| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
|
#1 | |||||||||||
|
||||||||||||
|
Views: 19682
|
||||||||||||
|
#2
|
|||||||||||||||
|
|||||||||||||||
Vukiza au fukiza? Vukiza linatokana na nahau ya "Vuka" yenye maana ya kupitisha kitu kwenda upande mwingine bila kukutana na kizuizi. Mf. Kuvuka mto, kuvuka daraja n.k Hivyo neno vukiza ni tendo lakutendewa ingawa neno linalotumika kwa usahihi ni "vukisha" na si "vukiza" Wakati mwingine watu wanalitumia neno hilo kwa makosa wakitaka kumaanisha "fukiza" Fukiza ni nahau yenye maana ya kupepea moshi, gasi n.k kuelekea upande fulani kwa makusudi. Ni hapo basi watu wanafukiza ubani, wanafukiza moshi wa maji ya mwarobaini n.k Vundika au vumbika? Vundika inatokana na neno "Vunda" lenye maana ya kitu kilichoharibika na kuchacha kwa sababu ya kukaa kwa muda mrefu bila kutumika na kimefanywa hivyo kwa makusudi. Ni tofauti na kitu "kuoza" Ni kwa sababu hiyo watu wanavundika mchele, mtama, ndivi n.k ili kutengeneza pombe au matunda mengine ili kutengeneza mvinyo. Vumbika, bila ya shaka linahusiana na kitu kuwekwa vumbi!!! Ila na Ingawa Neno "Ila" lina asili ya kiarabu ambapo maana yake haswa ni kusema "Isipokuwa" K.m Ni lazima mtu atii mamlaka ila ile isiyo ya halali! Ingawa ni neno lenye maana ya "licha ya kwamba" au "pamoja na ukweli kuwa" au "hata kama". mf. watu walienda shule ingawa mvua kubwa ilinyesha! Msanii ni neno lilatokana na neno "Sanaa". Aneyejishughulisha na sanaa huyo anaitwa msanii. Hata hivyo neno hilo siku hizi linatumiwa kuonesha kuwa mtu "ni mjanja mjanja na si mkweli" katika mambo yake. Kwa leo hayo yatosha.
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania" |
|||||||||||||||
|
#3
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Nashukuru... Naambiwa computa si kiswahili fasaha. Ila huyu kanijibu kwa PM. Ati ni tarakirishi. Shukrani kwa walionisaidia. Nina maneno mengi ningependa wenye upeo wa kuainisha kama mheshimiwa Mzee Mwanakijiji alivyosaidia hapo juu. Kuna maneno yamesalia sijapewa majibu, nikipata nitafurahi.
Internet kiswahili chake ni kipi? Mchakato ndiyo maana ya process? Kuna neno linakuwa linatamkwa mara nyingi SANJALI je lina uhusiano na Mkabala? Mzee naomba unisaidie kama unaweza. Nipo kizani na napenda kujifunza zaidi lugha hii kwa mapana. Ahsante
__________________
Welcome to JF Phase II... Contact me: Mobile: +255713444649 Email: maxence@maxence.co.tz Pls DO NOT send me Job applications... Read adverts carefully! |
|
#4
|
||||||||||||
|
||||||||||||
Kwa hiyo violesura vyangu vya word, excel, outlook na power point vyooote viko kwa kiswahili. Ni burudani flani hivi I must say.. maana kuna maneno ya ajabu ajabu hata sijui waliotafsiri wameyatoa wapi, kwa mfano ... kujibu swali lako .. pahala pa "My Computer" pameandikwa 'Ngamizi yangu'. Sasa hata sijui computer kuwa Ngamizi inangamiza nini! |
||||||||||||
|
#5
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Duh, hao wamefurahisha. Basi wacha niitembelee hiyo link. Tunapenda wazalendo wa aina yako! Ahsante
__________________
Welcome to JF Phase II... Contact me: Mobile: +255713444649 Email: maxence@maxence.co.tz Pls DO NOT send me Job applications... Read adverts carefully! |
|
#6
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Kuna maneno sijajibiwa lakini naamini kuna watanzania wanaweza kunisaidia. Kuna wanaosema Computer ni Tarakirishi, sasa naona kuna Ngamizi sijui ni lipi sahihi. Hivi hakuna mtanzania anayejua kiswahili chake kilichokubalika?
Nisaidieni tafadhali!
__________________
Welcome to JF Phase II... Contact me: Mobile: +255713444649 Email: maxence@maxence.co.tz Pls DO NOT send me Job applications... Read adverts carefully! |
|
#7
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
I do think sometimes tunalazimisha maneno ya kiswahili na as a result hata haileti maana wala ladha ya Lugha. Computer ni neno geni, yaani halikuzaliwa na waswahili. Therefore kama yalivyo maneno mengine ya kigeni tuliyorithi whay not call it KOMPYUTA kama yulivyozoea yaani tunaandika kama tunavyotamka neno ingawa ni la kigeni.
|
|
#8
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Haya niendelee:
Puchu - koswa, ni kama almanusura, mf. Aliponea puchu gari lilipomkaribia! kusisitiza mara nyingi husema puchu puchu yaani koswa koswa!! Mkwara - kwa kifupi lina maana ya vitisho ambavyo mara nyingi havitekelezwi. Lengo ni kuhakikisha matokeo yanayotakiwa. Mf. Alimpiga mkwara kuwa ampe shilingi 50 ama sivyo atamuambia mama! Mwake - sijaelewa umelitoa wapi maana lina maana nyingi na sijui ni ipi ambayo unaitafuta! Chuna - maana ya kwanza ni kuondoa ngozi bila kukata nyama! lakini linatumika katika kiswahili cha mtaani kumaanisha mtu kuchukuliwa pesa zake kwa hiari yake lakini bila yeye kutambua analaghaiwa! Pia lina maana ya mtu kutotaka kusema au kujieleza kwa namna yoyote ile kwa vile amekasirika au ameamua kutozungumza. Linaendana na neno "Nuna" ambapo aliyenuna ana sababu, aliyeu"uchuna" hataki kusema awe na sababu au la. Mbongo, ni neno la kiswahili cha mtaani likimaanisha mtu anayetoka Bongo (kama nchi) au anayetoka Dar.. lakini siku hizi inakubalika zaidi kuwa mbongo ni mtu anayetoka Tanzania!! Kompyuta kwa kiswahili sijui kwa nini inaitwa ngamizi. Kwa maoni yangu ingeitwa Kikokotoshi, kwani neno compute (ambalo ni chanzo cha neno computer) kinatokana na uwezo wa chombo hicho kukokotoa (calculate) hesabu kwa haraka kuliko kutumia kalamu na karatasi!
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania" |
|
#9
|
|||||||||||
|
|||||||||||
![]()
__________________
Thin line between creativity and madness |
|
#10
|
|||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||
|
WoRM, umeridhika?
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 06:36 PM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | |||||||||||||||||||||||