Nimekuwa nasikia maneno haya lakini yananichanganya kujua matumizi yake sahihi.
Vukiza au fukiza?
Vundika au vumbika?
Compyuta?
Mtandao
ila
ingawa
msanii
puchu
mkwara
mwake
chuna
mbongo
Ninayo maneno lukuki lakini nashindwa kuyaainisha yote hapa. Naomba wataalam wa lugha hii adhimu mnisaidie nitoke niliko walau hatua moja mbele katika kujifunza Kiswahili.
Ahsanteni
__________________ Welcome to JF Phase II...
Contact me:
Mobile: +255713444649
Email: maxence@maxence.co.tz
Pls DO NOT send me Job applications... Read adverts carefully!
Mi naomba kufahamishwa jambo moja, hivi inakuwaje watu wanaopiga kelele au kuongea kwa sauti kubwa yenye kukera, wakitakiwa kunyamazishwa utamsikia mtu anasema... mf: Jamani eeh! "Keleleni" au "kelelee"
Wakati mwingine utawasikia watu wanabishana na mmoja anamwambia mwenzie kwa sauti kubwa... "Kelelee...!"
Hii inamaanisha nini wakuu.
Naomba kuwakilisha...!
__________________
“I am the punishment of God... If you had not committed great sins, God would not have sent a punishment like me upon you.”
'O Allah! Keep me alive as long as life is better for me, and let me die if death is better for me.
Mi naomba kufahamishwa jambo moja, hivi inakuwaje watu wanaopiga kelele au kuongea kwa sauti kubwa yenye kukera, wakitakiwa kunyamazishwa utamsikia mtu anasema... mf: Jamani eeh! "Keleleni" au "kelelee"
Wakati mwingine utawasikia watu wanabishana na mmoja anamwambia mwenzie kwa sauti kubwa... "Kelelee...!"
Hii inamaanisha nini wakuu.
Naomba kuwakilisha...!
Wakati mwingine lugha haina mantiki ('logic'). Ni sauti za nasibu ambazo watu (jamii) 'inakubaliana' kutumia katika kuwasiliana. Maneno hayo pengine kimantiki hayakubaliki lakini jamii ya waswahili tumekubaliana kuyatumia kama yalivyo - na kwa kweli tunaelewana!. Mtu akikwambia kwa sauti 'kelelee'! unajua fika ana maana acha kelele. Ni kama vile neno 'acha' kwa makusudi linaachwa silent kwa sababu msemaji ana-assume msikilizaji (anaepiga kelele!)ataelewa.
Kiswahili kina maneno/misemo mingi tu ya jinsi hii. Kwa mfano mtu anaweza kusema:
- 'Mambo'? (akiwa na maana ya 'mambo vipi'?)
- 'Za saa hizi? (akiwa na maana ya 'habari za saa hizi'?)
- 'Za kwako?(akiwa na maana ya 'habari za (nyumbani) kwako'?)
- 'Nakuja!' - wakati in reality mtu anondoka' (akiwa na maana ya 'nitarudi punde' au 'nitakuja tena baada ya muda mfupi')
Hongera sana MAXENCE kwa kuuliza Maswali, na SHUKRANI SANA kwa Mzee M/Kijiji kwa majibu yake sahihi na yenye maelezo yanayojitosheleza. ama kweli JF ni Darasa la kutosha. Hebu tuendelee kujifunza na kuwa wazi kama kawaida badala ya Malumbano.
Heshima mbele wakuu..Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakiitwa 'Vihiyo' na pia baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikilitumia neno hili,,utakuta gazeti fulani limeandika(kwa mfano) "Kiongozi kihiyo aumbuka" ama utakuta mtu anasema "Balantanda ni kihiyo"...Hivi wakuu asili ya neno hili ni nini hasa??,,je,neno hili ni rasmi kwa sasa katika lugha yetu adhimu ya Kiswahili??,,na mwisho je,ni zipi sifa hasa za mtu kuitwa 'Kihiyo'...Naombeni msaada wakuu
__________________ Amantium irae amoris integratio est
Kihiyo alikuwa mbunge (Nadhani wa Temeke) alifoji vyeti kuwa alisoma Dar Technical college(siku hizi DIT).
Kihiyo huyo baada ya kuonekana kafoji vyeti akapigwa chini ubunge (Nadhani ndio kipindi Mrema akagombea na kuwa mbuge wa Temeke)
Kuanzia hapo watu waliokuwa wakionekana kama wamefoji vyeti au hawana utaalamu ktk field zao huitwa Kihiyo.Kwa viongozi utasikia viongozi Vihiyo.
Ni surname ya mtu hiyo ahaaaaaaaaaaaaaa,ila ndio imeingia katika kiswahili cha bongo ,ukizingatia kuwa moja ya sifa ya lugha ni kuwa lugha hukuwa na pia ni mpangilio wa sauti za nasibu zilizo kubalika na kutumika na jamii ya sehemu fulani.