Nimekuwa nasikia maneno haya lakini yananichanganya kujua matumizi yake sahihi.
Vukiza au fukiza?
Vundika au vumbika?
Compyuta?
Mtandao
ila
ingawa
msanii
puchu
mkwara
mwake
chuna
mbongo
Ninayo maneno lukuki lakini nashindwa kuyaainisha yote hapa. Naomba wataalam wa lugha hii adhimu mnisaidie nitoke niliko walau hatua moja mbele katika kujifunza Kiswahili.
Hilo neno maana yake ni "KUDIRIKI" - likiwa na maana "kufanya jambo fulani pamoja na kuwa jambo hilo linaweza kuwa na hatari au athari mbaya".
neno diriki ni sawa na thubutu ambayo kwa cha wenyewe wanasema "dare". Venture nadhani inaelekea huko huko na yawezekana kutumia "diriki" kutafsiri "venture" laweza kuwa sahihi.
__________________ Maskini ka-nzi kangu, wamekaminya mbawa Upanga! Sasa ntafanya nini?
I'm now twittering - If I know it...u'll know it too
The Following User Says Thank You to Mzee Mwanakijiji For This Useful Post:
Nadhani pia waweza kutumia neno 'mhanga' sina uhakika sana ila nadhani katika matumizi ya kiswahili na kutoa tafsiri ya neno kutoka lugha fulani, neno hilo linaweza kuongeleka au kuandikika kirahisi zaidi hata kama tafsiri yake kwenda kiingereza itakuwa si sahihi sana ukilinganisha na pale linapotumika ndani ya kiswahili.
Nimependekeza neno hili baada ya kufikiria matumizi ya venture kwenye mifano mbalimbali na hiyo hapo juu ya Mkjj.
my two cents!
__________________
Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi. SDD1-09.
Fikra ni nyenzo endelezi au potofu. Changamoto tuliyonayo ni kuchanganua na kutenganisha kati ya fikra endelevu na fikra potofu, kwani mwisho wa fikra ni matendo pale fikra hazibakii kuwa fikra. SDD6-07Rev.2-09.
The Following 2 Users Say Thank You to SteveD For This Useful Post:
neno diriki ni sawa na thubutu ambayo kwa cha wenyewe wanasema "dare". Venture nadhani inaelekea huko huko na yawezekana kutumia "diriki" kutafsiri "venture" laweza kuwa sahihi.
Venture is an undertaking which is daring.
Kuna tofauti kati ya kudiriki na kuthubutu?
__________________
The Following 2 Users Say Thank You to Tanzania2020 For This Useful Post:
a. "kudiriki" ni kufanya kitu kwa kudhamiria hasa pale inapozaniwa kuwa kitu hicho hakitafanyika. Katika hili kudirika kuna presume kuwa kitu fulani hakitafanyika.
mfano: "Alidiriki kumpinga hadharani" - hakuna aliyedhania atafanya hivyo lakini alifanya hivyo. Kitu ambacho mtu amediriki kukifanya hakikuonekana uwezekano wa kufanyika.
b. Kuthubutu ni kutenda bila ya kujali matokeo yake hata kama watu wanajua kitendo hicho kinaweza kufanywa. Mtu anayethubutu kusema au kufanya kitu anaweza kujua uwezekano wa matokeo fulani lakini bila kujali uwezekano wa ubaya/hatari/tatizo bado atafanya kitu hicho.
mfano: Alithubutu kumpinga hadharani licha ya kuambiwa kwa kufanya hivyo kutamfukuzisha kazi.
Kudiriki hakuoneshi mgongano ni kitendo kinachoendana na uungwana kuliko ukorofi, ugomvi, au kujitakia ubaya, lakini kuthubutu mara zote kunaendana na mgongano na uwezekano wa jambo baya kutokea.
M.M.
__________________ Maskini ka-nzi kangu, wamekaminya mbawa Upanga! Sasa ntafanya nini?
I'm now twittering - If I know it...u'll know it too
The Following 4 Users Say Thank You to Mzee Mwanakijiji For This Useful Post:
sasa hii inajibu vipi neno "venture"... naona bado niko kwenye kipeo cha kwanza!
--venture capitalist: bepari mhanga
--he/she ventured into something: alidiriki kufanya kitu fulani
--suicide terrorist: gaidi wa kujitoa mhanga
--suicide attempt: jaribio la kujiua
Hapo ndipo maana mimi nasema 'mhanga' laweza kuwa na nafasi yake kutegemeana na sentensi. Si lazima liwe na maana kamili katika kiingereza, as long as linaleta ladha nzuri na kueleweka kwenye kiswahili. Ndipo hapo unapokuta sisi hatuna she au he, lakini wao wanazo.
SteveD.
__________________
Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi. SDD1-09.
Fikra ni nyenzo endelezi au potofu. Changamoto tuliyonayo ni kuchanganua na kutenganisha kati ya fikra endelevu na fikra potofu, kwani mwisho wa fikra ni matendo pale fikra hazibakii kuwa fikra. SDD6-07Rev.2-09.
mhanga - inatumiwa vibaya sana. Mhanga kimsingi ni "victim" yaani mtu aliyekutwa na jambo baya SIYO mtu alinayefanya jambo ambalo ambalo laweza kuwa baya au zuri.
hivyo: tuna "Mhanga wa mafuriko ya Tsunami" - Victim of the Tsunami"
Walioharibu matumizi ya neno hilo naamini ni BBC ambao walianza kutafsiri neno "waliojitoa mhanga" wakifikiri wanamaanisha aliyejitolea kuua!
Kujitoa mhanga ni kuwa kujitolea ili wawe yakukute yale mabaya ambayo yalikuwa yawakute watu wengine; you become a victim. Kwa wale waliowahi kuiona filamu ya "War Bus" watakumbuka askari mmoja mlevi mlevi aliwaokoa wenzake liliporushwa bomu la mkono kwa yeye kujirusha juu ya bomu hilo na hivyo likamlipua yeye na kumuua na kuwanusuru wale wengine (waliokuwa wanahangaika kwenye basi kuondoka eneo hilo). HIvyo yule askari "alijitoa mhanga" kuwaokoa wengine, he became a victim.
Hivyo basi, "mhanga" ni mtu ambaye anakutwa na jambo ambalo ni baya (huwezi kuwa mhanga wa jambo zuri) aidha alilolitarajia (kwa kuweka maslahi yake nyuma) au pasipo kulitarajia (kwa bahati mbaya).
Naamini mhanga anaweza akawa aliyenusurika (siyo lazima afe) na pia anaweza kufa katika kujitahidi kuokoa au kufanya jambo ambalo linanusuru, kuokoa maisha ya watu wengine.
__________________ Maskini ka-nzi kangu, wamekaminya mbawa Upanga! Sasa ntafanya nini?
I'm now twittering - If I know it...u'll know it too
The Following User Says Thank You to Mzee Mwanakijiji For This Useful Post:
To venture one's fortune = 'cheza pata potea na mali za mtu'
to invest venture capital = 'kuwekeza mtaji pata-potea'
venture one's life = 'cheza patapotea na maisha'
2. venture = 'diriki/thubutu' mfano:
I venture to say that you are insane = 'nadiriki ama nathubutu kusema wewe huna akili timamu/mwehu'