuata na je inagharimu fedha yeyote?
Nawasilisha.

Reply With Quote
Follow Us Here