TiGo Maps
    Show/Hide This

    Topic: Tanganyika law society

    Report Post
    Results 1 to 16 of 16
    1. #1
      'The Choosen''s Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Location : Humuhumu
      Posts : 358
      Rep Power : 449
      Likes Received
      36
      Likes Given
      11

      Default Tanganyika law society

      TLS, UKIMYA WENU UNATUGHARIMU.
      Ni jambo la heri kuona kila mmoja anatimiza wajibu na malengo yake ipasavyo ili kusukuma mbele gurudumu la Taifa letu.Baba wa Taifa Hayati Mwalimu J.K.Nyerere aliwahi kusema:yawezekana,timiza wajibu wako.

      TLS (Tanganyika Law Society) ni Chama cha Mawakili cha Tanzania Bara(ambayo ndiyo iliyokuwa Tanganyika).Hii ni taasisi iliyoanzishwa kisheria mnamo mwaka 1954 kwa sheria ya ‘kikoloni’ ya Sheria ya Chama cha Mawakili wa Tanganyika,Sura Nambari 307 ya Sheria za Tanzania.Sheria hii iliundwa na Bunge la Kiingereza.Pamoja na mabadiliko ya hapa na pale yaliyofanywa kwenye Sheria hii,Mawakili wetu wamerithishwa Sheria hii-inawaongoza hadi leo.Ifahamike kuwa Chama hiki cha Mawakili hakihusishi kila Mwanasheria.Uanachama wake umeelezwa vyema chini ya kifungu cha 6 cha sheria husika.Pia kuna Sheria ya Mawakili,Sura ya 341 ya Sheria za Tanzania,pamoja na sheria ndogo na kanuni zilizoundwa kwayo, ambazo nazo zatumika pamoja katika kuwaongoza Mawakili hapa Tanzania. Ijumaa ya tarehe 17/12/2010, idadi ya Mawakili (wanachama wa Chama hiki) Tanzania ilioongezeka.Wapya zaidi ya 300 waliapishwa na Jaji Mkuu katika Sherehe maalumu zilizofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee.

      Chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Chama cha Mawakili,chama kimepewa malengo tisa.Haya ndiyo yanaobeba maana halisi ya uwepo wa taasisi hii,nguvu zake na zaidi sana umuhimu wake.Malengo manne kati ya hayo yanagusa mojakwamoja ima wadau wa sheria au umma kwa ujumla.Malengo hayo manne yanaelezwa hapa ili makala hii ipate mshiko wake stahiki.Kwanza,Chama kina lengo la kuendeleza na kuimarisha viwango vya utendaji na mafunzo ya kada ya sheria.Pili,kuwezesha upatikanaji wa uelewa wa kisheria kwa wanachama wake na wengineo.Tatu,kuisaidia serikali na mahakama kwenye masuala yote yahusuyo Sheria za Bunge,utawala na utendaji wa sheria Tanzania.Na nne,kuulinda na kuusaidia umma wa Tanzania katika masuala yote yahusuyo sheria.

      Kwa kutazama malengo hayo mema yaliyotolewa na Sheria kwa Chama cha Mawakili,ni wazi kuwa Jumuiya hii ya Mawakili ni ‘tegemezi’ sana kwa jamii nzima ya Tanzania.Chama hiki cha Mawakili kilitegemewa na wanasheria ambao ni lazima wajiunge na Shule ya Sheria ya Tanzania kwa ajili ya kupata mafunzo ya sheria kwa vitendo wawasaidie kuelewa vyema hatima yao.Mawakili walitegemewa kuwaeleza wanachama wao watarajiwa ni kwanini mafunzo hayo kwa vitendo ‘yameporwa’ kutoka kwenye mitaala yao ya Shahada ya kwanza ya sheria huku tasnia nyingine zote zikipata mafunzo hayo zikiwa vyuoni.Chama kilitegemewa kuwaambia wanachama watarajiwa juu ya wapi watapata fedha za kugharimia mafunzo yao hayo ya lazima ikiwa wengi wao,punde tu, walikuwa wanategemea Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.Pia,wangewaambia kwanini Sheria mpya ya Shule ya Sheria ya Tanzania,2007 ‘imeipanda kichwani’ Sheria ya Mawakili hata bila kubadili sifa za mtu kuwa Wakili kama zinavyoidhinishwa chini ya kifungu cha 39 cha Sheria ya Mawakili,Sura Na.341.Chama kingefanya hivyo,kingekuwa kinatekeleza na kulifikia lengo la kwanza.Ukimya mkuu umetanda juu ya hili.Kwanini?

      Sasa kuna suala la Katiba mpya.Kama ilivyotokea katika kipindi cha miaka ya 80, pale ambapo Chama hiki cha Mawakili kilisimama kidete na mstari wa mbele kuishinikiza Serikali kuweka Ibara zinazozungumzia Haki za Binadamu katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.Serikali ‘ilisikiliza’ sauti ya Chama hiki na wadau wengineo na kukubali kuingiza Haki za Binadamu ndani ya Katiba yetu mwaka 1984 kupitia Sheria Nambari 15 ya mwaka huo.Sasa,Ibara za 12-30 za Katiba yetu zinatulinda! Tulitarajia kuwa Chama hiki kingerudia harakati zake au zinazofanana na zile za miaka ya 80 kufanikisha uundwaji wa Katiba mpya.Chakushangaza,Chama hiki cha Mawakili kimekuwa kimya mno.Ni mwanachama mmojammoja tu ndiye anayejitokeza kutoa maoni yake juu ya Katiba mpya.Tumewasikia akina Profesa Issa Gulamhussein Shivji,Profesa Abdala Safari,na Arold Sungusia ‘wakitoka kivyao’. Kwanini kusiwe na tamko la pamoja la kuonyesha msimamo wa Chama juu ya suala hili la Katiba mpya? Lengo la nne lililoelezwa hapo juu litafikiwaje?

      Chama hiki cha Mawakili ni muhimu sana kwa watanzania wote.Sio tu kwa kuwapatia ‘watetezi’ kwenye kesi zao bali pia kuwafumbua macho na kuwasaidia kadiri ya uwezo wa kisheria kilichopewa.Watanzania wengi ni ‘majuha’ wa sheria.Wanatamani sana kusikia ufafanuzi wa kisheria wa mambo wanayoyasikia kila siku:Richmond,Meremeta,IPTL,Do wans,EPA,Kiwira,Buzwagi na mengineyo.Chama hiki kinawanyima uhondo-hakisemi ukweli.Wanachama wake wanabaki tu kuchangamkia nafasi za kuwatetea washtakiwa wa mambo kama haya na mengine wakisahau wajibu(malengo) wao.Wanabaki wakiwa ‘bize’ mahakamani kwa kesi ambazo kama wangeshiriki ipasavyo kutimiza wajibu wao kwa Taifa zisingekuwa hivyo zilivyo.

      Ni wakati muafaka sasa kwa Chama hiki cha Mawakili kuvaa uhalisia wake-kurudi kwenye malengo yake.Majibu ya mateso ya wanasheria juu ya Shule ya Sheria ya Tanzania na mengineyo muhimu kwa umma wa Tanzania yanasubiriwa kwa hamu.Mabegi makubwa ya wanachama wa TLS sasa yabebe pia hoja murajabu juu ya mustakabali wa Taifa letu badala ya kubeba tu hati za mashtaka za wateja wao,Sheria zinazowaoongoza na kalamu.Pia,wasiwe ‘bize’ tu kuchukuliana hatua za kinidhamu.Ni muda wa TLS kusema na Serikali isikie.Umma utasikiliza.Utamuona mbaya nani.Utamshughulikia.TLS anzisheni Tanzania yenye neema na si hii ya kuhema.Ni ukweli usio kifani kuwa ukimya wa TLS unatugharimu.
      VUTA-NKUVUTE likes this.


    2. #2
      ngoshwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st March 2009
      Location : everywhere
      Posts : 2,872
      Rep Power : 1140
      Likes Received
      268
      Likes Given
      355

      Default Re: Tanganyika law society

      Kutakuwa na AGM ya TLS tarehe 18-19/2/2011 mkuu. Ni muhimu kuwasilisha hzi hoja kwa Sekretariate ya TLS

      Mchango mzuri mkuu.
      "Mnataka kujua nini? Sikuzaliwa ili nipate nishani... "Please don't make it an issue, acheni suala hilo ni uchonganishi, acheni," - Malecela.

    3. #3
      MaxShimba's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 11th April 2008
      Posts : 12,714
      Rep Power : 3672
      Likes Received
      2180
      Likes Given
      361

      Default Re: Tanganyika law society

      Thanks for the post
      Dr. MaxShimba is a friend of God and a Bondservant of Jesus Christ

    4. #4
      Kapo Jr's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 31st January 2011
      Posts : 189
      Rep Power : 406
      Likes Received
      10
      Likes Given
      0

      Default Re: Tanganyika law society

      Muswada mzuri MaxShimba respectfuly idea,ni kweli asilimia kubwa watanzania wanahitaji elimu ya sheria kupitia TLS kupitia makongamano mbalimbali na semina ili kila mtu ajue haki zake

    5. #5
      Pokola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th July 2010
      Location : Tanzania
      Posts : 458
      Rep Power : 488
      Likes Received
      27
      Likes Given
      64

      Default Re: Tanganyika law society

      Tanzania haina wakili. Imejaa bunch of hypocrites, associated to form their segregative Society. Tabia za watu hawa ni za ajabu sana. Hupoteza muda mwingi wa maisha yao ktk kujisifu, na si kuisaidia jamii. Kila mtu mwengine duniani anawachakia sana watu hawa. Imeandikwa katika msahafu kuwa itakuwa vigumu kwa watu hawa, watoza ushuru na mathenashara kuurithi ufalme wa MUNGU.

      ANGALIZO: Mimi ni mwanasheria.
      Watanzania ikimbieni Rushwa!!

    6. #6
      Hammer's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th October 2010
      Posts : 25
      Rep Power : 389
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Tanganyika law society

      Mmmh! unafiki na kujipendekeza kwa watawala hatutaacha. Hiyo ndo nguzo yetu TLS.

    7. #7
      'The Choosen''s Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Location : Humuhumu
      Posts : 358
      Rep Power : 449
      Likes Received
      36
      Likes Given
      11

      Default Re: Tanganyika law society

      Hadi lini mambo haya? Stolla upo?
      Kumaliza unyama wa mabomu ya wanajeshi na risasi za polisi,kura zinyimwe kwa CCM...CCM hawana huruma hata kwa wapiga kura wao?!

    8. #8
      luluka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th October 2011
      Posts : 326
      Rep Power : 463
      Likes Received
      64
      Likes Given
      5

      Default Re: Tanganyika law society

      TlS wanaanza mkutano kesho arusha,so its time ya kupresent hayo malalamiko if possible.

    9. #9
      Buchanan's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 19th May 2009
      Location : Somewhere!
      Posts : 8,090
      Rep Power : 6316
      Likes Received
      469
      Likes Given
      183

      Default Re: Tanganyika law society

      Mkuu The Choosen,
      Mawazo yako ni maridadi sana, lakini bahati mbaya waTz hatufuati Sheria, ndio maana Katiba ya JMT, 1977 bado ina Cheo cha "Waziri Kiongozi" wa SMZ na tunachekelea kwamba its OK! Sasa kama Katiba yenyewe haiendani na uhalisia unategemea Sheria za kawaida kama The Law School of Tanzania Act, 2007 na The Advocates Act, Cap. 341 ndio zitakuwaje? Hata zigongane vipi, kwetu ni tambarare tu, bora liende!

    10. #10
      Bwa'Nchuchu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th February 2012
      Posts : 754
      Rep Power : 565
      Likes Received
      264
      Likes Given
      43

      Default Re: Tanganyika law society

      Quote By Pokola View Post
      Tanzania haina wakili. Imejaa bunch of hypocrites, associated to form their segregative Society. Tabia za watu hawa ni za ajabu sana. Hupoteza muda mwingi wa maisha yao ktk kujisifu, na si kuisaidia jamii. Kila mtu mwengine duniani anawachakia sana watu hawa. Imeandikwa katika msahafu kuwa itakuwa vigumu kwa watu hawa, watoza ushuru na mathenashara kuurithi ufalme wa MUNGU.

      ANGALIZO: Mimi ni mwanasheria.
      Teh teh teh...wenyewe wanajiita "wasomi"...utawasikia wanasema "learned brother"..."learned sister".....lol
      Context is everything.

    11. #11
      prakatatumba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th October 2011
      Posts : 427
      Rep Power : 417
      Likes Received
      43
      Likes Given
      8

      Default Re: Tanganyika law society

      Quote By Pokola View Post
      Tanzania haina wakili. Imejaa bunch of hypocrites, associated to form their segregative Society. Tabia za watu hawa ni za ajabu sana. Hupoteza muda mwingi wa maisha yao ktk kujisifu, na si kuisaidia jamii. Kila mtu mwengine duniani anawachakia sana watu hawa. Imeandikwa katika msahafu kuwa itakuwa vigumu kwa watu hawa, watoza ushuru na mathenashara kuurithi ufalme wa MUNGU. ANGALIZO: Mimi ni mwanasheria.
      haya briefcase lawyer, bush lawyer maana unatoa sababu bila kusema njia ya kulitatua


    12. #12
      VUTA-NKUVUTE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2011
      Posts : 485
      Rep Power : 428
      Likes Received
      194
      Likes Given
      62

      Default Re: Tanganyika law society

      Mawazo yako nimeyafikisha mahali stahiki.Stolla-Rais wa TLS ameniahidi kuyafanyia kazi.Asante kwa mawazo yako ya kujenga.

    13. #13
      Elungata's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th January 2011
      Posts : 983
      Rep Power : 565
      Likes Received
      46
      Likes Given
      0

      Default Re: Tanganyika law society

      dah,stolla F.K. ni jembe.bgup teacher wangu from way back BUSECO

    14. #14
      ha ha ha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th December 2011
      Location : Hapahapa
      Posts : 271
      Rep Power : 376
      Likes Received
      26
      Likes Given
      58

      Default Re: Tanganyika law society

      I concur...
      "If you find yourself in ahole, the first thing to do is stop digging"



    15. #15
      kajunju's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th June 2011
      Posts : 203
      Rep Power : 387
      Likes Received
      35
      Likes Given
      2

      Default Re: Tanganyika law society

      Kuna mwana sheria mmoja anaitwa Nshala rugemeleza.siku moja kwenye tv alisema TLS imepoteza mwelekeo.Viongoz wake ni wanafki na wachumia tumbo.alisema mawakili wengi wa tz ni mafisad kwani wanausika na mikataba michafu ya kuumiza ndugu zao.siku hiyo alimshambulia ngeleja kuwa kwenye sheria hajui kitu. Namfananisha kwa msimamo na tundu lisu japo ana kama ka-kigugumizi

    16. #16
      Mtundu Kisu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th September 2011
      Posts : 480
      Rep Power : 432
      Likes Received
      88
      Likes Given
      8

      Default Re: Tanganyika law society

      Kuhusu suala la katiba mpya hujaskia TLS walitoa tamko?Na walikua katika mchakato wa kuinstitute kesi high court kuchallenge sheria ya marekebisho ya katiba pia?

      Kuhusu Law school nakubaliana na mtoa hoja mia kwa mia.Hapo there is an issue,seriously.

    Similar Topics

    1. Tanganyika law society wabadili jina!?
      By Degedege in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 2
      Last Post: 14th December 2011, 14:27
    2. Replies: 61
      Last Post: 11th April 2011, 21:47
    3. Kazi: Tanganyika law society
      By CHAUMBEYA in forum Nafasi za Kazi na Tenda
      Replies: 2
      Last Post: 4th May 2009, 16:25
    4. Tanganyika Law Society-taarifa Kwa Umma
      By Kana-Ka-Nsungu in forum Jukwaa la Sheria (The Law Forum)
      Replies: 12
      Last Post: 24th November 2007, 12:15
    5. Tanganyika Law Society
      By JF XXL in forum Jukwaa la Sheria (The Law Forum)
      Replies: 1
      Last Post: 20th July 2007, 02:28

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...